Simulizi: Penzi ama kaburi?

Lemme subscribe, nitakuja isoma ikifika episodes za mbali huko...

Thanks...
Hii story inatolewa mara moja kwa week au mara mbili kukiwa na arosto za apa na pale naomba tuvumiliane jamani...
 
Sehemu ya 21

Rahim alikuwa mpweke chuoni, alikosa furaha kabisa kwa sababu kwa hapo chuo alipokuwa akisoma, hapakuwa na mwanaume yeyote yule ambaye angemwambia anampenda na hata kulala naye.

Mwili wake ulikuwa na hamu kubwa, hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia mwanaume yeyote kuwa alitamani kulala naye usiku kucha.

Kichwa chake kilikuwa na mambo mengi, kila siku usiku alipokuwa akilala, alikuwa mtu wa kufikiria mambo lukuki, kwenye chumba alichokuwa akikaa, kulikuwa na wanaume watatu, Hamisi, Alfonce na Maliki.

Kati ya watu hao wote, Hamisi ndiye alikuwa mtu wake wa karibu, rafiki waliyeshibana lakini hakuweza kugundua kama alikuwa akiendekeza mapenzi ya jinsia moja.

Kila siku kijana huyo alipokuwa akivua fulana yake na kubaki wazi, Rahim alichanganyikiwa, akili ilimruka, alipagawa kupita kawaida.
Alitamani kumwambia jinsi alivyomtamani lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa aliogopa.

Wakati yeye akifikiria hayo yote, Hamisi naye alikuwa na mambo yake kichwani mwake. Alimfikiria rafiki yake huyo. Kilichomuumiza ni kwamba hakuwahi kumuona na mwanamke yeyote yule.
Kwa kipindi chote hicho alichoishi naye kilimfanya kujiuliza maswali mengi.

Alitamani kumwambia tatizo lilikuwa nini, kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakimtaka lakini hakutaka kuwachukua, hakutaka kuwa nao kabisa.
“Kwani kuna nini Rahim?” aliamua kuuliza Hamisi huku akimwangalia rafiki yake huyo kwa macho ya mshangao.

“Ninamtumikia Allah!” alijibu.
“Allah?”
“Ndiyo!”
“Ndiye anakufanya usiwe na mwanamke yeyote?”
“Ndiyo! Ni dhambi kubwa sana!”
Hamisi akabaki akimwangalia Rahim, hakujua mwanaume huyo alimaanisha alichokuwa akikisema ama la.

Kile alichokizungumza Rahim kiliwezekana kabisa lakini kwa umri aliokuwanao, tena kwa jinsi alivyokuwa akipendwa na wanawake kulimfanya kuhisi kabisa alikuwa akikosea kufanya hivyo.

Hakutaka kuzungumza naye sana, alichokifanya ni kuondoka na kwenda kuonana na msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Hawa.

Alihitaji kumtumia msichana huyo kwa lengo la kwenda kumtega Rahim. Alihitaji kufahamu kama alikuwa na tatizo ama kulikuwa na sababu nyingine iliyomfanya kutokutamani kuwa na mwanamke yeyote yule.
 
Sehemu ya 22

“Hawa!” aliita Hamisi.
“Niambie!”
“Poa! Naomba kuzungumza nawe kidogo,” alisema Hamisi huku akimvuta Hawa pembeni, msichana huyo akakubali na hivyo kusogea pembeni.

Kwa kumwangalia tu, Hawa alikuwa msichana mrembo, aliyevutia, nywele ndefu, suruali ya jinzi na macho yake alibandika kope, midomo iliyopakwa lip stick, alionekana kuvutia.
“Kuna nini?”
“Kuna kitu nahitaji unisaidie,” alisema Hamisi.

“Kitu gani?”
“Unamfahamu yule rafiki yangu, Rahim?”
“Yule Mzanzibar?”
“Yeah!”
“Kafanyaje?”
“Ninataka umtege, uende naye chumbani, yaani umtege kwa staili hiyo!” alisema Hamisi, Hawa akashtuka.

“Nimtege?”
“Ndiyo!”
“Halafu!”
“Nitakulipa pesa! Kama laki moja hivi kama ukifanikiwa kulala naye,” alisema Hamisi, alijiahidi hata kulipia pesa lakini alihitaji kujua mengi kuhusu rafiki yake huyo.

“Mzanzibar?”
“Ndiyo!”
“Hivi wewe hujui michezo ya Wazanzibar?” aliuliza.
“Ipi?”

“Hahaha! Haloooo...”
“Mbona unacheka! Si uniambie!”
“Hivi unahisi siuthamini?”
“Huuthamini nini?”

“Nauthamini sana! Siwezi kudate na Mzanzibar! Naanzaje kudate naye! Eti natoka niende kwa Mzanzibar! Haiwezekani! Nauthamini sana! Wana michezo ya kifirauni sana wale,” alisema Hawa huku akionekana kugoma kabisa kumfuata mwanaume huyo.

Hamisi hakutaka kushindwa, alijitahidi kumbembeleza kijana huyo kukubaliana naye lakini ilishindikana kabisa. Hakutaka kuachana naye kwani aliamini mwisho wa siku angekubali na hivyo kufanya kama alivyokuwa akitaka kufanya.

Siku ziliendelea kukatika huku Hamisi akiendelea kumwambia Hawa kwamba lingekuwa jambo jema kama tu angekubaliana naye kumfuata rafiki yake huyo na kufanya naye mapenzi kama alivyokuwa amezungumza naye.
“Ila pesa ipo?” aliuliza Hawa kabla ya yote.

“Ipo!”
“Ila zungumza naye, yale mambo yao sitaki mie!” alisema Hawa, aliipenda pesa lakini wakati mwingine alikuwa na wasiwasi tele.

“Hahah! Hawa bhana! Sawa nitamwambia!” alisema Hamisi na hivyo kuondoka huku akimuacha msichana huyo afanye kile alichomwambia.

Hawa hakuwa na presha, alijiamini, alikuwa na umbo matata sana, kwa nyuma alijaa na kifua chake kilikuwa kidogo kabisa, sura yake iliita na mapaja yake manene yaliwachanganya wanaume wengi waliokuwa wakimwangalia.
 
Sehemu ya 23

Kila alipojiangalia, hakuona kama kungekuwa na mwanaume yeyote angetoka mikononi mwake endapo tu angeamua kwa roho moja kulala naye. Kwake, huyo Rahim hakuwa tatizo lolote ila kilichomuogopesha ni michezo ambayo alisikia ikichezwa sana kisiwani humo.

Aliogopa ila alipiga moyo konde na hivyo kuanza harakati zake za kumnasa mwanaume huyo. Siku hiyo ya kwanza kabisa alimuona akiwa darasani, amejikalia zake akiangalia muvi kwenye laptop yake.

Hawa akaingia na kumfuata Rahim pale alipokuwa. Alitembea kwa mwendo wa maringo, alivalia sketi fupi iliyobana kiasi kwamba kila alipokuwa akitembea darasani humo nyakati za jioni, watu waliokuwa wakipiga stori walinyamaza na kumwangalia yeye.

“Jamani sasa ni muda wa matangazo...” alisikika kijana mmoja, alikuwa mzungumzaji mzuri kwa wenzake, ila baada ya Hawa kupita, akatangaza muda wa matangazo, yaani watulie na kumwangalia msichana huyo.
“Koo...koo..koo..koo...” sauti ya viatu vyake vilisikika.

Alikwenda mpaka mahali alipokaa Rahim, hakuongea, kwanza akamwangalia mwanaume huyo, alihitaji kujua ni kwa namna gani angeanza kumtega kwa kumuonyesha alikuwa akimuhitaji sana.
Wakati akiwa amekaa, Rahim alitulia tu, ni kama hakumuona mtu aliyeingia hapo na kukaa karibu naye. Japokuwa kwa mwanaume yeyote rijali angeshtuka lakini kwake hata kumuangalia hakumwangalia.

Hawa akaona kama angeshindwa, alichokifanya ni kujiweka vizuri kitini na kukunja nne, mapaja yake yakaanza kuonekana vilivyo. Mlengwa wa kutegwa alikuwa Rahim lakini cha ajabu wanaume waliokuwa pembeni ndiyo walianza kutegeka lakini kwa mhusika hakusisimka hata kidogo, yaani ni kama mwanaume alikuwa akimwangalia mwanaume mwenzake.

“Rahim....” aliita Hawa baada ya kuona amepotezewa, Rahim akawa bize na muvi, alichokifanya ni kuvipitisha vidole vyake katika mkono wa Rahim, hapohapo akashtuka, akatoa earphones na kumwangalia msichana huyo.

“Mambo...” alisalimia kwa sauti ya kubembeleza kabisa.
“Poa!” alisema Rahim na kuendelea kuangalia muvi.
“Unaangalia nini?”
“Muvi...”
 
Sehemu ya 24

“Naomba tuangalie wote!” alisema Hawa, alijitahidi sana kuweka mapozi ya kike kumtega jamaa huyo lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze.

“Lete flashi nikuwekee...” alisema.
Hawa akaishiwa pozi, alimwangalia vizuri Rahim machoni, hakuamini alichokuwa amemwambia, yaani yeye alitamani kuangalia naye muvi lakini kitu cha ajabu kabisa mwanaume huyo alimwambia ampe flashi ili akaangalia kwa wakati wake.

Hakutaka kukubali, ilikuwa ni lazima aonyeshe umwamba na kuhakikisha anafanikiwa katika suala hilo. Aliendelea kuzungumza naye kwa dakika kadhaa, hapo ndipo alipobaini mambo machache kuhusu mwanaume huyu.

Wakati mwingine alikuwa akijisahau, alileta mapozi ya kike, alizungumza kikikekike lakini hata kwa jinsi vidole vyake alivyokuwa akiviweka wakati alipokuwa akibonyeza keyboard ya kompyuta ilimshtua Hawa.

“Mh!” alijikuta akiguna.
“Nini tena?” aliuliza Rahim huku akimwangalia msichana huyo.
Hawa hakutaka kubaki mahali hapo, haraka sana akasimama na kuanza kuondoka. Ni kama Rahim alijua kilichokuwa kikiendelea, hapohapo akasimama na kuanza kumfuata msichana huyo.

Katika mambo yote yaliyokuwa yakiendelea, hakutaka kabisa kuona mtu yeyote akifahamu kama alikuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ilikuwa ni lazima ailinde heshima yake kwa vyovyote vile.

Alijisahau mbele ya Hawa na kujikuta akifanya mambo kama mwanamke, aliamini kama angemuacha msichana huyo aondoke, kitu ambacho kingefuata mahali hapo ni kutangazwa kwamba alikuwa na chembechembe za umama, hivyo ilikuwa ni lazima alizuie hilo.

“Unakwenda wapi?” aliuliza Rahim huku akiwa amemuwahi msichana huyo na kumshika mkono.

“Nakwenda kupumzika!” alijibu Hawa huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Kwa hiyo unataka kuniacha hivihivi?” aliuliza.
“Hivihivi kivipi?”
 
Sehemu ya 25

“Umekuja pale, umenionyesha mapaja, halafu kweli rijali mimi unaniacha hivi? Haiwezekani!” alisema Rahim kama mwanaume kweli.
“Kwa hiyo sasa unataka kuniambiaje?”

“Na mimi nataka!”
“Unataka nini?”
“Kilichomfanya Samson anyolewe nywele.”
Hawa akabaki kimya. Alishangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Aliamini hapo kabla kwamba jamaa alikuwa na umama lakini kitu cha ajabu kabisa, alimuwahi na kumwambia anataka.

Kusudi lilikuwa ni kumpa, ndivyo alivyopanga lakini pia akaanza kujiuliza kama kweli alikuwa na uwezo au alitaka kujishembendua tu. Wakaendelea kuzungumza na kukubaliana kwamba siku inayofuata usiku waende kutafuta chumba sehemu na kumpa kama alivyotaka, ila alitakiwa kumlipa.

“Pesa si tatizo!”
“Basi haina shida.”
Kazi ikabaki kwa Rahim! Hakujiamini, alijua kabisa hakuwa na uwezo wa kulala na mwanamke lakini kwa sababu alihitajika sana kuonyesha ubavu wake ilikuwa ni lazima ajilazimishe.

Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Hapo akakumbuka kwamba kulikuwa na dawa za kuongeza nguvu za kiume zilizokuwa zikijulikana kama mkongo ama mputululu, ilikuwa ni lazima azitumie hizo kwa siku moja kumalizana na msichana huyo.

Hakujua angezipata wapi hivyo kitu alichokifanya ni kuwasiliana na dada yake, Shadya kwa lengo la kuzungumza naye kuhusu dawa hizo, angezipata vipi kwani alikuwa akienda kuaibika.

“Yaani siamini!” alisema Shadya alipoambiwa kuhusu dawa hizo.
“Naomba unisaidie! Nitakuja kuaibika! Naomba unisaidie kuzungumza na watu kuhusu dawa hizo,” alisema Rahim.

“Yaani umenichanganya sana!”
“Shadya! Usiponisaidia katika hili! Chuo kizima kitajua kwamba mimi nafanya michezo hiyo. Naomba unisaidie kutafuta,” alisema Rahim huku akionekana kuomba sana.

“Sasa wewe ni mwanaume, waambie wenzako naamini watakusaidia!” alisema Shadya.
“Siwezi!”
“Kwa nini?”
“Naona aibu!”
 
Sehemu ya 27

“Rahim! Wewe ni mwanaume!”
“Najua! Ila naona aibu! Naomba unisaidie!”

Shadya akashusha pumzi ndefu, hakujua ni kitu gani hasa alitakiwa kufanya. Ni kweli alihitaji sana kumsaidia kaka yake lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kupata dawa hizo na kumpatia kwani hakuwa na marafiki wengi.

“Gibson....” hilo lilikuwa jina la kwanza lililokuja kichwani mwake, ilikuwa ni lazima amtafute, amwambie amsaidie kwenye suala hilo. “Nitakusaidia!

Tuonane baadaye!”
Wakaagana na Shadya kuondoka. Kichwa chake kilivurugika, ilikuwa ni lazima amsaidie kaka yake huyo hivyo haraka sana akawasiliana na Gibson na kuomba kuonana naye.

“Nipo nyumbani! Kuna nini kwani?”
“Basi nakuja! Nina shida. Ila naomba usiniulize maswali! Nitahitaji unisaidie, nakuomba,” alisema Shadya.

“Sawa! Ila si uniambie kiasi gani kabisa nikatoe benki!”
“Sihitaji pesa.”
“Unahitaji nini?”
“Msaada wako ila si wa kifedha!”
“Sawa. Njoo home!”
“Kuna nani?”

“Leo nipo peke yangu!”
“Sawa nakuja!” alisema na kukata simu, akaanza kuelekea nyumbani kwa kijana huyo huku kichwa chake kikiwa kimechanganyikiwa kupita kawaida.
 
Sehemu ya 27

Shadya alitakiwa kupambana kwa ajili ya kaka yake, hakuwa tayari kuona akihadhirika na wakati alikuwa na uwezo wa kumsaidia.

Ilikuwa ni lazima azungumze na Gibson na kumwambia kwamba alikuwa akihitaji dawa hizo za kuongeza nguvu za kiume, iwe isiwe ilikuwa ni lazima amsaidie kwa kuwa aliamini alimpenda.

Akachukua bodaboda na kuelekea Sinza alipokuwa akiishi, alipofika huko, akakaribishwa na kuelekea ndani.

Alijisikia aibu sana kumwambia kuhusu jambo hilo lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima amwambie kwa kuwa bila kufanya hivyo ingeonekana kuwa hatari kwa maisha ya kaka yake chuoni.

Wakaelekea ndani, kwa jinsi Shadya alivyoonekana, hakuonekana kuwa sawa kabisa, alikuwa na mawazo mengi, kaka yake alimpa tabu na katika kipindi kama hicho ilikuwa ni lazima ampambanie mpaka ahakikishe anafanikiwa.

“Unaonekana kuwa na mambo mengi sana,” alisema Gibson, kwa kawaida kila alipokuwa na msichana huyo ilikuwa ni lazima awe na sura iliyokuwa na tabasamu pana.

“Yeah! Naomba nipumzike kwanza!”
“Chumbani ama sebuleni?”
“Sebuleni!” alisema na kutulia kwenye kochi.

Alimwangalia Gibson, kwa jinsi alivyoonekana, aliona kabisa kufanikiwa kwa kile alichokuwa amejiandaa kumwambia. Alipumzika kwa dakika chache ndipo akaamua kuingizia suala hilo.

“Kuna kitu nahitaji unisaidie,” alisema baada ya mazungumzo machache ya kujuliana hali.
“Kitu gani?” aliuliza Gibson.

“Daah!” alisema Shadya.
Hakutaka kumwambia moja kwa moja, kichwa chake kilitafuta lafudhi nzuri ya kulifikisha suala hilo, yaani atumie rejesta ambayo ingemfanya mwanaume huyo kuelewa kila kitu.

“Shadya!” aliita Gibson baada ya kuona ukimya wa sekunde zaidi ya ishirini.
“Abee!”
“Unahitaji nikusaidie nini?” aliuliza.
“Nina tatizo!”

“Lipi?”
Akakaa kimya tena.
Gibson alimshangaa, hakuelewa zaidi alichokuwa akikihitaji msichana huyo, alikuwa na maswali mengi lakini hakupata majibu ya maswali hayo yote.

Msichana huyo alimpigia simu na kumwambia alihitaji kumuona kwa sababu kulikuwa na jambo alilotaka kuzungumza naye, alimuita, alifika lakini hakuwa akizungumza kitu chochote kile.

Je nini kitaendelea.....
 
Sehemu ya 28

Kwa sababu alikuwa mwanaume wa Dar, akajiongeza. Kuna mambo ambayo msichana alipokuwa akiyahitaji, hakuwa na uwezo wa kuyawakilisha kwa maneno bali alitakiwa kubustiwa ili kidogo apate urahisi wa kuufikisha ujumbe wa kile alichokuwa akihitaji.

“Au anahitaji mambo yetu?” alijiuliza.
“Ngoja nimtesti!” aliisemea.
Hakutaka kulaza damu, aliamini alichokuwa akikihitaji msichana huyo ni kufanya mapenzi tu, ndivyo akili yake ilivyomtuma na kwa sababu alihitaji kumsaidia Shadya, akaamua kumuanza yeye.

Akamsogelea na kumwangalia usoni, Shadya ni kama alishtuka kwani huyu Gibson aliyeonekana muda huo alikuwa tofauti na yule ambaye alimkaribisha dakika chache zilizopita, huyu wa sasa alikuwa na mabadiliko mengi usoni mwake.

Akaupeleka mkono pajani mwake na kuanza kumsoma kama aliridhia ama angeleta purukushani.

“Gibson!” aliita kwa sauti nyororo, naye akaamini ili asaidiwe, ilikuwa ni lazima aanze kujilegeza kwa mwanaume huyo.
“Nakusikia!”

“Ninahitaji dawa!” alisema.
“Unaumwa?” aliuliza.

“Hapana!”
“Sasa unataka dawa ya nini?”
“Yaani nashindwa kulielezea hili!”
“Jitahidi tu! Huzioni siku zako?”
“Bora ingekuwa hivyo!”
“Kumbe kuna nini?”
“Unajua zile dawa zinazomfanya mwanaume anakuwa na nguvu?” aliuliza Shadya.

“Zipi? Energy ama?”
“Hapana! Si kinywaji!”
“Kumbe zipi?”
“Zile za kutoka Congo!”

Gibson alipoambiwa hivyo akashtuka, hakuamini alichokisikia, alimwangalia Shadya, alishangaa, kwa msichana kama huyo, mstaarabu asingekuwa na uwezo wa kumwambia maneno kama hayo.
 
Sehemu ya 29

Naye Shadya aliuona mshtuko huo, alichokifanya ni kuupeleka mkono wake kwa Gibson na kumwangalia machoni.
“Naomba unisaidie Gibson!” alisema Shadya.

“Nikusaidie dawa hizo?”
“Ndiyo!”
“Za nini?”
“Nina shida nazo!”
“Shida gani?”
“Naomba unisaidie!”
“Shadya! Siwezi! Kukupa dawa hizo ni jambo lisilowezekana! Yaani nikupe ukafanye mapenzi na mwanaume mwingine?” aliuliza.

“Gibson.....”
“Halafu mimi niwe kama mshika pembe, maziwa wakamue wengine!” alisema kwa unyonge.

“Si kama unavyofikiria!”
“Unataka nifikirie nini? Kwamba zinakwenda kutupwa?”
“Hapana!”
“Kumbe!”
“Kuna mtu nakwenda kumpa, azitumie!”
“Kwako wewe? Jamaa hapandi mlima ama?”

“Si kwangu!”
“Kumbe kwa nani?”
“Mbona maswali mengi Gibson! Love...naomba unisaidie! Nakuomba sana mpenzi,” alisema Shadya.

Alishindwa kuvumilia. Huyu Gibson tayari alionekana kuwa na shaka naye hivyo alichokifanya ni kujiebisha na kuanza kubadilishana mate.

Aliamini kwa kufanya hivyo angeweza kumshawishi. Gibson hakutaka kumuacha, alikuwa na hamu na msichana huyo, haikuishia hapo, ni kama dakika mbili hivi, hakujua ni kitu gani kilitokea, walijikuta wakiwa chumbani wakiwa watupu, yaani ni kama walipotea sebuleni kichawi na kutokea humo.

Kilichofuata ni sauti za mahaba ambazo zilichukua dakika arobaini na tano wakaanza kuangaliana. Shadya aliumia moyoni, alifanya mapenzi bila kutarajia kwa sababu ya kumsaidia kaka yake.

Alikuwa kwenye tatizo na ilikuwa ni lazima aonyeshe kwamba alikuwa naye bega kwa bega. Wakaanza kuangaliana.
 
Sehemu ya 30

“Kwa hiyo?” aliuliza Shadya huku akijiweka vizuri kitandani.
Gibson akachukua simu yake na kupiga mahali. Akaanza kuzungumza na mtu aliyejulikana kwa jina la Kaimu na kumwambia kuhusu hizo dawa ambazo kwa lugha ya mitaani ilijulikana kama Vumbi la Congo.

Ndani ya dakika ishirini, pikipiki ikafika mahali hapo, jamaa akateremka na kumpa Gibson dawa hiyo iliyofungwa kwenye kikaratasi.
“Mzee baba una shoo ya kibabe nini?” aliuliza Kaimu.

“Hapana!”
“Au kuna mtoto wa kishua amekuja unataka kumdatisha umle mapene yake?” aliuliza.

“Hapana! Nitakushtua baadaye!” alisema Gibson, jamaa akarudi kwenye pikipiki na kuondoka zake.

Gibson akaingia ndani na kumwambia Shadya kwamba mzigo alikuwanao mkononi mwake.

“Ila nikigundua kwamba umekwenda kuutumia wewe!” alisema Gibson.
“Utafanyaje?”

“Nitakuchukia!”
“Siwezi kufanya hivyo! Yaani inamaanisha kwako sijaridhika?”
“Sawa! Nenda!”

“Ila Gibson....”
“Niambie!”
“Naomba iwe siri!”
“Haina shida! Ila si mechi itarudiwa?”

“Ili utumie hii kitu?”
“Hapana! Hivihivi kama leo!”
“Tutaongea kwenye simu. Nakushukuru sana, hujui ni kwa jinsi gani umeokoa maisha ya mwingine. Nashukuru sana,” alisema Shadya, akasindikizwa mpaka nje, akaita bodaboda, akapanda na kuondoka mahali hapo.

Akawa amemsaliti Ngwali kwa ajili ya kaka yake, ila huo ulionekana kuwa si mwisho, alimuahidi asingeingilika na wanaume wa Dar, mtu wa kwanza akawa amefanikiwa kumvua, hakujua kama kulikuwa na wengine wangefuata baada ya huyo.
.
.
.
Je, nini kitaendelea?
 
Dah vumbi la Congo linasaidia wengi. Kuna jamaa alinihadithia na yeye huwa anatumia sio la mchezo mchezo
Asante shunie
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom