Simulizi: Ntagambi (1 _ 12)

0713417189

Senior Member
May 12, 2021
108
196
NTAGAMBI.......01
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 23 304.
Tanga.

SEHEMU YA KWANZA.

Upepo ukiwa unapuliza, vumbi lilitimka. Nyumba dhaifu zililalamika, kulia na kushoto miti ilipelekwa kwa lazima. Ilikuwa ni hali ya hewa katika kijiji Cha Omulenga nchini Bulilo chini ya uongozi wa mfalme Bunini.

Mfalme Bunini, alipingana na wasamalia wema, neno samahani lilikuwa ni adui mkubwa kwake. Roho zisizokuwa na hatia alizinyakulia uhai wake. Wazee, watoto wakaliangusha chozi mbele ya mfalme Bunini. Nchi ya Bulilo ilizungukwa na milima mikubwa na mirefu. Lakini uhaba wa maji ilikuwa ni changamoto. Wakinamama walidhurumiwa utu wao na kubakwa pindi, walipodamka usiku wa Kiza kinene, kwenda kujipatia maji angalau kidogo.

Kijiji cha Omulenga, ndipo yalikuwa makazi ya mfalme Bunini, hiyo haikutosha bado wananchi wake walipoteza maisha sababu ya mlipuko wa maradhi mbali mbali, vifo hivyo havikumstua wala kumnyima usingizi mfalme Bunini.

Unaweza ukapata vitu vingi, ambavyo huviitaji Sana. Na ukapata kidogo kile ambacho unatamani ukipate kwa wingi. Ndivyo ilivyokuwa kwa mfalme Bunini, alitamani sana kupata watoto wengi, ila akabahatika kupata mtoto mmoja tu wa kike, binti mfalme aliyeitwa Chidumu.

"Omulenga Kijiji changu, Bulilo nchi yangu, nitayaishi maisha haya mpaka lini!, ni heri ningelikufa mapema kuliko kuwa shuhuda wa mambo haya, nitampata vipi binti mfalme" alijisemea Ntangambi kwa sauti ya chini.

Ntagambi alikuwa kijana mrefu na mweusi kidogo, pua yake pana ka mgongo wa chura, iliupamba vyema uso wake. kwa waliobahatika kumuona walikuwa wakidiriki kusema ni jitu la miraba minne haswa. Misuli iliyotambaa katika mikono yake, ilionesha dhahiri ni mtu wa mazoezi. Umaarufu wake ulizidi kuenea kwa kasi Kama harufu ya manukato kutoka kisiwani pemba.

Ntagambi alikuwa ni masikini wa kutupwa. Kijumba chao hata mbuzi asingekubali kulala. Anaamua kufanya kila awezalo kumuoa binti mfalme. Hapa nguvu za Ntagambi hazikufua dafu, akajikuta ameingia katika vita mbaya na chungu ambayo, ilimtenganisha na tabasamu kwa usawa wa mbingu na ardhi.

Ntagambi alisimama, akaenda katika kaburi la Baba yake aliyefahamika kwa jina la Mzee Kibalangosha. Alikuwa ni mganga mkuu wa mfalme Bunini katika tiba za mitishamba. Lakini kichwa chake kilitenganishwa na kiwiliwili kwa kutumia jambia la mlinzi wa mfalme. Kosa lake alishindwa kumtibu mfalme pale alipougua. Ni mchezo mchafu ulichezwa na waganga wenzie wakachukua dawa zake na kuzibadili kumuwekea zisizo na uwezo.

Machozi njia mbili mbili Ntagambi aliyaachia yamdondoke, baada ya kuumizwa kwa mara ya pili na kumbukumbu hiyo.
"Pamoja na yote lazima nimuoe binti mfalme, ili tu niweze kuyafuta machozi ya wanakijiji wa Omulenga na nchi ya Bulilo kwa ujumla" alizungumza Ntagambi akiwa anang'oa nyasi juu ya kaburi la babake, na kupandisha udogo uliosogezwa kando na mvua.

"Mama, mwanao nishakuwa kijana mkubwa sasa, nakueleza ukiwa kama mtu muhimu katika maisha yangu. Nataka nifanye kila niwezalo mpaka nimuoe binti mfalme, liwake jua, inyeshe mvua. Maji nitayavulia nguo na kisha nitayaoga." alizungumza Ntagambi.
Mama yake alishtuka sana, akaangalia kulia na kushoto, kama kuna mtu anawasikiliza. Akachukua kachupa kake kadogo akatoa ugolo na kuuweka katika kinywa chake. Akamtazama mwanaye takribani sekunde ishirini kisha akazungumza,
"Mwanangu, usithubutu utauawa, wengi waliotaka kumuoa binti mfalme walipewa mitihani mizito sana, wakaangukia katika kifo chenye maumivu makali"

"Mbona sikuelewi mama!" Ntagambi alidakia.
"Utanielewa tu mwanangu, najua kupenda sana ni ugonjwa usiotibika. Ila wewe hujafikia uko bado. Ionee Imani afya yangu mwanangu, sina maisha, nasubiri tu wakati nikamilishe safari yangu hapa duniani. Ukitangulia wewe, nitateseka sana, uenda nikafia ndani na maiti yangu isipate mzishi. Tumebaki sisi na dunia yetu, ndugu zako wote waliuawa na jeshi la mfalme Bunini,"

Kufikia hapo si mama si mtoto, usikivu ulipotea wakaangua kilio kizito, ni kama walikumbushana upendo waliokuwa nao kabla ya kuingia kwa mtawala jeuri na mbabe anaepiga danadana nyoyo za watu.
"Nyamaza mama yangu, chozi la mnyonge aliendi bure," Ntagambi alimsihi mamake asiendelee kulimwaga chozi lake.
"Lakini umenielewa mwanangu?" aliuliza mamake Ntagambi.

"Nimekuelewa mama, lakini niruhusu nijitose mpaka nimuoe Chidumu binti mfalme,"
"Sawa mwanangu, mwenye Enzi akutangulie, maana umeingia katika pambano ambalo mshindi anajulikana tayari." alizidi kusisitiza mamake Ntagambi.

Ilikuwa ni siku rasmi ya kufanya usafi, nje na ndani ya makazi ya mfalme. Ilikuwa ni lazima na sio ombi, vijana wengi wa kike na kiume hasa wa Kijiji cha Omulenga walikuwa wakijitokeza kwa wingi miongoni mwao alikuwemo Ntagambi.
Kazi zilipangwa kwa makundi, wapo waliolisha mifugo, kujenga kuta kuimalisha ulinzi, wakati usafi ukiendelea majeshi ya mfalme yalikuwa yametapakaa kila Kona kuhakikisha mfalme Bunini anakuwa salama.

Binti mfalme hakuwa na tabia ya kujikweza, nae alishirikiana bega bega na vijana wenzie. Tabia hiyo ilimkera sana mfalme, akawatuma walinzi wamkamate na kumrudisha ndani.
"Wewe Chidumu kwanini hutaki kunielewa? ukipata matatizo uko nje! hizo kazi acha hao masikini wakutupwa wazifanye, wewe ni binti mfalme hupaswi kufanya kazi ngumu" alifoka mfalme Bunini.

"Hapana Baba, nami pia ni binadamu kama wao, acha nifanye kazi," binti mfalme alijibu.
Lakini jibu ilo kutoka kwa Chidumu, lilimghadhabisha sana mfalme, akafura kwa hasira. Akaamulu walinzi wa kike wamchukue na kwenda kumfungia chumbani kwake.

Ntagambi alipangiwa kitengo cha kubeba mawe mazito, na kwenda kuyapanga sehemu husika. Jasho jingi lilimchuruzika karibia kila kona ya mwili wake, kwapani, mgongoni lilimchuruzika kuelekea chini. Nguvu zake alizitumia haswa, alipoinama kubeba jiwe likawa zito kwake akalitupa chini, akasimama na kuangalia juu katika nyumba ya mfalme.

"Waooh! alikutana na tabasamu pana la binti mfalme, akiwa anachungulia dirishani. Wakaangaliana kwa sekunde kama mbili kisha binti mfalme akafanya ishara ya kumkonyeza Ntagambi kisha akafunga dirisha.
"Ni muujiza gani huu! lile tabasamu la malaika au binadamu, hapana aisee huyu binti mfalme ni malaika aliyevishwa ubinadamu," alinong'ona Ntagambi kwa sauti ya chini kabisa.

"Maajabu haya!," ilikuwa ni sauti ya Ntagambi. Lile jiwe lililomshinda hapo awali, awamu hii alilibeba na kukimbia nalo kwa kasi, hakuamini, alihisi Kama binti mfalme anamuona. Kweli mapenzi yana nguvu, hakuna mwanaume anaekili unyonge mbele ya yule mwanamke ampendaye.
************** ITAENDELEA *******************

NTAGAMBI.......02
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 23 304.
Tanga.

SEHEMU YA PILI.

ILIPOISHIA.....
"Maajabu haya!," ilikuwa ni sauti ya Ntagambi. Lile jiwe lililomshinda hapo awali, awamu hii alilibeba na kukimbia nalo kwa kasi, hakuamini, alihisi Kama binti mfalme anamuona. Kweli mapenzi yana nguvu, hakuna mwanaume anaekili unyonge mbele ya yule mwanamke ampendaye.

ENDELEA NAYO...
Kengele iligonga kuashiria muda wa kazi umekwisha. Vifaa vyote vikakusanywa, askari mkuu akatoa tangazo na kuwaruhusu watu warejee katika makazi yao, askari wakatapakaa kila kona na kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama.

"Nikusanyie waganga wangu wote uwalete hapa" ilikuwa ni amri kutoka kwa mfalme Bunini akimuagiza mlinzi wake. Baada ya dakika kama kumi kupita waganga wote walikuwa wamekusanyika.

"Mbona siwaelewi, mmenitengenezea dawa nyingi lakini bado sipati mtoto. Mnajua kabisa umri wangu umekwenda inabidi apatikane mtoto wa kiume aje arithi ufalme" alizungumza mfalme Bunini.

"Hapana bado tunaendelea kufanya utafiti, tuone ni mwanamke yupi utaweza kupata nae mtoto wa kiume," alijibu mganga wa kwanza.
"Mmh! sasa Kama ni hivyo, hawa wanawake wote zaidi ya ishirini aliojaribu hakuna mwenye bahati hiyo?" aliuliza mganga wa pili.
"Ngoja tupige ramli zetu kwa mara ya mwisho," alidakia mganga wa tatu.
Mfalme Bunini aliwapa siku saba waganga hao, kwamba kila mmoja aje na dawa au ufumbuzi wa yeye kupata mtoto wa kiume, haraka iwezekanavyo.

"Siku zinakwenda kasi, nitapambana na hisia zangu mpaka lini. Harakati za kuingia katika ulimwengu wa ndoa zimewadia, nikimaliza ilo sasa natazama namna ya kurejesha tabasamu la kijiji cha Omulenga na nchi ya Bulilo kwa ujumla," Ntagambi alizungumza uku akiwa anafanya mazoezi ya kuuweka mwili wake sawa.
Hatimaye zile ziku saba za waganga kuja na suluhu ziliwadia, kiongozi wa waganga wale alisimama mbele ya mfalme Bunini, kisha akaanza kuzungumza,

"Mtukufu mfalme wa nchi ya Bulilo, tumewaza na kuwazua, tumesoma vitabu vya mababu zetu, tukabaini dawa ambayo itaweza kukusaidia, ni mti uitwao Ochululungilo unapatikana katika nchi ya Wafwa. Mti huo umeelezewa vizuri sana mtukufu mfalme, lakini nchi hiyo ni ya ajabu sana, wengi waliojaribu kwenda uko, hawakurudi waliuawa njiani. Hakika ni nchi yenye binadamu wa hatari wanye miguu mitatu." alimalizia kuzungumza mganga.

Mfalme Bunini alijikohoza kidogo, akarekebisha vizuri lile vazi lake la kifalme. Kisha akazungumza, "Nasema hakuna kitu kitakachoshindikana hapa, nitawatangazia vijana nitawapa silaha imara kisha wataianza safari. Mpaka niipate hiyo dawa," alizidi kusisitiza mfalme Bunini.

Kengele ya dharura iligongwa, watu wakakusanyika kwa haraka, hofu iliwajaa wakahisi labda kuna watu wanaenda kupewa adhabu ya kifo. Nchi ya Bunini ilikuwa na watu wachache sana, Kijiji Cha Omulenga ndio palikuwa mjini, na wakazi wake pia hawakuwa wengi.
Askari mkuu alituliza watu, ila mioyo yao ni kama ilitaka kuchoropoka itengane na mwili. Ukatili wa mfalme Bunini uliwaogofya sana wananchi wake. Aliuwa ovyo bila kujali umri, aliamini kile akili yake ilichomtuma kufanya.

"Mtukufu mfalme wa ardhi ya Bulilo na Omulenga karibu uzungumze na watu wako" alizungumza askari mkuu. Mfalme alichukua glasi ya maji akabugia mafunda mawili, kisha akainua kichwa chake na kuwatazama wananchi.
"Bulilo oyeeeeeeeee..!!!"
"Oyeeeeeeeeee..!!!"
"Omulenga juuuuuuuu"
"Juuuuuuuuu...!!"
"Asante sana, ndugu wananchi wa Bulilo, na hasa katika kijiji chetu hiki cha Omulenga, nimesimama mbele yenu kama kiongozi wenu, sasa naomba vijana watakaopenda kujitolea, kwenda nchi ya mbali kidogo, inafahamika kama nchi ya Wafwa. Nitawapa silaha za kutosha mwende mkaniletee matawi na mizizi ya mti uitwao Ochululungilo. Mti huo unafanana hivyi" mfalme alionesha picha iliyomo katikati ya kitabu, kisha akaendelea kuzungumza,

"Atakayefanikiwa kufikisha dawa hiyo katika ardhi hii ya kijiji cha Omulenga, atamuoa binti mfalme."
"Alilililiiiiiiiiiiii..!!Awuwiiiiiiiiii...!!wayowayooo.."
Zilikuwa ni kelele za shangwe na furaha, kutoka kwa vijana wa kiume, baada ya kusikia kwamba wakifanikiwa watamuoa binti mfalme. Urembo wake uliwazuzua, ile sauti yake nyororo ka nyuzi za gita ilizidi kuwalevya pasi kutumia kilevi, liwalo na liwe. Kila kijana alijiapiza kwamba lazima afanikiwe kurudi na ile dawa katika ardhi ya Omulenga.

Walijitokeza vijana takribani mia mbili na hamsini, wakakabidhiwa upanga, wakapewa na farasi kwaajili ya kuianza safari. Waliagwa na umati mkubwa, kila mtu alisali dua yake. Lakini Ntagambi kabla ya kuondoka alikimbia mara moja mpaka nyumbani kwao kwenda kumjuza mamake. Kwani alikuwa anatembea kwa shida sana. Matukio makubwa ya hapo kijijini yeye alikuwa hashiriki.
"Mama kama nilivyokueleza, sasa naelekea katika hiyo nchi ya Wafwa, nitahakikisha narudi na hiyo dawa, ili niweze kumuoa binti mfalme. Kuna rafiki yangu nimemuachia maagizo, atakuwa anakuangalia kwa ukaribu sana, hasa kipindi hiki cha mvua. Na mashaka sana na haka kajumba ketu kasije momonyoka kama biskuti, maana hakawezi kuhimili vishindo," ilikuwa ni sauti ya Ntagambi akizungumza na Mamake.

"Ntagambi mwanangu, unaenda katika nchi ya hatari Sana, hakuna binadamu wa kawaida uko. Nitakupoteza mwanangu, kwa vile umeamua sawa, ila nitakukabidhi huu upanga sikuwahi kukuonesha. Alikuwa anautumia marehemu babu yako, ila babu yako uyo hakufa bali unauona ule mto, alitembea mpaka katikati kisha akazama na kupotelea mtoni. Mpaka leo katika huo mto, huwezi kuona mbwa, kuku, bata, njiwa na hata binadamu wakidiriki kuyatumia yale maji. Sawa mwanangu nakuombea sana, kwa mizimu ya ardhi ya Omulenga upate kurejea salama."

Ntagambi akaupokea upanga kutoka kwa mamake, ni upanga wa maajabu ulikuwa na matone matatu ya damu, katikati ya upanga huo. Ni ishara mbaya sana kwa adui yeyote ambaye atapitiwa na upanga huo hawezipona.

***************** ITAENDELEA *******************

NTAGAMBI.......03
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 23 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA TATU.

ILIPOISHIA.....
Ntagambi akaupokea upanga kutoka kwa mamake, ni upanga wa maajabu ulikuwa na matone matatu ya damu, katikati ya upanga huo. Ni ishara mbaya sana kwa adui yeyote ambaye atapitiwa na upanga huo hawezipona.
ENDELEA NAYO.....
Ntagambi alipofika nyumbani kwa mfalme, alikuta vijana wenzake wamekwisha ianza safari. Alipokabidhiwa upanga alikataa akajibu kwamba tayari anao, akachagua farasi mwenye rangi nyeusi.
Kabla ya kuondoka maswali kadha wa kadha yalikatiza kwa fujo katika kichwa chake, "Naelekea nchi ambayo ni ya hatari sana, sasa nikifa nitampata vipi binti mfalme?, sawa nitapambana mpaka tone la mwisho la damu. Nitarejea katika ardhi hii ya Omulenga nikiwa hai au mfu, potelea pwete. Nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja."
Ntagambi akachukua ile ramani, kisha farasi akaanza kutimua mbio. Binti mfalme kwa mbali alimuona Ntagambi akipotelea, akaachia tabasamu pana, akatamani Kama Ntagambi angeliona basi lingemuongezea nguvu katika safari yake hiyo ya hatari.
Binti mfalme moyo wake ulitamani kuhifadhiwa katika chemba Cha moyo wa Ntagambi. Ujasiri na nguvu za kijana huyo, zilifanya binti mfalme alegee na kuingoja kwa hamu siku atakayojilaza kifuani mwa Ntagambi. Lakini akifikiria ugumu uliopo wa yeye kukutana na Ntagambi japo aweze kumuelezea hisia zake. Aliishia kujifungia chumbani na kulia Kama mtoto mdogo.
"Baba kwanini lakini unaonea watu?, eeh!. Watu wanakufa sababu ya njaa, na ni jukumu lako kuhakikisha wanapata chakula. Kiukweli mimi najisikia vibaya Sana, nitatoroka hapa niende porini nikaliwe na wanyama. Moyo wangu unaumia, unamwaga damu za watu wasio na hatia," binti mfalme alizungumza.
"Wewe tulia, unazungumza upuuzi gani" alifoka mfalme.
"Kumbuka wewe ni mwanangu wa pekee, inabidi ufate mimi ninavyotaka" alisisitiza mfalme.
Chidumu ambaye ndiye binti mfalme, maneno ya Baba yake yalimchukiza sana. Akasimama kinyonge na kuelekea zake chumbuni. Mfalme hakupenda kuona binti yake akiipoteza furaha, alimuita akambembeleza na kumuahidi kwamba mambo yataenda vizuri.
Hatimaye Ntagambi alijikuta amevamia pori kubwa, lililofunikwa na ukimya wa ajabu. Milio ya ndege ilisikika kwa mbali, hapakuwepo na dalili yeyote ile ilioonesha kwamba kuna makazi ya watu maeneo yale. Ntagambi alipunguza mwendo. Alizidi kuduwaa, akaupiga moyo konde tu bila kujua ni hatima gani iliyokuwa inamsubiri. Alitetemeka mwili mzima kama mgonjwa wa homa, miguu ilikufa ganzi. Midomo ilikuwa inamcheza, akashuka juu ya farasi, akasimama na kuanza kutembea bila ya kujua anapoelekea.
Alipopiga hatua tano mbele, alistushwa na miili kumi ya wenzake waliomtangulia wakiwa wameuawa. Walijeruhiwa vibaya sana, utumbo wote ulimwagika nje. Mwili mzima ulimtetema, woga aliokuwa nao ukamfanya kujikojolea.
Alipoangalia vizuri akakuta rafiki yake nae kauawa, chozi lilimdondoka. Uchungu usioelezeka ulimshika, kwa kumuona rafiki yake ambaye sasa alikuwa ni mfu. Akawaza jinsi walivyopendana na kucheza pamoja akakumbuka walivyoleteana viazi vya kuchoma wakiwa shuleni. Alisikitika sana moyoni.
Ghafla upepo mkali ulianza kuvuma, miti ikatii amri kunesa kwenda kulia na kushoto. Vishindo vizito vilisikika mpaka miti ikawa inakatika yenyewe.
"Hiki nini tena!" alinong'ona kimoyo moyo Ntagambi.
Majani ya miti yaliyopo chini yalijikusanya kwa pamoja, vumbi kali likatimuka. Kwa mbali Ntagambi akaona mnyama mkubwa asiye wa kawaida. Alikuwa na miguu minne, pembe moja ndefu katikati ya kichwa, meno marefu yaliyotokeza kwa nje, alikuwa anaunguruma kwa jazba.
Kasi ya uyo mnyama ilimshangaza Ntagambi. "mama yangu, nimekwisha" ilikuwa ni kauli ya Ntagambi akiwa anakimbia kuelekea pale alipoiacha farasi, kugeuka nyuma anaona mnyama uyo kamfikia, akaongeza mwendo, akajikwaa katika mti na kudondoka chini.
Ntagambi alirukiwa mgongoni na kukwaruzwa vibaya sana. "Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..." alipaza sauti kwa uchungu, akauchomoa upanga wake, akarusha. Mnyama akakwepa. Ntagambi akachomwa na pembe kwenye paja akalia kilio cha kwikwi. Akachoma panga katikati ya mdomo wa mnyama uyo, panga likatoa moto mkali na kukimaliza kabisa kiumbe hicho cha kutisha.
Ntagambi alimeza funda la mate machungu. Akaishusha pumzi, akamfunga farasi wake vizuri, kisha yeye akasogea kichakani. Maumivu ya majeraha ongeza na njaa vilimzonga sana kwa wakati huo. Alijikaza na kusimama, akajikokota mpaka ulipo mti wa matunda aliyoyafahamu. Akayachuma yale yalioiva, alijitahidi kula kadiri ya uwezo wake mengine akayabeba na kuyaweka katika mifuko ya shati lake.
Akaelekea sehemu iliyokuwa na kivuli cha mti mkubwa akakaa hapo. Na kuendelea kula matunda. Ghafla bin vuuu alisikia kishindo cha watu wakiwa wanatembea upande wa pili. Woga usioelezeka ulimvaa mwili mzima. Akajisogeza kwenye sehemu ya ndani ya mti, palipokuwa na mimea midogo iliyojiotea pale, akatulia tuli, mithili ya maji ndani ya mtungi.
Aliona binadamu wa ajabu, Kama watano hivyi wakikatiza mbele yake, walikuwa na jicho moja kubwa katikati ya paji la uso, nywele ndefu zikigusa mpaka chini. Meno yao yalijipanga mdomoni kama ya simba. Katika mabega yao walikuwa wamening'iniza miili ya binadamu ikiwa imekatwa ovyo na kupasuliwa vichwa. Hakika walikuwa wamewaua. Mikono yao ilishika silaha za jadi, nyundo, panga na mashoka mazito ambayo binadamu wa kawaida hata kuyainua ni mtihani.
"Mmh! inaonekana hawa wanakula nyama za binadamu? Sio viumbe wa kawaida" alijisemea kimoyomoyo Ntagambi, akiwa ahamini kama viumbe hao wamepita mbele yake, bila kutambua kama pale kajificha mtu.
Alisimama taratibu, akatoka katika kile kichaka alichokua amejificha. Na hapo ni baada ya kujilizisha kwamba viumbe wale wa ajabu wamepotelea. Akaenda mpaka pale alipokuwa amemficha farasi wake akakuta yupo salama. Akapanda juu ya farasi, akaitoa ile ramani ya sehemu anayotakiwa kufika.
"Mmh! mbona safari bado ndefu, nitafanikiwa kufika nikiwa hai kweli?" alijiuliza Ntagambi, lakini hakuwa na majibu sahihi kwa wakati huo. Akaikunja vyema ile karatasi na kuiweka katika mfuko wake wa shati, kisha akaendelea na safari yake.
Jua liliamua kumtandika, lilimuadhibu haswa, na kumpa wakati mgumu katika safari yake. Yote hayo yalimuandama akiwa amefika katikati ya jangwa kubwa ambalo hakuweza kutambua jina lake, kwa wakati huo, hakutaka kupoteza muda kwa kuitazama ramani tena.
Alitamani angalau apate hata tone moja la maji, alainishe koo lake. Lakini ilikuwa ni bora ngamia apenye kwenye tundu la sindano, kuliko yeye kulipata ilo tone la maji.
Alipiga moyo konde, pindi alipokumbuka kauli ya mfalme kwamba, atakayefanikiwa kuifikisha hiyo dawa katika ardhi ya Omulenga, atamuoa binti mfalme. Ahadi hiyo ilimtesa sana Ntagambi, ikampa ujasiri ambao mwisho wake alihisi ni umauti uliojawa na maumivu karibia kila kona ya mwili wake.
Hatimaye alifanikiwa kulimaliza jangwa ilo. Muda haukuwa upande wake, uliyoyoma kwa kasi ya ajabu. Kwa mbali jua lilikubali kuondoka zake, ilikuwa ni jioni kiubaridi kikawa kinapuliza na kuiamuru miti idensi kuufwata upepo ulipoelekea.
Ntagambi rasmi aliingia katika pori kubwa, lilizungukwa na miti mbali mbali ikiwemo ya matunda. Ukijani wa pori ilo ulimvutia sana.. Ndege wenye rangi za kupumbaza na kuvutia walikuwa wakiruka na kuziachia mbawa zao kwa madoido. Hakika lilikuwa ni pori lenye mvuto wa kipekee.
Taratibu Ntagambi alishuka juu ya farasi, akamfunga pembeni, kisha akaanza kutafuta angalau maji apate kunywa. Ghafla aliona bwawa zuri kwa mbele, alipoangalia kwa umakini akaona mabinti wa kike watatu wakiwa wanaogelea, vifua vyao vilikuwa wazi. Akazishuudia zile titi changa zilizochongoka pale kifuani mithili ya mdomo wa kuku. Walikuwa na nywele ndefu zimemwagika mpaka mgongoni.
"Mmh! hivyi vibinti vya kiarabu mbona virembo sana, kumbe kuna watu wanaishi katika pori ili" alijisemea Ntagambi akiwa analivua shati lake nae akaoge kwa lengo la kuwapata wale mabinti. Akaweka mizigo yake chini pamoja na ule upanga.
******* ITAENDELEA *******
KUPATA SIMULIZI ZANGU, WASILIANA NAMI.... 0622 738 310.

NTAGAMBI.......04
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 23 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA NNE.

ILIPOISHIA.....
"Mmh! hivyi vibinti vya kiarabu mbona virembo sana, kumbe kuna watu wanaishi katika pori ili" alijisemea Ntagambi akiwa analivua shati lake nae akaoge kwa lengo la kuwapata wale mabinti. Akaweka mizigo yake chini pamoja na ule upanga.
ENDELEA NAYO.....
Akaanza kuzipiga hatua kuelekea lilipokuwa lile bwawa. Kadiri alivyozidi kusogea ndipo wale mabinti walizidi kumtamanisha kwa kuzishikashika chuchu zao. Ntagambi mate yalimtoka, mwili ukamsisimuka akajiapiza akifika lazima ampate mmoja wapo, ili aikate kiu yake ya muda mrefu, alikuwa radhi hata abake tu.
Alipofika katika lile bwawa, ghafla bin vuu wale mabinti walitoweka. Ntagambi aliduwaa, akatamani kupiga yowe lakini anaweza akazua balaa kubwa zaidi. Akatimua mbio mpaka pale alipoacha vitu vyake, anafika anakuta upanga haupo.
"Masikini ya Mungu wee! u wapi upanga wangu?" aliwaza Ntangambi. Akasogea alipokuwa amemfunga farasi wake, lakini pia hakumkuta. Alilia bila kupigwa, safari yote na misukosuko aliyokumbana nayo njiani haina maana tena.
Akazunguka kwa nyuma kidogo, akakuta farasi kalala chini, akiwa ameung'ata ule upanga mdomoni. Amejeruhiwa vibaya, damu zilikuwa zikimtoka kwenye paja, na ubavuni pia. Jicho la kushoto la farasi lilikuwa likidondosha machozi.
Farasi alitamani kama angelikuwa na uwezo wa kuzungumza, basi angelieleza jinsi alivyopambana na mabinti wale wa ajabu. Kumbe hawakuwa binadamu wa kawaida hata kidogo. Waliukwapua upanga na kutaka kuondoka nao, lakini farasi alikata kamba na kuanza kupambana, akafanikiwa kuubakisha upanga huo, katika himaya yake..
Ntagambi aligundua kabisa kwamba, kuna kitu farasi huyu kakifanya, ili kupatikana kwa upanga huo. Hakika farasi alihuzunisha, angelikuwa anaongea angelimkanya Ntagambi juu ya tamaa zake, na kusahau nini kilichompeleka katika ardhi ya mbali na kijiji cha Omulenga.
Ntagambi alikusanya vitu vyake, akamuinua Farasi tayari kwa kuianza safari. Lakini farasi alikuwa akikimbia kwa kuchechemea. Ntagambi akajawa na imani, Giza nalo tayari lilikuwa limeanza kuuvamia msitu huo. Akatafuta sehemu akamfunga farasi Kisha na yeye akakusanya majani na kuyaweka vizuri kwaajili ya kulala hapo.
Alipoamka asubuhi, mwili wote ulikuwa umeota chunusi, sababu ya baridi, alitetemeka mwili mzima. Hakuwa na muda wa kupoteza hata kidogo, alimtazama farasi wake, akamuomba Mungu kimoyomoyo kwamba isitokee farasi akashindwa kuendelea na safari.
Ilikuwa hivyo kama alivyoomba, farasi alisimama vyema kabisa. Safari ya machungu, machozi na maumivu ikaendelea.
Njiani kote walikopita, palikuwa kimya; hapasikiki chochote isipokuwa sauti dhaifu za kereng'ende. Hali ya hewa ilibadirika, jua lilikuwa limepotea na wingu kubwa kutanda. Muda si muda manyunyu yalianza kudondoka, radi kali na nzito zilitandika haswa. Mvua kubwa iliendelea kuicharaza ardhi hiyo. Ntagambi aliendelea kuchapa mwendo kwenye mvua hiyo. Akiiachia imcharaze na kumlowanisha kana kwamba inamsafisha.
"Wewe karibu nyumbani, nasema nawe karibu nyumbani. Njoo, nipate kunywa damu hiyo" Ilikuwa ni sauti nzito na yenye mikwaruzo, ikisikika nyuma ya mgongo wa Ntagambi. Akigeuka haoni mtu, ila upepo mkali ukiwa nyuma yake.
"Wewe usikii? au nikushushe mwenyewe," sauti ile ilisikika tena.
Maneno hayo yalimchoma sana Ntagambi. Hakuzoezea kabisa vitisho. Hasira zilianza kumnyemelea, zikapanda na kumsakama koo. Akafunua kinywa ili kutamka, lakini katu maneno hayakumtoka baada ya kupumua kwa nguvu.
"Simama tuyamalize" sauti ile ilisikika tena. Awamu hii Ntagambi tumbo lilijawa na uoga, akafungua kinywa chake tayari kwaajili ya kujibu, akiwa anapunguza mwendo wa farasi.
"Houyhnhnm..!! houyhnhnm..!!" ilikuwa ni sauti ya farasi akilia kwa uchungu. Lakini Ntagambi hakuweza kuelewa, akazidi kupunguza mwendo ili asimame na kuijibu sauti ile ya mtu asiyeonekana.
"Houyhnhnm..houyhnhnm..! houyhnhnm..!! houyhnhnm..!!" farasi alilia tena. Awamu hii alitimua mbio, na kukaidi amri ya Ntagambi ya kusimama. Ntagambi alibaki kinywa wazi, asijue ni nini kinaendelea.
Farasi alipofika mbele kidogo alisimama. Lakini eneo ilo lilikuwa linaogofya sana, lilizungukwa na miamba midogo mieupe inayotoa matone ya damu. Ntagambi kabla ya kuendelea na safari, akatoa ile ramani yake na kuanza kuangalia ni eneo gani lile.
Baada ya kusoma ramani, mwili ulimsisimuka. Kumbe hapo panaitwa Kulugongo, ni eneo baya na hatarishi sana. Akipita mgeni tu, ghafla bin vuu, mizimu ya eneo ilo inaanza kumsemesha akijibu au kusimama, basi kinakuwa kiama chake, anageuka mwamba mdogo na mweupe unaotoa matone madogo ya damu. Hiyo ni sadaka kwa mizimu ya eneo ilo wanaoabusu mwamba mkubwa unaoitwa Nyarukololobiwa.
Baada ya Ntagambi kuelewa uhalisia wa eneo ilo la Kulugongo. Alipigwa na butwaa kwa mara nyingine, akili yake ilifunguka ghafla, akajilaumu kuona safari imeingia masika.
Alisogea mbele kidogo, akaketi chini ya mti mkubwa,"ukupigao ndio ukufunzao." yalikuwa ni maneno ambayo yalikatiza kwa kasi katika kichwa chake.
Akiwa amekaa chini ya mti huo, machozi njia mbili mbili aliyaachia yamwagike, yakalowanisha mashavu yake, na kudondoka kwenye nyasi zilizokuwa pale chini.
"Sina tena tabasamu, roho yangu imevamiwa na uchungu usiokoma," alijisemea Ntagambi, machozi nayo yakiendelea kumwagika.
"Narudi nyumbani, njia ya safari yangu imejaa miba mingi inayochoma. Moyo wangu unasononeka kwa uchungu," alizidi kulalamika kwa simanzi Ntagambi.
Hasira zikamzidi, maumivu yakamponda ponda, akapoteza fahamu akiwa chini ya mti huo mkubwa, na hapo ndipo balaa lilipoanzia.
******** ITAENDELEA ********

NTAGAMBI.......05
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 23 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA TANO.

ILIPOISHIA.....
"Narudi nyumbani, njia ya safari yangu imejaa miba mingi inayochoma. Moyo wangu unasononeka kwa uchungu," alizidi kulalamika kwa simanzi Ntagambi.
Hasira zikamzidi, maumivu yakamponda ponda, akapoteza fahamu akiwa chini ya mti huo mkubwa, na hapo ndipo balaa lilipoanzia.
ENDELEA NAYO.....
Ntagambi akiwa bado amepoteza fahamu, pembeni yake kulikuwa na kaburi la zamani sana. Lilikuwa na nyufa kila kona, lilifichwa na nyasi ndefu, isingekuwa rahisi kwake kuliona.
Kaburi ilo lilipasuka katikati, kisha ukatokeza mkono mrefu, ulijawa na mifupa tu. Ilikuwa ikitikisika yenyewe, kana kwamba inayumbishwa na upepo. Ukiyastajabu ya Musa utayaona ya firanu, hakika msemo huu ulimata sana kwa nyakati zote mauzauza hayo ambayo yalikuwa yakiendelea.
Mkono huo ulimshika Ntagambi pamoja na farasi wake. Kisha kuwavutia ndani ya kaburi ilo. Ulikuwa ni ulimwengu mwingine kabisa, uko chini ya ardhi. mafuvu ya watu yalitawala kila kona, fisi wakiwa kama walinzi, miili ya binadamu ilikuwa imetundikwa juu ya miti huku ikiwa inachuruzika damu mbichi kabisa.
Hatimaye Ntagambi fahamu zilirejea, akaanza kushangaa ...
"Ni wapi tena huku? nchi gani hii? mbona miili ya binadamu wakiwa wamefariki imetapakaa kila kona!." kuangalia vizuri anakuta amelazwa juu ya maiti, farasi akiwa amesimama pembeni take, damu zikimtoka baada kukwaruzwa vibaya na fisi hao.
Ntagambi akiwa bado hajapata majibu, Ghafla bin vuuu.! alitokeza mtu na kusimama mbele yake, alikuwa na meno matatu marefu sana, jicho moja kubwa la mviringo,, mkono mmoja, pamoja na mguu mmoja. Ntagambi alijawa na hofu, haja kubwa na ndogo zilimtoka pasi yeye kujua.
Kiumbe hicho cha ajabu, kilikuwa na uwezo mkubwa sana, wa kuvuta harufu kwa umbali mrefu. Kilianza kucheka baada ya kugundua Ntagambi tayari kajisaidia papo hapo..
Kwa mara ya kwanza kiumbe hicho kilianza kuzungumza japo kwa shida sana..
"Oloto kaingule bugulaito kagole" Ntagambi hukuelewa ni lugha gani hiyo, akabaki ameduwaa. Kiumbe hicho kinajua lugha zote. Kikakodoa jicho na kutoa miale ya mwanga, ikatua katika kichwa cha Ntagambi, akagundua lugha anayoitambua Ntagambi. akaendelea kuzungumza,
"Karibuni sana katika ulimwengu wetu huu mzuri na wakupendeza. Nilikusikia ukiwa unalia pembeni ya kaburi langu. Ulinipigia kelele sana, nikaona nikulete huku, tuweze kupata damu yako angali ikiwa ya moto."
Kiumbe hicho kilinyamaza kidogo, kisha kikacheka kwa sauti kali yenye mwangwi...
"Hahah haahah ahaha..!! obuntu bulelooo, obhuluyoooo" kilivyocheka tu miti ikaanza kuweweseka kwa ukali wa upepo. Sauti za watoto wachanga zikasikika wakiwa wanalia. makaburi yakaanza kupasuka huku nyoka warefu wakiwa wanatoka ndani ya makuburi hayo.
Maajabu hayo yaliendelea kwa muda wa dakika moja, ndipo kiumbe hicho kikaunyoosha mkono wake ule mmoja hali ya hewa ikawa shwari kama mwanzo.
Kiza kinene kilitanda, mvua ikaanza kunyesha, matone ya damu ndio yakiwa yanadondoka kutoka angani.
Ntagambi alistaajabu sana, kuona watu wakioga uchi wa mnyama juu ya makuburi. Watoto wachanga wakiwa wanachinjwa na kuchukuliwa damu pamoja viganja vyao.
Fisi watatu wakubwa, walionekana wakikimbia kwa kasi, kuelekea alipo Ntagambi. Ntagambi kila alipojaribu kuutoa upanga, upanga ulikatalia katika kiuno chake. Hakuwa na njia nyingine ya kujinasua, zaidi ya kusubiri kitakachomsibu. Walikuwa wameshagundua kwamba Ntagambi ana nyota nzuri sana, mizimu ya ulimwengu huo wa giza, ilijiapiza katu haitamuachia. Mpaka waipate damu yake.
Fisi mmoja alimrukia Ntagambi, na kuanza kumburuza mpaka sehemu iliyoandaliwa, akakalishwa juu ya fuvu la binadamu. Kisha kile kiumbe kikampaka mafuta laini yalikuwa na harufu mbaya. Baada ya kupakwa mafuta hayo Ntagambi alishangaa kuona mji huo ukiwa umebadirika.
Maghorofa ya kifahari, mbuga za wanyama ni tofauti kabisa na mbuga za kawaida. Njia zenye vilima, mandhari ya kimapenzi, maporomoko ya maji, miamba na sanamu za kale.
"Eeeh! mbona kuzuri sana hapa!" Ntagambi alishangaa. Akawa anageuza shingo yake huku na kule, kila kitu kilichokatiza mbele yake hakuwahi kukiona katika maisha yake.
Akamshika farasi wake, na kuanzia kupiga hatua kusonga mbele, alipoitazama ramani yake haikumuonesha pale alipo ni wapi. Akageuka nyuma, anakutana na hoteli ya kifahari, ni mpya, yasadikika imejengwa miaka saba iliyopita.
Iko katika sehemu ya magharibi ya mji huo. Inavivutio vingi ikiwa ni pamoja na burudani ya watoto. Na maeneo mengine ni kimya sana.
Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa kutoka hotelini hapo, kama kilomita ishirini na tano. Jengo lilikuwa lina kumi na nne ghorofa, na lifti na ukumbi mzuri, bustani pia. Kulikuwa na
vyumba maalumu kwa wageni wenye ulemavu. Vyumba hivyo ni hewa kondisheni. Ntagambi alihisi anaota au anatazama tamthilia ya kuvutia kutoka falme za kiarabu uko Dubai.
Nje ya hoteli hiyo, kulikuwa na bustani yenye maua, walikuwa wakichoma kuku, mbuzi na nyama za aina mbalimbali. Mkusanyiko wa watu ulikuwa si mkubwa sana. Lakini nyama hizo zilikuwa zikitolewa bure. Vikundi vya burudani na muziki viliendelea kutumbwiza, nyimbo mbali mbali.
Ntagambi alikuwa tayari ashayavulia nguo na alijua kuwa hana budi kuyaoga. Alijua wazi kuwa huu ndio wakati wake wakupata nyama choma na kukata njaa iliomkaba kupita kiasi..
Ijapokuwa roho ilimwenda mbio, Ntagambi alijikarambusha na kukodoa macho kwa ujasiri. Akaelekea pale wanapogawa nyama, wale wagawaji walimshangilia sana. Mabinti warembo, wenye ule urembo wa mnato wenye kukinasa chochote kinachotua juu yake. Walimsogelea Ntagambi na kuanza kumkatikia viuno mbele yake
Kwa mara ya kwanza Ntagambi anatabasamu, nae akavishika vile viuno vilivyolegea. Akakatiwa nyama ya kuchoma, ikisindikizwa na maji bariiiiiiiiiidi"
"Nyama tamu sana hii" alisifia Ntagambi, akiwa anaendelea kubugia nyama hiyo.
"Houyhnhnm..houyhnhnm..! houyhnhnm..!! houyhnhnm..!!" farasi alilia kwa huzuni na uchungu, baada ya kumuona Ntagambi akila nyama ile.
"Houyhnhnm..houyhnhnm..! houyhnhnm..!! houyhnhnm..!!" farasi alilia kwa mara ya pili. Awamu hii aliinua juu miguu ya mbele akitaka kuikata ile kamba aliofungwa, lakini alishindwa.
Ntagambi alikuwa ameuacha upanga juu ya farasi. Kupitia yale matone matatu ya damu yaliopo katika upanga, yalianza kutoa matone ya damu na kudondoka juu ya mgongo wa farasi.

NTAGAMBI.......06
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA SITA.

ENDELEA NAYO....
Burudani ziliendelea kuliteka eneo ilo. Ntagambi akajiona kama yupo paradiso ya Duniani. Binti mmoja alionesha kumtamani Ntagambi, naam! hakika ilikuwa ni mbuzi kafia kwa muuza supu. Alipobisha tu hodi, Ntagambi akafungua mlango.
"Tusogee pale mbele kwenye kale kashamba" alizungumza binti huyo.
"Ni wewe tu" alijibu Ntagambi.
Mkono wa binti aliuweka katika kiuno cha Ntagambi, wakati mwenzie nae akiurusha wake katika mabega ya binti. Wakafika kwenye Kishamba iko kidogo kulikuwa na nyasi chache, akamwambia Ntagambi azivutie kwenye kona ya shamba ilo kisha azichome, waweze kuketi vizuri.
Mbele ya msichana Ntagambi hawajawahi kukubali unyonge hata siku moja. sekunde nne nyingi uchafu alikwisha ukusanya sehemu moja, akapewa kiberiti tayari kwa kuuchoma.
Ntagambi akiwa anapokea kile kiberiti, kwa mbali aliona farasi wake anakuja kwa kasi ya ajabu. Akagundua kwamba tayari kakata kamba.
Aliwasha moto, lakini akamuona mamake akiwa anateketea katika moto huo. Akiwa bado anashangaa, farasi alikuwa amekwisha fika na kuanza kuukanyaga kanyaga ule moto na kuuzima.
Ntagambi kugeuka nyuma amtazame yule binti, anakuta kaisha toweka muda mrefu. Akamtazama farasi wake kwa jicho la huruma sana. Akauchukua upanga wake juu ya farasi. Upanga huo ulitoa mwanga mkali ukapiga kwenye macho ya Ntagambi na kuiondoa ile dawa aliyowekewa, akaanza kuona uhalisia wa eneo ilo.
Alishangaa sana, ile hoteli kumbe palikuwa ni juu ya kaburi, wale wahudumu ni fisi waliodhoofu sana, alichoka baada ya kugundua zile alizokula zilikuwa ni nyama za viumbe waliokufa zamani wakiwemo na binadamu. Na yale maji ya baridiiii aliyokunywa ilikuwa ni damu mbichi ya paka aliyekaidi amri ya uko kuzimu. Ntagambi alichoka mwili roho pamoja na akili.
Vile viumbe vya ulimwengu huo wa kuzimu, viligundua kwamba Ntagambi kafunuliwa macho, anaona kila kitu kinachoendelea. Kengere ambayo ni fuvu la mtoto iligongwa kuashiria hali ya hatari.
Fisi, paka wakubwa walijitokeza kwa wingi, na kuanza kumsaka Ntagambi. Ilikuwa ni vunta n'kuvute ya aina yake. Upepo ulizidisha kasi, paka walilia, bundi wasiokuwa wa idadi walilivamia anga ilo. Hali ya hofu ilianza kumuingia Ntagambi, akakata shauri la kuendelea na safari. Lakini alipokumbuka ahadi kwamba akifanikiwa anatumuoa binti mfalme, pole pole alipanda juu ya farasi na kuanza kutimua mbio.
Weee! ukisikia shoo ya kiume, na kibabe inayopiganwa na wanaume pekee, ndio hii sasa. Fisi walikuwa na kasi isiyo ya kawaida, walijaribu kumtega farasi miguu ya nyuma. Lakini farasi hakuwa mzembe kiasi iko. Alizidi kuchanja mbuga, mvua ya ajabu iliporomoshwa na viumbe hao, vidimbwi vya maji vilitapakaa kila kona. Farasi alikuwa anavikwepa kama anavyoruka viunzi.
Bundi na ndege wa ajabu wenye vichwa, vya binadamu walianza kumzonga Ntagambi, asione anapoelekea.
"Khaa! nini hiki" alisonya Ntagambi, akauchomoa upanga, na kuanza kufyekelea mbali vichwa vya ndege hao. Weweee!! damu zilikuwa zinaruka kwa madoido kama shindano la ulimbwende, na kuzidi kuusafisha upanga, viumbe vilijuta kukutana na upanga huo.
"Oluyooooooo!!..gizaaalolulongo" ilikuwa ni sauti nzito na ya kukwaruza, ikiambatana na radi kali pamoja na ngurumo zisizokuwa na kifani. Sauti hiyo ilitoka kwa mkuu wa ulimwengu huo wa kishetani chini ya ardhi.
Baada ya sauti hiyo kutoweka kiza kinene kilitanda ghafla. Kiliendelea kutawala na kueneza utawala wake kote kote.
"Hapa nimemalizwa nitaona vipi napoelekea sasa?" alijiuliza kimoyomoyo Ntagambi, lakini hakupata jibu lililosahihi.
"Basi nimekwisha" alikata tamaa. Ule upanga aliokua ameushika uliachia mwanga mkali. Fisi na wale viumbe wengine waajabu wakaanza kuweweseka na kupoteza muelekeo.
Mwanga ule ulileta nuru mpya kwa farasi, aliiona njia walioingilia barabara. Alikimbia huku na huku mithili ya mja anaekimbizwa na shetani. Aliomgeza kasi mithili ya mwanambuzi anaemuogopa mbwa mwitu. Hatimaye walitokezea kwenye ule mti mkubwa, ambao ndipo waliponyakuliwa na kuingizwa katika ulimwengu wa kishetani.
Farasi alipoupita mti huo, mbele kidogo alisimama, akakunja miguu ya mbele akalala chini, Ntagambi alishuka. Wote walikuwa hoi bin tahaban. Walihema kwa fujo, purukushani ziliwachosha.
Ntagambi alianza kutapika mfululizo. Alitapika vitu vya ajabu kama, nywele, kucha na ngozi ya fisi iliyokaushwa. Alishangaa sana, ila baada ya kutapika alihisi kama ameutua mzigo mzito katika mwili wake.
"Nimechoka, nimechoka, mbona sifiki jamani, nafia njiani masikini ya Mungu" alihuzunika sana. Akaitoa ile ramani lakini haikuweza kumuelekeza ni wapi aelekee.
Aliwaza na kuwaza, akapanda juu ya farasi na kuamua kusonga mbele, bila ya kujua ni nini hatma yake ya yeye kuipata dawa hiyo ilioitwa ochululungilo.
Alisafiri umbali mrefu, alivuka mabonde na milima, mabwawa na mito mikubwa. Alipumzika pale alipochoka, matunda ya porini ndio chakula alichokitegemea kwa sana katika safari yake.
Jua kwa mbali lilianza kufifia, Ntagambi akavamia msitu mnene kiasi. Alipishana na wanyama mbali mbali, wengine aliwatambua ila baadhi aliwasoma kwenye vitabu.
Manusura tu amgonge Bi kizee aliyekuwa amesimama njiani, na kifurushi kidogo cha kuni katika kichwa chake. Alikuwa ni kikongwe haswa, alitetemeka mwili mzima mithili ya mgonjwa wa homa, kichwani nywele zilikuwa ni nyeupe kana kwamba kapaka rangi, kumbe zilikuwa ni mvi. Ngozi yake ilikunjamana na kuupoteza mvuto wake, alikuwa akitembea kwa kunyata sababu ya uzee.
Ntagambi, mapigo ya moyo yalimuenda kasi, "Ni heri kumsaidia mzee mzigo kuliko kumtwika" ni kauli ambayo alisisitizwa sana na mamake. Basi alishuka juu ya farasi akaelekea aliposimama yule Bibi.
"Bibi shikamoo" alisalimia Ntagambi.
"Maaa..rahaa" alisita kidogo, Bi kizee alikuwa akizungumza kwa taabu sana.
"Marahaba" hatimaye alifanikiwa kuitikia salamu. Ntagambi akauchukua ule mzigo wa kuni na kuubeba, kisha akawa anamfata kwa nyuma huyo Kikongwe, ili amfikishe mpaka kwake, amkabidhi mzigo kisha yeye aendelee na safari.
Hatimaye walifika, kilikuwa ni kijumba kibovu cha miti, kiliezekwa kwa unyasi wa porini. Mlango wake ulikuwa mfupi sana, Ntagambi akainama na kuingia ndani, farasi akiwa nje.
Kulikuwa na viti viwili vidogo, kitanda kimoja tu cha msonobari kilichotandikwa uzuri kabisa. Mito mitatu ya rangi ya hudhurungi ilitulia juu ya kitanda hicho kilichofunikwa na mashuka yenye picha za maua. Pembeni ya chumba hicho kulikuwa na kijimeza cha duara kilichotandikwa kitambaa cheupe juu yake kulikuwa na kichupa kidogo kilichojaa ugolo, pamoja na vito kadhaa vya dhahabu.
***************** ITAENDELEA ***********
Je Bi kizee huyo, kitu gani atamfanya Ntagambi?
Huruma ya Ntagambi itamponza au laa?
Mimi na wewe hatujui,

NTAGAMBI.......07
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA SABA.

ILIPOISHIA.....
Hatimaye walifika, kilikuwa ni kijumba kibovu cha miti, kiliezekwa kwa unyasi wa porini. Mlango wake ulikuwa mfupi sana, Ntagambi akainama na kuingia ndani, farasi akiwa nje.
Kulikuwa na viti viwili vidogo, kitanda kimoja tu cha msonobari kilichotandikwa uzuri kabisa. Mito mitatu ya rangi ya hudhurungi ilitulia juu ya kitanda hicho kilichofunikwa na mashuka yenye picha za maua. Pembeni ya chumba hicho kulikuwa na kijimeza cha duara kilichotandikwa kitambaa cheupe juu yake kulikuwa na kichupa kidogo kilichojaa ugolo, pamoja na vito kadhaa vya dhahabu
ENDELEA NAYO...
"Ukiyastajabu ya musa utayaona ya firauni" Ntagambi alikuwa akielea ndani ya msemo huu, kwa wakati huo.
"Hiki kijumba na vitu vilivyomo mbona ni tofauti kabisa" alijiuliza Ntagambi, akiwa anashangaa vito vya dhahabu pamoja na maua yaliyochorwa katika yale mashuka. Ntagambi aliombwa aketi chini, baada ya kikongwe kuwa ameingia ndani.
Ntagambi aliacha kushangaa, akaanza kuvuta fikra ili ajue namna ya kutoroka mahali pale. Hapa ndipo picha za matukio ya uzembe alioufanya awali zilimuijia akilini. Naam sasa alielewa fika kwanini mpaka sasa yupo mbali na nyumbani. "Sihitaji kurudia tena makosa" alinong'ona kwa sauti ya chini sana Ntagambi.
Vilio vya kwikwi, simanzi, huzuni na machozi yasiokoma yalitawala katika kijiji cha Omulenga nchini Bulilo. Taarifa zilizagaa kila kona ya nchi hiyo, kwamba karibia vijana wote waliokwenda nchi ya mbali kutafuta dawa wameuawa kinyama.
Kila nyumba waliomboleza kadri wawezavyo. Wengine walichimba makaburi na kuzika nguo za hao wapendwa wao. Mfalme Bunini alichukia sana, kila njia aliyotumia haikuleta mafanikio chanya kwake.
Waganga wa Karibu na mfalme walikuwa wapo hatarini kunyongwa. Waliapigania maisha yao kwa kuugeza usiku na kuwa mchana, yaani walikesha wakitafuta dawa ya kumsaidia mfalme aweze kupata mtoto wa kiume.
Juhudi zao hazikufua dafu, ilikua ni kama dua ya kuku isiyompata mwewe. Walisoma kila aina ya kitabu cha kale, wakaambulia patupu, bahata haikuwa upande wao.
"Nisipompata yule kijana, ntakufa angali nikiwa binti mbichi kiasi hiki" Chidumu binti mfalme alikuwa akizungumza mwenyewe chumbani kwake.
"Kama vijana wote yasemekana wameuawa, nitafanya nini mimi? Na yule naempenda atakua hai kweli?" alizidi kuwaza binti mfalme, hisia zilikuwa juu ya Ntagambi. Akatamani kama angeongozana nae kwenda kutafuta hiyo dawa.
"Leo ni siku maalumu ya kuwanyonga wale wote wanaopinga utawala wangu," alipaza sauti mfalme Bunini.
"Pia na wale mabinti wanne ambao mmeniletea nikaishi nao mwaka sasa, lakini hawajapata ujauzito nitakata vichwa vyao hadharani." alifoka mfalme, akiwa ameyang'ata meno yake kwa hasira. Lile tumbo lake kubwa lilikuwa linapanda na kushuka kwa jazba.
Askari maalamu walijipanga, wakawatia vitanzi wale wote waliokuwa wakimpiga mfalme,
"Sawa, tunashukuru. Tunyongeni tu, sisi tunatangulia nanyi mtatufata, hamuwezi ishi milele katika hii Dunia. Sote ni wakimbizi tunapita tu." Zilikuwa ni sauti za malalamiko kutoka kwa wale wanaonyongwa. Watu walilia lakini vilio hivyo vilikuwa kama nyimbo nzuri za kumbembeleza mfalme Bunini aweze kupata usingi.
Wasaa wa kukatwa vichwa wale mabinti wanne uliwadia. Askari wanne wakasimama nyuma ya kila binti, tayari kwaajili ya kufyekelea mbali vichwa vyao. Wakahesabu moja, mbili ile wanaenda kutamka tatu ili panga zitembee, ghafla alitokea mtu akiwa ameificha sura yake na kitamba cheusi.
Alijirusha juu na kuserereka kwa kutumia tumbo. Akiwa anatembeza panga kama njungu. Askari wa mfalme Bunini walijuta, wakatamani ni bora wangelikufa mapema kuliko kukutana na mtaalamu huyo wa kutumia upanga.
Mama yangu! kweli upele ulipata mkunaji. Mtu huyo, alikuwa na utaalamu mkubwa wa kutumia silaha. Aliendelea kutembeza panga zikiwapata askari wale na kuwaua papo hapo. Aliruka sarakasi moja, kisha akagandia kichwa huku akiendelea kutembeza panga za miguu kama hana akili timamu.
Duh.! watu walianza kukimbia, mpambano ulikuwa ni mkali. Mfalme Bunini, alipoona askari wake wameelemewa akaongeza wengine.
Hatimaye mtu huyo alizidiwa nguvu. Akaamua kuwachukua wale mabinti wanne, waliokuwa wakisubili kuuawa kwa kukatwa vichwa, akakimbia nao. Akiwa anakimbia alirushiwa panga likamkata begani. Damu nyingi zilimchuruzika, akatokomea pasipojulikana.
Mfalme Bunini alivimba manusura apasuke. Akaamulu vikosi vyote vya ulinzi vianze mazoezi makali, watumie mbwa na hata farasi, kuwasaka waharifu.
Binti mfalme akiwa chumbani kwake, alivua mavazi aliyokuwa amevaa, kisha akalitazama bega lake, alikuwa amekatwa vibaya sana, damu ziliendelea kumchuruzika. Kumbe binti mfalme ndie aliejitosa dimbani na kwenda kuwaokoa wale mabinti wanne. Hakuna alieweza kutambua ilo hata mmoja.
"Hapa nimfate yule daktari wa Baba anitibu" alijisemea mwenyewe Chidumu binti mfalme.
"Ole wake aitoe siri hii, atanieleza ni lini na wapi alipoona mtoto akizaliwa tu anacheka" alijiapiza binti mfalme, akasimama na kuelekea kilipo chumba cha Daktari huyo.
"Kon'konkoooo..!! Kon'kon'koo" binti mfalme aligonga mlango, ukafunguliwa.
"Eeeh! na wewe unataka nini usiku huu? Ondoka usije niletea balaa mimi" alifoka Daktari.
"Shiiiiii.!! Dokta chimati, kaa kimya, usiongee chochote kile" aligomba binti mfalme, akamrudisha Daktari huyo ndani. Akamuamulu amtibu haraka.
Matibabu yalianza haraka sana, akashonwa lile jeraha, na kupakwa dawa inayokausha haraka. Alipomaliza kutibiwa aliaga akaondoka zake. Lakini alijificha nyuma ya mlango, baada ya sekunde kadhaa kupita akasikia mlango wa daktari ukifunguliwa. Kumbe alikuwa anaenda kumuamsha mfalme amueleze kila kitu.
Alipopita tu kwenye ule mlango, binti mfalme alimkaba kwa nyuma, akamdunga kisu cha shingo, akamuua papo hapo. Kisha akamvuta na kumfungia kwenye kabati la chuma.
Mama Ntagambi alikuwa ameuuma mdomo wa chini kwa meno. Ni maumivu makali yalikua yakiuzonga mwili wake, kwa wakati huo. Alikodoa macho, kama ambaye alikuwa anagombana na ulimwengu uliompa mgongo. Mwili mzima ulimzizima kutokana na hisia za maumivu. Alikuwa ni mgonjwa, aliungua upande mmoja na kupata vidonda vikubwa. Mpaka leo ukimuuliza huo moto ulitokea wapi hana majibu.
Kumbe Ntagambi alipokuwa katika ule ulimwengu wa kishetani, alipochoma ule uchafu na kumuona mamake, ilikuwa ni kweli anaungua. Laiti asingelikuwa farasi kufika na kuuzima, basi Mamake Ntagambi angeteketea kabisa.
Mama Ntagambi hali ilikuwa mbaya, vidonda vilioza na kutoa harufu, alilia sana mama wa watu. Yule kijana aliekabidhiwa na Ntagabi kumuangalia, alitumia kila njia kumtibu lakini ukata wa fedha ukawa kikwazo kikubwa.
Mamake Ntagambi hali yake iliendelea kudhoofika haraka ajabu. Akamuita yule kijana anaemuangalia kisha akamwambia,
"Mwanangu, mimi sitapona,"
"Kwanini unasema hivyo mama?" kijana alimuuliza huku machozi yakimdondoka.
"Kila mwanadamu lazima afe, hii ni zamu yangu mwanangu. Wewe lakini nakuombea Mungu akujalie, kama Ntagambi atafanikiwa kurudi akiwa hai na mwenye nguvu, nawe ukapata fursa ya kuonana nae, mwambie jina Ntagambi linamaanisha mtu mpambanaji, jasiri na asiekata tamaa," Baada ya maneno hayo Mamake Ntagambi alinyamaza; hakuongea tena. Kijana huyo alimshika na hata kumtikisa tikisa. Alitaka kumueleza kuwa atafanya Kama alivyosema lakini hakujibu.
"Mama wa rafiki yangu, nitafanya kama ulivyosema," alipaza sauti na kumwahidi kuwa atafanya hivyo lakini hakujibu; alinyamaza tu. Kumbe alikuwa amekwisha fariki tayari. Huzuni kubwa ilimgubika kijana huyo.
LIKE, SHARE KISHA COMMENTS TUPATE KUENDELEA NA SEHEMU YA NANE. ( 08 )

NTAGAMBI.......08
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA NANE..

ILIPOISHIA...
"Mama wa rafiki yangu, nitafanya kama ulivyosema," alipaza sauti na kumwahidi kuwa atafanya hivyo lakini hakujibu; alinyamaza tu. Kumbe alikuwa amekwisha fariki tayari. Huzuni kubwa ilimgubika kijana huyo.
ENDELEA NAYO....
Akawaza afanye nini, akashirikisha rafiki zake watatu wakachimba kaburi na kumzika. Walifanya kama siri kwani uongozi wa mfalme Bunini ungejua ilikua ni kosa.
"Mama pumzika mahali hapa, urafiki wangu na mwanao ilikuwa ni zaidi ya urafiki. Wewe ulikuwa shuhuda mama. Maumivu na makovu yako yamekandamizwa na udongo mziiiiiito. Nakuahidi mbele ya kaburi ili, nitapambana mpaka pale nitakapofikwa na umauti," alizungumza kwa utulivu sana kijana huyo, huku machozi nayo yakimsindikiza na kuacha michirizi katika mashavu yake.
Alivyomaliza, aliingia ndani akachukua kalamu na karatasi akaandika ujumbe mrefu. Alipofika aya ya mwisho kuelezea maumivu aliopitia Mamake Ntagambi kabla ya kufikwa na umauti. Alishindwa kuvumilia, machozi njia mbili mbili aliyaachia yamwagike, yakalowanisha mashavu yake na kudondoka kwenye ile karatasi.
Alivyomaliza kuandika, aliikunja vyema karatasi hiyo, akaiweka juu ya kijimeza kidogo na kichafu kilichozongwa na vumbi, pamoja na utandu wa buibui. Akachukua koroboi na kuiweka juu, ili karatasi isipelekwe upepo. Alitaka ikitokea Ntagambi karudi basi apate kujua yote yaliotokea.
Nyumba ya mfalme, amani ilitoweka. Harufu ya damu za watu ilizidi kutapakaa. Kifo cha Dokta Chimati kilizua gumzo. Upelelezi wa kina ulifanyika lakini haikubainika ni muuaji gani huyo wa siri. Binti mfalme akawa anatoroka na kwenda msituni kuwapelekea chakula wale mabinti wanne. Hakuishia hapo aliwafundisha namna ya kutumia silaha.
Wakati Ntagambi akiendelea kuwaza na kuwazua, namna ya kutoroka. Katika kile kijumba cha maajabu pale msituni. Kikongwe huyo kwa mara ya kwanza alifungua kinywa chake na kuzungumza, "Kijana nashukuru sana, kwa heshima uliyoionesha kwangu. Kabla hujanieleza lakini najua kilichokuleta huku. Na usingesimama hapa, ulikuwa unaenda kuuawa. Sababu umeshapotea njia. Hiyo dawa unayoitafuta inaweza kughalimu maisha yako," Kikongwe huyo alisita kidogo kuzungumza. Akachukua ugolo wake na kuutia kinywani kisha akaendelea, .
"Nitakuelekeza njia ya mkato, lakini hapo palipo na dawa ni nchi yenye watu wa hatari, wana miguu mitatu, na wanapaa pia. Hapo nguvu zako hazitafua dafu, inatakiwa kutumia akili kubwa ili Kufanikiwa," alisisitiza Kikongwe huyo.
"Chukua kipande hiki cha mti, kitakusaidia, njia yenyewe ni ile, utafika mara moja" alimalizia kuzungumzwa Kikongwe huyo huku mwili ukiwa unamtetemeka.
"Asante sana Bibi," alishukuru Ntagambi akiwa anapanda juu ya farasi. Kabla ya kuondoka aligeuka nyuma, kile kijumba pamoja na yule Bi kizee havikuwepo tena. Ntagambi hakujali, Safari ya machozi, jasho na damu iliendelea.
Baada ya masaa kadhaa kupita, alikuwa amefika kwenye geti la kwanza, la mji huo wa Wafwa. Hali ya hewa ni tofauti, anga zima lilifunikwa na ukungu, baridi ilicharaza kwa kasi ya ajabu. Akiwa anavuka ilo geti, alitandikwa na kitu kizito katika kifua chake, akadondoka mpaka chini. Alisikia maumivu makali, akagusa kifuani kwake akaona amepigwa na kitu chenye damu.
Akajivuta pembeni na kujibanza hapo. Alipopata ahueni, alijikokota akamuendea farasi wake akapanda, safari ikaendelea, mara paap! Akalivamia geti la pili. Akainua kichwa chake na kutazama juu angani.
"Mama yangu wee! kile ni nini?" Ni hapo alipowaona wale binadamu wa hatari wenye miguu mitatu, na mbawa. Walikuwa wamelitawala anga, kana kwamba kuna kalamu wanasherekea huko. Walikuwa wanauwezo wa kuona mbali kuliko kiumbe chochote kile. Tayari walikuwa wameshamuona Ntagambi. Taratibu wakaanza kushuka.
Kijasho chembamba kilimchuruzika Ntagambi kwapani. Hofu ikaufunika mwili wake. Ile anaamulu farasi aongeze kasi, binadamu wa hatari tayari walikwisha fika. Nyuso zao zilikuwa zinaogofya, macho, pua ni kama binadamu wa kawaida ila midomo yao, meno yalipangana ovyo hata urefu wa ulimi sio wa kawaida.
Ntagambi alivutwa na kudondoshwa chini. Akazungukwa na binadamu hao takribani ya mia mbili. Na hapo ndipo Ntagambi alipojuta na kuilaani siku ile aliyozaliwa.
Sifa kuu ya binadamu hao, kunyonya damu ya viumbe hai wengine. Walikuwa na viganja vikubwa, virefu vyenye uzito usio wa kawaida. Ntagambi alipigwa makofi kila sehemu ya mwili wake, alilegea, akawa anatoa madonge mazito ya damu kinywani mwake.
"Nimwachweni" mdomo ulimvimba, hata kusema neno niacheni alishindwa, akatamka "nimwachweni"
Akili ya kuuchukua upanga ilimuijia angali akiwa hoi bin taaban. Aliushika vyema, lakini ukawa kichekesho. Upanga haukufua dafu kwa binadamu hao wa hatari. Kila alipojaribu kuwakata, upanga ulidunda na kutoa cheche za moto. Viumbe hao waliachia kicheko kizito chenye dhihaka ndani yake, baada ya kuona Ntagambi anavyohangaika na panga lake, ambalo ni kama butu kwao.
Miogoni mwa binadamu hao wa hatari, alikuwemo mmoja mwenye roho ya kikatili, aliitwa Obugainzige. Aliishika shingo ya Ntagambi, na kuutafuta ule mshipa mkubwa, tayari kwaajili kumtoboa na kunyonya damu.

NTAGAMBI.......09
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA TISA.

ILIPOISHIA...
Miogoni mwa binadamu hao wa hatari, alikuwemo mmoja mwenye roho ya kikatili, aliitwa Obugainzige. Aliishika shingo ya Ntagambi, na kuutafuta ule mshipa mkubwa, tayari kwaajili kumtoboa na kunyonya damu.
ENDELEA NAYO....
Akiwa anaenda kutoboa tu, wazo likamuhijia Ntagambi akashika kile kipande cha mti alichopewa na yule kikongwe.
Weee! hapo ndipo balaa lilipoanzia, kile kipande cha mti kilitoa moshi mzito. Wale binadamu wa hatari wakaanza kulegea na kukata mauno mpaka chini. Ungeweza kusema wanadensi nyimbo za kikongo. Kumbe ndio wanakufa hivyo.
Ntagambi alijikuta amebaki yeye pamoja na farasi wake tu. Macho yalivimbiana, alitapakaa damu mwili mzima. Alijitahidi kujikokota taratibu akasimama.
"Nateseka hivyi kwanini? ukute yupo mwenzangu kaishapata dawa na kuifikisha kwa mfalme," kauli ya kukata tamaa ilimtoka.. Nguvu za kupanda farasi hakuwa nazo, aliishika kamba na kuanza kupiga hatua taratibu, akaendelea na safari.
Hatua kadhaa mbele, aliona geti la tatu. Akapokelewa na bustani nzuri za maua. Miti mirefu ya kupendeza, ilitawala na kupamba eneo ilo. Ntagambi alishangaa uzuri aliokutana nao hapo. Akadiriki kupafananisha na bustani ya Eden waliyotimuliwa Adam na Eva baada ya kukaidi.
Alisita kuingia, akasimama takribani dakika kumi. "Sina cha kupoteza, tazama nilivyodhoofu acha niingie tu," alijisemea Ntagambi akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
Alipoingia ndani ya geti, akaona kiti kikubwa. Kikiwa kimefunikwa na kitambaa cheupe peee. Pendeni yake yalizungushwa maua rozi ya rangi mbali mbali. Katika kiti hicho alikuwa ameketi kikongwe yule aliyemsaidia Ntagambi kwa kumkabidhi kipande cha mti.
Kikongwe yule hakutaka kuzungumza. Aliinyoosha fimbo yake, na kumuelekeza mti wa dawa, anayohitaji Ntagambi. Hofu na uoga haukutaka kumuachia Ntagambi, taratibu akauendea ule mti na kuchuma matawi kadhaa, kulikuwa na chungu cha udongo pale chini akatia humo.
Ntagambi akataka asogee alipoketi Bi kizee huyo, aweze kumshukuru. Lakini, hakuwepo Bi kizee wala kiti chake vilitoweka kwa pamoja.
"Kwa hiyo hakutaka hata nimshukuru" alijihoji Ntagambi bila ya kupata majibu. Pamoja na maumivu aliyokuwa nayo, kidogo moyo wake ulichanua kwa kiasi kadhaa. Baada ya kufanikiwa kuipata dawa.
Alipanda juu ya farasi, akaanza safari ya kurejea katika ardhi ya Omulenga, Nchini Bulilo. Awamu hii, alikuwa kama ameogelea kwenye bahari ya furaha. Alipata faraja mithili ya kibogoyo alieota meno, tasa aliepata mtoto, kiziwi aliepata uwezo wa kusikia. Akatamani kama angekuwa na mbawa angeruka na kupaa angani awahi kuozeshwa binti mfalme.
Wale mabinti wanne, waliofichwa msituni na binti mfalme. Hatimaye walifuzu mafunzo, wakabatizwa na damu nyekundu ya roho mbaya. Wakapandikizwa chuki dhidi ya utawala wa mfalme na ikamea vyema.
Kuondoa uhai kwa binadamu yeyote yule, kwao ilikuwa kawaida, kama kupiga chafya. Aliewaongoza katika yote hayo ni binti mfalme.
Mfalme Bunini, aliamshwa usiku wa manane na moto mkali, uliokuwa unawaka nje ya jengo lake. Kengele ya hatari iligongwa, walinzi wakasambaa kila kona. Naam! mabinti wa kazi ndani ya gwanda za roho mbaya. Hii ni mtu nne ndani ya traki moja. Walikuwa wamesharuka uzio na kutua ndani ya himaya ya mfalme Bunini.
Walinzi walijuta, waliomba ni bora wangekutana na shetani mla watu, kuliko panga zinazotembezwa na binti hao. Himaya ya mfalme ilinoga kwa milio ya panga, Kama angelikuwepo mzee wa bwax, angelipata mapigo ya kuimbia singeli.
Askari walifyekwa vichwa, huku vifuani mwao wakiandikwa kwa damu, maandishi yaliyosemeka kwamba, "Mfalme atubu"
Mfalme Bunini, presha ilipanda na kushuka. Akaongeza kikosi kingine, mabinti wale wakaona mziki ni mnene, haooo..! wakatokomea zao kwa kuruka ukuta. Ardhi ya Omulenga ilitapakaa damu. Taharuki ikawaandama wananchi.
Nyumba zilichomwa moto, mali zikaporwa, Askari wakichinjwa. Ilikuwa vigumu watu kutembea, kula, au kufanya lolote. "Nani anaefanya haya mauaji? alafu wanasema mimi nitubu! naona wamenisahau sasa ngoja." alijihoji mfalme Bunini, huku akijiapiza kuwakomesha wahalifu hao.
Mfalme Bunini, alikusanya wanachi wote wakaingia ndani ya geti la himaya yake. Aliomba msaada kwa falme nyingine, zikamsaidia askari wa kutosha.
"Wanachi wa ardhi ya Omulenga, msiwe na hofu, hao washenzi tunaenda kuwamaliza" alipaza sauti mfalme.
"Aliliiiiiililili..!! alululululu..!! Alolilolololo" walishangilia wananchi, kwa kauli hiyo ya kishujaa, kutoka kwa mfalme wao.
Ntagambi alibakiza kijiji kimoja tu, aweze kuingia katika ardhi ya Omulenga, nchini Bulilo. Alikuwa akiyoyoma katika msitu mnene, wa kijiji cha Nyamuwabho. Ghafla alishtuka mshale unampata farasi shingoni. Farasi aligeuka haraka ili mshale umpate yeye. Asingefanya hivyo mshale ulikuwa unatua ubavuni kwa Ntagambi. Walianguka vibaya sana. Ntagambi alichubuka ovyo, damu zikawa zinamchuruzika kichwani.
Akachana shati lake, na kulifunga jeraha. Kile chungu kilichobeba dawa kilipasuka kwa chini, akachukua kipande cha kitambaa akaweka. Kuangalia kwa mbali akaona kuna watoto wanawinda. Akamchomoa farasi mshale huo, safari ikaendelea, japo kwa kuchechemea.
Hatimaye Ntagambi, alikuwa amefika nje ya geti la himaya ya mfalme Bunini. Alishangaa kuona watu wengi, na mfalme akiwa anazungumza. Walishangaa kumuona Ntagambi akiwa amerejea akiwa hai, huku ameshika chungu chenye dawa juu ya farasi. Watu walishangilia huku wakimkimbilia kwenda kumlaki.
Kabla hawajamfikia, ile Ntagambi anaingia tu ndani ya geti. Farasi alidondoka chini, akairusha miguu yake huko na huko, povu likamtoka kinywani, hakuamka tena, akawa amekufa. Sababu ni ule mshare kumbe ulikuwa na sumu kali.
Farasi alikufa kwa uchungu mwingi. Macho yake yalimtoka kama ambaye alikuwa anagombana na ulimwengu uliompa mgongo. Ntagambi, mwili mzima ulimzizima kutokana na hisia za kumuona farasi wake akiwa amekufa pale chini.
Uchungu usioelezeka ulimshika Ntagambi. Alikumbuka jinsi farasi alivyomsaidia katika safari yake, mpaka kurejea katika ardhi ya Omulenga. Ntagambi alisimama katikati ya watu, akiwa analia. Huku amekishika kile chungu cha dawa mikononi.
Watu walijiuliza kinachomliza ni nini, lakini hawakupata majibu. Muda si muda mvua ilianza kunyesha, radi kali zikawa zinapiga. Ntagambi alisimama kwenye mvua. Akiiachia imcharaze na kumlowanisha, huku akiendelea kulia, macho yake yakiwa yanamtazama farasi aliyelala pale chini. Akiwa ni sawa na mzoga sasa. Masikini ya Mungu weeee..!! alitia huruma sana Ntagambi.

NTAGAMBI.......10
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA KUMI
( 10 )

"Asante sana, nashukuru kwa yote" alinong'ona kwa sauti ya chini Ntagambi. Baada ya kuwa mvua imekata, na kuacha vidimbwi vya maji machafu, hapa na pale kando ya barabara za ardhi ya Omulenga.
Wananchi walikusanyika tena, kuja kuwa mashuhuda, Ntagambi akikabidhi dawa, na kupewa binti mfalme. Ilikuwa ni sherehe kubwa katika ardhi ya Omulenga. Ngoma za asili zilitumbuiza, navyo vikundi vya sarakasi havikuwa nyuma. Mji ulimeremeta, kwa maua na mapambo ya kila aina.
Binti mfalme alivishwa vazi jeupe. Akapakwa kila aina ya vipodozi. Mdomo uling'aa ka wekundu wa damu. Alitembea kwa madoido, akaketi sehemu alioandaliwa. Ntagambi, alikuwa katika mavazi yake yale yale ma kuu kuu. Hakuona umuhimu wa kupendeza zaidi ya kumpata binti mfalme.
Mfalme Bunini, akiwa amevalia vazi lake la kifalme, alikuwa ameketi kwenye kiti Cha kifalme. Pembeni yake alikuwepo Malkia, akiwa amevalia vazi jekundu. Wakati uliwadia sasa wa zoezi lile lililosubiliwa kwa hamu. Ntagambi aliitwa akasimama mbele, kisha akamkabidhi askari kile chungu cha dawa. Mfalme alikuwa akitabasamu muda wote, na kuyaacha meno yake yaonekane bila hofu.
Askari alikifungua kile chungu, akastaajabu, hakukuwa na dawa ya aina yeyote ile, ndani ya kile chungu. Watu walishangaa, miguno kila kona ilisikika. Ntagambi alipoangalia kile chungu akagundua, kile kipande cha kitambaa alichozibia chini ya chungu, kilikuwa kimedondoka. Hivyo hakuna jani hata moja lililosalia ndani ya chungu hicho.
"Unamdanganya mfalme?" alifoka askari, huku akimuachia kibao kizito Ntagambi katika shavu .
"Mwili uliokwisha kujeruhiwa, bado tena mnauadhibu," alilalamika Ntagambi.
"Tuambie dawa iko wapi?" alipaza sauti Askari.
"Dawa nilikuja nayo, hicho chungu kilipasuka kwa chini njiani. Nikakata kipande cha shati yangu na kuziba, lakini kumbe kipande hicho kimedondoka pasi mi kujua" alijitetea Ntagambi.
"Twende utuoneshe njia uliyopitia tukague" alizungumza askari huyo.
"Na hii mvua iliyonyesha hatuwezi kukuta kitu" baada ya kauli hii, kutoka kwa Ntagambi. Alipigwa na kitu kizito mgongoni, akadondoka chini. Binti mfalme aliumia, machozi yalianza kumdondoka. Baada ya kuona Ntagambi akipigwa.
Mfalme Bunini alikasirika, aliviambiana pale kitini kama mbogo. Akaamulu Ntagambi afungwe kamba na miguu. Askari watano walianza kumshughulikia, wanachapa kwa kupokezana kama mchezo wa kuigiza. Damu, maji na machozi vilimchuruzika Ntagambi. Aliangua kilio kisicho na mwisho.
"Anastahili kunyongwa mpaka kufa, mpuuzi huyu," alipaza sauti mfalme. Ntagambi akamwagiwa maji, na kuvuliwa nguo, na kubaki na nguo ya ndani tu. Binti mfalme aliona aibu, akainamisha kichwa chake chini. Angelifanya nini Ntagambi, wakati mikono na miguu imefungwa, lilikuwa ni swali lililoizonga akili ya binti mfalme.
"Majeraha yote, mateso, maumivu na manyanyaso niliyokumbana nayo njiani, ndio mshahara wake huu jamani?" alilalamika Ntagambi huku damu zikiwa zinamtoka kinywani.
"Mpelekeni mkamfungie gerezani, ntapanga siku ya kunyongwa kwake, ananidanganya mimi" alifoka mfalme, huku akiwa anainuka kwenye kiti chake, na kurejea zake ndani. Alivishwa nguo, akawa anabuluzwa chini, mpaka wakafika Katika mlango huo wa gereza. Wakamsukumia ndani, akakibamiza kichwa chake ukutani, alipiga yowe la uchungu.
"Msinipe adhabu ya kunyongwa, nitafanya lolote mlitakalo!" alilia kwa uchungu Ntagambi. Baada ya kuona geti la gereza likifungwa na makufuli makubwa na mazito. Lakini haikuwa hivyo, kilio chake hicho hakikuwagusa wala kuwaathiri Askari hao. Ilikuwa kama dua ya kuku isiyompata mwewe.
Baada ya majuma mawili kupita, ilikuwa ni siku ya ndugu, jamaa na marafiki. Kwenda kuwatembelea wafungwa gerezani. Ntagambi alipoinua kichwa chake, akamuona rafiki yake nje ya nondo zile za gereza.
Akajivuta taratibu akasogea, "Kabla ya yote, vipi hali ya mama yangu? maana nilikukabidhi unisaidie kumuangalia" alizungumza Ntangambi kwa sauti ya unyonge. Rafiki yake hakujibu kitu, ila chozi lilianza kumdondoka katika jicho lake la kushoto. Aliinua mkono wake na kumkabidhi Ntagambi ile karatasi aliokuwa ameandika. Aliamua kuifata kwao Ntagambi, baada ya kushuhudia rafiki yake alivyoumizwa mbele ya umati Kisha kuwekwa gerezani.
Ntagambi alivyopokea tu ile karatasi, askari waliona. Lilikuwa ni kosa kubwa sana, kumpa mfungwa kitu bila askari kukikagua. Basi askari huyo alikurupuka kwa fujo, akapitisha panga katika shingo ya rafiki yake Ntagambi, kichwa kikatengana na kiwiliwili huku damu zikifyatuka Kama bomba lililopasuka. Alifariki papo hapo masikini ya Mungu.
Ntagambi kulia hakuweza, akabaki ameyakodoa macho yake kwa mshangao. Alikuwa ni kama kachanganyikiwa, akatamani kama angeweza kuvunja geti ilo, akamfundishe askari huyo, namna ya kuthamini utu wa mwanadamu.
Ntagambi aliifungua karatasi hiyo, iliotapakaa machozi, jasho na damu. Alisoma aya moja moja, bila kuruka hata neno moja.. Mwisho wake ulkuwa ni mbaya. Aliangua kilio kama mtoto mdogo ndani ya gereza.
"Nimeikosea nini Dunia? utu wangu, upole wangu, ndio vinaniadhibu?. Mama! kwanini hukunisubiri nirejee ndio uondoke?. Umeniacha mahali pagumu sana. Mwanao, juhudi za kupambana kumpata binti mfalme, zimekuwa ni zawadi ya maumivu kwangu. Uliungua kwa moto, nisamehe mama, sababu ni mimi. Sina mtetezi mama, nimebaki mimi na Dunia yangu. Nanyongwa mama, kitanzi shingoni mwangu ndio mwisho wa kumpata binti mfalme. Naumia, naumia, naumia Dunia, naumia mama yangu. Ardhi ya Omulenga inaniua. Ooooh mamaaaaaaaa" alipaza sauti ya uchungu Ntagambi, akapoteza fahamu.

NTAGAMBI.......11
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA KUMI NA
MOJA.
( 11 )

Baada ya saa moja na nusu kupita, Ntagambi fahamu zilirejea.
"Habari za kutupigia kelele hatutaki hapa" alifoka mfungwa mmoja, aliekuwa amejilaza kiubavu karibu na Ntagambi. Kiza kinene kilikuwa kimetawala ndani ya chumba hicho kidogo. Ugeni ulimtesa Ntagambi, hakuweza kulala tena baada ya kusikia mtu akimpapasa katika makalio yake.
"Naijua vizuri michezo ya humu, inabidi nisinzie kama sungura." alijisemea kimoyo moyo Ntagambi. Ghafla aliona mwanga wa tochi ukipenyeza katika nondo. Akainamisha kichwa chake chini, wagundue kwamba kalala. Alihofia akijua ni askari wanafanya ukaguzi.
Ni wanadada machachali, awamu hii walikuwa watano. Mikononi mwao walishika panga na vyuma viwili virefu. Walihangaika kuvunja geti. Ntagambi alifanyiwa ishara ya kukaa kimya, walitaka wamtoroshe. Mbwa walibweka kwa fujo. Walinzi wakatahamaki na kuanza kuzunguka kila kona. Mabinti wakajificha pembeni ya nguzo za geti. Askari wakapita bila kugundua kwamba kuna watu pale.
Askari aliekuwa nyuma aliwaona, ile anaenda kurusha panga, wakaushika mkono wake na kumsukumizia kisu cha tumbo. Akadondoka chini mzima mzima. Askari walisikia kelele na kuamua kurudi nyuma. Mabinti wakakimbia na kwenda kujificha kwenye zizi la ngombe. Ngombe zilikatwa ovyo, matumbo yakatobolewa na upanga, utumbo ukatokeza nje. Miti ya kivuli na matunda ilifyekwa.
Askari walizunguka himaya nzima ya mfalme. Mabinti wakawa hatarini. Ile wanaruka ukuta, mmoja alipigwa mshale wa sumu mgongoni. Wakambeba na kujaribu kukimbia nae. Wakafika kwenye kichaka kilichozungukwa na miti kiasi, wakamlaza hapo.
"Chambuyale.! Chambuyale" walikua wakimtikisa mwenzao, waweze kugundua kama bado angali hai. Waliuchomoa ule msahale, na kuanza kumpatia huduma ya kwanza. Walizidi kumtikisa na kumuita kwa mara ya pili tena,
"Chambuyale.! Chambuyale.! amka"
"Mmmmmmh" aliguna kwa mbali huku akisema, "Nakufa, nakufa, siwezi kupona tena. Endeleeni na mapambano. Maumivu yanayopita ndani ya mwili wangu ni makali sana. Msilie kwaajili yangu, lilieni ardhi ya Omulenga mpaka muikomboe katika mikono ya shetani aliejivisha ubinadamu" baada ya kuzungumza maneno hayo, aliyafumba macho yake. Akainamisha kichwa chini, roho na kiwiliwili vikatengana akawa amefariki tayari.
Binti mfalme na wenzake walihuzunika sana. Wakakata matawi ya miti wakamfunika. Hawakua na mahali pakumpeleka, zaidi ya kumtelekeza hapo kwenye kijimsitu hicho kidogo.
"Sasa tumebaki wanne tu. Hii safari bado ni ngumu sana, tuwe tayari hata kuyatoa sadaka maisha yetu. Harakati za ukumbozi siku zote hazijawahi kuwa nyepesi" alizungumza binti mfalme, huku akiwa anawaaga wenzake. Akawaacha katika msitu huo uliokaribu na himaya ya mfalme. Yeye akaanza safari ya kurejea nyumbani kabla hakujapambazuka.
Kuku walianza kuwika. Ndege angani wenye rangi za kutamanisha na kuliwaza kwa pumbazo la kibakunja, hawakuachwa nyuma. Waliruka huku wakiziachia mbawa zao kwa madoido. Ni dhahiri walikuwa wakiikaribisha siku ya kipekee. Siku ambayo iliaminika vuli zingeungana na kuleta mvua kubwa ya masika....
Lakini kwa mfalme Bunini, na wananchi wa Omulenga, ilikuwa ni asubuhi chungu na mbaya. Walishangaa kukuta askari wakiwa wameuawa na miili yao kuchomwa moto. Ng'ombe zimelala chini utumbo ukiwa nje.
Mfalme kiti kilikuwa cha moto. Hakuweza kuupata usingizi, mawazo yalikizonga kichwa chake. Akaamua atangaze donge nono, kwa yeyeto ataeweza kufichua wauaji hao. Au kutoa siri ya kuwakamata. Naam! taarifa zikamfikia Ntagambi gerezani. Akaona sasa wasaa wakuisaidia nchi yake akiwa gerezani umewadia.
Kila asubuhi Ntagambi alikuwa akifanya mazoezi mepesi, kwaajili ya kuuweka mwili wake sawa. Alitamani aruhusiwe akawasake wauaji hao. Aweze kuwaleta wakiwa hai, au vichwa vyao akiwa amevitenganisha na kiwiliwili. Lakini hakuweza kuipata fursa hiyo, zaidi ya kusubiri kupangiwa tarehe ya kunyongwa.
"Mwenzio sijiwezi. Nataabika. Niko hoi dhidi ya penzi lako. Uonee imani moyo wangu. Kama ingelikuwa wewe ndiwe unataabika kisa ya penzi, ungefanyaje? Nimeridhia kukupenda. Kukuweka moyoni pangu. Ashumu, wewe ndiwe tabibu wangu wa dhati, utakayeiponya homa yangu ya mapenzi niliyonayo kwako. Njoo uwe mlezi wangu hapa gerezani. Ghadhari gani imekupata na kukusibu ewe ubani wangu wa moyo?"
"Nanena hadharani, maneno ya chembe cha moyo wangu. Nitapoteza maisha yangu, na utashtakiwa kwa kuniua kutokana na wivu wa moyo wangu. Nadata na penzi lako. Wewe ndiwe chaguo langu, mfariji wa moyo wangu uliojaa barafu na banguzi si kidogo." Ntagambi alikurupuka ghafla kutoka usingizini. Alikuwa amejiegesha kwenye ukuta, usingizi ukawa umempitia.
"Ni ndoto gani sasa hii ya mchana. Yaani naota naongea na binti mfalme, kama nilishampata hivyi. Japo nipo gerezani, ila binti mfalme hata nikikutana nae, katika maisha mengine baada ya haya ya hapa Duniani. Nitamkumbushia adhma yangu ya kuwa nae" alijisemea mwenyewe Ntagambi, huku akiwa anakaweka vizuri kakipande kake ka godoro aweze kujipumzisha tena.
"Mwanangu Chidumu!" malkia alimuita mwanae.
"Abee mama!" binti mfalme aliitika.
"Siku hizi sikuelewi kabisa binti yangu!"
"Kwanini mama?" binti mfalme alidakia.
"Mara nyingi usiku hauonekani hapa ndani, unarudi na majeraha. Itakua umepata mwanaume anakupiga hutaki kusema" alikazia malkia.
"Hapana mama, mimi uwa sitoki kabisa" alijibu Chidumu, huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
"Mficha maradhi kifo umuumbua, shauri yako!" alifoka kwa sauti ya chini malkia. Ili mfalme asiweze kuyasikia maongezi hayo.
Malkia alijikohoza kidogo. Kisha akaangalia kulia na kushoto, kama kuna mtu anaekuja. Baada ya kuridhika kwamba pako shwari aliendelea kuzungumzwa.
"Nisikilize mwanangu!"
"Nakusikilizia mama yangu!"
"Niliapa khatu kutotoa siri ya maisha yangu hapa ndani. Niliapa nitazikwa nife na siri zangu ila... Ila, taklifu ya moyo na msukumo wa maumivu yangu, vimenifanya niamue kuvunja mbarika. Ili wewe mwanangu, uweze kupata punje ya mtama wa maisha yangu machungu." Malkia alisita kidogo, takribani sekunde kumi. Kisha akaendelea zungumza,
"Nayokwambia hapa iwe siri yako!"
"Usijali mama!" Chidumu alidakia, kabla hata mamake hajamaliza zungumza.
"Baada ya kuolewa na mfalme Bunini, tuliishi miaka kumi na mitano, bila ya kupata mtoto. Nilihofia uhai wangu, nikajua muda wowote ningeweza kuuawa kwa kosa la kutomzalia mfalme" alinyamaza ghafla, baada ya kusikia vishindo vya mtu akiwa anakuja.
"Haaa! kumbe ni walinzi wanaangalia usalama" alizungumza Malkia, huku akiachia tabasamu hafifu. "Huyu mfalme unaemuona mwanangu, hana uwezo wa kumpa mwanamke yeyote yule ujauzito. Madaktari wanamfichia tu aibu. Anaua mabinti za watu bure, yeye ndo mgonjwa. Kwanza aliyewaokoa majuzi hapa wale mabinti wa nne wasiuawe, nilimpongeza Sana"
"Sijakuelewa hapo mama! Sasa mimi nilitoka wapi?" alidakia Chidumu na kumtwanga mamake swali.
"Tulia mwanangu, hapo ndio nilikuwa naenda kupaelezea sasa. Baada ya kuona mfalme anashida sana ya mtoto, nikaanzisha mahusiano na Daktari wake, tulipendana sana. Akanipa ujauzito, na kisha akamdanganya mfalme mimi ndiye nilikuwa na shida, hivyo amenipa tiba."
"Nasikitika sana mwanangu, utanisamehe kwa dhambi hii ya kukuficha. Nilisubiri mpaka ukue. Hivyo babako ni Dokta Chimati aliyeuawa majuzi hapa ndani kwa kuchomwa kisu. Kisha maiti yake ikafichwa kwenye ilo kabati la chuma"
"Eti unasemaaa.." alipaza sauti Chidumu. Taratibu akaanza kuregea. Mamake akamuwahi na kumdaka. Chidumu akapoteza fahamu akiwa kwenye mikono ya Mamake mpendwa.
Malkia alihangaika huku na kule. Akamlaza mwanae vizuri katika kochi. Akaanza kumpepea mpaka fahamu zikarejea.
"Mwanangu!" aliita malkia, aweze kuamini kama ni kweli kazinduka.
"Naam! mama" aliitika Chidumu, kwa sauti ya chini sana. Huku machozi yakiwa yanamdondoka.
"Ulipatwa na nini mwanangu?" malkia aliuliza. Lakini Chidumu hakujibu, aliendelea kulia tu. "Usilie mwanangu wa pekee, niambie umepatwa na nini?" alizidi kusisitiza malkia. Basi Chidumu ambaye ndie binti mfalme, aliyafuta machozi take, na kuanza kusimulia.
Alisimulia kila kitu. Alianza siku ile alivyowaokoa wale mabinti wanne. kisha na yeye akajeruhiwa begani. Hakuishia hapo, akaeleza alivyoenda kwenye chumba cha Dokta Chimati kutibiwa. Anamalizia jinsi alivyomchoma kisu na kumuweka kwenye kabati la chuma.
"Sikujua kama ni Baba!" alipaza sauti kwa uchungu binti mfalme, huku machozi nayo yakizidi kumchuruzika. Malkia alishindwa kujizuia. Machozi njia mbili mbili aliyaachia yamwagike, yakalowanisha mashavu take na kudondoka kwenye vazi lake nadhifu la rangi nyeupe.
Mama alimkumbatia mwanae, na kujaribu kumtuliza. Haikua kazi nyepesi, "Mwanangu usimwambie mtu yeyote siri hii, endelea kumuheshimu mfalme ka Baba yako" Malkia alimsihi mwanae. Chidumu aliyafuta machozi, akasimama na kuelekea lilipo kaburi Dokta Chimati. Baada ya kugundua ukweli kwamba yule ndie Babake na sio mfalme wa ardhi ya Omulenga.
Alipofika, alipiga magoti mbele ya kaburi ilo. Akaikusanya mikono yake kwa pamoja huku akisema, "Nisamehe sana Baba yangu. Sina amani katika nafsi yangu. Moyo wangu wote umepigwa na barafu la huzuni, umekufa ganzi. Najua kwamba nimekosea, nimikosea saana Baba yangu."
"Nazungumza maneno haya huku wingu kubwa la simanzi likiwa limegubika anga ya maisha yangu. Huku mvua kubwa ya masika ya machozi, ikiwa inamwagika na kulowesha kichwa cha mashavu yangu. Machozi ya kwikwi na kekevu za hapa na pale, zimeulemaza uwezo wangu wa kupumua, achia mbali uwezo wangu wa kuona. Bali na hayo, mashavu yangu yamegeuka nyanya mbivu. Najionea imani Baba."
Kuzungumza alishindwa, akabaki analia. Huku akiwa amekilaza kichwa chake juu ya kaburi.
_____________________________________
JE NINI KITAENDELEA?

NTAGAMBI.......12
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA KUMI NA
MBILI.
(12)

"Nenda Baba yangu, Nenda. Nenda salama. Nenda kahojiwe. Nenda kapatane na munkari. Nenda tu maana sina jinsi. Umeniachia historia pana na ndefu ambayo kamwe sihitaji kuikumbuka. Taswira ya sura yako ya upole inautesa mtima na akili yangu. Kinachoniumiza zaidi, ni mimi mwanao kuuondoa uhai wako."

"Mapigo ya moyo nayo yameridhia nilie kwa simanzi. Yanapiga na kukifanya kifua changu kipande na kushuka kama mahadhi ya ngoma ya Baikoko. Wapi na lini nitapata Baba kama we we? Jibu sina." alizidi kulalamika kwa huzuni binti mfalme. Akiwa anazivuta kamasi zake. Akasimama akiwa amejawa na hasira, dhidi ya mfalme na ardhi ya Omulenga. Akajiapiza anabadili mfumo wa maisha yake. Kwa yeyote atakayetofautiana nae, atajuta kuzaliwa.

Taarifa zilimfikia Mfalme Bunini. Kwamba kuna kijana yupo gerezani, lakini yuko tayari kupambana na kuhakikisha anawapata waharifu hao. Wanaouwa na kuchoma miili ya Askari. Naam! Mfalme alibariki. Akasisitiza kama atafanikiwa basi atafutiwa adhabu yake ya kifo.
Ntagambi alishangaa geti la gereza linafunguliwa. Akaitwa, alishtuka. Mapigo ya moyo yalimuenda mbio, akajua wasaa wake wa kufa kwa mateso umewadia. "Masikini ya Mungu, ndio naenda kunyongwa hivyo" alinong'ona Ntagambi, machozi nayo yakimsindikiza kuelekea safari yake hiyo ya mwisho, hapa Duniani.

Jambo usilolijua, ni sawa na usiku wa giza. Naam! ndivyo ilivyokuwa kwa Ntagambi. Alipewa maelekezo ni nini cha kufanya. "Adui wanafanya mauaji tunaomba uwalete hapa, itapendeza ukiwafikisha wakiwa hai" sauti hiyo ilijirudia mara kadhaa katika masikio ya Ntagambi. Ni kazi aliyopewa kuitekeleza.

Alipewa askari wa kutosha, pamoja na silaha. "Sasa tusubiri, giza liuvamie mji kidogo ndio tuanze kazi" alizungumza Ntagambi, akitoa maelekezo kwa kikosi chake. Awamu hii ule upanga alipokabidhiwa na mamake, hakujua ulipo. Na hana kumbukumbu ni wapi alipouacha kwa mara ya mwisho.

Ntagambi aliomba dakika kadhaa, akaone kaburi la mamake. Lakini alizuiliwa, kwa lengo la kupambana kwanza. Adui nao walipata taarifa kwamba wanatafutwa, wakajiami na kuweka mitego yao vyema kabisa.

Binti mfalme ni siku ya nne sasa, haonekani nyumbani. Mfalme aliona Kama kaibeba Dunia katika mabega yake. Aliahidi kwa gharama yeyote ile binti yake lazima apatikane. Ntagambi akapewa tena jukumu la pili amtafute yule ampendaye yaani binti mfalme.
Kiza kilianza kuuvamia mji taratibu. Ntagambi akaona ni wasaa mzuri kwake, kuanza utekelezaji wa jukumu. Alipewa askari wa kutosha. Wakaanza msako katika msitu huo ambao ni tishio. Kimya kilitawala, sauti ya wadudu na ndege baadhi walisikia wakilia katika viota vyao.

Umakini zaidi ulihitajika kuliko nguvu. Unamtafuta adui usiyemjua. Walitembea kwa mwendo wa kunyata. Ukimya wa msitu huo, uliwaogofya. Walifika sehemu kuna miti miwili mirefu. Kamba ilifyatuka ikiwa imefungwa mapanga matano makali.
"Laleni chini haraka!" alipaza sauti Ntagambi. Lakini alichelewa, askari kama watano walifyekelewa mbali vichwa vyao.

"Eeh! hii mbona ni hatari!" alijisemea mwenyewe Ntagambi, akiwa anatazama huku na kule. "Naombeni kila mtu ashike kikamilifu panga, na mkuki wake" alifoka Ntagambi
Mishale ilianza kumiminwa kama mvua. Ntagambi akachanganyikiwa, na asijue ni wapi mishale hiyo inatoka. Wakikwepa mitatu, mmoja unatua kifuani kwa mmoja. "Tutalala chini, na kutambaa kwa kutumia tumbo, mithili ya nyoka. Ni marufuku kuinua kichwa" alitoa maelekezo Ntagambi.

Kwa mbali Ntagambi aliwaona mabinti wanne, wakiwa na mapanga zaidi ya mawili mkononi. Lakini mmoja alikuwa ameificha sura yake. Ntagambi akaamulu wawazunguke kwa nyuma, basi wakafanya hivyo. Walipofika tu eneo ilo, moto mkubwa ukalipuka. Dua zisizokuwa na utaratibu zilisikika hapa na pale. Askari wengi walijitahidi kujinasua katika moto huo. Vilio kutoka ndani ya moto vilikua vingi. Sauti za askari hao waliokuwa wakiteketea kwa moto zikaanza kupungua. Moto pamoja na roho zilizokuwa zikiupigania uhai, moto ulishinda. Askari waliungua vibaya. Majivu na weusi ulitanda eneo ilo.

Ntagambi aliumia sana. Roho za walioteketea kwa moto, ziliangusha chozi lake. Akakivua kile kitambaa alichofunikia uso wake asitambulike. Akayafuta machozi, na kukivaa tena kitambaa hicho. Waliamua wajifiche sehemu mpaka kutakapopambazuka.
Hakuna alieweza kusinzia, kila mmoja alihofia maisha yake. Walibadilishana mawazo, huku kila mtu akitoa pendekezo, ni namna gani wafanye. Wapo waliokata tamaa, kwa kusema "Tunaowatafuta sio binadamu wa kawaida" lakini Ntagambi aliipinga vikali kauli hiyo.
Saa kumi na mbili na nusu za asubuhi, Ntagambi aliongoza msafara. Wakazidi kusonga mbele, panga zilikuwa juu, tayari kwa kukata kichwa chochote kile, ambacho kingejitokeza mbele yao. Upande wa pili wa msitu huo. Watu walisikika wakilia, watoto walilia kwa uchungu. Mapanga yalipigwa Kama ala za muziki. Ntagambi na askari wake wakaanza kusogea taratibu, kwa tahadhali kubwa. Walifika katika bonde miili ya wafu ilikuwa imetapakaa. Wakasimama na kuchunguza kwa makini, wakagundua tayari miili hiyo ni kweli ni wafu.
Kulikuwa kuna mitumbwi midogo kando ya mto. Ilikuwa ikitumiwa na wavuvi, kuvua samaki. Wakachukua mitumbwi kama kumi wakajaa askari wote. Wakavuka kuelekea ng'ambo.

Walitumia dakika thelathini, wakawa wamefika nchi kavu. Ile wanashuka wakasikia mwenzao mmoja anapiga kelele, wanageuka wanakuta anavutwa kuelekea ndani ya maji wakajua ni mamba. Kumbe ni maadui zao walikuwa wamezamia chini ya mto huo.
Ntagambi na jeshi lake waliposogea mbele zaidi, na kuuacha mto huo. Mabinti wale waliibuka na kuanza kuwanyelemea kwa nyuma. Naam! hapo sasa mitego ikawekwa sawa. Wakapeana ishara. Binti mmoja akatokeza na kupiga yowe. Ntagambi na jeshi lake wakageuka na kuanza kutimua mbio kuelekea alipo binti huyo. Aisee! walijuta kwanini wamemfata binti huyo. Kamba zilizokuwa zimetegwa katika miti zilifyatuliwa, wakaanza kufungwa ovyo, huku wengine zikiwabana shingo mpaka kufa. Walitoa sauti za muungurumo kama njiwa. Walilikoroga wenyewe wakalinywa kwa nguvu.

Ntagambi alichoka mwili mpaka akili. "Ni watu gani hawa! kwamba nishindwe kuwapata, nirudi nikanyongwe" alijiulizai, akasonya kwa hasira. Akasema haiwezekani. Akaushika upanga wake vyema na kuwaambia wenzake sasa hakuna kurudi nyuma. Naam! moto uliwaka, ardhi ikawa nyekundu sababu ya damu zilizotapakaa. Maadui wawili, wenye roho mbaya. Wakakutanishwa na umahili wa kutumia panga vyema.

Hali ya mfalme ilizidi kuwa mbaya. Kutokupatikana kwa binti yake, na askari kuuawa, kulimuongezea presha. Alikuwa hoi bin taaban, si wa uji wala chai. Mguu mmoja kaburini, mwingine kitandani. Akaulaani ujana kwa kosa la kutodumu. Akatamani kama angelikuwa na nguvu angelienda kupambana mwenyewe. Akakumbuka enzi za ujana wake, jinsi alivyompindua mfalme Chibwengele. Akasikitika kuona ujana ni Kama moshi ukienda hauji.

Ntagambi akakutana uso kwa uso, na maadui zake. Hapa mitego haikuwa na nafasi. Askari wakisubiri amri kutoka kwa Ntagambi. Panga zikaanza kutembea, Damu ziliruka, vilio mbali mbali vilisikika. Ukilegea tu unakutana na panga la shingo. Zilikuwa ni dakika thelathini za machozi, jasho na damu.

Ntagambi panga liliruka pembeni, akaanza kutumia ngumi. Aliiamini sana ile ngumi yake ya kushoto. Ikitua kwenye shavu la mtu, meno kuanzia matatu utayaokota chini. Askari waliuawa ovyo. "Hawa wanawake mbona wakatili sana" alijiuliza Ntagambi. Baada ya kurusha ngumi yake ikadakwa kwa dharau, na mkono laini wa mtoto wa kike.

"Ayaaaaaaaaa...!!" alipaza sauti Ntagambi kwa hasira. Akaanza kutembeza panga kama kachanganyikiwa hivyi. Aliwakatakata vibaya mabinti watatu, wakafa papo hapo. Akabaki na binti mmoja. Mafundi wa kutumia panga, walisumbuana, wakachoka. Kila mtu hakuwa na uwezo wa kurusha hata ngumi. Walikuwa wakiema kwa fujo. Ntagambi akafunua kile kitambaa alichoficha uso wake. Na yule binti nae akafunua cha kwake pia.

"Eeeeh.! wote wawili walishtuka, mithili ya mtu aliepigwa na kipande cha barafu usoni. Ntagambi hakuyaamini macho yake. Alipomuona binti mfalme akiwa mbele yake.
_____________________________________

JE, NINI KITAENDELEA?
received_153933766528024.jpg
 
NTAGAMBI.......13
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA KUMI NA
TATU.
( 13 )

ILIPOISHIA...

"Ayaaaaaaaaa...!!" alipaza sauti Ntagambi kwa hasira. Akaanza kutembeza panga kama kachanganyikiwa hivyi. Aliwakatakata vibaya mabinti watatu, wakafa papo hapo. Akabaki na binti mmoja. Mafundi wa kutumia panga, walisumbuana, wakachoka. Kila mtu hakuwa na uwezo wa kurusha hata ngumi. Walikuwa wakiema kwa fujo. Ntagambi akafunua kile kitambaa alichoficha uso wake. Na yule binti nae akafunua cha kwake pia.

"Eeeeh.! wote wawili walishtuka, mithili ya mtu aliepigwa na kipande cha barafu usoni. Ntagambi hakuyaamini macho yake. Alipomuona binti mfalme akiwa mbele yake.

ENDELEA NAYO
"Kwanini nilikuwa napigana na mtu naempenda?" alijiuliza Ntagambi. Binti mfalme machozi yalianza kumdondoka. Ntagambi akamsogelea na kumkumbatia. Kitendo hicho kilimfanya binti mfalme ahangue kilio kizito. Ntagambi nae, akashindwa kulizuia chozi lake, akaamua aliache limchuruzike.

Wakiwa bado wamekumbatiana. Ntagambi alianza kusimulia kila kitu. Kuanzia ile safari yake ya kuelekea wafwa. Kwenda kutafuta dawa ya mfalme. Alipoeleza jinsi alivyokutana na binadamu wa hatari wenye miguu mitatu. Chidumu alishangaa sana, na kuuliza alinusurika vipi. Ntagambi alijibu vyema kabisa.

"Nakupenda sana Chidumu. Leo siamini kama nimepata wasaa wa kukumbatiana na wewe" alizungumza Ntagambi.

"Nahisi mimi nilikupenda kabla yako. Niliamini ipo siku moja tutaonana. Na ndio leo, mpaka mimi kuwepo msituni hapa kupambana ni kwaajili ya kukuokoa wewe. Lakini tukajikuta tunapambana tena, mimi na wewe. Mfalme atakiwi kuwa hai mpaka sasa." alilalamika kwa huzuni, binti mfalme.

"Kwanini unasema asiwe hai? alisema nikibahatika kukupata, nafutiwa adhabu ya kunyongwa. Twende kabla giza halijauvamia mji" alizungumza Ntagambi.

"Siko tayari kurudi kwa sasa. Sina huruma nae yule, Sio Baba yangu" alifoka kwa sauti binti mfalme.

"Unasema!?"alidakia Ntagambi, akiwa amekenua kinywa chake kwa mshangao. Chozi lilianza kumdondoka Chidumu, akalifuta kwa kutumia kiganja chake. Kisha akamueleza Ntagambi Kila kitu. Alipoanza kuelezea jinsi alivyomuuwa Babake, bila ya yeye kujua, alilia sana. Ntagambi alimtuliza, huku akimuegemeza katika kifua chake.

Ntagambi, alikata miti, akajenga kijumba kidogo chini ya mti mkubwa. Kwa ndani alitandaza matawi ya miti. Kilipendeza, mtu akipita asingeweza kujua kama kuna kijumba pale. Chidumu alifurahi sana, akaona tayari ndoto yake imekwenda kutimia.

Kuna moto ulikuwa unawaka sehemu, akaufata na kuusogeza karibu. Kwaajili ya kufukuza wanyama wakali. Kiza kilitanda, Chidumu akaingia ndani ya kijumba hicho kupumzika. Ntagambi akabaki nje dakika kadhaa akiangalia usalama, kisha nae akaingia.

Ilikuwa ni usiku wa pekee. Usiku ambao hakuna miongoni mwao alioutegemea, si Ntagambi wala Chidumu. Walihisi wako ndotoni, lakini ukweli haugeuki. Ntagambi aliunyoosha mkono wake na kuanza kumpapasa Chidumu kifuani. Miguno ya mahaba ilisikika kupitia kinywa kitamu cha binti mfalme. Walikuwa wakijikunja huku na kule mithili ya nyoka. Wakakumbatia kwa nguvu.

"Nakupendaaaa..!!" ilikuwa ni sauti ya mtetemo kutoka kwa Chidumu.

"Nakupenda pia, mahabuba wangu!" alijibu Ntagambi. Huku akiwa anaiondoa suruali ya Chidumu.

"Ntakupenda! da...da.. daimaa" alishikwa na kigugumizi Chidumu, baada ya utamu kumzidia. Ntagambi nae alizondoa nguo zake zote. Kilichofatia baada ya hapo, hakistahili hata kusimuliwa. Havikuwa vilio vya huzuni vilivyosikika. Bali ni vilio vya furaha. Maneno matamu yalisikika, kila mtu akisifia uhodari wa mwenzake. Katika vita hiyo, iliyofanyika ndani ya kijumba cha miti.

"Asante!, asante saaaana, umeniweza. Umenipeleka ulimwengu wa mbali" alisifia Chidumu, akiwa anahema juu juu. Akimfuta Ntagambi matone ya jasho yaliyokuwa yamelizunguka pua lake.

Baada ya vita hiyo isiyoumiza, waliangaliana usoni kisha wakatabasamu kwa pamoja. Uchovu wa mapigano ya mchana, ongeza uchovu wa vita ya sirini usiku. Matokeo yake wakapitiwa na usingizi mzito.

Ndege wenye sauti za kupumbaza, walikuwa wakilia, huku sauti zao zikipishana kwa utulivu kabisa. Ilikuwa ni asubuhi, mwanga wa jua ukapenya kwenye miti ya kijumba hicho. Na kufika pale alipolala Ntagambi. Ndipo akashtuka kwamba tayari kumekucha.

"Nahisi njaa laazizi wangu!" alizungumza Chidumu kwa sauti ya upole. Ulikuwa mtihani mzito kwa Ntagambi. "Nafanya nini sasa? jukumu lote la kuhakikisha mtu huyu anakuwa salama, liko mikononi mwangu. Ngoja nione namna ya kufanya" alijisemea mwenyewe Ntagambi. Akiwa anamtazama Chidumu usoni.

"Nakuja ngoja nikatafute chakula!" aliaga Ntagambi.

"Sawa kipenzi changu!" aliitikia Chidumu. Huku akiachia busu ziiiiiiiito, shavuni kwa Ntagambi. Hakika mahaba yalinoga. Ntagambi alichukua panga akaelekea ulipo mto, akasimama takribani dakika ishirini na tano. Akivizia wale samaki wanaoelea juu. Akiwa anahangaza huku na kule akaona samaki mkubwa akikatiza. Akamchapa na upanga, samaki akakosa muelekeo akamshika.

"Huyu anatosha kabisa, ngoja nimuwaishe" alinong'ona Ntagambi, akiwa anazipiga hatua kuelekea kule kwenye kijumba chao. Alivyofika tu Chidumu alimrukia na kumkumbatia, kwa furaha tele. Kisha akampokea samaki.

"Sijui tunampika vipi! vifaa hatuna!" alihoji Ntangambi.

"Wewe tulia, subiri kula, hii kazi niachie mimi" alidakia Chidumu, huku akitabasamu. Chidumu alibahatika kupata elimu, hivyo ana utaalamu wa vitu vingi. Alichukua vijiti viwili, akavifikicha mpaka ukapatikana moto, akamchoma samaki. Ntagambi akatoa pili pili zilizojiotea zenyewe porini, akampaka samaki. Alikuwa mtamu sana, walikula huku kila mtu akisifia upande wake. Mara oooh! mimi ndie nimemchoma vizuri. Ntagambi nae akivutia upande wake kwamba kavua samaki mzuri.

Walipomaliza kula, Ntagambi alikata miti mingine. Na kuendelea kuimarisha kijumba hicho. Maana anga lilikuwa limechafuka. Muda wowote ule, mvua ingeshuka. Na kuicharaza vyema ardhi hiyo. Akiwa anaendelea na zoezi ilo, alishangaa kuona askari wengi wakiwa na silaha. Alijua wazi kwamba ni binti mfalme pamoja na yeye wanasakwa. Japo mfalme Bunini na wasaidizi wake walisemezana kwamba, Ntagambi itakuwa hakupambana. Bali alitumia mwanya huo kutoroka, wakasisitiza lazima apatikane.

Ntagambi alishuka juu ya mti. Akaingia ndani ya kajumba kao, akaufunga mlango na kutulia tuli. Askari walipita bila kujua kwamba, hapo kuna makazi ya watu wale wanaowatafuta. Ntagambi akachungulia katika upenyo mdogo. Akashuhudia askari wakizidi kutokomea.

"Mmh! sasa nimepumua. Hawa wapuuzi wangetuona" alizungumza Ntagambi, akiwa anahema sababu ya kujawa na hofu.

"Hata wangetuona, wasingetuchukua kirahisi kama unavyodhani!" alijibu binti mfalme, Kisha akacheka.

Mfalme wa ardhi ya Omulenga, alikata tamaa kabisa, ya kumuona tena mwanae. Malkia pia kila muda alikuwa akilia. Hakuzoea mwanae kukaa siku zote hizo bila kurejea nyumbani. Aliwaza mengi, likiwemo la mwanae kufariki.

Baada ya miezi minne kupita. Chidumu alianza kujisikia kuumwa. Hakujua tatizo ni nini, chuchu zilianza kuvuta na kuwasha, maumivu ya tumbo. Aliwaza sana ni wapi atapata dawa. Hali iliendelea kubadirika, matiti yalivimba na kukua. Akijisikia kuchoka muda wote. Akawa anakojoa mara kwa mara. Ila alipokoswa hedhi, ndipo alipogundua kwamba ana ujauzito. Alifurahi Sana, akatabasamu huku akilibonyeza tumbo lake.

ITAENDELEA
 
@moneytalk mambo yamenoga huku.
 
NTAGAMBI.......14
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.

SEHEMU YA KUMI NA
NNE.
( 14 )

"Mpenzi wangu wa pekee! katika hii Dunia. Nina mimba yako!" alizungumza Chidumu, kwa sauti ya upole. Akiwa anamtazama Ntagambi usoni. Ntagambi hakujibu kitu, alikodoa macho yake kwa mshangao, kana kwamba anatazama filamu ya kutisha.

"Najua unajiuliza tutaishi vipi! sasa nisikilize, nimeamua mwenyewe, niko tayari kwa kila jambo litakalo tokea. Sitakuwa tayari kuifanya chochote mimba hii, mpaka nitakapojifungua," alizungumza Chidumu, akiwa amemkazia macho Ntagambi.

"Kama ulikuwemo ndani ya akili yangu. Asante sana kwa kauli yako ya kishujaa" alizungumza Ntagambi, akamkumbatia Chidumu kwa nguvu, Kisha wakatabasamu kwa pamoja. Siku hazigandi baadhi ya wahenga walikwisha nena hivyo. Mimba ya Chidumu ilizidi kukuwa, alibagua vyakula. Ikawa ni mateso kwa Ntagambi, aliwaza namna ya kupata vitu anavyohitaji mpenziwe. Alifika mpaka sehemu za hatari, akafanikiwa kupata matunda yanayoongeza damu kwa mjamzito. Aliyachuma ya kutosha, mengine akiyaweka katika mifuko yake ya shati.
Hatimaye miezi tisa ilitimia. Maumivu ya tumbo, pamoja na mgongo viliongezeka. Akahisi kama viungo vya mwili vinaachana. Uchovu ulikuwa mkali zaidi, akaanza kutokwa na maji sehemu za siri. Zilikuwa ni dalili za uchungu, kwa Chidumu. Akawa anahangaika huku na kule. Analala, anakaa, yaani ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, akayang'ata meno yake kwa maumivu makali.

"Wahhh.! wahhh..!! wahhhh...!! wahhhhh" sauti ya mtoto mchanga akilia, ilimstusha Ntagambi, pale alipokuwa amesimama. Akatimua mbio kuelekea ndani ya kijumba chao. Chidumu alikuwa amejifungua. Akamkuta akiwa amechoka sana, mtoto akimlaza juu ya kipande cha nguo. Alianza kumsaidia, akamsafisha mtoto vizuri na kumlaza pembeni. Ntagambi alifurahi baada ya kuona wamepata mtoto wa kiume.

Chidumu alikuwa anaendelea vizuri kabisa. Alitabasamu pindi alipokuwa akimtazama mwanae usoni. Ntagambi akapendekeza jina la mtoto, akaitwa Nyamitwengoli. Naam! wote walilibariki jina ilo la mtoto wao wa kwanza. Giza lilipoanzia kulitawala anga. Ntagambi alijiaanda akauchukua upanga wake, aende kule katika ardhi ya Omulenga. Akaibe japo nguo za kumstili mtoto, na vyakula.

"Kumbuka umeniacha mimi na mwanao. Kuwa makini" alisisita Chidumu, akiwa anamuaga Ntagambi. "Sawa kuwa na amani, kipenzi changu" alijibu Ntagambi. Alifanikiwa kutuwa vyema, ila kwenye miti alikumbana na matangazo yenye sura yake kwamba anatafutwa. Picha hizo zilichorwa kwa rangi. Katika vipande vya ubao. Ilikuwa ni ishara ya hatari sana, katika ardhi ya Omulenga.

"Nifanye kwanza kilichonileta! kuhusu hizi picha za mimi kutafutwa, nitazishughulikia baadaye" alijisemea Ntagambi, akiwa anaanuwa nguo katika kamba ya nyumba ya jirani na shamba la mfalme. Ile anaondoka kuna askari alimuona akaita wenzake, na kuanza kumkimbiza.

"Eeeh! mbona umahema hivyo?" aliuliza Chidumu.

"Yaani wee acha tu! nimefukuzwa na askari kama kumi, manusura wanikamate. Ila nilijificha kwenye mti, nilichowafanya nimefyekelea mbali vichwa vyao. Lakini mmoja alikimbia huku akidai anaenda kutoa taarifa kwa mfalme, kwamba kaniona nilipoelekea" alizungumza Ntagambi. Mapigo ya moyo yakimuenda mbio. Na kukifanya kifua chake kipande na kushuka.

"Mpaka sasa tunavyozungumza, eneo hili si salama tena kwetu tuondoke" alishauri Chidumu. Wakakusanya mizigo yao na kuianza safari. Tayari palikuwa panaanza kupambazuka. Walitembea umbali mrefu sana. Walikuwa wakichoka wanatafuta kivuli na kupumzika hapo. Sababu Chidumu alikuwa bado anamaumivu ya uzazi.

Kuna sehemu walifika, wakasimama na kuanza kushangaa mandhari iliyowapagawisha. Ni pori ambalo limepakana na Gwenkulu upande wa magharibi, Chiboyali na Sungusisi upande wa kusini na Ochwenkelesi upande wa mashariki.

Ziwa la Wamuwasu kaskazini, ambalo ndilo ziwa kubwa kuliko yote Nchini Bunini. Maji ya ziwa ( Wamuwasu ) ni baridi yasiyo kuwa na magadi. Vile vile ni pori linalopatikana kutoka usawa wa bahari mita 1,140. Hakika ni pori lenye mandhari nzuri, yenye kupendeza kama vile majabali ya mawe na vilima vyake vya hapana pale, yaani linaitwa pori la Nyamuwabho.

"Waooo! pazuri sana hapa, kama bustani ya Eden," Chidumu alizungumza, akiwa anakunywa maji yanayotiririka kwenye miamba. "Hakika panastahili, wapendanao kama siye, kuweka makazi hapa," alisema Ntagambi, kwa furaha tele aliyokuwa nayo huku akiwa anambembeleza mtoto.

Ntagambi hakutaka kupoteza muda. Alitafuta mahali palipotulia. Juu ya mwamba mmoja ukiwa umenyooka vyema kabisa. Pembeni yake kulikuwa na mti mkubwa sana. Basi Hapo ndipo Ntagambi alijenga kajumba safi kabisa na imara. Kwa kuunganisha miti, akatengeneza sehemu ya wao kulala, ikiwa juu kidogo. Kuhofia wanyama na wadudu wanaotambaa chini. Katika huo mti palikuwa tulivu kabisa, hakukusikika sauti ya ndege yeyote ile. Utulivu huo ulimvutia sana Ntagambi.

Jua lilianza kufifia, na kuliachia anga kwa aibu. Kiupepo cha wastani kilikuwa kikipuliza. Ntagambi aliwasha moto, akachukua vile vyombo alivyoiba. Akakoroga uji, ulivyoiva akammiminia Chidumu katika kikombe. "Eeeh! uji mtamu, japo hauna sukari" alisifia Chidumu, akiendelea kuubugia uji huo. Kiza lilichanganyia, pori zima likamezwa na kiza hicho. Ntagambi walimaliza kula ugali na samaki. Akajipongeza na kuubariki wizi huo, uliompa vitu hivyo vya kupika.

"Waahhhh.! wahhhh.! waaahhh!" mtoto alikuwa akilia kwa uchungu, kana kwamba ameng'atwa na mdudu. Ntagambi alihangaika kubembeleza mpaka akachoka. Wakaanza kupokezana yeye na Chidumu. Mtoto alivyonyamaza tu, Ntagambi akaona kwa mbali mwanga wa moto, kuchungulia vizuri akaona watu wakiwa uchi wa mnyama. Walipofika karibu, akaona kama wawili wakiwa wamevaa matambara yaliyokuwa yamechanika. Macho yao yalikuwa yameingia ndani. Walikuwa wanatia huruma.

Ntagambi aliogopa. Chidumu hofu ikamkumba, akamkumbatia mwanaye. Huku akijisemea kama ni kuuawa basi auawe na mwanaye. Ntagambi akaushika upanga wake, kwaajili ya kuitetea familia yake. Msafara huo wa watu walioshika visiki vya moto. Ulifika pale kwenye ule mti mkubwa, uliopo pembeni ya kijumba cha Ntagambi. "Masikini ya Mungu! tumekwisha" alinong'onga Ntagambi, huku akiwa anachungulia kwenye kaupenyo kadogo alikounganisha miti miwili.

Bibi kizee aliye mtupu kabisa, alianza kuwazunguka wengine kutoka kushoto kwenda kulia na kutoka kulia kwenda kushoto. Alikuwa akinuiza maneno ambayo hata Ntagambi hakuweza kuyaelewa yanamaanisha nini. Akaanza kuwagusishia kwenye makalio yao kibuyu kilichozungushiwa shanga nyekundu. Akatoa hirizi kubwa imefungwa kitambaa cheupe na cheusi. Ikizungushwa kwenye pembe la ng'ombe. Ilikuwa ni kama inapumua. Walikuwa wamebeba damu katika vibuyu kumi na viwili. Wakaanza kuinywa, walivyomaliza tu, jeneza likashuka toka juu ya mti huo. Wakaingia wote, kisha jeneza hilo likapotelea katikati ya mti huo.

Ntagambi na Chidumu, walikuwa wakiyashuhudia mauzauza hayo. Tumaini likatoweka, wakajwa na hofu juu ya usalama wao.

"Wahhhhhh.! Wahhhhh" mtoto alilia tena kwa sauti ya maumivu. Lakini awamu hii tumbo lilikuwa likivimba, pamoja na miguu. "Uchungu wa mwana aujuaye mzazi" Chidumu alishindwa kuvumilia, nae akaanza kulia. Ntagambi akawa na jukumu la kuwabembeleza wote wawili.

JE HIZO NDIO DAKIKA ZA MWISHO, MTOTO HUYO KUUPIGANIA UHAI WAKE? UNGANA NAMI SEHEMU INAYOFUATA.
 
Mmh mimi haya mambo ya watoto kuteseka tena jaman ntashindwa japo ni hadithi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom