Simulizi fupi ya Rama mla watu ya 9 miaka jela

namvumi king

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
682
1,000
RAMADHAN MUSSA - Rama Mla Watu.
.
Imepita miaka 12 sasa tangu kijana wa miaka 12 akamatwe na walinzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili akiwa amebeba mfuko wa Rambo ukiwa na kichwa cha mtoto wa miaka 3 aliyetambulika kwa jina la Salome.

Wakati mmoja akiwa kwenye kipindi cha mahojiano na Global TV, Rama alisema siku ya kwanza kuingia Gerezani wafungwa wote walikua wakimuangalia kwa tahadhari, inasemekana kabla hajafika Segerea wafungwa walikua wameshaomba akifika awekwe chumba chake mwenyewe asichanganywe...
...na watu wengine. Basi alivyofika hakutengwa aliwekwa kwenye ukumbi wanaolala watu wote. Anasema usiku ule jamaa hawakulala walikuwa wametulia kwenye magodoro yao wanamwangalia asije akafanya mambo yake. Rama kutokana na upweke na aibu alichukua blanketi na kujifunika gubi...

...gubi ili asiangaliane nao. Blanketi lile lilikua na vumbi mno hivyo baada ya muda akaanza kukohoa na akalifunua kwa nguvu, kile kitendo cha kujifunua tu ilikua patashika jamaa walitimua mbio kama wamepata wazimu. Rama baada ya kuona watu wanakimbia naye akahisi kuna hatari...
....hivyo akakimbia kuwafuata wanakoenda. Jamaa wakazidi kuchanganyikiwa wakapiga mayowe ya nguvu huku wakiparamia ukuta, milango na madirisha mpaka pale askari walipokuja na kuwatuliza. Rama anasema baadae aliwekwa kwenye chumba cha peke yake lakini siku zilivyozidi kusogea walimzoea na alirudishwa kwenye ukumbi wa watu wote na kwa maelezo yake alikuja kuwa nyapara pale Gerezani. Rama alitoka Gerezani mwaka 2017 ikiwa ni baada ya kukaa kwa miaka 9. Kwenye mahojiano hayo alikaririwa akisema watu wanamuogopa sana mtaani kiasi kwamba akipita watu wanamnyooshea vidole wakiwa mguu sawa kwa lolote. Aliongeza kuwa siku hizi hawezi kukaa tena Buguruni kwa sababu hakuna anaetaka kukaa nae karibu wala kupiga nae stori

'MWISHO View attachment 1459627 View attachment 1459625
IMG_20200525_215142.jpg
View attachment 1459626 View attachment 1459628

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,525
2,000
Stori hii ni ya kweli na ilibamba sana mwaka huo wa 2008....sema tatizo kubwa kwa waandishi wa-Tz ni kutoipa kipaumbele "developing story" !!

Asante Mkuu kwa kutujuza alipo Rama mla nyama za watu, nilikuwa nikijiuliza huyu dogo aliendaga wapi? Ila Leo Nina majibu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,430
2,000
Sasa hii ni simulizi gani haielezi huyo Rama alifanya nini na alikula nyama za watu vipi bali inaeleza tu kafungwa jela.

Au mleta mada unadhani kila member humu anamfahamu huyo Rama?
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
16,968
2,000
Jamani wengine ni watoto wadogo au walikua chini ya mawe hata taarifa ya habari hawakuweza kuwa na access nayo.

Nakumbuka hii ishu ilirushwa ITV. Kwamba kuna mtoto amekutwa na kichwa kwenye kisado, na alikamatwa na walinzi wa hospitali ya Mhimbili.

Ila kama mjuavyo waandishi wa Tz, hakuna aliyewahoji walinzi wala Rama, although in their defence wanaweza dai hawakumhoji dogo kwakua dogo alikua kama kapumbazwa kiasi walidai ni ushirikina ndiyo ulitumika kumfanya dogo aweze kua na ujasiri wa kwenda kufuata kichwa mle ndani.

Anyway, sijasikia stori yake muda mrefu na nilishasahau.
 

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
5,127
2,000
Jamani wengine ni watoto wadogo au walikua chini ya mawe hata taarifa ya habari hawakuweza kuwa na access nayo.

Nakumbuka hii ishu ilirushwa ITV. Kwamba kuna mtoto amekutwa na kichwa kwenye kisado, na alikamatwa na walinzi wa hospitali ya Mhimbili.

Ila kama mjuavyo waandishi wa Tz, hakuna aliyewahoji walinzi wala Rama, although in their defence wanaweza dai hawakumhoji dogo kwakua dogo alikua kama kapumbazwa kiasi walidai ni ushirikina ndiyo ulitumika kumfanya dogo aweze kua na ujasiri wa kwenda kufuata kichwa mle ndani.

Anyway, sijasikia stori yake muda mrefu na nilishasahau.
Hata mimi nilishasahau habari za huyu dogo ila baada ya kusoma huu uzi taswira yake yote imenijia kichwani ile siku aliyokamatwa pale muhimbili. Ni tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom