Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 152,886
- 453,430
Mtunzi Ally Katalambula
Sehemu ya 01
Jina langu naitwa Sofia ni mama wa mtoto mmoja. Katika familia yetu, mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, wadogo zangu wawili wote wakiwa ni wavulana. Nilitokea kwenye familia masikini, familia ya mzazi mmoja, yanii mama tu, ingawa kwa sasa naye tumekwisha mzika.
Kuhusu baba, yeye hatukuwahi kumjua wala kumwona maishani, ingawa mama alitueleza baba alikuwa ni raia wa nchi ya Nigeria ambaye alikutana naye kijiji cha Ntumbatu mkoani Morogoro alikokuwa akijishughulisha na ulanguzi wa viazi vitamu na kuvisafirisha jijini Dar es salam.
Mama anasema, baada ya kukutana na baba yetu raia wa Nigeria, penzi lao lilikuwa motomoto, kiasi cha kutosikia la muadhini wala mnadi swala, penzi liliponoga zaidi, akaamua kuhamia kijiji cha ntumbatu ambapo ndipo yule bwana alikokuwa akiishi.
Mama aliendelea kutusimulia kuwa, baada ya wazazi wake kupata habari kwamba yupo kwenye uhusiano na raia wa Nigeria, walimkanya kwa kumtahadharisha ajichunge na wageni kutoka nchi za mbali, hususani Afrika Magharibi kwani wanaume wengi wa huko ni matapeli.
Lakini kutokana na utamu wa penzi la baba yetu, mama aliweka masikio pamba, raha ya penzi ikamfanya anenepe na kuiona dunia yote ni yake.
Kama wasemavyo waswahili, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, kufumba na kufumbua mama akajikuta amezalishwa watoto watatu na yule bwana.
Uzazi wa kila mwaka ukaifanya haiba ya urembo wake kunyauka, mama anasema, miaka michache baada ya kutuzaa sisi, tukiwa angali wadogo kabisa mwanaume huyo alimuaga alimwambia kuwa alikuwa amepata simu kutoka kwao, kwamba wazazi wake walikuwa wamefariki, akamwahidi akishamaliza mazishi ya wazee wake angerejea tena Tanzania kutuchukua ili tukaishi nchini Nigeria.
Mama akabikia na matarajio hayo. Yule bwana alivyondoka hakurudi tena. Hadi leo amebakia kuwa historia.
Mama anasema baada ya hali hiyo, ghafla maisha yalibadilika, akaogopa kurudi kwao, kwa kuwa awali aliwapinga wazazi wake juu ya tahadhari waliyompa. Ndipo kuanzia wakati huo mama akawa na jukumu moja tu. Kupambana kwa kila hali kuhakikisha watoto wake tunaishi maisha mazuri .