SIMULIZI: Pendo lisilo kifani (muonjo wakati taabu itakapokuwa imekwisha)

SEHEMU YA 9

Katikati ya bustani karibu na
mti wa uzima ulisimama mti wa
ujuzi wa memam na mabaya Mungu
aliuumba mti huu mahususi kwa ajili
yao ili kutoa ushahidi wa utii, imani na
upendo wao kwake. Bwana aliwaamuru
wazazi wetu wa kwanza kutokula matunda
ya mti huu wasije wakafa. Aliwaambia kuwa
waweza kula matunda ya miti yote ya
bustani isipokuwa mmoja tu na
ikiwa watakula matuda ya mti huu
watakufa

Wakati Mungu alipowaweka Adamu
na Hawa katika ile bustani nzuri
walikuwa na kila kitu ambacho
wangeweza kukihitaji

Kwa ajili ya furaha yao. Lakini katika
mipango yake ya hekima kamili, Mungu
alichagua kuujaribu uaminifu wao
kabla hajawafanya kuwa salama
milele. Shetani iliruhusiwa kuwajaribu.

Iwapo wangeshinda jaribu lile
wangepata kibali cha Mungu na
malaika wa mbinguni milele zote.
Shetani alishangazwa na hali yake
mpya. Furaha yake ilikuwa imeondoka.
Aliwaangalia malaika ambao, kama
yeye walikuwa na furaha mno hapo
mwanzo

Lakini ambao walifukuzwa kutoka
mbinguni pamoja naye. Miongoni
mwao mlikuwa na migogoro
kutokuelewana na shutuma kali.
Kabla ya uasi wao mambo haya
hayakufahamika kabisa kule mbinguni
Shetani sasa aliona matokeo ya
kutisha ya uasi wake.

Iwapo sasa angepata tena nafasi ya kuweza
kuwa kama alivyokuwa wakati alipokuwa
msafi, mkweli na mwaminifu kwa
furaha angeweza kusalimisha madai
yake ya
Mtepetallah Mwifwa @ the bold
 
SEHEMU YA 10

mamlaka lakini alikuwa
amepotea! Uasi wake usio
na msingi na wa kijeuri ulimweka
mbali mno na ukombozi.

Lakini alikuwa na zaidi.
Alikuwa amewaongoza wengine
katika uasi na hali hiyo hiyo ya
kupotea pamoja na yeye-yaani malaika,
ambao kamwe walikuwa hawajafikiria
kuhoji mapenzi ya mbingu au
kukataa utii wa sheria ya
Mungu hadi pale

Alipoiweka fikra hiyo katika akili zao
sasa walikuwa katika machafuko
kutokana na matumaini yaliyovunjika.
Baadala ya wema kuongezeka
walikuwa wakipitia matokeo ya
kuhuzunisha ya kutotii na
kudharau sheria ya Mungu

Shetani atafakari Njia Yake-
Shetani alitetemeka alipoangalia
kazi yake akiwa peke yake aliwaza
kuhusu siku zilizopita, wakati uliopo,
na mipango yake siku za usoni.
Katika uasi wake hakuwa na sababu
ya kwenda njia aliyoendea na
kwa namna isiyoweza kuponyeka

Alkuwa amejiangamiza japo si
yeye peke yake bali pia safu
kubwa ya malaika ambao bado
wangeweza kuwa wanaendelea
kupata furaha mbinguni kama
wangedumu kuwa wakweli.
Sheria ya Mungu inaweza
kuhukumu lakini haina
uwezo wa kusamehe

Badiliko hili kuu la cheo
alikuongeza upendo wake kwa
Mungu au kwa sheria yake ya
hekima na haki. Shetani
aliposhawishika kikamilifu kuwa
hakukuwako na uwezekano wa
yeye kurejeshwa katika kukubaliwa
na Mungu, basi alidhihirisha
kusudi lake ovu

Kwa chuki iliyozidi na hasira kali
mno. Mungu alifahamu kuwa
uasi wa kudhamiria
Mtepetallah Mwifwa
 
SEHEMU YA 11

jinsi ile usingezimika wenyewe.
Shetani angebuni njia ya
kuwachokoza malaika wa
mbinguni na kuonyesha dharau
kwa mamlaka yake. Maadamu
alikuwa hana ruhusa ya kuingia
kwenye malango ya mbinguni
angeweza kuvizia pale kwenye
malango, ili kuwadhihaki na
kujaribu kuhojiana nao
walipokuwa wanaingia
ndani na kutoka nje.

Angejitahidi kuharibu
furaha ya Adamu na Hawa
angefanya kila juhudi kuwachochea
kuasi, huku akifahamu kuwa
jambo hili lingesababisha
huzuni mbinguni

Njama dhidi ya jamii ya Wanadamu-
Shetani aliwaambiwa wafuasi
wake kuhusu mipango yake ya
kutaka kuwavuta mbali kutoka
kwa Mungu Adamu na Hawa
walikuwa waadilifu kama kwa
njia Fulani angeweza kuwadanganya
kutokumtii Mungu angeweka
njia fulani ya kuwasamehe
ndipo yeye pamoja na malaika wote

Walioanguka wangetumia fursa
hiyo kudai kuwa na sehemu
katika rehema ya Mungu pamoja
na Adamu na Eva

Iwapo ili lingeshindikana
wangeweza kujiunga pamoja
na Adamu na Hawa kwa sababu
kama wangelivunja sheria ya Mungu
wao pia wangekabiliwa na
gadhabu ya Mungu, kama
shetani na malaika zake ambao
kwa sababu hiyo wangejiunga na
Adamu na Hawa kuimili Edeni na

kuichukua kama maskani yao na
iwapo wangepata nafasi ya
kuufikia mti wa uzima uliokuwa
katikati ya bustani nguvu yao
waliwaza ingeweza kuwa sawa
na ile ya malaika watakatifu na
hivyo hata Mungu asingeweza
kuwafukuza.
Mtepetallah Mwifwa
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 12

Adamu na Hawa waonywa-
Mungu aliwakusanya malaika ili
wapate kuchukua hatua ya kuzuia
uovu uliokuwa uantishia kutokea.
Iliamuliwa katika baraza la
mbinguni kuwa malaika watembelee
Edeni na kumwonya Adamu
kuwa alikabiliwa na hatari
kutoka kwa adui yule

Malaika waliwapa Adamu
na Hawa kisa cha kuhuzunisha
cha uasi na anguko la Shetani.
Ndipo kwa uwazi waliwajulisha
kuwa mti wa ujuzi uliwekwa
bustanini kama njia kwao

Ya kuahidi utii na upendo wao
kwa Mungu. Malaika watakatifu
wangeweza tu kudumisha hali
yao ya juu nay a furaha kwa
sharti la utii, na wao Adamu na
Hawa pia ilikuwa ni kama hiyo
wangeweza kutii sheria ya
Mungu na kuwa na furaha
isiyoelezeka

Au kutokutii na kupoteza hadhi
yao ya juu na kuingia kwenye
kukatishwa tama kusiko na
matumaini

Malaika waliwaambia Adamu
na Hawa kwamba malaika
aliyetukuka zaidi ya wote
aliye mfuata Kristo kwa cheo
alikataa kutii sheria ambayo
Mungu aliiweka ili kuwaongoza
viumbe wa mbinguni ambavyo
vilisababisha muasi huyo

Kufukuzwa kutoka mbinguni
uasi huu walisema ulisababisha
vita mbinguni ambavyo
vilisababisha muasi huyo
kufukuzwa kutoka mbinguni na
kila malaika aliyeungana na
kiongozi huyu katika kuhoji mamlaka
ya Yehova mkuu alifukuzwa kutoka
mbinguni. Malaika huyu aliyenguka
sasa alikuwa ni adui wa kila kitu
ambacho Mungu pamoja na
Mwana wake walikuwa wakikipenda
sana
 
SEHEMU YA 13

Waliwaambia kuwa Shetani
alikusudia kuwadhuru na kwamba
ilikuwa muhimu kwao kuwa
macho kwa sababu wangeweza
kukutana na adui huyu aliyeanguka.
Asingeweza kuwadhuru hata
hivyo wakati ambapo wangeweza
kulitii agizo la Mungu kwa sababu
kama ingelazimu kila malaika kutoka
mbinguni angekuja kuwapa msaada
kuliko kuruhusu apate
kuwadhuru kwa namna yoyote ile.

Lakini iwapo wasingelitii agaizo
la Mungu ndipo shetani angekuwa
na uwezo wa kuwaudhi,
kuwafadhaisha na kuwataabisha
tangu wakati ule na kuendelea

Kama wangezidi kuwa imara dhidi
ya madokezo ya awal ya uovu
kutika kwa shetani wangekuwa
salama kama malaika wa
mbinguni walivyo.

Lakini iwapo wangeshindwa
na majaribu Mungu yuleyule
ambaye hakuwaachilia malaika
walioutukuka asingewaachia
wao lazima wapate adhabu ya
dhambi yao, kwa kuwa sheria ya
Mungu ilikuwa ni takatifu kama
yeye mwenyewe alivyo na alihitaji
utii wa dhati kutoka kwa wote
walioko mbinguni na duniani

Malaika walimunya Hawa
asije akajitenga kutoka kwa mume
wake katika kazi zake ndani ya
bustani, kwa sababu angeweza
kukutana na adui huyu
aliyeanguka kama wangetengana

Wangekuwa katika hatari
kubwa zaidi kuliko pale walipokuwa
pamoja Adamu na Hawa
waliwahakikishia malaika wale
kuwa kamwe wasingeacha kutii
amri ya wazi ya Mungu. Hata
hivyo ilikuwa ni furaha yao
kubwa mno kutenda mapenzi yake
 
SEHEMU YA 14

Jaribu na Anguko- Shetani
alichukua umbile la nyoka na
kuingia katika bustani alijiweka
juu ya mti wa ujuzi na kuanza kula
matunda yake taratibu bila kutambua
mwanzoni Hawa alijitenga kutoka kwa

mume wake alipokuwa akihudumia
bustani alipotambua kile kilichotokea
alihisi kuwa kungeweza kutokea
hatari lakini tena alifikiri kuwa alikuwa
salama hata kama

hakudumu kuwa karibu pembeni
mwa mume wake alikuwa na
hekima ya kutambua pale ambapo
hatari ingekuja na

nguvu za kuweza kukbaliana nayo
malaika walikwisha kumuonya
kutotenda hili Hawa lijikuta akikaza
macho yake na kuangalia tunda la
mti uliokatazwa akiwa na
mchanganyiko wa shauku ya
uadadisi na kuvutiwa.

Aliona lilikuwa la kupendeza mno
na kuwaza moyoni mwake kwa
nini Mungu aliwazuia vikali kiasi
kile wasile sasa ilikuwa fursa ya
Shetani alisema naye kana
kwamba alikuwa na uwezo wa
kusoma mawazo yake.

Ati! Hiyi ndivyo alivyosema Mungu
msile matunda ya mti yote ya
bustani? Kwa maneno laini naya
kupendeza na sauti ya kimuziki
aliongea na Hawa aliyestaajabishwa
alishangazwa sana kusikia nyoka akiogea

Kwa vile alifahamu kuwa Mungu
hakuwa amempa nyoka uwezo wa
kunena udadisi wa Hawa uliamshwa.
Baadala ya kuondoka pale kwa haraka
alitega masikio kumsikiliza nyoka akiongea
 
SEHEMU YA 15

Haikufahamika moyoni mwake
kuwa huyu ndiye angekuwa yule
adui aliyeanguka akitumia nyoka
kama chombo ni shetani aliyekuwa
akiongea wala si nyoka Hawa alivutiwa
na akadanganyika na kupumbazwa
iwapo angekutana na mtu mwenye staha

Mwenye umbile kama la malaika
na anayefanana na wao angeweza
kujihadhari sauti hii ya ajab ingetosha
kumkimbiza kwa mume wake na kumwuliza
kwa nini mtu mwingine aongee naye
kwa uhuru jinsi ile bali aliingia
katika mapambano na nyoka

Alilijibu swali lake “Matunda ya
bustani twaweza kula lakini matunda
ya mti ulio katikati ya bustani Mungu
amesema msiyale wala msiyaguse msije
mkafa” shetani alijibu “Hakika
hamtakufa kwa maana Mungu anajua
kuwa siku mtayokula matunda ya mti
huo mtafumbuliwa macho

Nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua
mema na mabaya shetani alitaka
wadhani kwa kula matunda ya mti
huo uliokatazwa wangepokea maarifa
mapya ya kigeni na yaliyo bora zaidi ya
yale ambayo tayari

walikuwa nayo. Hii imekuwa ni kazi
yake maalumu yenye mafanikio makubwa
tangu alipanguka kuwaongoza watu
kudadisi siri za Mwenyezi na wala
kutoridhika na kile

ambacho Mungu amedhihirisha na
wala wasiwe waangalifu kutii kile
alichokiagiza anataka awafanye
wasitii amri za Mungu na kisha
kuwafanya waamini kuwa wanaingia
katika uwanja wa ajabu wa maarifa
hii ni dhana tupu na ni udanganyifu
wa kutisha.

Wanashindwa kufahamu kile ambacho
Mungu amefunua na wanadharau
amri zake za wazi na kuitamani
hekima isiyo mtii
 
SEHEMU YA 16

Mungu wakitafuta kufahamu
kile ambacho amechagua
kuwaficha wenye miili ya
kufa wanafurahishwa na
mawazo yao ya kuendelea
kuvutiwa na falsafa zao
wenyewe zilizo tupu lakini
wanapapasa-papasa katika giza la usiku
wa manane kuhusiana na maarifa
ya kweli. Hayakuwa mapenzi ya
Mungu kwamba wanandoa hawa
wasiokuwa na dhambi wapate
ufahamu wowote wa mabaya

Kwa hiari aliwapa mema tele lakini
alizuia mabaya Hawa alidhani
kuwa maneno ya nyoka yalikuwa
ya hekima na alikubali dai lake thabiti “Hakika
hamtakufa kwa maana Mungu anajua
ya kwamba siku mtakapokula matunda
ya mti huo mtafumbuliwa macho
nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua
mema na mabaya” huku kulikuwa ni
kumfanya Mungu kuwa mwongo

Shetani kwa ushupavu alidokeza
kuwa Mungu alikuwa amewadanganya
kuwazuia wasipate maarifa ambayo
yangwafanya wao kuwa sawa na yeye
(Mungu) mwenyewe Mungu alisema

Mkila mtakufa hakika Nyoka alisema
mkila hakika hamtakufa mjaribu
alimhakikishia
Hawa kuwa mara tu baada ya kula
tunda lile angepokea ujuzi bora
ambao ungemfanya kuwa sawa
na Mungu alielekeza fikra za
Hawa kwake yeye mwenyewe

Alisema sababu iliyomfanya
apate uwezo wa kusema ni kwa
kuwa amekula katika mti uliokatazwa
kwao alidokeza kwamba Mungu
asingeweza kutekeleza neno lake
ilikuwa ni tishio tu ili kuwaogopesha
na kuwazuia kupata kilicho bora.

Pia aliwaambia kuwa wasingeweza
kufa. Je hawakuwa wamekula
katika mti wa uzima
 
SEHEMU YA 17

ambao ungedumisha
kutokufa? Aliwaambia kuwa
Mungu alikuwa anawadanganya
ili kuwazuia kufikia hali ya juu
zaidi ya maisha na furaha kubwa
zaidi mjaribu alichuma tunda na
kumpa hawa alilichukua mkononi
mwake sasa alisema mjaribu
mlikatazwa hata kuligusa msije mkafa.
Alimwambia kuwa asingepata hisia
yoyote ya uovu na kifo kwa kulila
tofauti na huko kuligusa au kulibeba
tunda hilo

Hawa alitiwa ujasiri kwa sababu
hakuhisi mara moja ishara za
Mungu kutopendezwa alidhani
maneno yote ya mjaribu lazima
ni ya hekima na sahihi

Alikula na alifurahishwa na tunda
lile. Lilielekea kuwa tamu sana
kwake kwa ladha na alidhani alihisi
matokeo ya ajabu ya tunda lile

Hawa anakuwa mjaribu- Ndipo
alipochuma yeye mwenyewe
matunda na kuyala akiwaza kuwa
alikuwa akihisi uwezo utiao nguvu
wa maisha mapya naya hali ya juu
zaidi kutokana na matokeo ya
kufurahisha ya tunda lililokatazwa
alikuwa katika msisimko wa ajabu

Na usio wa kawaida alipokuwa
anakwenda kumtafuta mume wake
mikono yake ikiwa imejaa matunda
yaliyokatazwa alimwambia mambo
ya hekima ambayo nyoka aliyasema

Na alitaka mara moja kumchukua
kwenda kwenye mti wa ujuzi
alimwambia kuwa alikuwa amekula
baadhi ya matunda yake na baadala
ya kuhisi hali yoyote ya kifo alipata
uzoefu wa hisia ya kupendeza na ya

kufurahisha mara baada tu ya Hawa kutotii aligeuka kuwa chombo chenye nguvu
 
SEHEMU YA 18

ambacho kupitia kwake Shetani
angesababisha anguko la mume wake

Adamu alifahamu vyema kabisa
kuwa mwenzi wake hakulitii katazo
pekee ambalo Mungu aliwapa ili
kupima uaminifu na upendo wao.
Hawa alitoa wazo kuwa Nyoka
alisema kwamba hakika hawatakufa
na maneo yake lazima yatakuwa kweli,
kwa kuwa hakuhisi ishara yoyote
ya Mungu kuchukizwa bali hisia ya
kupendeza

Kama vile wavyojisikia malaika
alidhani Adamu alijuta kuwa Hawa
alitoka kando yake lakini sasa tendo
limekwisha kutendeka ni lazima
atenganishwe kutoka kwa mtu aliyempenda
sana na kumfurahia kama mwenzi wake
angewezaje kuruhusu hili litokee?
Upendo wake kwa Hawa ulikuwa
na nguvu na kwa

Kukata tama kabisa aliamua kushiriki
msiba wake aliwaza kuwa Hawa alikuwa
ni sehemu yake mwenyewe na kama
itabidi afe, basi atakufa pamoja naye

Kwa vile hataweza kuvumilia wazo
la kutengana naye alikosa imani
kwa Muumba wake mwenye rehema
na aliye mwema hakufikiria kuwa
Mungu aliyemfanya

kutoka katika mavumbi ya ardhi
kuwa kiumbe hai kilicho kizuri na
kumuumba Hawa kuwa mwenzi wake
angeweza kujaza nafasi yake hata
hivyo je maneno ya nyoka huyu mwerevu
hayawezi kuwa sahihi?

Hawa alikuwa amesimama mbele yake
mzuri na wa kupendeza dhahiri bila hatia
kama vile alvyokuwa kabla hajakosa kutii
alikuwa akidhihirisha upendo mkuu na
wa hali ya juu kwake akidai kwamba
haya
 
SEHEMU YA 19

yalitokana na kula tunda lile hakuona
dalili zozote za kifo ndani yake aliamua
kujaribu bahati zake alinyakua tunda na
haraka akalila na kama alivyokuwa Hawa
hakuisi matokeo yake mara moja

Uhuru wa mwanadamu wa kuchagua-
Mungu aliwaelekeza wazazi wetu wa
kwanza kuhusu mti wa ujuzi na walikuwa
na taarifa kamili kuhusu anguko la shetani
na hatari ya kusikiliza mapendekezo yake

Mungu hakuwanyima uwezo wa kula tunda
lililokatazwa aliwaacha kama mawakala huru
wa kuamini neno lake kutii amri
zake na kuishi au kumwimini mjaribu
kutokutii na kuangamia upendo
wa kuvutia na amani

na furaha kamili ya kuridhisha ilionekana
kuondolewa kutoka kwao na baadala
yake kukosekana kwa kitu Fulani
kulikuja juu yao ambako kamwe
walikuwa hawajapata kuhisi hapo
kabla ndipo mara ya kwanza waligeuza
fikra za macho yao kuelekea kwa vitu vya

nje hawakuwa wamevaa nguo bali
walikuwa wamefunikwa na nuru kama
malaika wa mbinguni walivyokuwa
nuru hii iliyowafunika kabisa sasa ilikuwa

imeondoka ili kusaidia hisia zao za uhitaji
na uchi waliokuwa wamehisi walitafuta
namna Fulani ya vazi kwa ajili ya miili yao
kwani ni vipi wangeweza kukutana na
macho ya Mungu na malaika wakiwa uchi?

Shetani alifurahishwa mno na mafankio
yake sasa alikuwa amemjaribu mwanamke
kutomwamini Mungu kuhoji hekima yake na
kujaribu kujipenyeza katika mipango
yake isiyo chunguzika

Na kupitia kwake pia alimwangusha
Adamu ambaye kwa sababu ya
upendo wake kwa

Hawa aliacha kutii amri ya Mungu
na hivyo kuanguka pamoja naye.
Bwana alimtembelea Adamu na
Hawa na kuwaambia matokeo ya
kutotii kwao waliposikia mjongeo wa
Mungu wa kifahari walijaribu kujificha
wasionwe na yeye waliyefurahi kukutana
naye pale walipokuwa na hali ya kutokuwa
na hatia na utakatifu “Bwana Mungu
akamwita Adamu

akamwambia” ukowapi? Akasema “
Nalisikia sauti yako bustanini nikaogopa
kwa kuwa mimi ni uchi nikajificha” ni nani

aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je!
Umekula wewe matunda ya mti
niliyokuagiza usiyale?

Bwana aliuliza swali hili si kwamba
alihitaji taarifa bali ni kwa sababu ya
kuwasadikisha wale wanandoa juu ya
hatia yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom