101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,119
RAMADHAN MUSSA - Rama Mla Watu.
.
Imepita miaka 12 sasa tangu kijana wa miaka 12 akamatwe na walinzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili akiwa amebeba mfuko wa Rambo ukiwa na kichwa cha mtoto wa miaka 3 aliyetambulika kwa jina la Salome.
Wakati mmoja akiwa kwenye kipindi cha mahojiano na Global TV, Rama alisema siku ya kwanza kuingia Gerezani wafungwa wote walikua wakimuangalia kwa tahadhari, inasemekana kabla hajafika Segerea wafungwa walikua wameshaomba akifika awekwe chumba chake mwenyewe asichanganywe...
...na watu wengine. Basi alivyofika hakutengwa aliwekwa kwenye ukumbi wanaolala watu wote. Anasema usiku ule jamaa hawakulala walikuwa wametulia kwenye magodoro yao wanamwangalia asije akafanya mambo yake. Rama kutokana na upweke na aibu alichukua blanketi na kujifunika gubi...
...gubi ili asiangaliane nao. Blanketi lile lilikua na vumbi mno hivyo baada ya muda akaanza kukohoa na akalifunua kwa nguvu, kile kitendo cha kujifunua tu ilikua patashika jamaa walitimua mbio kama wamepata wazimu. Rama baada ya kuona watu wanakimbia naye akahisi kuna hatari...
....hivyo akakimbia kuwafuata wanakoenda. Jamaa wakazidi kuchanganyikiwa wakapiga mayowe ya nguvu huku wakiparamia ukuta, milango na madirisha mpaka pale askari walipokuja na kuwatuliza. Rama anasema baadae aliwekwa kwenye chumba cha peke yake lakini siku zilivyozidi kusogea walimzoea na alirudishwa kwenye ukumbi wa watu wote na kwa maelezo yake alikuja kuwa nyapara pale Gerezani. Rama alitoka Gerezani mwaka 2017 ikiwa ni baada ya kukaa kwa miaka 9. Kwenye mahojiano hayo alikaririwa akisema watu wanamuogopa sana mtaani kiasi kwamba akipita watu wanamnyooshea vidole wakiwa mguu sawa kwa lolote. Aliongeza kuwa siku hizi hawezi kukaa tena Buguruni kwa sababu hakuna anaetaka kukaa nae karibu wala kupiga nae stori
'MWISHO View attachment 1459627View attachment 1459625
View attachment 1459626View attachment 1459628
Sent using Jamii Forums mobile app