SIMULIZI: Nilipata nafasi ya kuongea na Gurus wawili wenye mitizamo miwili tofauti kuhusu Kuzaliwa, Kifo na uwepo wa Mungu pamoja na Dini

Khs kitabu nmeelezea hapo juu na comment mbili zilizotangulia kabla ya hii.

Ofcoz nmeshajua kwa nn nlifail, kuna energy fln wengine hatujazaliwa nazo pia kuna energy fln unaweza kuwa nayo ya kufanya watu muhimu wakupotezee tu, hio situation ni hatari kuliko ya kwanza. Unaweza kukuta umewekewa hio expelling energy bila kujua au ulizaliwa nayo, either way inabidi ufanye juu chini aidha kuitoa ama kuweza kuipurify hapo ndipo utakuta watu wanaenda kanisani kuombewa ama kwa waganga lkn wababe wengine wanatumia 'Cultivation' japo inahitaji discipline sana
Kuna energy watu wanakurushia ili kukuzuia katika Mambo mbali mbali. Muhimu kufahamu namna ya kuzitoa izo nguvu bila kuzuia. Vipi unaweza kushare izo Mbinu za kuondoa nguvu hasi ambazo watu uzirusha kwa wengine.
 
Kuna energy watu wanakurushia ili kukuzuia katika Mambo mbali mbali. Muhimu kufahamu namna ya kuzitoa izo nguvu bila kuzuia. Vipi unaweza kushare izo Mbinu za kuondoa nguvu hasi ambazo watu uzirusha kwa wengine.
No mkuu bado sikufikia huko. Hio elimu ni ndefu sana
 
Hello bosses....... Nimekaa na hii experience kwa muda mrefu ila leo nikakutana jamaa fln wanabishana khs dini nimeona ni bora niisimulie labda inaweza kusaidia. Ni story ndefu ila nitajitahidi kufupisha na pia sina uzoefu sana kuandika makala za namna hii hivyo kiswanglish na typos tutavumiliana.

Baada ya janga la Corona makampuni mengi yameamua kuchukua utaratibu wa 'Work From Home' hii ilifanya wafanyakazi wengi kwenye nyanja ya technology hasa hasa programming, pentesting na designing kufanyia kazi makwao. Silicon valley(Center of tech in USA) ilibakiwa na ofisi tupu nyingi kwa sababu ya hili jambo. Basi maampuni mengi yakaanza kutumia sana mitandao maalum kama vile zoom, github etc.. ili kufanikisha kazi zao na mikutano. Mwaka 2021 mwanzoni nikapata mdau mmoja online yeye alikua ni Senior Software developer kwenye kampuni fln la usafiri USA (jina kapuni) akaanza kunipa mentorship na namna ya kufanikiwa kucrack interviews mbali mbali ili kupata kazi coz baada ya kuanza remote working makampuni mengi yaliamua kuanza kuajiri watu 'remotely', yaan mfano kama ww ni designer au programmer unaotea tu chance then unatuma CV na project zako then wakikukubali mnafanya interview kupitia ZOOM meeting, ukicrack hio interview basi unapewa kazi. Niliamua kutafuta mentor coz nilifail interview 3 in a row na zote nilifail hatua ya mwisho tu (Hio face to face interview kupitia zoom). Hivyo ikawa lazima kuwa na mentor wa kizungu ili anisaidie na kunipa mentorship. Ila namna nilivyompata hadi akanikubali ni story nyingine lkn leo nitawasimulia kama title inavyosema...


Huyo mentor (tumuite Mr C) ni mzungu (info inatosha kuhusu yeye) niliwasiliana nae kwa kupitia DM kwenye forum fln hv lakini ilichukua miezi miwili hadi akaja kunijibu. Baada ya hapo tukaanza kuwasiliana sana kupitia DM ya hio forum na emails. Baada ya kumset vizuri na akakubali kuwa mentor tulianza kufanya kazi baadhi pamoja, alikua ananitumia vitabu baadhi ambavyo vingenisaidia kuwa deep zaidi kwenye hii field yangu ya software development.

Sasa siku moja akanitumia vitabu vitatu kimoja wapo kilikua ni cha mambo ya Spirituality, hiki kitabu kiukweli kilikua ni very addictive. Baada ya kukisoma kwa juujuu nilimuuliza kwenye email ".........Why did you send ........" jamaa alinambia "Were you not rejected 3 times in a row ?, that book is an integral part of your key to cracking any of your future interviews no matter where & when". Sikudadisi zaidi coz sio vizuri kumdadisi mentor wako, ni bora uangalie kama anachokwambia kitakusaidia na hakipo nje ya principle zako kisha utaona kama ukifuate au kukiacha kimya kimya.

Jibu lake lilinipa hamasa sana ya kusoma hicho kitabu kwa sababu najua niko vizuri sana kwenye kazi yangu na nmefanya projects nyingi sana nikiwa kama freelancer, sasa kwa nini nakataliwa na huwa napita steps zote hadi mitihani yao navunjavunja lkn mwisho hizo meeting na hao HR wa kizungu natolewa njee? Nikiangalia nina hamu kweli ya kufanya kazi za Software kwenye kampuni ya kizungu hasahasa zenye chimbuko lao Silicon Valley coz skills zangu zinaruhusu hilo, lkn kwa nini nakataliwa?

So nikasema potelea pote ngoja nianze kusoma hiki kitabu. Sasa nilichokikuta humo aisee... Sijawahi kufunguliwa macho kiasi kile tangu nijitambue.... Sisemi kama nilikubaliana na yalioandikwa humo. Lakini yalikua yanashawishi sana. Baada ya kuona falsafa za kwenye hicho kitabu nikajikuta naanza ku-question sana imani ya dini yangu. Lakini mie nimezaliwa na hio dini na ni dhambi kufanya hivyo (kutokana na dini, inaitwa kukufuru) so nikaamua kuachana na hicho kitabu. Baada ya wiki mbili nikajikuta na-miss kusoma zile concepts ikabidi nikirudie, The more I read, the more I felt going against my faith & the more I had confidence on my own abilities. Daah baada ya wiki akili ikarudi kwenye imani yangu nikasema this time sikisomi tena, So nikachukua maamuzi magumu nikakifuta kwenye storage yangu na nikafuta ile email message alonitumia hivyo vitabu kutoka kwenye inbox yangu. I regret this coz ningeweza kukishare na nyinyi hapa, na mbaya zaidi nakiita kitabu coz kinadeserve kuwa kitabu lkn actually ilikua ni kama Academic Paper fln hivi wanazoandika scholar (wahusika mtanielewa) ambayo haikuwa officially published.

Ila kuna muda nikawa bado nakikumbuka na natamani tena kukisoma coz kiukweli kimetaja practices ambazo baadhi nilishajaribu kuzitumia (sio exactly zilivyo ila from my memory) na zikanipa effect kubwa ambayo sikutegemea hata kama effect ingekua kubwa kiasi hicho. Baada ya siku kadhaa nikafikiria nikaona ni bora nichukue zile practice na beliefs ambazo haziendi kinyume na principles zangu coz baadhi ya practice na beliefs kutoka kwenye kile kitabu zimeleta matokeo chanya na pia baadhi naziona zikitumiwa na watu maarufu wanapoongea au kufanya kazi zao (iwe sanaa, siasa, technology etc....) ili kupata ushawishi na mafanikio.

Baada ya kukikumbuka hicho kitabu nikatamani kumrudia yule mentor anitumie tena. Kiukweli nilifikiria sana sababu ya kumwambia ili anipe tena ile PDF ya hiko kitabu lkn baada ya kufikiria sana, (huku mafunzo baadhi ya kwenye kile kitabu yakizidi kunikalia akilini, na polepole rohoni) nikaamua kumwambia reason halisi bila kumdanganya. Niliamua kumwambia hivyo kwa sababu mbili Kwanza nilijua ni mtu mwenye akili saana coz ni wale developer (computer programmer) ambao hawafanyiwi interview bali wanaalikwa kupewa kazi, yaani wanaombwa wakafanye kazi sehemu hio. Pili kwa nilichokiona kwenye kile kitabu Page ya Authors haikuwepo so nadhani ilikua imekatwa coz page number zilizo pale chini imeruka kutoka v (5) hadi vii(7) nikimaanisha page vi(6) haikuwepo yaan imekua cut-out. Hio niliigundua coz nna tabia ya kuandika quotes na kuhighlight kila interesting fact ninayosoma, so lazima nijue page number. Hio imenifanya kuwa lazima napitia page number kabla au baada kusoma page fln ya kitabu. So nikiwa na observation hio wakati nafikiria reason ya kumwambia akilini kwangu nikabet kwamba inawezekana jamaa ni mojawapo ya authors wa hio makala na hakutaka nijue. Kiukweli I have been making Computer Systems tangu nikiwa teenager so I have dealt with many Ifs.....and elses....... kutokana na hilo pia nikaunganisha factors nyingine na mwisho wa siku nikaja kubashiri huyo jamaa ni moja wa authors by 90%.

Nilimtumia email khs kazi fln ambayo alinipa na baada ya kuireview akanijibu then nikamtumia hilo ombi la PDF. My mentor akanambia hv "Why resending it, dont tell me your antivirus doesn't work" akimaanisha kwamba nisimwambie imeliwa na virus kwamba antivirus yangu haifanyi kazi (We're tech guys so we use techie jokes). Nikamjibu kwamba niliifuta na nikampa detailed answer ya sababu za kuifuta pia nikamwambia nafikiri yy ni author wa hio paper. Jamaa hakujibu kwanza akaniuliza kwa email fupi mno akitaka kujua kwa nn nasema yy ndo author. Nikampa deduction yangu kama nilivyoelezea hapo juu. Kiukweli jamaa hajawai kuni-appreciate hata kwenye kazi nlizokua nafanya nae lkn akasema hakudhani kama ninge-note hio kitu kuhusu pages na flow ya deduction yangu ilikua 'somehow cool'. Mwisho akasema hawezi kunitumia tena coz inaonekana sijamatch na hizo philosophy zilizomo mule na hio itapelekea kunipoteza zaidi ya kunijenga, ni bora nibaki kwenye njia niliopo coz nayo inaweza kuwa sahihi (utaelewa maana yake hapa mbeleni kdg). Aliongezea kusema kwamba "kama kuna vitu baadhi ulivisoma na unavikumbuka tutakua tunadiscuss hivyo hivyo nikipata muda" (in english, nmetafsiri ili ieleweke) mwisho akamalizia "Coding all the time is boring, atleast we've got some new stuffs to talk about"....... Baada ya hapo tukaendelea na issue nyingine na sikumlazimisha sana akitume tena coz hata kuniruhusu tu kuongea nae khs hizo issue ilikua tyr ni nafasi kubwa sana kwangu.

Nikisema niweke mambo yote tuloongea na tunayozidi kuongea khs Spirituality na baadhi ya issues kwenye kile kitabu nitajaza Database bure, ila napenda niongelee mambo baadhi nlojifunza kutoka mule na kutoka kwenye mtazamo wake. Huyu Yeye ndiye namuita Guru wa kwanza na ni Taoist mzuri tu. So concepts zake nyingi utazikuta kwenye Taoism pia. Guru wa pili sitomsimulia zaidi namna nnlivyokutana nae lkn yeye imani yake aisee iliniacha ubongo wazi. Kiufupi kabisa yeye anasema binadamu inabid tupigane na miungu coz wanatula( they feed on us). Yaan hii cycle ya life and death imetengenezwa ili kuipa miungu hio nguvu. Chukulia wewe unavyokuwa na kuku wanazaliana ili uwale. Hii concept nitaielezea tukifika huko, ila kwa sasa nitaongelea concept ya dini hizi zilizopo kutokana na maoni ya Guru wa kwanza.


1)MTAZAMO WAKE KUHUSU UWEPO WA MUNGU NA DINI.
Huyu jamaa yeye anaamini uwepo wa Dao au Tao. Hii ni njia/way ya maisha ambayo ndio inaendesha kila kitu duniani. Haielezeki na haionekani na haishikiki. Kwa maana nyingine kwenye hizi dini utasema ndio Mungu. Kuna msemo kwenye Taoism unasema "The Dao that can be explained is not eternal Dao" Hii inamaanisha chanzo na kiendeshi (Dao au tuseme Mungu au Nguvu Kuu) haielezeki wala haishikiki, na ukiweza tu kuielezea basi inakua sio tena Dao. Yaani kama wewe ni mkristu na ukiweza kumwelezea namna Mungu wako alivyo au anachotaka basi huyo sio Mungu tena, same kwa dini zote. Anasema kwamba kitu kikubwa duniani ni ku-align na nature wala sio kufuata written rules & dogma, yaan kufuata natural order. Kuna energy fln ambayo ipo kwenye nature, hio inaitwa nascent energy. Wachache wanaweza kuiabsorb kutoka kwenye nature. Ukiwa na hio energy unaweza kufanya baadhi ya mambo na hata ukaweza control fikra za wengine(viumbe, wanyama au roho zilizopo kwenye nature) . Kuna practices nlizokua nasemea ndizo zinahusika hapa ili kuvuta na ku-absorb hio energy. Sasa ukishapata hio energy na ukaweza kui-control na kui-manipulate ndipo utaweza kuwa na uwezo fln ambao baadhi hawana. Wengine wamezaliwa na kiasi kadhaa cha hio energy na ndo hawa unakuta wana extra-ordinary talents au wanaweza kuongea na spirits etc...........

Sasa hio energy ni kama reward fln au favor kutoka kwenye nature. Anaiita reward coz kuna mda nature(Dao) inaweka hio energy kwa kiumbe kinachozaliwa au kuanza safari yake kwenye universe, pia anaiita reward coz kuna muda nature inaweka hio energy kwenye kiumbe baada ya hicho kiumbe kufanya practices fln zinazo(ki)align kiumbe hicho na nature/Dao. Mfano kuna aina ya hio nascent energy ambayo mtu/kiumbe akiwa nayo basi anakua na mvuto fln wa ajabu. Unaweza kushangaa mtu kila akipita watu waamuangalia, au kila akiomba kazi watu wanamkubalia, au kila akiongea watu wanamsikiliza etc....... Sitotoa mifano hai khs hizo occurences coz ni wazi tunaona watu ambao wanamvuto tu ghafla yan. Hapa ndipo ilipokuwa sababu ya huyo mentor kunitumia kile kitabu coz kama nilivyosema nilikua nimekosa kazi mara 3 mfululizo japo napita skills test zote ila Face to Face interview inanitoa nje...


Hapo juu nlisema khs watu kubishana khs ipi dini ni sahihi, kutokana na maono ya huyu mentor yeye anasema wote tunaseek/ tunatafuta hio energy kwa njia mbalimbali. Kwa kuwa hio energy ndio chanzo cha mafanikio sehemu mbalimbali basi watu wako radhi kufanya juu chini ili kuipata. Kutokana na huyo mentor anasema ukikuta watu wapo kanisani wanaomba ujue wana sababu, aidha wanataka kuishi zaidi, kuwa na mali mingi etc...... Pia ukikuta watu wanaabudu shetani (so called) au wanafanya uchawi (sorcery) ujue wanatafuta hio hio energy kwa namna yao wanayoona inafaa. So kiufupi kabisa kutokana na huyo guru(mentor) ni kwamba wote wanaoomba mali, mafanikio, wake wazuri etc... wote wanaoomba hio energy lkn kwa namna tofauti tofauti na pia hio nascent energy inajidhiirisha kutokana na namna unavyoimanipulate wewe. Hapo juu nimesema kuna vitu viwili khs hii energy, Kui-absorb(kuinyonya ikaingia kwako) na kui-manipulate (yaan kuitumia namna fln fln ili ifaye kazi baadhi). Tuongezee kitu cha tatu "Kuicontrol ikae mwilini mwako ili isije ku-backfire na kukuletea madhara", too much money, too much fame tumeona zilivyotupotezea remarkable people hapa duniani, ni mfano tu wa ku-backfire.


Somo khs hii energy ni gumu na refu sana lkn jamaa alisema kwenye ile makala kwamba kuna aina kuu mbili za hii energy moja ni Pure nascent energy na ya pili ni Impure nascent energy. Pure ni ile ambayo ukiipata unaweza kuimanipulate ikafanya kazi zaidi ya moja, hii inaweza kuwa transmitted kwa kufuata baadhi ya practices, impure ni ile ambayo iko specific kufanya mambo fln na haiwezi kuwa transmitted kwa namna yyt. Hii impure pia inaweza kutokea pale mtu mwenye pure nascent energy akaimanipulate na kumuingizia mtu mwilini mwake ili ikafanye specific job tu. Hili somo la hio energy ndilo linalokuja kuelezea pia uwezekano wa mambo yote ambayo kwa kawaida tunaona hayaendani na laws of physics kama vle uchawi, etc.. au tuyaite Metaphysics.

Kitu ambacho alinishangaza ni kwamba kwa wale wanaojua physics ni kwamba hii energy ina uhusiano mkubwa sana na magnetism (usumaku), japo alinambia kuelewa uhusiano uliopo ni ngumu sana na inahitaji akili ya ziada. Ila kwa wale wenye experience na mambo ya majini au spirits kuna vile vifaa vinavyotumika kugundua existence ya hivyo viumbe na vingi hutumia compass (usumaku) au mizani fln hv maalum ya madini kama ya chuma (magnetic materials) coz hivo viumbe vina pattern fln ya nascent energy inayoweza kuwa detected namna hio. Mshana Jr Sijui hapa niko sahihi au nilipigishwa chenga.


So uwepo wa dini yeye haupingi lakini anasema ni njia mbalimbali tu zinazopoint sehemu moja. Nilisema kuna mahala nliposoma hicho kitabu nikawa na confidence sana na uwezo wangu binafsi coz mule alielezea baadhi ya practices ambazo ukizifanya hautakua na ulazima wa kupitia kwenye dini au cults ili kupata unachokitaka (just a form of nascent energy). Coz hizo practices zitaku-align na nature na kisha utapata nascent energy kama reward.

Kwa maelezo yake ni kwamba sie tuko kwenye ecosystem, ni kama food chain. Chanzo cha nishati ni Jua lakin hio hio nishati ambayo ni jua ndiyo unakuja kuila kama dinner au supper coz inakua tyr ishafanyiwa manipulation na kuwa in another special form. Huwezi achama mdomo ukasema unakula jua, lakini kila unapokula tunda lolote wanasayansi watakwambia unakula energy ambayo chanzo chake ni Jua. refer Photosynthesis. The same inaapply kwa hii nascent energy. Mtu ukiwa unaenda kanisani kuomba mali ujue in other ways unaenda kuomba nascent energy fln. Sasa inategemea kama hio source yako itakupa access kweli ya hio energy.

mwisho wa hio part alisema basically kuna aina mbili tu za kupata hio nascent energy. Moja ni Direct access, ambapo mtu anafanya practices ili kujialign yeye kama yeye moja kwa moja na Nature(Dao), hii haihitaji intermediary (dini, cults, shetani, etc....). hapa mtu anafanya kitu kinaitwa 'Cultivation' ambayo huuhusisha meditation na kusoma. Watu ambao wako addicted na hii njia wengi utawakuta wanajiita Atheists. Ila kiukweli kuna namna wanafanya kupata hio nascent energy either kwa kujua au kutokuajua coz ndio energy of nature, Cc with all due respect Mr Kiranga . Njia ya pili ndio hii Indirect ya kutumia dini au cults mbalimbali ambamo wanaamin viongozi wao wanauwezo wa kupata hio energy, kuimanipulate na kuwawekea waumini wao. Hio njia ya pili ndiyo imetutengenezea fujo sasa kwenye jamii coz kila mtu anataka njia yake ionekane ndio sahihi japo kiukweli zote zinapoint kwenye Sehemu moja. Rejea mfano wa energy ya Jua, Food chain na ecosystem.


Nikipata muda nitaendelea ila kwa sasa nlipanga kusema hayo ili kuondoa haya mabishano kuhusu dini coz kiukweli wote tunapoint sehemu moja ila ni maamuzi tu ya njia gani ya kutumia

.... Ciao.
~ kali linux
Uko sahihi kwakuwa kila kilichopo kwenye uso wa dunia kinachoonekena kwa macho ya nyama asili yake na chanzo chake ni rohoni.. In fact ni replica ya kiroho

Uvutano uunao kwenye sumaku uko hata kiroho na ndio maana huvutiwa kumpenda mtu ama kumchukia at first glance

Mizani nayo ni hivyo hivyo kati ya kundi la watu ukapewa ugawe vitu kuna ambao bila sababu utajisikia kuwapunja ama kuwapendelea ama kuwapa kabla ya wengine wanaostahili
 
Uko sahihi kwakuwa kila kilichopo kwenye uso wa dunia kinachoonekena kwa macho ya nyama asili yake na chanzo chake ni rohoni.. In fact ni replica ya kiroho

Uvutano uunao kwenye sumaku uko hata kiroho na ndio maana huvutiwa kumpenda mtu ama kumchukia at first glance

Mizani nayo ni hivyo hivyo kati ya kundi la watu ukapewa ugawe vitu kuna ambao bila sababu utajisikia kuwapunja ama kuwapendelea ama kuwapa kabla ya wengine wanaostahili
Nilitaka kuendelea na maoni ya wale wazungu lkn mods wameuweka huu uzi mahala ambapo sipo.

Moderator hii sio riwaya rudishen jukwaa la Intelligence
 
Kwa uelewa na nijuavyo. Hapa inafanana na Christian, mambo ya powers of nature, metaphysics, binarbeats, waves. In Christianity source of positive power is Jesus Christ. The power of attraction, power of positive connection. Jesus Christ ndie chanzo cha positive energy. Ukijiconnect utafanya mashangao.
 
Back
Top Bottom