Simulizi: Scaila Michael

SEHEMU YA 17

Nilibaki kimya kwa sekunde kadhaa, nilitamani kumwambia akatae kuolewa lakini ilishindikana kabisa. Nilimwangalia, Shasta alikuwa mrembo mno, niliamini hakustahili kuolewa na mwanaume mwingine zaidi yangu.

Alijua ni kwa jinsi gani niliumia, maumivu yangu yalionekana hata machoni mwangu tu. Sikutakiwa kumzuia, hilo lilikuwa jambo jema kwa ajili ya maisha yake hivyo nikamwambia nilikubaliana naye, aolewe tu.

“Umeniruhusu kwa moyo wote?” aliniuliza huku akiniangalia.
“Kabisa!”
“Ila usijali! Utakapokuwa ukinihitaji, niambie, nitamtoroka hata mume wangu kwa ajili yako,” aliniambia Shasta.

Nilishtuka kusikia hivyo, nikagundua kwamba kweli ndoa zilikuwa ngumu sana. Unapompata mtu wa kumuoa, ukamuoa jua kulikuwa na mtu ambaye ulimpokonya tonge mdomoni na kama mtu huyo alikuwa akihitaji tonge lake, kulila lilikuwa rahisi sana.

Nilimwangalia Shasta, kile alichokisema kilikuwa kama alamu kwangu, siku zote niliamini mla vya mwenzake na vyake lazima viliwe tu, hivyo kama kweli Shasta angeolewa na kulala naye hata siku moja ilikuwa ni lazima jamaa mmoja siku moja aje kulala na mke wangu.

“Nilale na Shasta, halafu baadaye jamaa mwingine aje kulala na Scaila! Haiwezekani,” nilijisemea huku nikimwangalia msichana huyo.

“Au hutotaka nije kwako?” aliniuliza.
“Hapana! Shasta! Unaolewa, naomba utulie kwenye ndoa yako,” nilijikaza kisabuni na kumwambia maneno hayo.
Aliniangalia, akaachia tabasamu, aliamini kabisa nisingeweza kumzuia kama siku moja angeniambia anakuja kunisalimia nyumbani.

“Basi sawa!”
Baada ya hapo tukaondoka, nilimsindikiza mpaka Kigogo na kuelekea nyumbani kwao. Nilibaki nikimwangalia kwa uchungu mno, sikuamini kama lile tunda langu kulikuwa na jamaa alilichuma na alikuwa tayari kulila maishani mwake mwote.

Sikutakiwa kulifikiria zaidi hilo kwa sababu kulikuwa na mtu ambaye nilitakiwa kuishi naye, mbali na huyo Shasta, Mungu aliniandalia mwanamke mwingine mzuri kabisa.

“Scaila!” nilijisemea.
Sikutaka kupoteza muda, nilimkumbuka sana msichana huyo, hapo Kigogo nikaunganisha na barabara iliyokuwa ikielekea Mburahati na Manzese na kuelekea huko Tabata.
 
SEHEMU YA 18.

Njiani nilikuwa na mawazo tele, nilikuwa nikimfikiria Scaila kwa mara nyingine tena. Nilitamani nionane naye, nizungumze na hatimaye mambo mengine yaendelee.

Kutoka hapo Kigogo mpaka Tabata hapakuwa mbali sana, ila kabla ya kufika kwao nikapitia kwenye genge moja na kununua matunda kadhaa, nikawekewa kwenye mfuko na kuanza kuelekea huko.
Nilichikua dakika kadhaa, nikafika nje ya nyumba yao kubwa na kuteremka garini kisha kugonga hodi kwenye geti lao, mlango ukafunguliwa na dada wa kazi.

“Karibu sana shemeji,” alinikaribisha.
Nilishtuka kusikia naitwa jina hilo, ila moyoni mwangu nilijisikia faraja kubwa kwa sababu tayari ilionekana kama nimekubalika ndani ya nyumba hiyo.

Dada wa kazi akanipokea mzigo wa matunda na kuelekea ndani pamoja naye. Nilikuwa na presha kubwa sana, nilitamani kuonana na Scaila kwani nilimkumbuka kupita kawaida.

Mlangoni macho yangu yakatua kwenye viatu vingi vya kike, kwa jinsi nilivyoviona, nikagundua kulikuwa na wageni ndani, hivyo nikapiga moyo konde na kuingia.

Nilipovuka mlango, macho yangu yakatua kwa wasichana kama watano, wote wakageuka kwa pamoja na kuniangalia. Kwa kweli ni kama Scaila aliamua kufanya uamuzi sahihi kabisa.

Yeye alikuwa mrembo sana, na nilipokuwa nikiwaangalia hao marafiki zake, ilikuwa ni balaa, yaani ni kama waliamua kuchaguana wazuri wote na kuwa marafiki.

“Karibu sana,” alisema Scaila, akasimama na kunisogelea, aliponifikia, akanikumbatia.
Nikahisi mwili wangu kama umelowanishwa maji, roho yangu ikawa nyeupe kama imeoshwa kwa sabuni.

Kumbatia lake lile likanifanya nisahau shida zangu zote, matatizo yaliyokuwa yakinikabili na likanifanya kuhisi kama nilikuwa paradiso nikimsifu Mungu na malaika kadhaa.

“Unanukia vizuri...” nilimwambia kwa sauti ya chini kabisa.
“Nashukuru sana! Hata wewe unanukia vizuri mpenzi...” aliniambia.

Eti aliniita jina la mpenzi! Alinichanganya sana. Jina hilo kilikuwa kitu nilichohitaji sana kusikia kutoka kwake. Nilikuwa na mipango naye, nilitamani sana kumuoa na kuishi naye, hivyo lile jina likanichanganya kupita kawaida.
 
SEHEMU YA 19.

Tukaachiana na kuanza kuwasalimia marafiki zake. Sikutaka kuleta macho ya tamaa. Wanaume huwa tunakuwa na matatizo, tunapokutana na marafiki wa wapenzi wetu akili zetu huwa zinaruka, yaani ni kama tunachanganyikiwa na mwisho wa siku unatamani uwe na hao wote.

“Mungu nisaidie! Huu mtihani mgumu sana,” nilijisemea kimoyomoyo huku nikiendelea kuwasalimia kwa kuwashika mikono yao laini iliyoniachia harufu mbalimbali za manukato yao.
“Jamani huyu ndiye aliyenisaidia,” alisema Scaila huku akiwaangalia wenzake.

“Jamani kumbe ni kaka mzuri hivi,” alisema msichana mmoja, alikuwa mweupe, ana mwanya na nywele zake alizinyoa kwa staili ya panki, alivalia skin tight nyeusi, japokuwa alikuwa amekaa, lakini kwa jinsi bastola zilivyoonekana, niligundua alikuwa na mzigo wa haja.
“We Janeti! Koma,” alisema Scaila huku akijifanya kukasirika, hapohapo akaanza kucheka kwa kicheko cha taratibu.

“Oh! Anaitwa Janeth! Mungu endelea kunipigania kijana wako, napata tabu sana, yaani nateseka,” niliendelea kujisemea moyoni mwangu, hakukuwa na kipindi kilichokuwa kigumu kama hicho.

Tuliongea mambo mengi mahali hapo, Scaila hakuisha kunisifia, alizungumza maneno yote mazuri kuhusu mimi kiasi kwamba marafiki zake walihisi walikutana na malaika kwa jinsi nilivyoonekana kuwa mwema.

Baada ya nusu saa, marafiki zake wakaaga, wakasimama na kuanza kuondoka. Hapo ndipo nilipomfaidi huyo Janeth. Alikuwa si mchezo, yaani kila nilipokuwa nikimwangalia kwa kuibia, nilijikuta nikimsifu Mungu kwa uumbaji wake maridhawa.

“Mungu nisaidie! Mungu nisaidie! Bila wewe mimi siwezi!” niliendelea kujisemea.
Nilikuwa nikikutana na ugumu mkubwa sana mbele yangu, kulikuwa na mapambano mazito ambayo nilitakiwa kuyashinda kwa nguvu zote.

Huyo Janeth na wale wengine walionekana kudhamiria kabisa kuniingiza kwenye matatizo na Scaila kwani hata walivyokuwa wakiondoka, walikuwa wakiondoka kimitego sana.

Kwa kawaida mpaka muda huo ilikuwa ni lazima ugundue kuwa siku zote rafiki wa mwizi lazima awe mwizi lakini kwangu sikuhisi hilo kabla.
 
SEHEMU YA 20

Yaani nilivyokuwa nikiwaangalia marafiki wa Scaila niligundua walikuwa ‘malaya’ tu lakini kwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda msichana huyo, nilimuona kama malaika vile, yaani eti malaika alikuwa kwenye kundi la mashetani.

Baada ya kuwasindikiza, akarudi na nikaanza kuongea naye mambo mengi sana. Alionekana kuwa mtu aliyechangamka sana, alinisifia kwa jinsi nilivyokuwa na mambo mengine mengi.
“Kwanza naomba namba yako,” nilimwambia.

“Tena afadhali! Jana nilitaka tuongee lakini ilishindikana!” aliniambia.
Tukabadilishana namba na mambo mengine kuendelea. Sikufichi, kipindi hicho nilijisikia furaha isiyo kifani, kuwa karibu na Scaila ilionekana kuwa bahati moja kubwa mno.

Pale kochini alipokuwa, nikamsogelea, nikamwangalia usoni na kuanza kutoa tabasamu pana ambalo lilikuwa ni kama matayarisho ya kitu fulani.

“Unataka kufanya nini? Hapana! Hapana Nye...” aliniambia huku akitoa tabasamu lakini hata kabla hajamaliza, alichokuwa akitaka kunikataza tayari nikaanza kukifanya, tukaanza kubadilishana mate kwa sekunde kadhaa, halafu tukaanza kuangaliana.

“Oh! It my fault, I’m sorry...” (Oh! Ni kosa langu, samahani...) nilimwambia huku tukiangaliana.

“Kwa nini umenifanyia hivi?” aliniuliza.
“Ndiyo maana nimesema samahani! Nilizidiwa!” nilijitetea, nikaona haitoshi, kulikuwa na kiumbe kingine nilikuwa sijakisingizia kesi, haraka sana nikakisingizia.

“Shetani alinipitia...”
Scaila akatabasamu, hapohapo haraka sana akanisogelea na kuanza tena. Niliona mtoto alidhamiria hivyo kumshika zaidi kwa dakika moja na kuachiana.

Naweza kusema huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mapenzi yetu. Nikatokea kumpenda Scaila kuliko mwanamke yeyote yule. Niliona kama malaika fulani ambaye Mungu aliamua kunishushia, kumbe sikujua kama mwanamke huyu alikuwa na roho mbaya, ya kikatilia hata zaidi ya shetani.

Nilihisi kama nimeokota embe chini ya muarobaini kumbe niliopata shubiri chini ya mkomamanga.

|
|
|

Hii hadithi itakuwa inatoka Jumatatu na Alhamisi.
 
Mmh huyu jamaa anaonekana mlafii
Sehemu ya 09.
|
|

“Samahani mama! Mwenye simu amepata ajali!” nilimwambia bila hata salamu.
“Uwiiiiii...unasemaje?” aliniuliza huku akionekana kupaniki.

“Ameumia kidogo! Nilimsaidia! Yupo Mwanyamala anapatiwa matibabu, hakuumia sana mama usijali,” nilimwambia mama yake, hata kabla hajaniambia kitu kingine, simu ikaishiwa chaji hapohapo, ikazima.

Nilichanganyikiwa ila sikuwa na jinsi, nilichokifanya ni kuondoka na kurudi hospitalini, ilikuwa ni lazima nifanye hivyo kwa sababu ni utu kumsaidia mtu na hata kumjulia hali kutokana na kile kilichokuwa kimetokea lakini pia ilikuwa ni lazima nimpelekee simu yake.

Nilipofika, niliulizia na kuambiwa mahali alipokuwa na hivyo kwenda kule. Aliponiona tu, kwa mbali akaanza kutoa tabasamu, nilishindwa kugundua kama huyo msichana ndiye aliyepata ajali kwani alionekana kuwa mzuri kupita kawaida.

Kama nitaambiwa nimzungumzie sifa zake, zilikuwa nyingi sana, alikuwa mweupe, kama Mpemba fulani hivi, mwembamba kidogo, miguu ya kawaida, alikuwa na vishimo viwili mashavuni ambavyo vilionekana kila alipokuwa akitabsamu, alikuwa na nywele ndefu, yaani kwa jinsi alivyokuwa ilikuwa ni kama nilikutana na jini katika daraja la Salenda.

Nikabaki nikiushangaa uzuri wake. Msichana huyo aliitwa Scaila John ambaye ninataka nianze kukupa stori yake hii ndefu na ya kusisimua mno ambayo itaweza kukufundisha mambo mengi katika maisha yako.

|
|
Je, nini kitaendelea?
 
haki hapa nyemo amenichekesha sana
SEHEMU YA 19.

Tukaachiana na kuanza kuwasalimia marafiki zake. Sikutaka kuleta macho ya tamaa. Wanaume huwa tunakuwa na matatizo, tunapokutana na marafiki wa wapenzi wetu akili zetu huwa zinaruka, yaani ni kama tunachanganyikiwa na mwisho wa siku unatamani uwe na hao wote.

“Mungu nisaidie! Huu mtihani mgumu sana,” nilijisemea kimoyomoyo huku nikiendelea kuwasalimia kwa kuwashika mikono yao laini iliyoniachia harufu mbalimbali za manukato yao.
“Jamani huyu ndiye aliyenisaidia,” alisema Scaila huku akiwaangalia wenzake.

“Jamani kumbe ni kaka mzuri hivi,” alisema msichana mmoja, alikuwa mweupe, ana mwanya na nywele zake alizinyoa kwa staili ya panki, alivalia skin tight nyeusi, japokuwa alikuwa amekaa, lakini kwa jinsi bastola zilivyoonekana, niligundua alikuwa na mzigo wa haja.
“We Janeti! Koma,” alisema Scaila huku akijifanya kukasirika, hapohapo akaanza kucheka kwa kicheko cha taratibu.

“Oh! Anaitwa Janeth! Mungu endelea kunipigania kijana wako, napata tabu sana, yaani nateseka,” niliendelea kujisemea moyoni mwangu, hakukuwa na kipindi kilichokuwa kigumu kama hicho.

Tuliongea mambo mengi mahali hapo, Scaila hakuisha kunisifia, alizungumza maneno yote mazuri kuhusu mimi kiasi kwamba marafiki zake walihisi walikutana na malaika kwa jinsi nilivyoonekana kuwa mwema.

Baada ya nusu saa, marafiki zake wakaaga, wakasimama na kuanza kuondoka. Hapo ndipo nilipomfaidi huyo Janeth. Alikuwa si mchezo, yaani kila nilipokuwa nikimwangalia kwa kuibia, nilijikuta nikimsifu Mungu kwa uumbaji wake maridhawa.

“Mungu nisaidie! Mungu nisaidie! Bila wewe mimi siwezi!” niliendelea kujisemea.
Nilikuwa nikikutana na ugumu mkubwa sana mbele yangu, kulikuwa na mapambano mazito ambayo nilitakiwa kuyashinda kwa nguvu zote.

Huyo Janeth na wale wengine walionekana kudhamiria kabisa kuniingiza kwenye matatizo na Scaila kwani hata walivyokuwa wakiondoka, walikuwa wakiondoka kimitego sana.

Kwa kawaida mpaka muda huo ilikuwa ni lazima ugundue kuwa siku zote rafiki wa mwizi lazima awe mwizi lakini kwangu sikuhisi hilo kabla.
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom