Simulizi: Jinsi binti alivyoweza kuwatoa wazazi wake kwenye umasikini

iranna

Senior Member
Aug 4, 2021
149
617
Haya ni maneno aliyoyatamka Linda, binti wa pekee kwa wazazi wake. Baba yake alikua mlinzi wa majengo ya serikali kwa miaka mingi. Mama yake alikua mama wa nyumbani aliyejishughulisha na biashara ya vitafunio vya asubuhi kama chapati, maandazi, sambusa na vitumbua.

Linda na wazazi wake waliishi katika nyumba ya kupanga na walimudu kodi ya chumba kimoja tu. Wazazi wote walitegemewa na ndungu na wao kuishi Dar ilikua ni uokozi wa ukoo. Aliyeugua alifikia katika chumba cha kina Linda wakati akipata matibabu Muhimbili na Mloganzila.

Kilichowafurahisha na kuwapa faraja wazazi wa Linda ni uwezo wa akili za darasani aliobarikiwa binti yao. Kidato cha nne alipata ufaulu wa daraja la kwanza na kuwenda kuendelea na kidato cha tano katika shule ya serikali.

Chuoni Linda alisoma accounts, masomo kwake yalikua ni marahisi mno na aliwasaidia wengi darasani kwake. Kuna kijana mtoto wa tajiri sana alitokea kumpenda Linda. Walisaidiana kwa mengi shuleni Linda akipokea full boom. Waliahidiana kuona.

Wakati Linda anasoma aliweka kiasi kidogo cha boom kama akiba. Alipomaliza chuo, kwa kujua hali ya ajira ilivyo ngumu, aliamua kufungua biashara kama ya mama yake lakini kidogo ali up grade. Alitafuta containers na alipack chapati moja, andazi moja, kitumbua kimoja na sambusa moja. Hii ikiitwa breakfast package nayo iliuzwa sh 2, 500. Aliitangaza biashara Instagram na alipeleka order maofisini.

Baada ya miezi sita tu mpenzi wake alimvalisha pete, na mahari ilitolewa. Linda aliolewa ndani ya mwaka mmoja baada ya kumaliza shule. Mume wake akiwa Deputy Director wa kampuni za baba yake. Baada ya harusi akiwapa nyumba ya vyumba vinne vya kulala iliyo ndani ya gate wakwe zake. Mama Linda aliacha kupika vitafunww, wazazi walipewa allowance ya kuwaweka mjini kila mwezi.

Biashara ilipochanganya, mmoja wa marafiki wa Linda wa chuoni alimuomba msaada wa pesa. Linda alimpa milioni tatu kwa ahadi ya kuziridisha ndani ya miezi mitano.
Mume wa Linda alimuachisha Linda kufanya biashara baada ya harusi. Linda alikua mama wa nyumbani na alibarikiwa kupata mtoto wa kiume.

Baada ya miaka miwili ya ndoa, mume wa Linda alianza kumpiga, kitu cha ajabu huwa anampiga mpaka kumtoa damu baadae abambembeleza. Mara ya kwanza Linda alikimbilia kwa rafiki aliyewahi kumkopesha milioni tatu, yule rafiki alimpigia simu mume wa Linda aje amchukue.

Mara ya pili alikimbilia nyumbani kwao. Wakati yuko pale mume wake alikuja na gari kama zawadi kwa wazee. Wazee walimshauri Linda arudi kwa mune wake. Mara ya tatu alikimbilia kwa rafiki yake mwingine wa shule amabae anauza mama lishe. Mume wake alimtafuta alibemeleza na wakarudiana.

Aliporudi nyumbani mara ya tatu siku mume wake alipoinua mkono ampige, Linda aliweza kumpiga kofi la nguvu, jamaa alianguka chini siku hiyo Linda alimpiga kisawasawa. Baada ya hapo waliishi kwa heshima. Linda alisema nyumbani kwako ni lazima uishi kwa amani.
 
Story ya Linda imeenda fasta fasta

Mwisho Linda akamlabua Kofi mumewe chalii, na hivyo ndio jinsi alivyo wakwamua wazazi kwenye umaskini
Linda baada ya kumlabua mume wake kisawasawa alisema “hapa duniani unatakiwa uishi kwa amani nyumbani kwako na kaburini. Kama kuna issue nyumbani inakufanya usiwe na amani deal nayo. Hiki ndiyo kilikua kichwa cha habari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom