Simulizi: Kwanini Mimi? 01

SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 07
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611


Tulipoishia -
Mkewe bila ubishi alisimama kuelekea chumbani alikomuweka mtoto.Alifungua mlango na kuingia ndani.Alitoa neti pale kitandani na kumfungua yule mtoto nguo ambazo zilikuwa zimemfunika.Baada ya kumfunua nguo na kumuanglia mwanae ,mke wa juma Alishtuka na kurudi nyuma huku akisema " aaah baba tatuu,baba tatuu,baba tatu"

Endelea nayo.

Sauti ya mkewe akipiga kelele ilimshtua juma .Haraka alisimama na kukimbilia chumbani aliko mke wake." vipi mke wangu.Kuna nini?"

" baa baaa......." mke wa juma alitaka kutamka baba tatu lakini aligairi.

" Niambie kuna nini mke wangu?"

" aaah! Mtoto amenishtua sana.Niliona kama amebadilika"

"Mmmmmmh! Amebadilika imekuwaje? Mbona yupo vile vile? Halafu mbona nimeiona kusikia umemtaja baba tatu? Kafanya nini uyo baba tatu?

" hata sielewi mume wangu.Labda yatakuwa mawazo yangu tu.Maaana alinishtua sana"

" mmmmh punguza mawazo basi mke wangu." aliongea juma kisha akaondoka mle ndani na kumwacha mkewe akimnyonyesha mwanae.

" mmmmh! Hivi nilichokiona ni nini? Mbona kama mtoto alikuwa na sura ya baba tatu? Inawezekana vipi? ,Au hii mimba ilikuwa ya kwake? Mmmh hapana,kama kukutana naye mbona nimekutana naye miaka mingi sana iliyopita.Miaka karibu kumi imepita tangu nilipokutana naye.Sasa inakuwaje leo mtoto wangu awe na sura yake" aliwaza mke wa juma.

Alimnyonyesha mwanae kisha akamlaza kitandani .Akatoka kuelekea barazani.

" lakini mke wangu muda ule unapiga kelele nilikusikia umetamka baba tatu.Nimekuuliza pale umenijibu juu juu tu?"

"Mmmh utakuwa ulinisikia vibaya mume wangu.Mbona sikutamka ivyo" aliongopa mke wa juma.Alijua akisema kuwa alitamka baba tatu .Basi ugomvi ungekuwa mkubwa.

"Ok sawa.Basi tushauriane.Tunafanyaje kuhusu huyu mtoto."

" Tunafanyaje kivipi mume wangu?"

"Maisha yake tu.unajua mpaka sasa hata jina hatujampa?"

" mmmh! Jina si anatoa baba.Mpe wewe jina unaloona litamfaaa."

" Hapana nakupa ruhusa wewe.Amua wewe mwanao tumuiteje"

" Mmmh! Mume wangu huu ni mtihani.Lakini nakumbuka kipindi nipo mjamzito uliniambia kama atakuwa mtoto wa kiume basi utampa jina la baba yako au "

" aaaah aaaaah kumpa jina la baba yule haiwezekani.Mbona ayo yatakuwa matusi makubwa sana.Mzee huko kaburini anaweza kutoka .Tumpe jina lingine tu"

" Lakini ujue yule mtoto ni wakwetu,na anahitaji upendo wetu.Maneno yako ayo inakuwa kama unamtenga.Yaaani saizi hutaki kumpa jina la baba yako kwakuwa tu amezaliwa na matatizo.Hivi unazani akiwa mkubwa halafu akasikia kuwa baba yake mzazi alikataa kumpa jina la baba yake unazani atajisikiaje?"

"Mmmmmh! Sawa mke wangu.MUNGU anakusudi lake katika hili.Acha tumpe jina ilo ilo la marehemu baba.Kuanza sasa jina lake litakuwa ayubu" aliongea juma.Maneno ya mke wake kuwa mwanae akikua atajisikia vibaya yalimwingia juma.

" ok sawa mume wangu,nashukuru kwa upendo."

" usijali.Halafu ule mkia tunaufanyaje? "

" mmmh? mimi sijui "

" mimi naona ni vizuri tukiukata saizi akiwa mdogo .Maana kadri anavyozidi kuwa mkubwa ndivyo unavyozidi kukomaa.Hivyo nazani kesho nitaenda hospital kumuuliza yule daktari vizuri.Kama itawezekana itabidi amkate"

"Ok sawa haina shida.ila mume wangu kiukweli nafsi yangu inaniuma sana."

" kwanini inakuuma.kama jambo limeshatokea ,hatuwezi kulibadilisha"

" kinachoniuma ni kuhusu marafiki zangu.Ujue tangu nimejifungua hawaji kuniona,na wanaokuja wanakuja tu kumuangalia mtoto wangu ili wakanicheke "

" hao ndio binadamu mke wangu.Ni jambo la kawida ilo ,itabidi uzoee"

" mmmh! Sawa.Halafu muda umeenda sana mume wangu.Twende ndani tukalale"

"Aisee mimi silali saiz .Wewe tangulia kalale.

" sawa.Halafu nilitka kusahau kitu.Hivi yule askari aliyetusaidia usiku ulienda kumshukuru"

" daaah! Aisee nilishasahau.Nitaenda kesho asubuhi kumshukuru.Lakini nazani itakuwa vizuri kama nitampa hata elfu kumi kwa ajili ya mafuta.Maana katusaidia sana.Bila yeye ukute saizi tungekuwa tunaongea mambo mengine."

"Sawa,halafu na wale vibaka unampango nao upi?"

" Wale mimi nimewasamehe mke wangu.Unajua hata nikisema niwatafute nilipe kisasi itakuwa haina mana.Watu wenyewe wanatumia madawa ya kulevya .Unaweza kwenda ukasema ukalipe kisasi kumbe ukawa unajitafutia balaaa,unajua mtu anayetumia madawa uwa ajali chochote"

" ok sawa basi mimi naenda ndani kulala" aliongea mke wa juma na kuelekea chumbani.Juma aliendelea kukaa pale barazani akiwaza.Akili yake bado ilikuwa haijakaa vizuri.Aliamua kukaa barazani kwakuwa hakupenda kumuona yule mtoto.

Alikaa pale barazani akiwaza hadi akapitiwa na usingizi pale pale.

.....

Asubuhi ilipofika yeye alikuwa wa kwanza kuamka.Alienda chumbani kwake akajiandaa kisha akamuaga mkewe kuwa anaenda kazini.Akiwa njiani anaelekea kazini alikutana na rafiki yake aitwae rashid ambae anajifanyaga mganga.

" sikiliza juma.Nimesikia kuhusu tatizo lako.Nimeambiwa mkeo amezaa mtoto mwenye mkia.sasa mimi nataka nikusaidie shida yako"

" unisaidie kivipo rashid."

" nina dawa nataka nikupe ambayo utaenda kumwambia shemeji awe anamuogeshea hiyo dawa"

"Iyo dawa itasaidia nini? Maana mwanangu anamkia na pia anasura ya ajabu sana.Sasa tukimuogeshea iyo dawa itamsaidia nini?"

" vyakumsaidia ni vingi.Kwanza ule mkia utamtoka na pia ile sura yake itakaa sawa"

" mmmmh! Rashid mwenzio kichwa changu hakipo vizuri ivyo nakuomba acha hizo habari za dawa"

" aaah kwahiyo utaendelea kuisho naye vile vile bila kufanya lolote?"

Juma hakumjibu .Aliongeza mwendo na kumuacha rashid akiongea peke yake.Akili ya juma haikuwa pale.Alikuwa anawaza mbali sana.Mwili wake ulikiwa pale barabarani lakini akili yake ilikuwa mbali sana.Aliendelea kutembea mpaka akafika kazini kwake.

Kufika tu kazini aliitwa kwenye ofisi ya mkuu wa shirika lao .

" pole na hongera juma.Nimekupa pole kwakuwa mtoto mliyempata anamapungufu fulani,lakini pia nimekupa hongera kwakuwa mtoto ni mtoto tu " aliongea mkuu wake wa kazi.

" asante."

" Nimepata taarifa kuwa mkeo kajifungua mtoto wa kiume.Hivyo hongera sana ndugu yangu.Unajua nimesikia mengi kuhusu mtoto.ila mimi naomba nikuambie kitu kimoja"

" kitu ganii icho?"

" ni kuhusu mwanao.Nataka nikutie nguvu.unajua kila kitu kinatokea kwasababu.Hivyo naomba ujue kunasababu ya wewe kupata mtoto wa vile.Naomba umpende na umpe mapenzi yote.Nina uhakika MUNGU atakusaidia na kukuongoza"

" sawa mkuu nimekuelewa"

" Halafu kitu cha pili ninachotaka kukuambia ni kuhusu kazi yako .Ni hivi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu,tumeamua kupunguza wafanyakazi.Hivyo kuanzia leo.Wewe sio mfanyakazi wa hapa tena.Ukitoka hapa nenda ofisi inayofata kwa ajili ya maelekezo zaidi.Barua yako ya kusimamishwa kazi ni hii hapa."

" aaah lakini mkuu kosa langu ni nini? Kwanini gafla hivi? Kama unavyojua mkuu nina majukumu mazito ,naomba msinisimamishe kazi.Nitaishi vipi bila kazi mimi?"" aliongea juma huku akiwa amepiga magoti lakini hakueleweka.Baada ya kuona jitihada zake zimegonga mwamba.Alisimama na kuelekea chumba cha pili kama alivyoelekezwa kwa ajili ya taratibu za kusimama kazi.

..............

Majira ya saa tisa usiku juma na mke wake walikuwa wamelala usingizi.Mke wake alitega alarm ya simu kuwa ifikapo saa tisa aweze kupiga kelele ili aweze kuamka na kumnyonyesha mtoto.Alitega alarm kwakuwa mtoto wake alikuwa haliii. ilipofika saa tisa ile alarm iliita ,mke wa juma akaamka hili amnyonyeshe mwanae.

Lakini cha ajabu baada ya kuamka.Alimwangalia mwanae pale alipokuwa amelala hakumuona." aaah mwanangu yupo wapi?" aliongea kwa sauti.Alimtafuta kitandani kote bila mafanikio.Alichanganyikiwa na kuanza kupiga kelele," mwananguuuu,mwananguu yuko wapi?"
ITAENDELEA
 
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 08
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611


Tulipoishia -
Lakini cha ajabu baada ya kuamka.Alimwangalia mwanae pale alipokuwa amelala hakumuona." aaah mwanangu yuko wapi?" aliongea kwa sauti.Alimtafuta kitandani kote bila mafanikio.Alichanganyikiwa na kuanza kupiga kelele," mwananguuuu,mwananguu yuko wapi?"

Endelea nayo.

Kelele zile zilimshtua juma." aaah! Wewe mwanamke vipi?,mbona makelele hivi usiku huu?"

" mtoto hayupo?,simuoni mtoto"

" humuoni vipi wakati ulilala naye hapo?"

" Ndiyo nililala naye hapa.ila nimeamka nimnyonyeshe cha ajabu simuoni?"

"Acha masihara.Usiku wa saa tisa atakuwa kaenda wapi mtoto mchanga ambae hawezi kufanya lolote?,hebu pisha hapo niangalie" aliongea juma huku akiangalia pale ambapo mke wake alimuweka.

" mmmmh! Mbona maajabu.Yaaani mtoto ambaye hata wiki hajatimiza anapotea kimaajabu hivi.Hebu shuka kitandani umuangalia hapo chini labda alidondoka"

Walishuka wote kitandani na kumtafuta mtoto mle ndani bila ya mafanikio.Walitoa nguo zote kitandani lakini hawakumuona.Hali ile iliwashtua.Wakawa kama watu waliochanganyikiwa.

" mmmmh! Mke wangu au mtoto ulimwacha barazani ? Maaana haiingii akilini mtoto kupotea.Hebu kamuangalie barazani kwanza"

" sawa ngoja niende ila nina uhakika mwanangu nilikiwu naye huku huku chumbani" aliongea mke wa juma huku akielekea barazan.

Kufika barazan aliparaganya makochi lakini hakuona kitu.Alimtafuta baraza nzima bila mafanikio.Juma naye alikuja barazan kumsaidia kumtafuta.Walimtafuta sana.Baada ya kuona ndani ya nyumba haonekani walifungua mlango na kwenda nje kumtafuta.

" lakini mume wangu,mtoto mchanga yule huku nje atakuwa alifikaje?.kivyovyote vile lazima atakuwa ndani .Me nilikuwa naona tukazane kumtafuta ndani"

"Ndani kila sehemu tumeangalia hatujamuona.Sasa tutaendelea vipi kumtafuta ndani.Wacha tumuangalie na huku nje.Akili yangu inaniambia haiwezekani yule mtoto kutoka mwenyewe lakini katika mazingira yalivyo hakuna jinsi,itabid tumtafute kila sehemu."

" sawa "

Waliendelea kumtafuta bila mafanikio.Pamoja na kuhangaika kumtafuta,Moyoni mwao wote walifurahi.Walitamani kama inawezekana yule mtoto asionekane tena.

" kama amepotea mwenyewe sawa tu.Wacha apotee moja kwa moja.Lakini haiwezekani akawa amepotea.Hapa lazima mke wangu kuna kitu atakuwa amekifanya ,inawezekana akawa amemchukua na kwenda kumtupa chooni" aliwaza juma moyoni.

Wakati juma anawaza ayo.Mke wake pia naye alikuwa anawaza kama vile alivyokuwa anawaza juma."mmmmmh! Haiwezekani mtoto mchanga akapotea mwenyewe kwenye mazingira kam aya.Hapa lazima kuna kitu.Mume wangu atakuwa kamchukua na kwenda kumtupa.Lazima atakuwa yeye" aliwaza mke wa juma.

Kila mmoja alimuhisi mwenzie vibaya.Mke wa juma moyoni alihisi kupotea kwa mtoto wake, mume wake anahusika.Lakini pia Juma na yeye alihisi kupotea kwa mtoto, mke wake anahusika.Hakuna aliyemwambia mwenzake kwasababu kwa namna fulani kila mmoja alikuwa anafurahia ile hali.

Baada ya kuona hapatikani.Waliamua kurudi ndani ." sasa mke wangu sijui tunafanyaje?"

" tunafanyaje kivipi mume wangu?"

" kuhusu kupotea kwa mtoto.Lazima tufanye kitu."

" Bado sijakuelewa mume wangu.unataka tufanye kitu kipi?,"

" ipo hivi mke wangu.Watu wakisikia kuwa mtoto kapotea hawatatuelewa.kila mmoja atazani kuwa sisi tumehusika na kupotea kwake.hivyo ni lazima tutafute kitu cha kufanya ili jamii isituhisi vibaya"

" mmmmh! Lakini kwanini sasa jamii itatuhisi vibaya? ,na ata kama mtoto amepotea .Mtoto si wakwetu .Wao inawahusu nini?"

" unajidanganya mke wangu. Kwa taarifa yako mimba ikitunga tu,tayari yule mtoto anakuwa wa serikali.Japokuwa mimba umebeba wewe na kumlea mtoto unamlea wewe lakini mtoto ni mali ya serikali,ndio maana ukimfanya kitu chochote kibaya mtoto wako unashtakiwa"

" mmmmh!"

" usigune !, ipo hivyo.Sasa tatizo ninaloliona hapa ni jamii kutuhisi vibaya sisi "

" Lakini kwanini watatuhisi vibaya?"

" Watatuhisi vibaya kwakuwa mwanzoni mimi na wewe tulimkataa mtoto.Si unakumbuka pale hospitali wewe ulimkataa mtoto.Na sio wewe tu hata mimi waliponiletea nimuone nilimkataa.Sasa lile lilikuwa kosa.Tukiwaambia hapa saizi watu kuwa mtoto wetu kapotea na wakati kule hospital tulimkataaa hakuna atakaye tuelewa."

" sasa tunafanyaje " alioongea mke wa juma huku akikaa pale barazani kwenye kiti."

" daaaah! Mwenyewe hata sielewi.Maana tukisema twende polisi kivyovyote vile hawatatuelewa"

" mmmh! Hapo hakuna jinsi mume wangu wakituelewa watuelewe na wasipotuelewa wasituelewe hivyo hivyo"

" Sawa halafu nilisahau kukuambia kitu.Mwenzio kazi nimesimamishwa.Na sifahamu kwanini! Kwahiyo kuanzia sasa tulichokuwa nacho kitumie kwa umakini"

," mmm!h! Mbona kama kuna mkosi fulani unatuandama."

" mkosi kivipi?"

" we jaribu tu kufikiria.Wakati tunaenda hospitali tulivamiwa na vibaka.Tumefika hospitl nimejifungua mtoto wa ajabu.saizi na wewe umesimamishwa kazi.Lazima kutakuwa na kitu"

" mmmh! Kama mkosi dawa yake ni ndogo.itabidi tufanye maandalizi, tukafagie makaburi ya wazee na kupika sadaka"

" sawa " waliongea mengi pale barazani.Lakini wakwa kwenye mazungumzo walisikia sauti ya mtoto akilia ndani.

" mke wangu mbona kama sauti ya mtoto chumbani" aliongea juma huku akisimama na kuelekea chumbani.Mke wake naye akamfata kwa nyuma.Kufika chumbani walimkuta mtoto kalala pale pale kitandani.Wote walishikwa na butwaaa na wakawa wanaangaliana wasijue cha kufanya.

"hivi tumechanganyikiwa au ?,yaaani muda wote huu kumbe mtoto alikuwa hapa hapa chumbani"

" mmmmh! Hapana huyu mtoto hakuwa hapa.Alikuwaje hapa wakati hadi shuka la kitanda tulilitoa kumtafuta yeye.Haiwezekani"

"Mchukue mnyonyeshe,si unamuona anavyolia kwa uchungu.itakuwa ananjaa sana."

" Hapana mume wangu .Mimi namuogopa,huyu mtoto atakuwa sio wa kawaida.Anapoteaje usiku na kurudi tena mwenyewe.Hapana mimi naogopa kwakweli"

" acha upumbavu.Kwahiyo unataka afe kwa njaaa au?.Hebu mchukue haraka umnyonyeshe.Tena sasa hivi?" alifoka juma kwa hasira.Mke wa juma hakuwa na ujanja.Alimchukua mwanae na kumnyonyesha. kila mtoto alipokuwa ananyonya, damu ya mke wa juma ilikuwa kama inachemka.Kila mtoto aliponyonya ilikuwa kama kuna kitu flani kinatoka kwenye mwili wake.

" mmmmh! Mume wangu huyu mtoto anavyonyonya nahisi kama damu inachemka,Halafu pia nahisi kama kunakitu kinanitoka mwilini"

" kitu kukutoka mwilini ni kawaida.Mtoto anavyonyonya lazima maziwa yatoke.Hivyo icho unachokiona kinakutoka ni maziwa"

Mke wa juma alimnyonyesha vile vile mwanae .Baada ya muda yule mtoto alipatwa na usingizi akalala.Mtoto alivyolala na wao wakalala.

Asubuhi na mapema,mtoto alianza kulia tena.Mke wa juma alitoa nyonyo na kumpa anyonye.Lakini kama mwanzo kila mtoto alipovuta maziwa mke wa juma alihisi tofauti.Alihisi kama kuna kitu kinamtoka mwilini mwake.Aliendelee kuvumilia lakini mwishowe alishindwa, taratibu macho yake yakapoteza mwanga akaanguka chini kama mzigo paaah.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 09
MWANDISHI : MJAMAA SAMWELY
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611

Tulipoishia - Asubuhi na mapema,mtoto alianza kulia tena.Mke wa juma alitoa nyonyo na kumpa anyonye.Lakini kama mwanzo kila mtoto alipovuta maziwa mke wa juma alihisi tofauti.Alihisi kama kuna kitu kinamtoka mwilini mwake.Aliendelee kuvumilia lakini mwishowe alishindwa taratibu macho yake yakapoteza mwanga akaanguka chini kama mzigo paaah.

Endelea nayo.

Juma alikuja kushtuka mkewe akiwa kaanguka chini.Alimtoa mtoto haraka na kumweka kitandani.Alimtikisa mkewe kwa nguvu bila mafanikio.Alimwangalia vizuri akajua kuwa amezimia.Alifikiria haraka haraka afanye nini.Alikimbia nje. Nje ya nyumba yao kuna mti ambao unaharufu kali sana.Na mara nyingi unatumika kuwazindua watu waliozimia.Alichuma majana ya ule mti na kwenda nayo ndani.

Alimtikisa mkewe kisha akamnusisha yale majani ,na pale pale akapiga chafya.Fahamu zake zikawa zimemrudia.Lakini alionekana kama hana nguvu kabisa.

" vipi mke wangu"

" mmmh mmmh mmmh" alikuwa anahema tu kwa nguvu bila kusema lolote.

" mke wangu vipi mbona ivyo gafla"

" Nipeleke hospital.Hali yangu sio nzuri" aliongea kwa tabu mke wa juma.

" aaaah hospital asubuhi hii.Kwani umefanya nini mpaka ukazimia?"

" Mwili wangu hauna nguvu kabisa,halafu nasikia kizunguzungu sana" aliongea kwa tabu mke wa juma.

" daaah! Sawa " juma alimjibu kisha akatoka nje haraka kwenda kutafuta usafiri.Akiwa mlangoni kwa mbali aliiona bajaji.Aliita kwa mkono kisha akaenda ndani kumchukua mkewe.Alimpakiza kwenye bajaji na safari ya kuelekea hospital ikaanza.

Haikuchukua muda wakawa wamefika hospital.

........
Twende kwa hans.

Hans tangu aliposhiriki ngono na mama tatu hakuwahi kuonana naye tena.Kila alipompigia simu haikwenda.Mama tatu alikuwa amemblock.Kitendo kile kilimuumiza kichwa akaamua aende nyumbani kwa mama tatu.

" huyu mwanamke mbona hivi.Kwenye simu hapatikani,na hata kunitafuta hakuna.Hivi nitaishiji bila yeye.Yaani sazi nina siku kama saba sijashika hata shilingi mia.Hela zote alizonipa zimeisha" aliwaza hans.

" daaah! Lakini mwili wangu haupo vizuri kabisa.Yaani tangu siku ile nishirikiane naye nimekuwa tofauti sana.Kuna muda naona kama kuna kitu kimepungua kwenye mwili wangu,Lakin pia kuna muda naona kama kuna mzigo kwenye mwili wangu" aliwaza hans huku akifunga mlango na kutoka nyumbani kwake.

Mfukoni alikuwa hana hata mia.Kutokana na imani aliyokuwa nayo kuwa akienda kwa mama tatu atapata hela,aliamua kuchukua pikipiki na kumwambia dereva atamlipa wakifika.Dereva alivuta moto na haikuchukua muda mrefu wakawa wamefika nyumbani kwa mama tatu.Wakati wanafika walikuta geti likiwa linafunguliwa na gari linatoka.Hans alipoliangalie lile gari ,lilikuwa la mama tatu.Haraka alilisogelea na kutaka kulisimamisha huku akimpungia mkono mama tatu.

Mama tatu alimwangalia hans kama mtu ambaye hamfahamu.Aliendesha gari bila kusimama na kupotea eneo lile.Hans hakuamini macho yake. " aaah yaani huyu mwanamke leo ananipita kama hanioni?,mmmh kuna nini? Nimemkosea nini? " Alijiuliza hans.

Wakati anajiuliza dereva boda boda alimfata na kumwambia ampe hela yake ." broo naomba hela yangu niondoke basi" aliongea yule dereva boda boda.

Hansa alikuwa mpole asijue afanye nini.Mtu aliyemtegemea atampa hela kampita kama hamuoni na akijaribu kumpigia simu hampati." aisee ukisikia kudhalilika ndio leo.Sasa sijui huyu jamaa nitampa nini" aliwaza moyoni hans.

" oya mwana unanichelewesha.Au utalipia na waiting charge.Kama utalipia na hela ya mimi kukusubiri haina shida."

" daaah! Broo naomba nisamehe ,hela yako nitakupa siku nyingine.Mtu niliyetegemea atanipa hela kanizingua"

" acha masihara wewe.Naomba hela yangu.Tusizinguane kabisa.Yaani asubuhi asubuhi unataka kuniletea gundu.Usilete masihara hata kidogo.Naomba hela yangu aisee"

" broo si umeona , mtu mwenyewe alivyonipita kama hanijui.Naomba nivumilie broo nitakulipa siku nyingine"

" Ilo haliwezekani ndugu yangu.Unajua shida yenu nyie vijana wa sasa mnataka kulelewa.Yaani baada ya kufanya kazi unakaa kusubiri kulelewa na mwanamke.Sasa kwa taarifa yako mimi sikuachi hapa mpaka unipe hela yangu.Kama hauna nakuvua viatu sasa hivi"

" broo tunafika hadi kwenye kuvuana viatu tena?"

" sio viatu tu.Nitakuvua mpaka suruali."

Hans alijua ni kama utani kuwa jamaa hawezi kumvua nguo kwasababu ya shilingi elfu moja.Akiwa ameduwaa,jamaa alishuka kwenye pikipiki na kwenda kumvamia .Alimshika na kuanza kumvua viatu.Hans alipojaribu kujitetea jamaa alimshika kisawaswa.Hans alikurupuka na kuanza kuleta vurugu.Kitendo kile kilifanya watu wajae.Madereva boda boda walifika na kumuuliza mwenzao tatizo ni nini.

" huyu boya kanikodi halafu kumbe hana hela.Nataka nimvue nguo na viatu kufidia hela yangu" dereva boda boda aliwaambia wenzake.

Baada ya kuambiwa ivyo walimsaidia mwenzao wakamshika hans kwa nguvu na kumvua nguo zote.Alibaki na bukta tu." daaah yaani mimi leo ndio wakufanyiwa hivi?," aliwaza hans.

" fanyeni kazi nyie vijana.Acheni kutafuta wanamama wakuwalea" aliongea baba mmoja aliyekuwa pale.

" daaaah! Hii dunia inamambo sana.Yaani kijana mzima kama yule anakaa kumtegemea mama tatu.Hajui kama mama tatu kazi yake ni kubadilisha wanaume tu" aliongea mama mwingine.

Hans kwa aibu taratibu akaanza kutembea kurudi nyumbani kwake.

............

Turudi kwa juma na mkewe.

Baada ya kufika hospital daktari aliwapokea na kumfanyia vipimo mke wa juma." Aisee mbona mkeo hana damu kabisa.Yaani hana damu hata kidogo.Halafu huyu si amejifungua juzi tu hapa." aliuliza daktari.

" ndio daktari"

" sasa kama amejifungua juzi tu ,na juzi alikuwa sawa .inakuwaje damu ipungue hivi .Mbona haiwezekani binadamu damu ikampungua kwa spidi hii.Yaani inakuwa utafirikiri kuna kitu kinamnyonya damu.Halafu mbona maziwa yake yapo vile vile.Inamaana hanyonyeshi au?,maana maziwa ninavyoyaona inaonekana hajawahi kumnyonyesha mtoto tangu ajifungue."

Kauli ya daktari ilimchanganya juma."mmmh hajamnyonyesha mtoto kivipi wakati asubuhi hii amaetoka kumnyonyesha? Halafu hii damu kupungua hivi maana yake nini? Au huyu mtoto ananyonya damu ?". Alijiuliza juma moyoni.
ITAENDELEA

Full vipande vyote 27 vinapatikana kwa buku tu. Lipa kupitia halopesa namba 0621249611 kisha nitext whatsapp kwa namba hyohyo
 
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 10
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611

Tulipoishia -
Kauli ya daktari ilimchanganya juma."mmmh hajamnyonyesha mtoto kivipi wakai asubuhi hii amaetoka kumnyonyesha? Halafu hii damu kupungua hivi maana yake nini? Au huyu mtoto ananyonya damu ?". Alijiuliza juma moyoni.

Endelea nayo.

" huyu mtoto atakuwa ananyonya damu sio bure" aliwaza juma.

" Naomba tafuta ndugu wa kumtolea damu mkeo" aliongea daktari.Juma alitoka nje kwenda kuwatafuta ndugu.Akiwa nje aliingiza mkono mfukoni hili achukue simu .Simu haikuwepo.Alipapasa mifuko yote hakukuta kitu.

" aaah! Sijui akili yangu iko wapi? Yaani natafuta kitu ambacho akipo.Simu niliporwa siku ile halafu saiz nimesahau najifanya kuitafuta." aliwaza juma moyoni.Alifikiria aanzie wapi hakupata mwanga.

Aliamua kwenda nyumbani kwa mama yake mzazi ili amuombe mdogo wake aende kumtolea damu.Kutokana na kutokuwa na hela ya nauli ilibidi atembee kwa miguu.Alitembea umbali mrefu sana hadi akafika.Alibisha hodi na kuingia ndani.

" afadhali umekuja mwenyewe.Yaani hapa nilikuwa napanga nije huko huko nyumbani kwako" aliongea mama juma.

" mbona ivyo mama? Kuna usalama kweli?"

" usalama haupo kabisa.Moyo wangu bado unaumia sana.Kuna muda uwa nawaza kama kweli wewe ni mwanangu au walinibadilishia"

" aaaah! Mama maneno gani ayo.Kwanini umasema ivyo lakini.Mbona kauli kali sana iyo.Mimi mwanao uliyenizaa wewe mwemyewe na kunilea maisha yangu yote leo unaniambia ivyo mama"

" kwanini nisikuambie?,kwani unayonifanyia wewe ni mazuri?""

" mmmh! Nimekufanyia nini mama.Mbona sioni ubaya niliokufanyia"

"Hivi una akili wewe mtoto? Uoni ubaya kivipi?,hivi uoni kama umetuletea mkosi kwenye familia yetu.Hivi mkeo yule mtoto aliyemzaa ni mtoto au ni kindondocha kile"

" mama tafadhli usimwite ivyo mwanangu.Kwanza nimeshampa jina.Kuanzia sasa acha kumuita majina ya ajabu.Jina lake ni ayubu.Nimeona nimpe jina la baba yangu ili kumuenzi baba."

" unasemaje wewe mwanaharamu? Umempa yule mtoto jina la baba yako.Naomba ushindwe katika ilo.Yaani ukome kabisa na ulegee.Jina la mume wangu kipenzi huwezi kumpa mshenzi yule.Sasa naomba unisikilize kwa umakini.Ukitaka mimi niendelee kuwa mama yako naomba yule mwanamke kamfukuze pamoja na mtoto wake."

" aaah sasa mama namfukuza aende wapi? Yule ni mke wangu ,na tulikubaliana tutasaidiana kwenye shida na raha.Namfukuza saizi aende wapi ? Na ukizingatia mkoa huu yeye hana ndugu"

" anaenda wapi ilo sisi halituhusu.Kitu ninachotaka mimi aondoke.Ametuletea gundu sana.Mtoto gani yule aliyezaa."

" kwani mama yeye kosa lake nini? Kwani yeye ndiye aliyepanga iwe vile? Ile si imetokea tu?"

" mmmmh! Imetokea tu wapi? Wala haijatokea tu.kilichasababisha mtoto azaliwe vile ni yeye kuchanganya mbegu.Alikuwa anakutana na wewe halafu anatoka tena kwenda kukutana na wanaume wengine.Matokeo yake ndo ayo"

" si kweli mama"

" eeeh wewe mtoto nimechoka kubishana na wewe.Ukikubali sawa ukikataa sawa ila kuanzia sasa wewe sio mtoto wangu na ninaomba utoke nyumbani kwangu."

" mama usinifanyie ivyo.kwanza mwanao nimekuja hapa nina shida.Mke wangu amelazwa hospital kaishiwa damu.Nilikuwa naomba huyu mdogo wangu akamtolee damu"

" mmmh utakuwa na wazimu wewe.Yaani mwanangu huyu aanze tu kwenda kumtolea damu yule mwendawazimu.Aisee ilo haliwezekani.Kwanza toka nyumbani kwangu" aliongea mama juma huku akimshika mwanae na kumtoa nje.

Juma alitolewa mkuku mkuku mpaka nje.Kinyonge na taratibu kichwa akiwa kakiinamisha chini aliondoka.Aliwatafuta marafiki zake wa msaidie .Akawapata wawili na yeye akawa watatu.Walienda hospital wakapimwa damu zao zikaonekana zipo sawa.Mke wa juma akawekewa damu.

.........
Turudi kwa mary yule mwanafunzi wa chuo

Mary tangu alivyokutana kimwili na baba tatu,alikuwa akimpigia simu baba tatu lakini simu yake haikupokelewa.Alipiga simu asubuhi mchana na jioni bila mafanikio yeyote.Moyoni alianza kuingiwa na wasiwasi.

" mmmh! Yule mbaba vipi? Mbona simuelewi?. Kwanini hapokei simu yangu.au hakufurahia mapenzi niliyomuonesha.mmmh! Hapana bana ,mapenzi alifurahia labda atakuwa na tatizo fulani" aliwaza mary.

Habari ya yeye kutembea na baba tatu alimwambia rafiki yake aitwae mage.Kwa jinsi mary alivyomsifia baba tatu kuhusu kutoa hela,mage na yeye aliingiwa na tamaa.Alimvizia rafiki yake akiwa amejiziuka akachukua simu yake na kuiba namba ya baba tatu.

Wakati mage anafanya ivyo mary alikuwa kwenye mawazo mazito.Alikuwa anawaza ni jinsi gani afanye hili aweze kukutana na baba tatu tena.Kitendo cha kutopokea simu yake kilimchanganya sana.Akiwa kwenye mawazo mazito rafiki yake mage alimshtua.

" mmmmh shoga,mbona ivyo? Utakufa na mawazo rafiki yangu.Tatizo nini?" aliuliza mage.

"Mwenzangu lile danga langu nililokuambia si alipokei simu yangu.Yaani toka jana namtafuta hewani simpati.Halafu naisi kama ameniblock .Maaana nikipigia simu inakata yenyewe bila kuita wala nini?" aliongea mary huku akionekana kama mwenye huzuni sana.

" mmmh shoga yangu wanaume ndivyo walivyo.We achana naye tu.Lamsingi mshukuru MUNGU amekununulia iyo laptop na pia kakupa hela nyingi za matumizi"

" mwenzangu kumshukuru namshukuru lakini mwenzio hela alizonipa sijafanyia chochote cha maana."

" aaah kwanini sasa?"

" si nilijua kila siku atakuwa ananipa.Sasa bahati mbaya ndio ivyo saizi hataki kabisa kupokea simu yangu."

" mmmmh! Halafu shoga nikuulize kitu?"

" uliza tu "

" mchumba wako alfani umemwambia laptop umepata wapi? ,maana tangu jana ananiulizia kweli .Na inaonekana kama hana amani kabisa."

"Nimemdanganya nimepewa na baba.Lakini tatizo ni kuwa siku ile naondoka na yule mzee na yeye aliniona,hivyo anahisi nimeongwa na yule mzee."

" duuuh! Kwahiyo kumbe anahisi tu ila hana uhakika"

" ndio.Anahisi tu ila hana uhakika kama nilitembea na yule mzee.Naomba ukikutana naye nisaidie kumwelewesha basi.Maana kiukweli nampenda sana.Huyu mzee mimi nataka kumchuna tu.ila mpenzi wangu wa kweli ni yeye" aliongea mary.

Mage ni rafiki mkubwa sana wa mary.Siri zote za mary, mage anazijua.ila pamoja na kuwa shoga yake mkubwa ,mage amekuwa akimuonea wivu mary.Mara nyingi alikuwa akitamani vitu alivyokuwa navyo mary.Mara nyingi amekuwa akimtega alfani ambaye ni mpenzi wa shoga yake.

Baada ya kupiga story na kuachana .Mage aliondoka akaenda kununua vocha na kumpigia baba tatu,kwani namba yake aliiba kwenye simu ya mary.Alimpigia na kujitambulisha kuwa yeye ni mwanachuo na alikuwa na shida naye.

Baba tatu baada ya kuisikia sauti ya mage kwenye simu alivutiwa na alijua kuwa hajawahi kukutana naye.Alimpa maelezo sehemu ya kuonana.Mage baada ya kuambiwa aende sehemu flan,alirudi hostel na kuoga mara tatu tatu.Alivaa nguo hii nakutoa,kila nguo aliyovaa aliiona haimpendezi.Mwishowe aliamua kuvaa ivyo ivyo.

Alichukua taksi kama alivyoelekezwa na kwenda kwenye hotel ambayo baba tatu alikuwa akimsubiri.Kama kawaida ya baba tatu akulaza damu,akifanya naye mapenzi kisha akampa hela ya matumizi na wakaagana na kuondoka .

..........
Turudi kwa mke wa juma.

Siku zilienda mke wa juma akaruhusiwa kutoka hospital.Yeye na mumewe wakaongozana mpaka nyumbani.Mawazo ya kutengwa na ndugu zake yalikuwa yanamsumbua juma.

" daaaah! Maisha bila kuelewana na mama nilikuwa siyataki kabisa.Sasa yametokea sijui itakuwaje" aliongea juma.

" kuna wakati mtu unakuwa hauna namna inabidi ukubaliane nayo ivyo ivyo.Wewe unazani utafanyaje.Kama ubaya ,hakuna ubaya wowote ambao sisi tumemtendea."

" mmmmh! Sawa lakini mke wangu.Kuna kauli ambayo mama aliiongea ambayo hadi saizi nikiifikiria nashindwa kuelewa.Sasa sifahamu kama ni kweli au la?"

" kauli ipi tena mume wangu?"

" mama amesema huyu mtoto kuzaliwa hivi imetokana na wewe kuchanganya damu"

" mmmmh! Kuchanganya damu kivipi tena?"

" Amesema inawezekana wakati upo mjamzito uliwahi kutembea na mwanaume mwingine ndiyo maana imekuwa hivi?.Kwa maelezo yake yeye anasema haiwezekani mwanamke akazaa mtoto wa ajabu kama hajafanya kitu chochote kibaya"

"Msema kweli ni mpenzi wa MUNGU mume wangu.Toka uliponioa sijawahi kushiriki mapenzi na mwanaume mwingine zaida yako.ilo naapa mbele ya MUNGU.Kama nasema uongo MUNGU anihukumu leo hiii hii"

" wewe mtaje taje tu MUNGU ovyo.Shauri yako mwenyewe.Kama umewahi kuchepuka ni bora ukawa muwazi ili tujue tunakusaidia vipi?"

" niliyochokuambia ni ukweli mtupu.Tangu uliponioa sijawahi kukutana na mwanaume mwingine kimwili.ila wakati tupo wachumba kabla hujanioa niliwahi kutembea na baba tatu.Na nilikuambia ukweli wote."

" ilo nakumbuka.Kuhusu baba tatu uliniambia.Si yule mzee aliyekurubuni kwa hela nyingi?"

" Ndiyo" alijibu mke wa juma kisha akaingia chumbani kumlaza mtoto.Muda ulikuwa umeenda.Baada ya kumlaza mtoto alienda kukaa barazani kupiga story na mume wake.Wakiwa wanapiga story ,gafla walisikia sauti ya paka ikilia kutoka chumbani.

" mmmmh! Mke wangu umemsikia paka uyo akilia ndani?"

" Ndio nimemsikia ila nashindwa kuelewa kaingia vipi chumbani?" aliongea mke wa juma kisha akasimama kuelekea chumbani.Kufika chumbani aliwasha taa.Alipoangalia sauti ilipokuwa inatoka alishika kichwa kwa mshangao." aaaah! Mwanangu" alitamka na kuacha mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 11
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611

Tulipoishia -
" Ndio nimemsikia ila nashindwa kuelewa kaingia vipi chumbani?" aliongea mke wa juma kisha akasimama kuelekea chumbani.Kufika chumbani aliwasha taa.Alipoangalia sauti ilipokuwa inatoka alishika kichwa kwa mshangao." aaaah! Mwanangu" alitamka na kuuacha mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.

Endelea nayo.

" Hivi ni nini kinaendelea?" aliongea mke wa juma huku mikono akiwa kashika kichwani.Kauli yake ya mshtuko ilimshtua juma aliyekuwa barazani.Alisimama .Haraka sana akawahi chumbani.Kufika pale na yeye hakuamini alichokiona.

Ile sauti ya paka aliyekuwa analia ilikuwa ni ya mtoto wao.Mtoto wao alikuwa analia kama paka.Tangu walipotoka hospital mtoto wao hakuwahi kulia.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza.ilikuwa ni mara ya kwanza kulia lakini sauti aliyoitoa ilikuwa ni sauti ya paka.

"Nafanya nini na huyu mtoto.Mtihani gani huu.Ewe Mungu nionee huruma tafadhali.Mitihani uliyonipa inatosha sana.ikiwezekana naomba kichukuie kiumbe hiki.Nisamehe kwakusema ayo.ila naomba unisaidie tafadhali " aliongea juma moyoni .

Mtoto aliendela kulia.Sauti yake ilikuwa ni ya paka.Mke wa juma alimsogelea na kumchukua kisha akambamiza chini kwa hasira.Juma alimuwahi mke wake na kumzuia.kitendo cha kumpiga chini kilimfanya mtoto azidi kulia.Alilia kwa nguvu zaidi.

Lakini kule kumbamiza chini kulimfanya achanike kichwa kidogo na damu zitoke.Ajabu yule mtoto baada ya kuona damu kidogo kwenye sakafu aliacha kulia akawa anazilamba zile damu.

" Mungu wangu" alitamka juma huku akirudi nyuma.Baada ya kulamba zile damu yule mtoto aliendelea kulala pale pale chini alipotupwa." Hebu mchukue mtoto " aliongea juma.

"Mume wangu saizi nimeamini huyu si mtoto.Huyu siyo mtoto kabisa.Mimi siwezi kumchukua ,siwezi kumchukua nasema" aliongea mke wa juma.

" sasa mke wangu.Kama wewe mama yake unamtenga watu wengine watafanya nini? Wewe ni mama yake.Huyu mtoto amekaa tumboni kwako kwa muda wa miezi tisa.Katika watu wote,wewe ilibidi uwe na uchungu kutushinda sisi wengine"

" hapana mume wangu.Nimevumilia ila kwakweli imetosha.Siwezi tena mimi.Siwezi ,kwakweli siwezi " aliongea mke wa juma.Juma alimsogelea mke wake na kumkumbatia." yatapita mke wangu. Hii ni mitihani ya maisha.Tuombe MUNGu atusaidie" aliongea juma huku akimpapasa mke wake mgongoni.

Taratibu mke wa juma akaanza kujirudi.Alitoka kwenye mikono ya mume wake na kwenda kumchukua mtoto pale chini.Mtoto alikuwa amenyamaza kulia baada ya kulamba zile damu.

Alimchukua kisha akatoa nyonyo na kumpa anyonye.Mtoto aliifakamia ile nyonyo na kuanza kuvuta.Ajabu kila alipovuta mke wa juma alilamika,alihisi kama ananyonywa damu.Kila mtoto alivyovuta mke wa juma alihisi damu yake inavutwa.Alijaribu kumtoa mtoto kwenye nyonyo alishindwa.Taratibu aliishiwa nguvu na akaanguka chini na kupoteza fahamu.

" aaah mke wangu,mke wangu" aliita juma bila mafanikio.Alipoona mkewe haamki alisimama nakutoka nje kuomba msaada.Ndani ya dakika kazaa jirani yake mmoja akawa amefika.Kwakutumia simu ya jirani yake walimpigia mtu wa bajaji akaja kuwachukua.

Walimkimbiza mpaka hospital.Kufika hospital daktari alimfanyia vipimo kisha akamuita juma ofisini kwake .

" kijana hivi mke wako haumpendi sio?"

" Kwanini unasema ivuo dokta"

" Nasema ivyo kwasababu haufati maelezo yangu.Nilikuambia mpe vyakula vinavyoongeza damu,lakini wewe haumpi.Matokeo yake ndiyo aya .Kila siku anazimia kwakupoteza damu.Sasa hebu fikiria majuzi tu tumemuongezea damu.Na leo tena inabidi tumuongezee damu" aliongea kwa ukali daktari.

Juma alikuwa mpole asijue chakufanya.Daktari alimwagiza akatafute watu wa kumtolea damu mke wake.Kwa shingo upande alitoka pale hospital na kwenda kuwatafuta watu wa kumuongezea damu mke wake.

............
Twende kwa baba tatu

Baba tatu alikuwa yupo na mama tatu barazani wakipiga story.Wakiwa kwenye mazungumzo yao .Simu ya baba tatu ililia.Aliichukua na kuiangalia.Alikuwa ni mtoto wao Tatu ambaye alikuwa anasoma jijini dodoma.

"Baba shikamoo"

"Marahaba mwanangu .Vipi za masomo?"

" Nzuri baba.Sijui nyie hapo nyumbani mnaendeleaje?"

" sisi tunaendelea vizuri tu.Mambo yetu yanaenda safi tu."

" ok sawa.MUNGU akipenda wiki ijayo nitafika huko kwa ajili ya field"

" mmmh mwanangu kwani field ni lazima uje kufanyia huku.Kwanini usitafute huko huko.Maana maisha ya huku sio mazuri kama huko"

" mmmh baba kumbe hunipendi mwanao.Yaani hutaki hata kuniona kweli?"

" Hapana mwanangu sio ivyo.Nataka sana kukuona ila masomo yako ni muhimu kuliko sisi.wewe fanya kila kitu ukimaliza chuo ndio uje kutuona"

"Mmmmh! Sawa" alijibu tatu kisha akakata simu.

"Mwanao anataka kuja "

" Umefanya vizuri kumkatalia.Akija hapa itakuwa shida.Ni bora abaki huko huko."

" sawa tuachane na ayo.vipi hakuna dada yoyote uliyenitafutia mumeo nifurahi."

" aaah! Yaaani wewe kila siku unataka mimi nikutafutie wewe tu.Mbona mimi hunitafutii"

" mmmmh! Kwani wote uliolala nao uliwatafuta wewe.Mbona wengine nilikutafutia mimi.Tena karibu wote ni mimi niliyekutafutia.Hilo ukubali ukatae lakini ukweli ndio huo.Mimi nimekutafutia wanaume wengi sana mke wangu" aliongea baba tatu huku akisimama.

" mbona unasimama.Safari ya wapi tena?"

" aaah natoka nje kunyosha nyosha miguu ,unajua mtembea bure sio sawa na mkaa bure.Kwenye kutembea tembea naweza nikaopoa kimwana" aliongea baba tatu kisha akafungua mlango na kutoka nje.

.......

Turudi kwa juma.

Baada ya kuhangaika sana juma alifanikiwa kuwapata watu wa kumuongezea damu mke wake.Baada ya kuongezewa damu na afya yake kukaa sawa waliruhusiwa kurudi nyumbani.Juma alimsaidia mkewe kubeba mtoto na wakarudi nyumbani.

Kufika nyumbani mke wa juma alionekana mwenye mawazo sana.Muda wote alikuwa anaangalia sehemu moja na kuwaza sana.Usiku wa saa nane Wakiwa wamelala ndani alimuaga mume wake anaenda chooni .Alisimama na kutoka nje.

Juma akiwa kitandani alishangaa kuona muda unaenda bila ya mke wake kurudi." mmmh! Huyu ameenda chooni kweli au anamambo yake" aliwaza juma huku akisimama kitandani na kutoka nje kwenda kumuangalia mke wake.Alienda mpaka chooni lakini hakukuta mtu.Alizunguka nyumba nzima kuangalia lakini hakumuona mke wake.

" mmmmh! Huyu ameenda wapi usiku huu." aliwaza juma.Baada ya kuzunguka na kuona kimya aliamua kuanza kuita kwa sauti.Aliita bila mafanikio.

Wakati mumewe anamuita mke wa juma alikuwa mbali kidogo ya pale, alisikia sauti ya mumewe ikimuita. ." utanisamehe mume wangu.Nimeshindwa kuvumilia.Nimeona bora nikimbie niende mbali.Kuishi na huyo mtoto nimeshindwa kwakweli" alijisemea moyoni mke wa juma huku akiongeza mwendo.

........

Ilipofika saa tisa kamili usiku,baba tatu na mama tatu walivua nguo zote na kuingia kwenye chumba chao cha siri ambacho wanaingiaga kila siku inapotimia saa tisa usiku.

Kwa upande wa juma baada ya kuona anamwita mke wake bila mafanikio.Aliamua kurudi ndani .Lakini cha ajabu baada ya kufika kitandani alikuta mtoto hayupo.Alitawanya nguo kitanda kizima kumtafuta lakini hakumuona.

"Mmmmh! Hapa kuna kitu ambacho,sio cha kawaida.Siku zile huyu mtoto alipotea saa tisa usiku na leo tena saa tisa usiku anapotea tena.Hapana hapa si bure" aliwaza juma.

== kwanini kila inapofika saa tisa usiku mtoto wa juma anapotea? Na kwanini kila saa tisa usiku baba tatu na mama tatu wanaingia chumba chao maalum? Kuna mengi yaliyojificha.Tuendelee kufatilia =

Full vipande vyote lipia Tshs 1000 tu kwenda Halopesa namba 0621249611 kisha njoo whatsapp kwa namba hyohyo
 
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 12
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611

Tulipoishia -
Kwa upande wa juma baada ya kuona anamwita mke wake bila mafanikio.Aliamua kurudi ndani .Lakini cha ajabu baada ya kufika kitandani alikuta mtoto hayupo.Alitawanya nguo kitanda kizima kumtafuta lakini hakumuona.

"Mmmmh! Hapa kuna kitu ambacho,sio cha kawaida.Siku zile huyu mtoto alipotea saa tisa usiku na leo anapotea tena saa tisa usiku. Hapana hapa si bure" aliwaza juma.

Endelea nayo.

" kuna kitu kisicho cha kawaida kuhusu huyu mtoto.Lakini kumtafuta huyu mtoto ni kupoteza muda.Kama amepotea wacha apotee,kama kuna watu wananifanyia mchezo wacha waendelee kunifanyia.ila mimi ni mtu wa MUNGU.Yeye mwenyewe atanisimamia" alijisemea moyoni juma.

" Lakini huyu mwanamke usiku huu ameenda wapi?,kwanini na yeye ananifanyia hivi lakini? Yaaani kumvumilia kote nilikomvumilia malipo yake ni aya?" alijiuliza juma. Juma alijilaza pale kitandani, akapitiwa na usingizi.Kutokana na uchovu wa kutokulala muda mrefu juma akawa anakoroma sana.

Kelele za mbwa waliokuwa wakigombania mzoga karibu na dirisha lake walimzindua kutoka usingizini." mmmmh! Kumekucha" aliongea juma baada ya kuzinduka usingizini.Aliangalia kushoto ajabu yule mtoto alikuwa pale pale amelala.

" mmmmh! Huyu sio mtoto.Huyu sio mtoto kabisa." aliwaza juma.

" wewe si uliondoka hapa kichawi? Kwanini umerudi tena? Kwanini?" aliongea juma.Wakati anaongea ayo kumbukumbu za mke wake zikamjia " daaah,mke wangu sijui ameenda wapi?,bila shaka amekimbia kulea huyu mtoto,ila sio shida kama yeye ameona akimbie sawa mimi nitamlea ivyo ivyo.Japo ana mambo mengi ya ajabu,ila sinabudi kumlea kwakuwa ni damu yangu.

..........

Turudi kwa baba tatu na mkewe.

Saa kumi na mbili asubuhi baba tatu na mama tatu walitoka kwenye chumba chao cha siri kisha wakajiandaa. Kila mmoja akaelekea njia yake.

Baba tatu yeye alipanga kutoka nje ya miji ili kutafuta mtu wa kushirikiana naye ngono.Upande wa mama tatu yeye alipanga kwenda chuo kuwavizia wanafunzi wa chuo

WAliingia kwenye magari yao na kuondoka.Kila mmoja akaelekea njia yake.

Kwa upande wa mary ,Tangu alivyotembea na baba tatu mikosi ilikuwa inamuandama sana.Kila alilojaribu kufanya pale chuo lilifeli.Na hii haikuwa kwake tu.Ilikuwa kwa mage pia.Naye tangu alivyolala na baba tatu maisha yake hayakuwa sawa.

" mmmmh! Hivi nina nini? Mbona maisha yangu hayapo sawa kabisa.Mwili wangu ni kama umepungukiwa na kitu.Halafu mbona kama siku hizi nimekuwa na mikosi sana." aliwaza mary huku akiwa anaelekea kwenye ghetto la mpenzi wake alfani.

Wakati mary anawaza ayo akiwa njiani kwenda kwa alfan.Shoga yake mage alikuwa kwa alfan ambaye ni mpenzi wa mary.Mage alikuwa anampenda sana alfan.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom