Simulizi: Scaila Michael

Sehemu ya 21

Naweza kusema siku hiyo ilikuwa ni ya kukumbuka katika maisha yangu, nilikuwa na furaha kupita kawaida. Huyu Scaila alinichanganya sana, muda wote kila nilipokuwa nikimwangalia, nilihisi kama nilikutana na malaika fulani hivi.

Niliondoka na kurudi nyumbani. Nilikuwa nikizungumza naye kwenye simu kila wakati. Nilihitaji kumuonyeshea kwamba nilimpenda na kumjali kuliko mwanamke yeyote yule chini ya jua.

Alifurahia sana, nikajua kwamba na yeye kwa kipindi kirefu alikuwa akitafuta mwanaume ambaye angekuwa na msimamo wa maisha yake, amchukue na kuishi naye.

Nilipofika nyumbani, nilimwambia Grace kile kilichojiri, alifurahi sana, katika maisha yake alitamani sana kuona nikifanikiwa, kwa kipindi kirefu alikuwa akiniuliza ni lini ningeoa kwani muda ulikuwa ukienda na hakuona mategemeo yoyote yale.

“Kwa hiyo tutakula ubwabwa hivi karibuni?” aliniuliza huku akicheka.
“Kabisa. Yaani suti nitakayoinyuka siku hiyo! Nadhani itakuwa si mchezo,” nilimwambia, akacheka sana.

Usiku mzima nilikuwa nikichati na Scaila, alitokea kunipenda sana, nilimvutia na muda mwingi aliniambia ni kwa namna gani alikuwa akinipenda na kunihitaji.
Siku iliyofuata sikutaka kuchelewa, kwa kuwa na mimi nilitaka nionekane najua kuchagua, nikawapigia simu washikaji zangu na kuwaambia kuhusu Scaila, jinsi nilivyokutana naye mpaka hatua ambayo niliifikia.

“Huyo demu yupo vipi mpaka umedata hivyo?” aliniuliza mshikaji wangu, Boniface Ngumije ambaye nilikuwa ninafanya naye biashara.
“Huyo siyo demu! Ni msichana fulani hivi mzuri, wife material...” nilimwambia Ngumije kwa mbwembwe.

“Acha masihara! Yaani unataka kuoa?”
“Ndiyo! Yaani hapa nikichelewa, nitakuta kaolewa na mwingine,” nilijibu.
“Na Shasta?”
“Dah! Kumbe sikukwambia! Shasta anaolewa! Wazazi wake walinibania kisa dini!” nilijibu.

“Pole sana! Ila wewe na Shasta mliendana sana, ngoja nimuone na huyo mpya naye yupo vipi,” alisema Ngumije.
Sikuishia kwake, niliendelea kuwapigia simu washikaji zangu wengine na kuwaambia mengi kuhusu Scaila, alivyokuwa mrembo na nilivyokubalika kwa haraka sana nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 22

Naweza kusema nilichanganyikiwa, na kama sikuchanganyikiwa basi nilikuwa nafanya mambo haraka haraka kwa sababu nilikuwa kwenye stress za kukataliwa kumuoa Shasta.

Ilikuwa vigumu sana kwa mwanaume kuingia kichwa-kichwa kwa msichana ambaye humjui, umeonana naye siku moja halafu ukaanza kupanga mipango ya kumuoa pasipo kumjua kwa undani zaidi.

Mbali na hayo yote, pia hata marafiki zake walitakiwa kunitia hofu sana na nihisi kuwa msichana huyo alitakiwa kuwa chini ya uangalizi mkubwa sana lakini hayo yote sikutaka kujali kabisa.

Kwa Scaila, hapakuwa na mwanamke mwingine wa kuuchukua moyo wangu, nilimuingiza, nikamuweka kwenye chumba maalumu huku nikisubiri huyu Shasta aondoke kabisa moyoni mwangu na msichana huyo kuwa mtawala mpya.
“Baby! Lini nije kwako?” aliniuliza kwenye simu.

“Oh! Unataka kuja nyumbani? Njoo hata kesho!” nilimwambia kwenye simu huku nikiachia tabasamu pana kana kwamba alikuwa akiniona.

“Basi kesho jioni nitakuwa mgeni wako,” aliniambia.
“Wala usijali baby! Kwanza naomba unitumie picha zako,” nilimwambia.

“Unataka ngapi?”
“Hata mia moja!”
“Jamani! Zote hizo!”
“Yeah! Ninataka nikuone kwenye mapozi mbalimbali!” nilimjibu.
“Basi nakutumia nilizokuwanazo mpenzi!”
“Sawa.”

Nilikuwa na lengo kubwa la kumwambia anitumie picha, nilitaka nimfanyie sapraizi moja kubwa sana. Nilichohitaji ni kusafisha picha zake tatu, niziwekee fremu na kisha nizibandike ukutani.

Hicho ndicho nilichokitaka. Aliponitumia, kesho nikachagua picha tatu na kwenda kuzisafisha kisha kuziweka kwenye fremu na mbili kuzibandika sebuleni na moja kuibandika chumbani.

Nilihitaji kumuonyeshea Scaila kwamba nilimpenda sana, moyoni mwangu hapakuwa na msichana yeyote zaidi yake tu.

Grace alipoziona picha zile, yeye mwenye alichanganyikiwa, kwa jinsi Scaila alivyokuwa mrembo, alihisi kama picha ile ilikuwa na mtu fulani kutoka huko Brazil.
“Kaka! Huyu ndiyo huyo Saila mwenyewe?” aliuliza kwa mshangao.

“Siyo Saila...Scaila..!” nilimwambia.
“Ndiye huyu?”
“Ndiyo! Hebu cheki mtoto huyo!”
“Jamani ni mzuriiiiiii...”
 
Asante shunie.jamaa ana haraka ya kupenda. Utafikiri msukuma kaona mwanamke mweupe
 
SEHEMU YA 23.

“Kama ameshushwa vile. Sasa huyu ninakwenda kumuoa na kumuingiza humu ndani. Huu uzuri utauona kila siku ukiamka. Halafu hebu fikiria mtoto atakayetoka, simpatii picha, nadhani kama ni kidume wenye watoto wa kike watafuga mbwa wakali,” nilimwambia Grace.

“Na hivi ulivyo mweusi na yeye mweupe, itakuwa si mchezo huyo mtoto...” aliniambia.

“Yaani wewe acha tu!” nilimwambia.
Sikutaka kumwambia Scaila kitu chochote kile, nilihitaji ashtuke sana kuona picha zake zikiwa ukutani nyumbani kwangu. Siku hiyo jioni nikamfuata nyumbani kwao, nikakutana na mama yake na kumwambia kwamba nilimfuata mtu wangu nilihitaji kuondoka naye.

“Haina shida baba yangu...” aliniambia, hapohapo nikamuachia kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuondoka na binti yake.
Ndani ya gari tulikuwa na furaha tele, nilikuwa nikimwangalia Scaila, alikuwa msichana mrembo mno na muda wote nilihisi uzuri wake ulikuwa ukiongezeka maradufu.

Hatukuchukua dakika nyingi tukafika nyumbani, nikaliingiza gari ndani ya geti na kuteremka, nikamfungulia mlango na kuelekea ndani.

Kwa jinsi nyumba ilivyokuwa nzuri, alichanganyikiwa, alikuwa na furaha na hakuamini kama nilikuwa nikiishi kwenye nyumba nzuri kama hiyo.

Nikamshika mkono na kuanza kuelekea naye ndani, tulipoingia, hakuamini macho yake, picha zake mbili kubwa zilikuwa ukutani, nilizibandika, akapigwa na mshtuko kiasi cha kuufumba mdomo wake kwa viganja vyake.

Nilibaki nimesimama, nilimwangalia huku nikitabasamu, akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye ukuta ule na kuziangalia picha zile kwa umakini mkubwa sana, alihisi kama kile alichokuwa akikiangalia hakikuwa kwenye maisha halisi.

“Just for me?” (kwa ajili yangu?) aliniuliza huku akiniangalia.
“Yap! I did it for you!” (ndiyo! Nilifanya kwa ajili yako) nilimjibu.

Akanisogelea na kunikumbatia huku kwa mbali machozi yakimlengalenga. Grace aliyekuwa jikoni alihisi kama anapitwa, harakaharaka akaja mpaka sebuleni na kuanza kumwangalia Scaila.

“Mh! Ni mzuri kama picha zake,” alisema Grace kabla ya salamu, Scaila akaanza kumwangalia.
 
SEHEMU YA 24

“Scaila! Huyu ni Grace! Msichana anayenisaidia kazi humu ndani. Grace...sina haja ya kukutambulisha huyu ni nani! Nadhani ulimjua kabla ya yeye kukujua,” nilimwambia.

“Karibu sana wifi!” alimkaribisha Grace huku akitabasamu.
“Ahsante! Nimekwishakaribia wifi yangu!”

Baada ya yote, chakula kikaletwa, wote watatu tukakusanyika mezani na kuanza kula, tulikuwa tukizungumza mambo mengi, utani wa hapa na pale na mambo mengine mengi.

Wakati hayo yakiendelea, simu ya Scaila ikaanza kuita, akaichukua, akaangalia kioo, akapuuzia, akabonyeza kitufe cha kuzima, simu kama ikapigwa giza lakini ilikuwa ikiendelea kuita japokuwa haikutoa mlio.

“Janeth huyo! Nikiwa nakula huwa sitaki kuongea na simu...” alisema huku akitoa tabasamu kwa mbali.
“Na si vizuri kuongea na simu wakati wa kula!” nilimwambia.

“Kabisa.”
Tuliendelea kula kama kawaida, baada ya dakika moja, simu ile ikaanza kuita tena, ilikuwa mezani, macho yangu yalikuwa shapu sana, niliangalia kioo, jina nililoliona nakumbuka lilikuwa Alfred ama Albert, lakini akafanya kama alivyofanya.

“Huyu Janeth sijui ana nini...mpaka anaanza kunikera,” alisema, baada ya hapo, akaamua kuizima kabisa.
Niwe muwazi kwamba hapo ndipo nilipoanza kuwa na hofu na Scaila.

Nilikuwa na uhakika kabisa kwamba yule mtu aliyekuwa amepiga simu aliitwa Alfred ama Albert lakini kuambiwa kuwa alikuwa ni Janeth, haikuniingia akilini hata kidogo.

Sikutaka kuonyesha hofu yoyote ile, nilikuwa nikitabasamu muda wote kana kwamba sikuhisi jambo baya lolote lile. Tulikula na tulipomaliza, tukaenda chumbani.

Tulipofika, alipoiona picha yake moja humo, hakuamini, alisimama na kuanza kuiangalia, alifurahi kupita kawaida, akanifuata na kunikumbatia tena.
“Nashukuru kwa kunipenda na kunijali,” aliniambia huku akiniangalia.

“Usijali mpenzi! Nitakupenda siku zote za maisha yangu!” nilimwambia, akaanza kukiangalia kitanda, halafu akayarudisha macho usoni mwangu, akatoa tabasamu, nilijua anamaanisha nini! Nikamsukumia kitandani.

“Kiss me like you will never kiss me again, Nyemo...” (Nibusu kama hutokuja kunibusu tena, Nyemo...) aliniambia na kunivutia kwake. Ni ndani ya sekunde ishirini tu, kila mmoja akabaki mtupu kama alivyozaliwa.
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom