Simulizi: Ntagambi (1 _ 12)

0713417189

Member
May 12, 2021
98
150
NTAGAMBI.......18
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )
0622 738 310.
Tanga.


SEHEMU YA KUMI NA
NANE.
( 18 )

ILIPOISHIA......
Ntagambi alifika mbele, akakutana na mto mkubwa. Akawaza na kuwauza. Akisema asimame atashikwa, akaamua apite. Ile farasi anaruka kuingia katika mto huo, mtoto aliteleza kutoka kwa mamaye aliyekuwa bize na upanga. Akatumbukia mtoni.

ENDELEA NAYO.......
"Wewe endelea na safari, mimi naingia mtoni kumtafuta mtoto!" ilikuwa ni sauti kutoka kwa Ntagambi. Aliruka mtoni akamchukua mtoto, alikuwa hoi bin taaban. Alikunywa maji ya kutosha. Akaanza kumminya tumbo angalau aweze kumpa haueni mtoto.

Chidumu alisonga mbele akiwa analimwaga chozi lake. Hakuamini Kama kamuacha mwanaye akiwa ametumbukia mtoni. Kila sekunde alikuwa akigeuka nyuma, mpaka akaumaliza mto huo. Ntagambi hakuwa na lakufanya alitoka ndani ya mto, askari wakawa wamefika. Wakaanza kumchapa na nyaya, walimpiga kila Kona ya mwili wake, akajikuta amemuachia mtoto na kudondoka chini. Ntagambi alilia na mtoto alilia pia.

Chozi la mtoto halikumgusa askari yeyote yule. Bali waliendelea kumsulubu Ntagambi.

"Hahahahahahaha..." alicheka kwa dharau askari kiongozi, mguu mmoja akiwa ameuweka juu ya kichwa cha Ntagambi.

"Mnaniumiza!" alilia kwa sauti Ntagambi. Lakini hakuna aliyemjali ni kama dua la kuku lisilompata mwewe.

"Yaani wewe umetusumbua sana, tueleze alipoelekea binti mfalme!" alihoji askari, huku akiwa anamtandika Ntagambi mgongoni.

"Nisogezeeni mwanangu, nimbembeleze!" aliomba Ntagambi.
"Unasemaje? huyu mtoto tunamuuwa mbele yako" alijibu askari, kisha akacheka na kumtazama yule mtoto.

"Ni bora mkaniua mimi, kuliko mwanangu!" alijitetea Ntagambi.

Hakuna aliyemsikiliza Ntagambi, mijeledi iliendelea kutuwa katika mgongo wake. Wakampiga na kitu kizito kichwani damu zikaanza kumchuruzika mithili ya kuku aliyekatwa kichwa.

"Mnaniuwa!" alilalamika Ntagambi.

"Funga mdomo mchafu huo!" alifoka askari. Ntagambi akajaribu kurusha ngumi, askari akaidaka, kisha akamtandika teke la tumbo.

"Ohiiiiiii..!!" alipaza sauti ya uchungu Ntagambi.

"Tutakufikisha mbele ya mtukufu mfalme ukiwa mfu!" alitoa amri kiongozi wa askari. Kauli hiyo ilimuumiza sana Ntagambi. Macho yalivimbiana, machozi na jasho vikaungana kuuchafua uso wake. Alijitahidi kuinua kichwa amtazame mwanaye, lakini maumivu yakamzidia.

"Naenda kunyongwa namuacha mwanangu!" alijisemea kimoyomoyo Ntagambi, huku maumivu yakikatiza kwa kasi katika mwili wake. Alivyofikiria kuwaacha Chidumu na mwanaye, nguvu zilimuijia akajikuta amekwapua upanga wa askari na kuanza kupambana.

"Mapambano yalikuwa makali, panga zilitembea, damu zikiruka huku na kule. Wingi wa askari ukamuelemea Ntagambi. Akajikuta kazungukwa akiwa amedondoka chini na kushindwa kuamka. Chuma alichopigwa nacho mgongoni ndicho kilifanikiwa kumpeleka chini.

Mikono ililegezwa, Ntagambi hakuweza kushika kitu chochote kile. Akabaki analia kama mtoto. Nyimbo za ushindi zilisikika kutoka vinywani mwa askari. Waliinua silaha zao juu huku wakizidi kumuadhibu Ntagambi.

"Wewe si ni mbabe, uko wapi ujeuri wako?" alihoji askari. Lakini Ntagambi hakujibu kitu, alikuwa ameyang'ata meno yake, akiashiria anakabiliwa na maumivu mazito.

Ntagambi alipoyainua macho yake, anakuta mwanaye kaning'inizwa kichwa chini, miguu juu. Mtoto alilia Sana. Ntagambi hasira zilifukuta ndani ya mtima wake. Akatamani asimame na kupambana, lakini mwili haukuwa na nguvu hata chembe.

"Mbona hawafiki hawa?" alijiuliza Chidumu. Uwoga ulianza kumuingia, akahisi baridi angali jua kali likipiga. Akaona nafasi ya kukutana na wapendwa wake wakiwa hai ni ndogo sana. Akajilaumu nafsini mwake kwamba, ni kwanini alikubali kuondoka pekee. Alipomkumbuka mwanaye, chozi lilidondoka pasi ya kupigwa.

"Naomba msinipige, mmeniumiza vya kutosha!" alilalamika Ntagambi. Pamoja na ujasiri aliokuwa nao, maumivu yalimuelemea. Akazidi kusikitika baada ya kusikia askari hao, wakisemezana kwamba lazima wamfikishe kwa mfalme akiwa mfu.

"Wahhhhhhh.! Wahhhhhh" mtoto alilia kwa uchungu. Walikuwa wamembeba vibaya. Sauti hiyo ya kilio kutoka kwa mtoto, ilipenya masikioni kwa Ntagambi, ikamuumiza sana, nakusikia kama ikimwambia aamke apambane. Ila maumivu aliyokuwa nayo asingeliweza kulishika hata panga.

"Mvuteni chini huyo!" alitoa amri askari. Basi waliendelea kumvutia chini, alichubuka mgongoni, kwenye mikono na sehemu mbalimbali za mwili wake. Alipochapwa na kipande cha mti katika uso wake, hapo ndipo alipolia kilio kikuu.

Kwa jinsi mtoto alivyokuwa amebebwa, ni asilimia ndogo sana za kutambua kama bado yupo hai au laaah!. Ilikuwa ni safari ngumu na ya kilio kwa Ntagambi. Ujasiri na nguvu alizokuwa nazo, hazikuweza kumsaidia kwa wakati huo.

Ilikuwa bado mwendo kidogo tu waweze kuikanyaga ardhi ya Omulenga. Askari walizidi kupiga kelele za ushindi. Wakatamani wangelikuwa na mbawa, wangelipaa na kufika haraka kwa mfalme. Ntagambi aliutamani uhai lakini uhai ukawa mbioni kuchomoka.

Alipoinua kichwa Ntagambi, kwa mbali aliona Jengo la mfalme. Alilia sana, huku akijisemea mwenyewe kwamba, "Sasa nimekwisha". Zilibaki kama mita mia wafike, Ila mbele kidogo alionekana binti akiwa ameificha sura yake kwa kutumia blauzi yake. Ndani ya sidilia zilionekana titi changa zilizochongoka mithili ya mdomo wa kuku. Tumbo lake dogo lililotuna kwa mbele kiasi, mkono wake wa kuume alikuwa ameshika panga. Naam je ni nani huyo na analengo gani.

*"Kupata muendelezo wa simulizi hii, nione kupitia nambari, 0622 738 310.
Kwa shilingi 3000/=
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom