Simulizi: Mchawi

Jamaa anaudhi sana...

Binadamu mwenyewe anayemuhangaikia anamuacha kitandani anakwenda kulala na jirani...

Kuna binadamu wanasikitisha sana... Ngoja tuone.
.


Cc: mahondaw
 
Sehemu ya 53

Moyoni sikukubali kuona naonewa vile, nilipanga kwenda popote koya yote ya dunia kuutafuta uchawi hata nchini Nigeria ili kuhakikisha naupukutisha ukoo wao wote.

Kwa uchungu wa kumpoteza baba yangu na mwanangu nilikuwa radhi kufilisika lakini nihakikishe nimelipa kisasi cha mla mbuzi kulipa ng’ombe.

****
Mwezi mmoja baada ya kifo cha mwanangu, katika kuulizia sehemu gani kuwa waganga wakali. Jamaa yangu mmoja pale kazini aliyekuwa dereva wa magari makubwa aliyeaminika kwa ushirikina, ambaye alijiamini sana hata alipofanya makosa hakufukuzwa kazi. Nilimfuata na kumuuliza jeuri ile anaipata wapi.

“Kazala maisha kuangaika, nimeteseka sana, walimwengu si watu. Haki yangu mwenyewe ilinifanya nipoteze mke na watoto,” Kanyenye alinieleza kwa majonzi.
“Haki yako ipi na tukio hilo limetokea lini?”

“Miaka saba iliyopita ilikuwa miaka miwili kabla ya wewe kuja kufanya kazi hapa. Baada ya kupata kazi nilidunduliza vijisenti ambavyo nilipeleka kijijini kwetu kununua shamba. Nilifanikiwa kununua shamba ambalo nilikodisha watu kunilimia. Baada ya muda nililetewa taarifa kuwa jirani yangu kaingia eneo langu.

“Nilifunga safari hadi kijijini kuonana na jirani yangu, jamaa alikuwa kama alikuwa ananitafuta. Baada ya kufikishana serikali ya kijiji na kumshinda, aliapa kunionesha. Baada ya muda nilianza kuandamwa na mabalaa magonjwa vifo vya mke na wanangu kwa mpigo.

“Huwezi kuamini nimezika watu watatu kwa mpigo, vifo vyao vilipishana kwa masaa, nilitaka kuwa mwendawazimu lakini nashukuru Mungu alinipa nguvu.
“Hakuishia hapo, nami akanilaza kitandani kwa miezi mitatu nikiwa sijui nini kinaendelea.

Nimekwenda kuponea Mlandizi sehemu moja inaitwa Disunyala kwa mtaalamu mmoja ambaye ndiye aliyeninyanyua kitandani.

Ila alikataa kuua, alisema yeye anatibu tu. “Nilimshukuru kwa msaada wake baada ya kupona vizuri, nilitafuta waganga wa kunilipizia kisasi wengi walichemka, ilionekana jamaa kajidhatiti.

“Ndipo nilipo mpata jamaa mmoja aliyenielekeza kwenda sehemu moja ipo ndani kidogo ya nchi ya Msumbiji inaitwa Silver Makua. Kwa vile nilitaka kulipa kisasi niliuza sehemu ya shamba langu na kumfungia safari. “Nilipitia Mtwara kuingilia boda ya Namoto mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Nilitumia usafiri land lover za kizamani na kufika kwenye kijiji hicho. Nilifanikiwa kuonana bibi mmoja mzee sana. Baada ya kumweleza na yeye kuangalia aliniambia atanisaidia.

Usiku wa siku ule nilichimbiwa shimo na kufukiwa nakabakia kichwa nje.
“Nilikaa nje peke yangu mpaka asubuhi huku fisi na wanyama wa kutisha wakipita karibu yangu bila kuinifanya kitu.

Bundi walitua juu ya kichwa changu bila kufanya kitu na kuondoka. Nilipewa masharti nisipige kelele kwa chochote nitakachokiona. Bila hivyo vitu nilivyoviona usiku ningekufa kwa presha. Kazala uchawi upo na unatisha.

“Alfajili ya siku ile nilinyweshwa dawa nikiwa bado sijafukuliwa baada ya kunyweshwa nilifukuliwa na kuoshwa. Kisha lipelekwa kwenye makaburi na kupewa kisu nichome katikati ya kaburi nilifanya vile.
Baada ya zoezi lile niliambiwa naweza kuondoka.”

“Basi huo ndiyo uganga uliofanyiwa baada ya kusafiri umbali mrefu?”
“Yule bibi aliniambia, hakuna wa kuniua nitakufa kwa amri ya Mungu na kila aliyeshiriki kuiua familia yangu lazima na yeye atazikwa.

Nilirudi nyumbani, wiki moja baada ya kurudi familia ya jirani yangu ilianguka kama kuku wa mdondo, hivi sasa nyumba na shamba limebakia gofu wanaishi paka na popo.”

“Aisee naomba na mimi unipeleke,” nilijikuta nikiwa na hamu ya kwenda huku ambako niliamini ndipo fanaponifaa sana.

“Ni muda mrefu lakini nitakuelekeza, ukifika pale kijijini jina la yule bibi ni maalifu sana hakuna asiyemjua, Ulizia Nyangunda.”

“Hakuna tatizo mwisho wa mwezi nikipokea mshahara nitaomba likizo lazima nami niendende nikawabakize watu nyumba zao magofu waishi paka na popo.”

Japokuwa sehemu niliyotaka kwenda ni mbali lakini nilijua ile ndiyo dawa niliyokuwa nikiitafuta. Muda wa kumaliza msiba ulipofika mama alihamia kwenye nyumba yangu mpya na kukaa na mkwewe na wajukuu.

Moyoni nilibakia na siri nzito ambayo sikutaka kumweleza mtu yeyote, kwa vile vita ile ilikuwa siri yangu, basi niliendelea kuifanya siri yangu bila familia yangu kujua kilichokuwa kikiendelea.

Nilijipanga kwenda Silver Makua kutokana na maelezo ya Kanyenye safari yake japokuwa ilikuwa ya nchi jirani lakini zilikuwa zinahitajika siku tatu, ya kwanza unaishia Mtwara siku ya pili unafika unapokwenda tena mapema saa tano asubuhi kama ukiwahi kuondoka alfajiri.

Baada ya kila kitu kukamilika niliomba ruhusa kazini ya wiki nzima, nyumbani niliwaaga nakwenda kuangalia mradi mpya wa kufungua mkoani, walinikubalia.

Niliondoka siku ile jioni na mabasi yanayotoka Mwanza na kufika Dar saa nne usiku, nilala kwenye nyumba ya wageni iliyokaribu wa kituo cha mabasi cha Ubungo ili alfajiri nipande mabasi ya Mtwara.

Asubuhi ya siku iliyofuata niliondoka na basi kuelekea Mtwara ili niunganishe kwenda Msumbiji kwenye mji wa Silver Makua. Niliwasili Mtwara saa kumi jioni sikukaa niliunganisha na magari madogo mpaka Namoto kwa ajili ya asubuhi niunganishe kwenda Silver Makua.

Nililala Namoto Asubuhi ya siku ya pili baada ya kuchenji fedha na kupata za Msumbiji, kutokana na maelezo niliyopewa na Kanyenye lazima niondoke na kijana mmoja pale mpakani anayejua Lugha ya kule kunisaidia kuwasiliana na wenyeji.
Nilimchukua kijana mmoja ambaye alikuwa akizungumza lugha zaidi ya zaidi ya moja. Alikuwa akizungumza kiswahili kireno kitindiga na kingereza cha kuungaunga.

Tulipanda gari dogo kuelekea Silver makua. Nilifika Silver Makua saa tano na nusu asubuhi. Bila kuchelewa tulimuulizia bi Nyangunda kwa kumtumia mkalimani wangu aliyeuliza kwa lugha ya kitindiga.

Tuliambiwa alifariki muda mrefu zaidi ya miaka miwili iliyopita akiwa mzee sana.
Nilianza kuiona nuksi mbele yangu, mzee Kidereko kabla ya kukamilisha kazi yangu alifariki, naye bi Nyangunda alifariki miaka miwili iliyopita. Nilijiuliza nini hatima ya maisha yangu.

Nilimweleza mkalimani wangu aulize kama tunaweza kupata mganga eneo lile.
“Mmh! Kwa hapa hakuna mganga kama yule bibi, baada ya kufa watoto na wakujuu zake walikataa kurithi mikoba yake.” Alijibu na mkalimani wangu alinitafasilia.

“Hakuna mwingine?” niliuliza nikiwa nimekata tamaa baada ya safari ndefu, lakini imekuwa haina matumaini.
“Mmh! Hebu subiri,” jamaa aliondoka kwenda kumuuliza mtu wa jirani aliyekuwea akitengeneza bai, baada ya muda alirudi.

“Sikilizeni, kama mnaweza panda gari mpaka Msibwa Daplaya, pale muulizeni mzee mmoja anaitwa Ngugude, wanasema ni kiboko kuliko hata marehemu bi Nyangunda.”

“Anasema kweli?” nilishtuka.
“Yule mzee kiboko.” Alitujibu yule kijana.
“Amesema yupo wapi?”
“Msimbwa Daplaya.”

“Kuna umbali gani toka hapa?”
“Mwendo wa saa tatu.”
“Kiasi gani?”
“Mnasema mmetokea Namoto?”
“Ndiyo.”
“Nauri yake haipishani sana kama kuzidi ni kidogo sana.”

Tulimshukuru na kuagana na yule kijana, tulielekea kwenye kituo cha basi kilichokuwa mbele kidogo na tulipokuwa. Haukupita muda ilisimama Toyota Coaster iliyokuwa ikitokea Silver Makua.
Baada ya kuteremka abiria zaidi ya watano kituo kile tulipata nafasi ya kukaa. Tulifika Msibwa Daplaya saa tisa alasiri.
Niliteremka na kusogea kwenye duka ambalo alikuwa kijana mmoja, mkalimani wangu aliuliza na kuelekezwa, alinifuata na kunieleza.
“Itabidi tupande baikeli tupelekwe kwa mganga aliyekuwa akikaa nje kidogo ya mji.”

“Hakuna tatizo.”
Tulielekezwa sehemu panapokodiwa baiskeli, tulikodi mbili na madereva wake. Safari ya kutoka nje ya mji ilianza. Tulijikuta tukipanda na kushuka milima huku vijana waliotupakia wakionesha uwezo wa kuendesha baiskeli kwa masafa marefu tena kwenye barabara mbovu.

Tuliingia vijijini vya ndani kwa kutumia muda wa zaidi ya saa moja na nusu. Tulifika kijijini kwa mganga Ngugude saa kumi na moja na nusu.

Kama kawaida mkalimani wangu ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu, baada ya kupokewa na binti mrembo wa kike aliyekuwa amejifunga kaniki na kuuacha mgongo nje. Baada ya mazungumzo ambayo mi sikuelewa anazunguza nini. Baada ya mazungumzo alinieleza tumfuate.

Tuliongozwa kuelekea kilingeni, kilikuwa kiko mbele kidogo ya nyumba nzuri za mganga aliyeonekana kajijenga kimaisha, pembeni ya kilinge kulikuwa na zizi kubwa la ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Tulifika kwenye kilinge kilichokuwa kumezungushwa uzio wa mmea ya minyaa. Tulipoingia ndani ya uzio tulikaribishwa kwenye vigoda, baada ya kukaa aliyetupeleka aliondoka kurudi sehemu aliyotupokea.

Tulikaa kwa robo saa kisha alitoka kijana aliyekuwa amevaa rubega la kaniki na kuzungumza maneno ambayo yalikuwa kama ya Kimakonde huku akiashilia kutuita.

Sikusimama nilimsikiliza mkalimani wangu ili kujua yule kijana anasema nini.
“Tunaitwa ndani,” mkalimani wangu alinieleza huku akinyanyuka.

Nilimfuata hadi ndani ya kilinge na kukaribishwa kwenye ngozi ya chui, tulikaa mbele yetu kulimkuta mzee aliyekuwa amekula chumvi. Kichwa na ndevu zake zilikuwa nyeupe
 
Imekufundisha nini mkuu
Kwanza wakati mwingine ni bora kukubali kuwa mjinga na kumove on, kama jamaa angekubali mkewe hayupo naye tena akafocus na kazi zake taratibu angepona na angepata mke mwingine. Lakini pia nimejua kuwa kumbe ukianza safari za kwenda kwa waganga ndo umeanza yaani safari yako inaweza isiwe na mwisho ukajikuta umefika mpk kuzimu kwa shetani mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom