Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 152,975
- 453,778
- Thread starter
- #181
Sehemu ya 101
Niliinua kichwa kama vile naona nikijikuta kama nategemea kupata kitu fulani kutoka kwenye maombi hayo.
Kichwa kiliniuma zaidi ya nilivyowahi kuumwa siku za nyuma, lakini sikutaka kutoka mpaka nione nini matokeo yake.
Ghafla macho nayo yakauma kama vile yaliingia mchanga. Ilibaki kidogo tu nipige kelele za kuomba msaada kutoka kwa wale wenye nyumba yao, lakini sijui nilipata wapi ujasiri nikatulia kimya nikisubiria nisikie hayo maombi yatakavyokuwa yakiombwa na yule mtu aliyekuwa akisema.
"Kwani akiomba hivyo hata mimi wa nyumbani ninayeona naweza kupona?" niliwauliza.
"Ndiyo maana wamekitangaza kwenye tivii ili kila mtu aone," alijibu mwanamke.
"Kwa hiyo mimi nitajuaje kama nimepona?"
"Utajua tu, kinachokuuma kitapona," aliposema hivyo nikabaki navumilia tu litakalotokea na litokee sasa kwani nilikuwa tayari kwa lolote
Nikiwa katika hali ya kutoona, nilijiwa na picha ya ajabu sana. Yule mama jirani alinisimamia mbele yangu na kuniuliza.
"Unadhani utakuwa umemaliza tatizo siyo?"
Nilimjibu ndiyo nitakuwa nimemaliza tatizo, akaniuliza tena.
"Na nyumba hii unayokaa utahama au?"
Nilijibu sihami kokote, liwalo na liwe kwa sababu mwenye nyumba hatuna ugomvi naye.
Akanisogelea huku akiinua mikono juu na kukunjua vidole kama vile alitaka kunikaba sehemu. Nikamkwepa akacheka sana huku akizidi kunisogelea.
"Naombenu mtu anishike mkono," niliwaambia wale wenyeji wangu. Lakini mwanaume akasema itakuwa vyema wanipeleke kwangu kama ni imani tayari nimeshaonesha sana mbele ya Mungu, lakini nikakataa kwamba sitaki mpaka nione mwisho wa maombezi yale siku ile.
Nikamsikia muombaji akisema kuwa, kama magonjwa ni mengi au kuna matatizo ulalie juu ya kifua chako upande wa moyo kwani ndiyo binadamu alipo.
Nilifanya hivyo kisha nikaanza kumsikia akiomba kwa sauti. Alisema nguvu zote za giza zikashindwe. Mipango yote ya shetani pia ikashindwe mara moja kwa kila mtu aliyekuwa ukumbini au kanisani kule na au waliokuwa wakiangalia tivii.
Mara ghafla, macho yangu yakaona tena na pia kichwa kikapona pale pale haraka sana. Sikuamini, niliangalia huku na kule na kutaka kupiga kelele, lakini mwenye chumba kile akanizuia akisema kuwa, si busara kama ni kusema nisubiri kwanza.
Nilikuwa mwepesi sana tofauti na siku nyingine yoyote. Nilijihisi kuwa, nilikuwa nimebeba mzigo mzito kwa siku nyingi sana sasa nilikuwa nimeutua kwa hiyo nilikuwa sina mzigo tena. Lo! Nilisema mwenyewe.
Nilijaribu kufumba macho na kuyafumbua, nikaona kama kawaida tu.
Kila mtu mle chumbani kwa mwenyeji wangu aliniangalia mimi na mahubiri yalikuwa yamemalizika wakati huo.
Pale pale mjukuu wa mwenye nyumba alibisha hodi akaulizia kama niko kule naitwa na bibi yake.
"Amesema uende haraka sana," yule mjukuu aliniambia.
"Kuna nini kwani, anaumwa?" nilimuuliza.
"Sijui, amesema uende haraka," alisema akiondoka zake.
Niliwaaga wale watu huku wakiniambia kama nilijisikia kupona nihakikishe habari hizo siziweki hadharani haraka vile, nikawakubalia.
Niliingua kwa yule bibi na kumkuta amekaa na wajukuu wake wengine na binti yake wa mwisho wakiongea.
Bibi aliponiona tu mimi alikunja sura ingawa ilikuwa usiku lakini nilitambua hilo.
"Kaa hala, nyinyi ondokeni," aliseam akimaanisha mimi nikae watoto waondoke pale sebuleni kwake.
"Nimekuita kukwambia jambo moja tu muhimu. Kuanzia kesho nakitaka chumba changu unachoishi, tena ninaposema nakitaka kesho maana yake nakitaka haraka sana. Kama ni pesa bado unayoitumikia kukaa hapa mimi nitakurudishia, nimegundua wewe si mtu mwema kwangu, unataka kuniua wewe."
Je, nini kiliendelea?