EeehMsome imeandikwa kitaendelea kesho
Kesho tena ShunieSehemu ya 98.
Siku hiyo hiyo saa kumi na moja jioni nilikuwa nimekwenda nyumbani kwa mzee mmoja ambaye aliniita kwa ajili ya kwenda kumsaidia kurekebisha kitasa cha mlango wake.
Ili kufika nyumbani kwa yule mzee unapita jirani na nyumba ya yule mama.
Wakati natengeneza kitasa yule mzee aliniuliza kwa nini napatana sana na yule mama wakati watu wengine majirani wanamuogopa kama ukomo. Sikumjibu zaidi ya kutabasamu tu.
Wakati narudi kibandani kwangu sasa huku nikiwa peke yangu, nilipofika usawa wa nyumba ya yule mama, kwenye dirisha la chumba cha mwisho kabisa, dirisha lilikuwa wazi nikachungulia ndani ili kuona.
Ni ajabu lakini ndivyo ilivyokuwa jamani. Niliona mlima wa majeneza ndani ya chumba hicho kilichokuwa na mwanga hafifu sana.
Niliganda kwa muda nikikodolea macho kuangalia ndani zaidi. Kila kona ya chumba hicho hicho majeneza yalikuwa yamesimamishwa kwa kubebanishwa kila moja juu baada ya jingine.
"Mungu wangu," nilisema kwa mshangao baada ya kuona yale majeneza.
"Unashangaa nini! Mwanaharamu wewe," sauti iliniambia bila kumwona aliyekuwa akisema.
Nikaondoka haraka sana.
Nilitembea huku nikijaribu kuikumbuka ile sauti kama inaweza kuwa ya mtu ninayemfahamu. Lakini sivyo. Haikuwa ya yule mama wala ya mwanamke mwingine ninayemfahamu.
Nilifika kibandani kwangu huku nikijishika mdomo kwa kuendelea kushangazwa na tukio lile. Niliweza kuyakumbuka karibu majeneza matano kati ya yote niliyoyaona kwamba, niliyatengeneza mimi.
Mfano hata lile lililochukuliwa siku hiyo hiyo na wale watu lilikuwa juu zaidi ya mengine kwenye ukuta wa mbele kabisa wa chumba kile.
"Huyu mama ana matatizo gani! Ina maana majeneza yoote yale namtengenezea yeye au? Mbona yapo mle kwake?" nilijisemea moyoni huku nikiangalia nyumbani kwa yule mama.
"Ulikuwa una shida gani kijana?" yule mama aliniuliza akitoka nyumbani kwake akija kwangu. Sura yake ilionekana kukasirika kupita kawaida.
"Hapana mama angu nilikwenda kutengeneza kitasa cha mlango hapo nyumba ya jirani," nilimjibu huku nikitetemeka mwili mzima kwa woga.
Tangu nilipoanza kumfahamu huyu mama, sikuwahi kumwona yule mama jirani akiwa amekasirika kama siku hiyo. Na sidhani kama itakuja kutokea tena siku kama ile.
"Unanidanganya hata mimi siyo. Unanijua vizuri wewe?" aliniuliza kwa sauti ya ukali sana.
Macho yake yalianza kubadilika rangi na kuwa mekundu kama yaliyojaa damu. Halafu alionekana kwamba kama angekuwa na silaha yoyote ile angenitwanga nayo. Hata kama ni jembe la kulimia kwani alikuwa akisema huku akiangaza huku na kule kama anayetafuta kitu cha kunipigia.
"Hapana mama. Kweli kabisa hata ukienda nyumbani kwa yule mzee watakuambia kwamba nilikuwa pale nikitengeneza kitasa cha mlango," nilisema kwa sauti ya kuomba huruma.
Nguvu ziliniishia kabisa baada ya kugundua kuwa, yule mama amebadilika sura siku hiyo kuliko siku yoyote ile nyuma ambazo niliwahi kumwona.
Hakuwa rafiki ingawa wa mashaka kama zamani. Alinigeukia kabisa.
"Twende nyumbani kwangu haraka sana," aliniambia akiwa amesimama mbele yangu huku amenishikia kiuno kama vile alikuwa akisutana na mimi.
Mambo ambayo sikuyazoea mimi katika makuzi yangu.
"Sawa mama," nilimkubalia huku nikianza kutembea. Na yeye alianza kutembea kuelekea nyumbani kwake lakini huku kila baada ya hatua mbili anageuka nyuma kuniangalia kama naendelea kumfuata.
Alipopandisha ngazi za nyumbani kwake, mimi pia nilipandisha licha ya kwamba aligeuka kuniangalia kama bado niko nyuma yake.
"Ingia ndani," aliniambia kwa amri.
Nilihisi kutaka kujisaidia haja ndogo pale pale, lakini nikaibana.
Je, nini kiliendelea?
Tukutane kesho...
Hivi kesho??????Sehemu ya 98.

Umenikumbusha mchezaji Vincent Price alikuwa anapenda kuigiza kama Dracula, niliwahi kumsikia alikuwa hapendi kuangalia filam zake kwa vile zilikuwa zinatisha na hata alikuwa akiwashauri wanawe eti wasiangalie.Inaogopesha mno
Nani alitoa ushauri wa ajabu huokwahiyo ndo umefata ushauri wa yule aliyekuambia uwe unatupostia kidogo dogo sio
kuna jamaa anaprofile ya mwendazakeNani alitoa ushauri wa ajabu huo
Mzigo nimeshauoata online Sema siwezi post hapa nitakuwa nimeshamfedhehsha mleta hadithikuna jamaa anaprofile ya mwendazake
nipe basi mimiMzigo nimeshauoata online Sema siwezi post hapa nitakuwa nimeshamfedhehsha mleta hadithi