Simulizi : Beyond Love (Zaidi Ya Mapenzi)

SEHEMU YA 43 YA 50

“Lakini nina wazo mume wangu,” mama yake Mariam akamwambia mumewe.

“Wazo gani mama Mariam?”

“Tunahangaika na tutahangaika sana, lakini ipo njia moja tu tunayopaswa kuitumia!”

“Ipi?”

“Tumesahau kumuomba Mungu, nakuhakikishia kama tukimshirikisha yeye kila kitu kitakuwa sawa, ni lazima tuwe karibu na Mungu baba Mariam.”

“Ni kweli, tumefanya kosa kubwa sana mke wangu, hatuna haja ya kupoteza muda, tunatakiwa kuanza kusali sasa hivi.”

“Haya simama tuombe mume wangu.” Wote wakasimama, kisha wakashikana mikono, mama Marim akaongoza sala.

Walianza na nyimbo za kuabudu, ambazo waliimba kwa robo saa kabla ya kuingia kwenye maombi yaliyowachukua saa nzima! Kila mmoja alikuwa akimuomba Mungu wake, amuepushie Mariam kwenye mateso na shida zote na hata kama alikuwa na mawazo mabaya ambayo yalikuwa yanateka akili yake, yashindwe!

“Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth tumeomba na kushukuru...”

“Aaamen...” baba Mariam akaitikia.

“Mungu ndiyo kila kitu mume wangu, nakuhakikishia tutaona majibu yake, Mungu wetu siyo mwongo, maana yeye mwenyewe tumuombe naye atatujibu, hawezi kutoa ahadi ya uongo, lazima atatujibu tu, lazima.”

“Ni kweli mke wangu, twende chumbani tukalale.”

Wakaongozana hadi chumbani kulala, angalau sasa mioyo yao ilikuwa na amani baada ya kufanya maombi.

*******

“Acha!” Mariam alisikia sauti hiyo ambayo hakuelewa ilitokea wapi.

Alihisi alikuwa ndotoni, hivyo akapuuza, akaamua kuipandisha glasi yake hadi kinywani, akiwa anataka kuanza kunywa, ghafla akahisi mkono wake ukitetemeka kwa kasi, ukazidisha kasi hadi glasi ikaanguka chini.

Mariam hakuelewa kilichotokea, chumba kizima kikawa kinanuka harufu ya sumu ya panya. Ilikuwa harufu mbaya sana, Mariam alichanganyikiwa, hakujua kwanini jambo lile lilitokea, alichoamua kwa muda huo, ilikuwa ni kurudi tena dukani na kununua sumu nyingine ili aweze kuendelea na zoezi lake.

Akiwa ndiyo anataka kufungua mlango ili atoke nje, akashangaa miguu yake inakuwa mizito, sauti nyingine tena ikasisika, tena kwa sauti ya juu na ya msisitizo zaidi; “Wewe ni msichana mzuri sana, unayevutia na ambaye una mpenzi mzuri sana, siyo kweli kwamba baada ya kufa utakuwa umekimbia matatizo, achana na mawazo hayo.

“Unachotakiwa kufanya sasa ni kwenda kwa wazazi wako, uwaangukie na kuwaomba radhi, bado una nafasi ya kuendelea kuishi. Mariam badili uamuzi wako...” Mariam alizidi kuchanganyikiwa, hakuweza kuelewa ilikuwa sauti ya nani na wapi ilipotokea.

Katika hali ambayo hata yeye mwenyewe hakuitegemea, alijikuta akiahirisha kujiua, moyo wake ukawa umekunjamana na kuhisi uhitaji wa radhi za wazazi wake.

“Lazima nirudi nyumbani, lazima tena usiku huu huu wa leo,” Mariam akawaza na kuchukua begi lake dogo lililokuwa na nguo zake chache kisha akafunga chumba na kushuka hadi chini ambapo aliingia kwenye taxi.

“Wapi sister?”

“Jeti, Lumo!”

“Poa.” Dereva akawasha gari na safari ya kwenda nyumbani kwa wazazi wake ikaanza.

Kwa kuwa hakukuwa na foleni, dakika ishirini zilitosha kabisa kutoka Magomeni Mapipa katika hoteli aliyokuwa akiishi hadi Jeti, Lumo. Tayari ilikuwa imeshafika saa saba kasoro za usiku. Kwa bahati nzuri, nyumba yao ilikuwa barabarani, hivyo alimlipa dereva akashuka na kuanza kugonga geti.

Muda mfupi baadaye baba yake akafika getini.

“Nani usiku wote huu?”

“Ni mimi baba!”

“Mariam!”

“Ndiyo!”

“Karibu mwanangu, ngoja nikufungulie!” Mlango ukafunguliwa na Mariam akaingia.

Mapokezi aliyokutana nayo hakuyategemea kabisa, baba yake akampokea begi na kuingia naye hadi ndani ambapo alimwita mama Mariam ambaye hakuamini kilichokuwa mbele yake.

“Mariam ni wewe mwanangu? Karibu nyumbani mama...” mama yake alisema huku machozi yakianza kumlengalenga.

“Ahsante sana mama, nawaombeni msamaha wazazi wangu, najua ni kiasi gani nimewavunjia heshima, nimewakosea adabu na hata kuwadhalilisha mbele ya jamii. Nawaahidi nitakuwa mtoto mwema kwenu, naachana na mambo yote ya kale na sasa naanza upya maisha yangu.

“Kama siyo Mungu, kesho mngepata taarifa za kifo changu, tayari nilikuwa na sumu ambayo niliitayarisha kwa ajili ya kujiua, nikasikia sauti ya ajabu ikiniambia niache, hapo ndipo nilipoamua kurudi kwenu wazazi wangu.

“Naamini mkinisamehe na kunibariki nitaishi maisha mapya,” Mariam alikuwa akisema huku akilia. Mama yake naye alikuwa akilia sana, maneno ya mwanaye yalikuwa makali sana na hakuamini kuwa mwanaye alipitia mateso makali kiasi kile.

“Mwanangu, sisi tumekwishakusamehe siku nyingi sana, huna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya hilo,” baba yake Mariam akasema.

“Nashukuru kusikia hivyo wazazi wangu, lakini nilikuwa na ombi moja ambalo nawaomba sana mnikubalie!”

“Ombi gani mwanangu, we sema tu!”

“Naomba mniahidi kwanza kuwa mtanikubalia!”

“Sema tu!”

“Au basi, tuache tu...” Mariam akasema akionekana kuwa na wasiwasi sana.

“Akha! Kwanini tena.”

“Basi tu!” Mariam akaanza kulia, tena kwa sauti ya juu kama ambaye alikuwa amefiwa.

Wazazi wake walishindwa kuelewa alikuwa na tatizo gani kubwa kiasi cha kushindwa kusema. Vichwa vyao vikawaka moto, mwenye siri hiyo alikuwa ni Mariam mwenyewe.







Furaha waliyokuwa nayo wazazi wa Mariam ilikuwa haielezeki, lakini sasa ilianza kuyeyuka taratibu. Kutokuwa na mwanao kwa muda mrefu kiasi kile tena wakiwa hawafahamu mahali alipo lilikuwa pigo kubwa sana kwao, lakini kilichowachanganya zaidi vichwa vyao ni Mariam kusema ana jambo alilotaka kuwaomba wazazi wake lakini ghafla anakataa.
 
SEHEMU YA 44 YA 50

Vichwa vyao vikawaza upande wa mabaya zaidi, kwamba yawezekana alikuwa katika hali ya matatizo makubwa na alikuwa akiogopa kuwashtua wazazi wake. Mama akaanza kulia kwa uchungu akiamini lazima Mariam alikuwa na tatizo kubwa lililomkabili.

“Lakini Mariam ni nini? Sema kinachokusumbua basi mwanangu!” Baba yake akasema kwa uchungu sana akimwangalia Mariam usoni.

“Acha tu baba, naona niachane na hayo mambo!”

“Kwani kuna tatizo?”

“Halijawa tatizo baba!”

“Halijawa tatizo? Unamaanisha nini kusema hivyo?”

“Yaani halijafikia kuwa tatizo na ndiyo nimeona niliache ili lisiwe tatizo!”

“Hapana, wewe ni mtoto wetu wa pekee, na mimi na mama yako hatutaki kukuona unasononeka, kama kuna kitu kinakusumbua ni bora ukaeleza kwa uwazi ili tujue jinsi ya kukusaidia!”

“Baba ni usiku saa hizi, naomba tuzungumze kesho.”

“Lakini ingekuwa ni afadhali tulale tukijua mzigo ulionao umeshautua!”

“Basi baba, acha niwaambie lakini naomba mniahidi kitu kimoja kwanza.”

“Nini?”

“Kwamba mtanikubalia.”

“Sema tu mwanangu, kama nilivyokuambia, hatupendi kukuona ukiwa huna furaha kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu...eleza nini tatizo mwanangu!”

“Baba ni kweli niliwakosea kwa mambo mengi, lakini pia napenda kuwaeleza kilichopo moyoni mwangu!”

“Enheee...”

“Nakubali Tom alinitesa, alininyanyasa na kunifanyia kila aina ya ubaya lakini mama na baba yangu, bado kuna kitu moyoni mwangu. Bado nahisi kumpenda sana Tom!” Mariam alizungumza kwa sauti iliyojaa huruma sana.

“Bado unafanya nini? Hivi una akili kweli Mariam? Ni mangapi amekufanyia yule mpuuzi, una sababu ya kuendelea kuona kwamba eti ana nafasi kwako, kwanini hutaki kutumia akili yako mwanangu?” Mama yake akamwambia akiwa ameukunja uso kwa hasira.

“Lakini mama nampenda!”

“Unapenda matatizo? Hivi we’ mtoto una akili gani?”

“Basi mama, tuachane nayo...nimekubali kuachana na Tom, lakini naomba mniruhusu kufanya jambo moja!”

“Jambo gani?”

“Naombeni mniruhusu nimhudumie mpaka apone, lakini sitakuwa na uhusiano naye kabisa!”

“Hilo haliwezekani.”

“Sasa nini kinawezekana?”

“Hakuna kinachowezekana.”

Walizozana kwa muda mrefu sana, hadi saa tisa za usiku walipoingia vyumbani kulala bila kuwepo na maafikiano. Asubuhi hakuna aliyezungumzia juu ya jambo hilo, lakini akilini Mariam aliamua kukaa kimya akiwaza jinsi atakavyomhudumia Tom bila wazazi wake kufahamu.

Tom alikuwa kila kitu katika maisha ya Mariam, alimpenda kwa mapenzi yake yote na wala hakuweza kujua ni kwanini alijikuta akimpenda Tom kwa kiasi kile. Hata hivyo hakutaka kujiuliza maswali hayo, alichojua yeye ni kumpenda Tom tu.

“Nampenda sana Tom wangu, ukweli huu nitausimamia siku zote na ni lazima nihakikishe naulinda msimamo wangu huu. Najua siku moja Tom ataujua ukweli kwamba mimi ndiye mwanamke wa maisha yake, mimi pekee ndiye ninayempenda na wala siyo Mayasa kama anavyofikiria, hili litadhihirika!” Mayasa akawaza.

Kwa wiki nzima Mariam alikuwa anashinda nyumbani bila kwenda hospitalini, moyo wake ulimuuma sana lakini aliamua kufanya hivyo ili kuwapumbaza wazazi wake wasahau kabisa kuhusu Tom. Siku moja asubuhi baada ya baba yake kwenda kazini, Mariam alimuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumuona rafiki yake.

“Nani?”

“Clara mama!”

“Lakini kwanini yeye asije?”

“Mama yake ni mgonjwa, amenipigia simu jana kunipa taarifa na kama unavyojua sisi ni marafiki, naona hii ni nafasi yangu ya kuonyesha ninavyomjali kwa kumfariji mama!” Mariam akadanganya.

“Sawa mwanangu, lakini jitahidi basi kuwahi!”

“Usijali mama!”

Mariam akajiandaa kisha akatoka na kwenda zake Muhimbili tena akitumia gari la mama yake. Aliingia wodini na kumkuta Tom akiwa amelala kimya kitadani, bado alikuwa akipumulia mashine. Mariam akapiga magoti pembeni ya kitanda chake, akambusu usoni huku akitamka; “Nakupenda sana Tom wangu, najua yote uliyonifanyia ni kwa sababu ya shetani tu, wewe na akili yako huwezi kufanya hayo.

“Namwomba Mungu akujalie, siku moja usimame tena, uone jinsi ninavyokupenda, naamini siku hiyo itafika na utajua ukweli kwamba mimi ndiye mwanamke pekee ambaye nakupenda kwa moyo wangu wote.”

Mariam alijikuta akilia akimtizama Tom. Zilikuwa kumbukumbu za kuhuzunisha sana katika maisha yake, alitamani sana siku moja Tom aamke na warudiane tena kama mtu na mke wake. Hilo aliamini lazima siku moja litatokea. Baadaye akatoka na kwenda ofisini kwa daktari wake ili kupata maelezo ya maendeleo ya Tom.
 
SEHEMU YA 45 YA 50
“Ndiyo Dokta anaendeleaje sasa?”

“Matumaini yapo, lakini kama ulivyomuona bado hajazinduka.”

“Unadhani itamchukua muda gani?”

“Kwa kweli siyo rahisi kukuambia maana bado kuna vipimo vingine vinaendelea kufanyika, ila tunashukuru kidogo mapigo yake yanaanza kurudi vizuri, nafikiri baada ya wiki mbili tatu, ataweza kuanza kupumua mwenyewe.”

“Nitashukuru sana dokta, kwa hiyo atapona?”

“Mategemeo yetu yapo kwa Mungu dada yangu, nafikiri ni vyema kama tutamwachia yeye!”

“Nashukuru sana dokta!”

“Ok!”

Mariam aliendelea kukaa pale hospitalini hadi usiku kabisa, baada ya kuhakikisha Tom alikuwa ameshaoga na kula kwa kupitia mpira. Akarudi nyumbani usiku sana, maelewano na mama yake hayakuwa mazuri lakini alisingizia kwamba hali ya mama wa rafiki yake haikuwa nzuri, hivyo asingeweza kumuacha akiwa katika hali mbaya peke yake.

“Lakini kwanini hukutoa taarifa?”

“Nilipitiwa mama!”

“Ndiyo na simu uzime?”

“Iliisha chaji mama!”

“Angalia sana Mariam, sitaki unigombanishe na baba yako!”

“Nisamehe mama.”

Mariam aliendelea kumhudumia Tom kila siku, alifanya hivyo kwa siri kubwa hadi siku mama yake alipogundua na kumwambia baba yake. Mariam akatakiwa kuamua jambo moja, kuondoka nyumbani aendelee kumhudumia Tom au abaki nyumbani lakini aachane na Tom.

“Mama nimechoka na haya masimango yenu, sili chakuka kikashuka...basi bora niondoke hapa kwenu, nikamsaidie Tom wangu, kwanza kumbukeni nimefunga naye ndoa. Yule ni mume wangu halali, na nilimuahidi kuwa nitaishi naye katika shida na raha, sasa kwanini nimtese?”

“Kama unayajua hayo, mbona yeye alikusaliti? Mbona yeye alikutesa?”

“Umeshasema yeye...kwani huoni kama kuna tofauti kubwa kati ya yeye na mimi, ninafanya kile nilichoahidi na yeye kwa nafasi yake anatakiwa kufanya alichoniahidi.”

“Kwahiyo?”

“Narudi Mbezi, nyumbani kwangu, nitaishi maisha yoyote na nitaendelea kumhudumia mpaka atakapopona, hayo ndiyo maamuzi yangu,” Mariam alionyesha msimamo wa hali ya juu sana, ilifikia hatua wazazi wake wakashindwa kumzuia zaidi.

Mariam akaondoka na kwenda zake Mbezi katika nyumba ya Tom waliyokuwa wakiishi. Nyumba ilikuwa chafu na haikuwa katika mpangilio mzuri, baadhi ya vitu vilikuwa havipo. Hakusumbua sana kichwa kugundua kwamba ilikuwa ni kazi ya Mayasa.

Alichokifanya ni kuhakikisha nyumba inakuwa safi, kisha kazi yake kubwa ikawa ni kumhudumia Tom.

********

MIAKA MINNE BAADAYE

Kama kawaida, asubuhi hiyo Mariam alikwenda Muhimbili, hiyo ilikuwa ni kama ndiyo kazi yake. Siku hiyo alihisi moyo wake ukienda kasi sana, alijaribu kujiuliza sababu za hali hiyo kumtokea lakini hakupata majibu. Akaingia wodini kisha akaketi kitandani akimtizama Tom aliyekuwa akipumua kwa kutumia mashine.

Kwa miaka minne sasa alilala kitandani bila kujitambua! Hata hali ya afya yake haikuwa nzuri tena, Tom alitia huruma! Katika hali ya kushangaza sana, akaona macho ya Tom yanafumbuka taratibu. Tom akatabasamu, lakini alipogundua kwamba aliyekaa mbele yake alikuwa ni Mariam akakasirika sana.

“We’ mwanamke umefuata nini hapa? Ondoka utakuja kupigwa na Mayasa wewe...Mayasa ni mkorofi, kwanini unaendelea kunifuatafuata? Toka...toka Mariam usije kunisababishia matatizo...” Tom akazungumza kwa sauti kubwa huku akiyatoa macho.

Hakujua kilichotokea katika maisha yake tena, hakuwa na habari kwamba alilala kitandania kwa zaidi ya miaka minne. Aliendelea kufoka huku akimuamrisha Mariam aondoke. Mariam alijikuta akishindwa kuzungumza, machozi yakaanza kumtoka.

“Tom mume wangu, Mayasa hayupo hapa na wala hawezi kutokea Tom...mimi ndiye Mariam, mwanamke wa maisha yako, ambaye nakupenda kwa mapenzi yangu yote. Nakupenda kwa mapenzi ya kweli, sikujali pesa wala utajiri wako Tom, lakini Mayasa uliyemuona anafaa, leo hayupo unateseka na mimi kwa miaka yote uliyokuwa umelala.

“Mayasa ameuza kila kitu, amekuachia kibanda cha kulala tu, hakuna kitu tena mpenzi wangu. Lakini yote hayo najua ni shetani, ndiyo maana nipo hapa leo kukuonyesha kwamba mimi nina mapenzi ya dhati kwako,” Mariam aliongea akilia.

Tom alishindwa kuelewa alichokuwa akizungumza Mariam, ni kama alikuwa akizungumza vitu vigeni. Amelala miaka minne kitandani? Kivipi? Hilo hakulielewa na wala hakutaka kulipa nafasi kabisa akilini mwake.

“Hivi una kichaa Mariam? Unavyosema Mayasa ameuza vitu vyangu unamaanisha nini? Nimekuambia toka hapa Mayasa atakukuta na kukufanyia fujo...ni bora ukaondoka Mariam...” Tom alisema maneno hayo kisha akajitahidi kuamka, lakini akashindwa!

Hapo akagundua kwamba alikuwa amelazwa hospitalini tena alikuwa akipumua kwa kutumia mashine! Hakujua kilichotokea, lakini alivyotulia kwa muda akakumbuka alivyovamiwa na majambazi na kurushiwa risasi akiwa getini kwake!

Tom akaanza kulia. Mariam naye akaungana naye. Machozi yakatawala wodini.

“Tom unanipenda?” Mariam akamwuliza Tom, lakini hakujibu zaidi ya kuendelea kulia.



“Tom niambie basi kama unanipenda?” Mariam anazidi kumkazania Tom swali hilo huku mvua ya machozi ikiendelea machoni mwake.Tom hajibu kitu zaidi ya kuendelea kulia kama mtoto mdogo!“Tazama ninavyokupenda Tom, umenisaliti,ukaniletea mwanamke mpaka ndani, ukanifukuza lakini yote hayo nilishayasahemehe, kilichokuwa ndani ya moyo wangu ni upendo wa dhati, upendo
 
SEHEMU YA 46 YA 50

ambao siku zote umekuwa silaha yangu yakweli, umeniwezesha kuwa mvumilivu na mwenye ahadi za kweli, niliuahidi moyo wangu kutokukusaliti asilani na ndivyo nilivyofanya mpenzi wangu.“Ni miaka minne umelala hapa hospitalini, ukiwa huna kumbukumbu ya jambo lolote lile, nikihangaika na wewe kwa kila hali, nikawa tayari kugombana na wazazi wangu kwa ajili yako Tom, naomba uaminikwamba nakupenda, upendo wa dhati kutoka katikati ya moyo wangu...nakupendasana Tom, naomba uniamini kwa hilo.”Mariam alikuwa na uchungu mwingi sana moyoni mwake, pamoja na uchungu aliokuwa nao, ilikuwa ni siku ya furaha kubwa katika maisha yake, hakutegemea kuisikia tena sauti ya Tom, kumuona akifumbua macho yake mazuri na kumtizama uso wake. Alijisikia furaha isiyona kifani, kwake Tom alikuwa mpenzi mwema, awe mgonjwa au katika hali yoyote, alichojali ni kumuona Tom wake akiwa mzima!“Hujanijibu bado Tom wangu, niambie basiunanipenda?” Mariam akamwuliza tena.“Nakupenda Mariam!”“Nashukuru kusikia hivyo,” Mariam akasema kisha akambusu katikati ya midomo yake.“Nakupenda pia mpenzi wangu, wewe ni wangu wa maisha, nilijua Mayasa alikuwa anakupoteza na nina imani haikuwa akili yako mume wangu, lazima yule malaya atakuwa alikuwekea kitu.“Hata hao majambazi waliokuvamia, nina wasiwasi nao sana, yawezekana ikawa Mayasa alitengeneza mchezo!”“Huna haja ya kuwaza sana mambo yaliyopita mpenzi, tuyaache kama yalivyo. Enhee Mayasa yupo wapi?”“Mayasa?”“Ndiyo!”“Ngoja nikupe stori!” Mariam akaanza kumsimulia Tom kila kitu baada ya yeye kuamua kwenda kijijini kwao Matombo, Morogoro, akamweka wazi kwamba alisikia Mayasa alitoroka na aliuza mali zote akiwa mgonjwa.Hakumficha kitu chochote, aliweka wazi jinsi alivyoteseka kwa ajili yake. Wote walilia sana. Tom akaona thamani ya penzi la Mariam kwake, akauahidi moyo wake kuwa mtulivu na kuendelea kuwa na Mariam pekee, hakutaka kuhaingaika tena.“Enhee na mama yuko wapi?”“Mama?”“Ndiyo!”“...Yupo nyumbani!” Baada ya kufikiria sana,Mariam akaamua kudanganya, hakuona sababu ya kumweleza ukweli juu ya kifo cha mama yake, kwani alijua wazi ni kiasi gani angemuumiza.“Mbona hukuja naye?”“Huwa tunakuja kwa zamu, wiki hii ni yangu, wiki ijayo ni yake, ila akijua kwamba umeshapata fahamu lazima atakuja!”“Nitafurahi sana!”“Pole sana mpenzi wangu, najua ni kiasi gani ulivyokuwa katika mateso makali kwa muda mrefu!”“Usijali Mariam wangu, nashukuru pia kwa kuonyesha penzi lako la dhati, hakika haya ni zaidi ya mapenzi, wewe ni mpenzi wangu wa kweli!” Tom akasema akitoa machozi.“Nashukuru kwa kutambua hilo mpenzi, nitakupenda milele!”“Hata mimi pia!”Wakiwa katikati ya maongezi, Muuguzi alifika na kushangazwa na hali aliyomkutanayo Tom, hakutarajia kumuona mgonjwa wake akiwa amerejewa na fahamu baada ya kulala kitandani kwa siku zote hizo. Akakimbia ofisini kwa daktari haraka kwenda kumpa taarifa hizo.“Yule mgonjwa amezinduka!”“Yupi?”“Tom!”“Kweli?”“Ndiyo dokta!”“Hebu twende!” Dokta akaongozana na Muuguzi hadi kitandani kwa Tom.Alipomkuta akizungumza na Mariam, akamkataza.“Mariam mwache kwanza apumzike, bado hajawa na nguvu ya kuzungumza sana kwa wakati huu, anahitaji muda mwingi wa kupumzika kwanza!”“Sawa dokta!”“Hebu tupishe kidogo!”“Sawa!”“Enhee Tom, unajisikiaje?”“Nina nafuu sasa, Mungu amenipigania!”“Ni kweli lazima umshukuru sana Mungu maana yeye ndiye aliyekupa uzima ulionao!”“Amen!”“Pole sana!”“Nashukuru sana dokta!”Baada ya pale Daktari alimwita Mariam ofisini kwake, kumpa taarifa za maendeleoya Tom.“Mariam kwanza tunamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha Tom kurejewa na fahamu tena, lakini kuna jambo moja lazima ulijue, mgonjwa wako amepooza kuanzia shingoni hadi miguuni, kwasasa kinachofanya kazi ni kichwa tu, lakini napenda kukutoa wasiwasi kwamba, kama Mungu huyo huyo ndiye aliyemzindua leo baada ya kulala miaka minne kitandani, basi Mungu huyo huyo ndiye atakayempa nafuu tena. Kifupi tutegemee muujiza wa Mungu!” Daktari akasema kwa utulivu sana.Mariam alikaa kimya kwa muda akifikiria, ni kweli Tom alikuwa na tatizo, lakini kwake halikuwa tatizo kubwa sana kama angekufa kabisa! Akamshukuru Mungu kwa kumzindua Tom wake, tegemeo kubwa lilikuwa kwake.“Hakuna shida daktari, nimefurahi kumuonaakifumbua macho yake tena, mambo mengine hayo, nayaacha mikononi mwa Mungu mwenyewe!”“Mungu atawasaidia!”“Nashukuru sana, kazi njema.”Magazeti ya mchana ya siku hiyo yalipambwa na habari ya Tom kuzinduka, haikujulikana ni muda gani waliingia wodinina kuwapiga picha Mariam na Tom, wakatiMariam alipokuwa akimbusu Tom mashavuni.Gazeti la Za Leo ndilo lililokuwa na picha hiyo, pamoja na kichwa kikubwa chahabari kilichosomeka; HAYA NI ZAIDI YAMAPENZI! Lilikuwa gazeti pekee lililouzika zaidi kutokana na kuwa na picha ya wapenzi hao wakiwa pamoja hospitalini asubuhi ya siku hiyo.*******Usiku Mariam alishindwa kulala, alikuwa anawaza ni jinsi gani angeweza kumdanganya Tom kuhusu mama yake, hakika alikuwa na kazi kubwa sana ya kuzungumza naye na
 
SEHEMU YA 47 YA 50

kumweleza ukweli.Hata hivyo, pamoja na kuwaza kwa muda mrefu, baadaye alipitiwa na usingizi mzito.Asubuhi yake aliamka na kujiandaa kama kawaida kisha akaenda zake hospitalini. Akamkuta Tom akiwa amelala kitandani macho yake yakiangalia juu.“Vipi sweetie?”“Salama mama vipi?”“Shwari lakini siyo shwari!”“Kwanini?”“Sijielewielewi kabisa, mwili wangu kama umekufa ganzi hivi!”“Ni kawaida mpenzi, umelala kitandani kwamuda mrefu sasa, tena nilikuwa nazungumza na Dokta jana, kasema hali hiyo ni ya kawaida na itapotea polepole ingawa itachukua muda kidogo!”“Siamini...” Tom akasema.“Naomba kukuliza Tom, unaamini kama kuna Mungu?”“Ndiyo!”“Unaamini yupo Roho Mtakatifu?”“Ndiyo!”“Pia unaamini kwamba Mungu alimtuma mwanaye mpendwa Yesu Kristo ili afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu?”“Ndiyo!”“Kwahiyo unaamini juu ya Utatu Mtakatifu?”“Hakika!”“Basi mwachie haya mambo Mungu mwenyewe, naamini utukufu wake utadhihrika!”“Ni kweli mpenzi wangu, ahsante sana kwakunipa moyo, acha Mungu afanye awezavyo, najua hataniacha nikaabika!”“Nashukuru kwa kutambua hilo mpenzi!”“Enhee mama yupo wapi?”“Unasema?”“Mama yupo wapi?”Mariam hakujibu, alikaa kimya akiwa ameyatuliza macho yake usoni mwa Tom, huku machozi yakianza kumtiririka machoni mwake. Tom alishindwa kuelewa maana ya machozi ya Mariam.“Sasa unalia nini mpenzi wangu, Mungu atanisaidia, huna sababu ya kulia... kwaninihujaja na mama? Nina hamu sana na mamayangu!” Maneno ya Tom yalikuwa msumari wa moto moyoni mwa Mariam, kwani alikuwa na siri nzito sana ambayo kuitoa kwake lazima awe amejiandaa vya kutosha!Haikuwa jambo jepesi kumwambia Tom, moja kwa moja kwamba mama yake alishafariki, tena alizikwa na Halmashauri ya Jiji. Hilo lilikuwa jambo gumu sana.Je, nini kitatokea? Mariam atamweleza ukweli? Nini kitafuata katika maisha yao?







Kama mapenzi ni raha, basi kwa Mariam hayakuwa na maana yoyote, kwani siku zote yameendelea kuwa msumari wa moto katika maisha yake. Kila anapokaribia kupata faraja, lazima kuna kitu kinaingia na kuharibu furaha hiyo. Mariam anakuwa mtu wa kulia kila siku. Machozi hayakauki machoni mwake. Yote hayo yanasababishwa na mwanaume mmoja tu, Tom, ambaye hathamini wala kuheshimu penzi lake.

Anapata mateso makubwa, kusimangwa, kufukuzwa nyumbani na mengine mengi. Jambo linalosababisha aamue kukimbia mji na kwenda kwa bibi yake anayeishi Matombo, Morogoro. Akiwa huko anaanza maisha mapya na kufanikiwa kumsahau kabisa hadi pale alipoona gazeti mjini alipotumwa na bibi yake.

Matatizo yakafumuka! Akaanguka na kupoteza fahamu ambapo kijana Ramsey ndiye aliyejitolea kumsaidia hadi alipopata nafuu akasafiri naye hadi Dar es Salaam na kwenda kumwangalia Tom aliyekuwa amelazwa.

Mariam anakuwa tayari kugombana na wazazi wake kwa ajili ya Tom, anaamua kuishi hotelini na Ramsey ambaye baadaye anamtaka kimapenzi jambo lililopingwa vikali na Mariam. Hata hivyo baadaye anamkubalia, lakini hakuwa tayari kufanya naye mapenzi, kitu kilichomuudhi sana Ramsey aliyeamua kumuacha na kurudi zake Morogoro.

Mariam akaamua kujiua, lakini kabla ya hajafanya hivyo anajikuta akijisikia mwenye dhambi sana kujitoa uhai wake. Akaamua kuahirisha, hapo ndipo alipoona umuhimu wa kwenda kwa wazazi wake ambao walimpokea kwa mikono miwili.

Akiwa nyumbani kwa wazazi wake, anapanga safari ya uongo ya kwenda kwa rafiki yake Clara, lakini ukweli ni kwamba alikuwa anakwenda Muhimbili. Huo ukawa ndiyo utaratibu wake wa kila siku, hadi siku apoamua kusema ukweli mbele ya mama yake.

Mzozo mkubwa unaibuka lakini mwisho wake, Mariam anaamua kurudi nyumbani kwake Mbezi, anakuta nyumba chafu sana yenye mpangilio mbovu, anaweka vitu sawa na kufanya usafi kisha anaanza maisha upya huku jambo kubwa linalokuwa mbele yake likiwa ni kumhudumia Tom.

Miaka minne badaye, Tom anazinduka mbele ya Mariam, anamfukuza akimwambia aondoke kwani Mayasa akifika ingekuwa ugomvi! Kwa kifupi Tom amekupoteza kumbukumbu kabisa, lakini baadaye anapata picha kwamba alivamiwa na majambazi usiku akiwa anarudi nyumbani.

Tom anapooza kuanzia shingoni hadi miguuni, taarifa ambazo Mariam alipewa! Mariam hamwelezi Tom ukweli juu ya kifo cha mama yake. Kila anapomuuliza, anajaribu kumficha! Lilikuwa jambo gumu sana kumweleza Tom kwamba mama yake alifariki dunia, tena alizikwa na Halmashauri ya Jiji. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO....



Hakukuwa na kitu kingine chenye thamani katika maisha ya Tom kama mama yake, hapakuwa na mtu muhimu zaidi maishani mwake kama mama yake! Kwa Tom, mama yake alikuwa kila kitu. Alikuwa uhai wake, furaha yake, kila kitu chake. Kumuona mama yake akiwa hai tu, ilitosha kabisa kumfanya mwenye furaha siku zote.

Sasa mama yake hayupo tena duniani, mbaya zaidi hajui na wala hana taarifa zozote juu ya kutokuwepo kwa mama yake duniani. Pamoja na kutokujua hilo, moyo wake ulikuwa mzito kuliko kawaida, alihisi kama ganzi fulani ikizunguka moyoni mwake, alihisi kitu.
 
SEHEMU YA 48 YA 50

Tom akayatoa macho yake katika hali ambayo hata Mariam mwenyewe alishindwa kuelewa kilichokuwa akilini mwake. Midomo yake ikaanza kutingishika.

“Mariam!”

“Nakusikiliza mpenzi wangu!”

“Unanipenda?”

“Hata moyo wako unalitambua hilo!”

“Utakuwa tayari kuniacha niendelee kuumia?”

“Hapana!”

“Unaweza kumdanganya mpenzi wako?”

“Hapana!”

“Nahitaji kujua ukweli, mama yangu yupo wapi?!” Tom alisema akiwa hana chembe ya furaha usoni mwake.

“Unamaana gani?”

“Nataka kujua mama yangu alipo!”

“Ngoja nikuambie ukweli mpenzi wangu, jana nilienda nyumbani nikiwa na furaha sana, nilitamani sana kukutana na mama ili nimweleze kuhusu hali yako, lakini nilipofika nyumbani sikumkuta mama, aliacha maagizo kwamba anakwenda nyumbani Musoma, lakini majuzi alikuwa akinieleza nia yake ya kuanza kukushughulikia kienyeji, nadhani atakuwa huko,” Mariam akasema maneno hayo akiwa macho makavu.

Haikuwa rahisi kupingana naye, hasa kutokana na jinsi alivyokuwa akizungumza kwa kujiamini huku macho yake akiwa ameyatuliza usoni mwa Tom ambaye alianza kuamini maneno ya Mariam.

“Sawa mpenzi wangu, kama ni kweli, lakini kama ni uongo ni wazi kwamba hunipendi!”

“Nakupenda mpenzi wangu!”

“Lakini kuna kitu nahisi!”

“Ondoa hisia nyingine zozote nje ya penzi lako la kweli kwangu mpenzi wangu!”

“Ok!” Tom akajibu.

Jambo hilo likaisha wakiwa na maelewano kwa pamoja, Mariam akambusu Tom midomoni mwake, macho yake yalikuwa yanazungumza jambo, lakini bado akaongezea kwa kinywa chake.

“Nakupenda sana Tom!”

“Nakupenda pia Mariam wangu!”

******

Tom aliendelea kukaa hospitalini kwa mwezi mzima zaidi huku hali yake ikiendelea vizuri lakini hakuweza kuinuka kitandani. Marim alikuwa msaada pekee kwa Tom, lakini siku zote hakumweleza ukweli wa kifo cha mama yake.

Hiyo iliendelea kuwa siri iliyopo katikati ya moyo wake. Baada ya miezi miwili, Tom aliruhusiwa kurudi nyumbani kwa sharti la kupelekwa Kliniki kila baada ya mwezi mmoja kwa ajili ya kuangalia upya maendeleo ya afya yake.

Hilo ndilo lililofanyika, maisha hayakuwa mazuri nyumbani kwao kwani hawakuwa na uwezo kifedha wala vitega uchumi vya kuwaingizia kipato. Siku moja usiku wakati wa chakula cha usiku, Mariam alimweleza mumewe wazo alilokuwa nalo juu ya maisha yao.

Waliishi kwa upendo na Tom hakumkumbuka tena Mayasa, alimfananisha na shetani ambaye aliharibu maisha yake, kwake Mariam akawa ndiye kila kitu. Maisha yale magumu hayakumfurahisha kabisa Mariam, alitakiwa kufanya jambo moja muhimu sana ili kuyafanya maisha yao angalau yawe yenye furaha kutokana na kutengwa kwao na watu wanaowazunguka hasa wazazi wa Mariam ambao kwa wakati huo wangepaswa kuwa msaada pekee kwa maisha yao.

“Baby kuna kitu nimefikiria kwa muda mrefu sana na kupata ufumbuzi,” Mariam akamwambia Tom aliyekuwa ameegemea kwenye mto, akila.

“Ni nini hicho mpenzi wangu?”

“Tutaishi maisha haya hadi lini?”

“Unamaanisha nini mpenzi?”

“Maisha haya yasiyo na uhakika wa kesho, tutaendelea nayo hadi lini? Lazima nifanye kitu mpenzi wangu!”

“Umefikiria kufanya nini?”

“Nadhani ni bora nitafute kazi.”

“Sawa, naungana na wewe!”

Ndivyo ilivyokuwa, siku iliyofuata Mariam akaanza kutafuta kazi sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam, alituma maombi sehemu nyingi sana na mwishowe akaitwa katika Benki ya CRDB kwa ajili ya usaili. Baada ya kufanyiwa usaili akabahatika kuchaguliwa kuanza kazi rasmi kama Afisa Biashara wa Tawi la Vijana jijini Dar es Salaam.

Wiki moja baadaye Mariam akaanza kazi rasmi katika Benki ya CRDB Tawi la Vijana. Maisha yakabadilika, alichokifanya ni kumuajiri msichana wa kazi ambaye alikuwa akimhudumia mumewe Tom. Waliishi maisha ya furaha sana, kwake kumuona Tom akitabasamu ilitosha kabisa kumfanya awe mwenye furaha.

Kila ifikapo mwisho wa mwezi alihakikisha anampeleka hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi. Kila kitu kilikwenda sawa, lakini tatizo lilikuwa moja tu, kila Tom alipouliza kuhusu mama yake, alijibiwa kwamba yupo kijijini. Jioni moja, hali ilikuwa tofauti, Tom akamwambia kama ni kweli mama yake alikuwa amekwenda kijijini, basi aende akamfuate.

“Lakini alisema atakuja.”

“Kwani ni muda gani tangu nimetoka hospitalini?”

“Ni mrefu ndiyo!”

“Sasa kama ndivyo, unadhani mama anaweza kukaa muda mrefu kiasi hicho bila kuja kutizama hali yangu? Haiwezekani Mariam, kuna kitu unajaribu kunificha, naomba nieleze ukweli Mariam, mama yangu yupo wapi?” Tom alibadilika, alionyesha ukali ambao hata Mariam mwenyewe hakuutarajia kabisa.

Mariam akashindwa kuzungumza, akajikuta machozi yakianza kuchuruzika machoni mwake kama maji! Alianza pole pole, lakini akajikuta anaanza kulia kwa sauti kubwa zaidi huku akitaja jina la mama yake na Tom.

“Kwani kuna nini?”

Mariam hakujibu.

“Kuna kitu unajaribu kunificha Mariam, tafadhali naomba niambie ukweli!”

“Tom, sina sababu ya kuendelea kuificha siri hii!”

“Siri gani?”

“Juu ya mama!”

“Niambie basi, kuna nini?”
 
SEHEMU YA 49 YA 50

“Naomba usinifikirie vibaya Tom, ilikuwa lazima nitunze siri hii, lakini ni wazi kwamba isingewezekana kuendelea kukaa nayo kwa muda mrefu zaidi. Naomba upokee taarifa hii kama ilivyo. Uikubali, uiamini na uichukue kama ilivyo!”

“Mbona sikuelewi Mariam, hebu naomba nieleze kinachoendelea, achana na mafumbo ambayo ni giza kwangu!”

“Tom mpenzi wangu, nakuomba sana, usipaniki juu ya hili nitakalokuambia mume wangu!”

“Kama hutaki kusema acha...maana naona unanitibua sasa!”

“Siyo hivyo mpenzi, ni kwamba....mama alishafariki Tom!” Mariam akasema akihema kwa kasi sana.

“Unasemaje?”

“Mama alishafariki....” Mariam hakuweza kumalizia sentesi yake, tayari mvua ya mchozi ilishafunika macho yake.

Huzuni ikatanda chumba kizima.









“Kwanini ulinificha jambo hili siku zote?”

“Ilikuwa ni mapema sana kukuambia mpenzi wangu, lakini nakuomba sana tena sawa, piga moyo konde, huo ndiyo ukweli ambao hakuna kitu cha kuweza kuubadilisha!”

“Mama...umekufa nikiwa bado nakuhitaji mama yangu...bado nilikuwa nahitaji sana busara zako mama yangu...umeniacha na upweke mama! Sina la kufanya mama yangu, nenda mama nasi tupo njia moja na wewe!” Tom alisema maneno hayo akilia sana.

Kila alipokumbuka mapenzi ya mama yake kwake, alizidi kuchanganyikiwa, mama yake alikuwa kila kitu katika maisha yake, kila alipokumbuka shida na dhiki zote walizopitia ndivyo alivyozidi kupatwa na machungu. Tom alizidi kulia.

“Nyamaza mume wangu mpenzi, kashaenda huyo, Mungu amemwita katika ufalme wake, hakuna kinachoweza kumrudisha, mwache apumzike kwa amani. Kazi yetu kubwa kwa sasa ni kumwombea tu!”

“Mungu amlaze mahali pema peponi!”

“Amen!”

“Inabidi unipeleke mahali alipolala mama yangu, natakiwa kupaona, angalau ning’olee hata majani juu ya kaburi lake!”

“Naomba uvumilie na hili mpenzi wangu!”

“Lipi?”

“Mama amezikwa na Halmashauri ya Jiji!”

“Unasema?”

“Huo ndiyo ukweli Tom, wakati mama anafariki sikuwa Dar, nilipata taarifa hizi nikiwa Morogoro kama nilivyokuambia mwanzoni!”

“Mama yangu anazikwa kama mbwa? Anakosa heshima anayostahili binadamu? Nimekukosea nini Mungu wangu mimi jamani? Kwanini mambo haya yanatokea kwangu tu jamani? Kwanini? Kwanini lakini?” Tom alipiga kelele, lakini Mariam akajitahidi kumnyamazisha.

Ilikuwa kazi ngumu sana, lakini mwisho wake Tom akanyamaza. Kila alipokumbuka sura ya mama yake, Tom alikuwa akimwaga machozi. Mama yake alikuwa ni kila kitu katika maisha yake. Maisha yaliendelea kama kawaida, kasoro kubwa ikiwa ni ulemavu alionao Tom pamoja na kumkosa mama yake mzazi.

Lingine kubwa zaidi ni kwamba, mpaka wakati huo, wazazi wa Mariam waliamua kumtenga, hawakutaka kushirikiana naye kwa jambo lolote. Walimwachia maisha yake na Tom, ambaye kwao alikuwa sawa na shetani. Yote hayo hakuwa aliyeyaweka akilini wala kuona kama kuna tofauti kubwa sana katika maisha yao. Kwako upendo wa kweli ndiyo ulikuwa kila kitu.



MWAKA MMOJA BAADAYE

Jambo kubwa lililofanyika ndani ya mwaka mmoja, ilikuwa ni kurudisha uhusiano kati ya wazazi wa Mariam na wao, ilikuwa kazi ngumu sana, lakini kwa kupitia wazee wenye hekima, suala hilo liliisha bila matatizo. Wazazi wa Mariam wakawasamehe Tom na Mariam kwa yote yaliyotokea, wakafungua ukurasa mpya.

Wakawa wanatoa ushirikiano kwa kila kitu, hata katika mambo yaliyohusu fedha, kila kitu kikawa kimepita, wakawa karibu wakihangaikia afya ya Tom pamoja. Mpaka muda huo Tom alikuwa bado hajaamka kitandani, mwili wake ulikuwa umepooza.

Pamoja na juhudi za mkewe na wazazi wake kumuhangaikia katika Hospitali mbalimbali, ndani na nje ya nchi, lakini mafanikio yalikuwa hakuna. Mariam alifikia hatua ya kuchukua mkopo kazini kwao ili aweze kumhangaikia Tom wake, angalau aweze kuamka, lakini ilishindikana.

Hilo lilizidi kuongeza maumivu katika ndoa yao, ambayo yeye aliifananisha na ndoa ya mateso. Hata hivyo, mara zote Tom alikuwa akimkataza juu ya matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuhangaikia afya yake, akisisitiza kwamba haikuwa rahisi kupona.

“Lakini kwanini unasema hivyo mpenzi wangu? Napenda sana kukuona ukiamka tena!”

“Sawa, lakini naamini nitaamka siku ambayo Mungu mwenyewe atakuwa ameichagua!”

“Hapana darling, hupaswi kukata tamaa mapema kiasi hicho!”

“Lakini pia hupaswi kutumia fedha nyingi kiasi hiki katika jambo ambalo linaonekana dhahiri kuwa ni gumu kufanikiwa!”

“Unanikatisha tamaa tu mpenzi wangu!”

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao, kila kukicha Mariam alikuwa akihangaika kutafuta dawa hadi za kienyeji kwa ajili ya kurudisha afya ya Tom, lakini haikuwezekana. Pamoja na hayo, kuna jambo moja ambalo lilimshangaza sana Mariam.

Tom, alikuwa na kawaida ya kumuita Mariam akionyesha kutaka kumwambia jambo, lakini akifika ghafla anaonekana kusahau. Tatizo hilo liliendelea kwa mwaka mmoja zaidi, kiasi kwamba Mariam akawa anampuuza, kwani kila anapotaka kusema anajikuta amesahau.

“Lakini una nini Tom? Mbona kila unapotaka kusema jambo unasahau?”

“Hata mimi nashindwa kuelewa, ila ni jambo muhimu sana, kila nikitaka kusema nashangaa nasahau, lakini kuna siku nitakumbuka, na utaona jinsi jambo hilo lilivyo kubwa na muhimu!”

“Haya hebu tungoje huo muujiza!”
 
SEHEMU YA 50 KATI YA 50..............MWISHO

Hiyo ikaendelea kuwa kawaida ya Tom, kila mara alimwita mkewe na anapotaka kusema anaonekana kusahau. Mariam alihuzunika sana, alishindwa kuelewa mumewe alikuwa na jambo gani kubwa kiasi kile, na analisahau kila anapotaka kusema. Mariam akaamua kwenda kwa Dokta wake, ambaye alimwambia kwamba ile ilikuwa hali ya kawaida na kumbukumbu zake zitaendelea kurejea taratibu.

“Kweli Dokta?”

“Ndivyo ilivyo, inaonekana aliumia kidogo, sehemu ya ubongo wake, ndiyo maana anapoteza kumbukumbu, lakini zitaendelea kurudi polepole!”

“Kweli kabisa?”

“Nakuhakikishia!”

“Nashukuru sana Dokta!”

“Ok!”

**********

Ilikuwa ni Jumamosi usiku, tayari Tom na mkewe walikuwa wameshalala. Ulikuwa ni usiku wa saa saba na dakika zake. Mariam akashtuliwa na Tom ambaye alikuwa akimvuta kwa nguvu.

“Kuna nini?”

“Amka, amka haraka sana!”

“Nini saa hizi Tom?”

“Amka nimeshakumbuka, amka haraka kabla sijasahau!”

“Enhee sema!” Mariam akasema akiwa ameshawasha taa.

“Sikiliza kwa makini sana!”

“Nakusikiliza!”

“Nenda nje sasa hivi, pale kwenye ule mlimao, fukua chini kisha utoe kiroba utakachokiona!”

“Kina nini?”

“Kina madini, nilikuwa najitahidi sana kuvuta kumbukumbu, afadhali sasa nimekumbuka!”

“Unasema kweli Tom?”

“Huo ndiyo ukweli, nenda haraka kaangalie kama bado kipo!” Tom alisema haraka haraka huku akihema kwa kasi sana.

Mariam akatoka na jembe usiku huo bila kuogopa, kukuta kile kiroba kungemaanisha kuachana na maisha ya umasikini tena. Maisha yao yangekuwa mapya yasiyo na chembe ya dhiki. Alipofika nje, zoezi la kuchimba eneo la kuzunguka ule mlimao lilianza haraka sana.

Hakufika mbali sana, akaanza kuhisi kitu kigumu, aliendelea kidogo, akaona mfuko wa salufeti, akauvuta kwa nguvu, ukatoka ukiwa na madini ndani yake. Akatoka nao mbio hadi chumbani kwa mumewe. Hakusema kitu, walipoufungua walihisi kuchanganyikiwa! Kile kiroba kilikuwa kimejaa dhahabu tupu!

“Umasikini kwaheri....kwaheri umasikini...” Tom alipiga kelele akiwa haamini kilichotokea.

“Ndiyo maana ulikuwa unasahau kila wakati? Yaani unasahau utajiri?” Marim akamwambia Tom akicheka.

“Yaani acha tu, Mungu mkubwa mke wangu! Sasa andaa safari kabisa, kesho nenda Nairobi ukauze sehemu ya haya madini ili upate nauli ya kwenda Marekani ukaeze dhahabu yote huko!”

“Sawa!”

Usiku huo hawakuweza kulala, walikuwa wakipanga mipango mbalimbali juu ya maisha yao yajayo ambayo yangerejea kwenye utajiri kama kawaida.

“Mayasa alikuwa hafahamu kama pale uliweka hizi dhahabu?”

“Nilimuamini kwa kila kitu, lakini sijui ni kwanini sikumweleza kuhusu pale, ilikuwa ni siri yangu mwenyewe!”

“Hakuna mwingine zaidi ya Mungu mume wangu!”

“Na ni kweli ni Mungu mwenyewe ndiye aliyefanya yote haya!”

Walizungumza mambo mengi sana hatimaye wakalala, masaa manne baadaye walikuwa macho, Mariam akijiandaa kwa safari ya kwenda Nairobi. Saa kumi na mbili kamili, Mariam aliondoka na kwenda Uwanja wa Ndege, kwakuwa alishapanga mipango ya tiketi mapema, haikuwa kazi kubwa sana, alifika na kuondoka na ndege ya saa moja kamili.

Alifanikiwa kufanya mauzo vizuri kisha akarejea Tanzania kabla ya safari nyingine ya kwenda Los Angeles, Marekani. Huko akauza dhahabu yote na kurejea Tanzania akiwa na mabioni yake.

“Pole sana mke wangu!”

“Ahsante baby, sasa ni wakati wa kupanga mipango yetu, hatuna muda wa kupoteza zaidi!”

“Ni kweli!”

Ndicho kilichofanyika, halikuwa jambo gumu sana kwao, kikubwa kilichofanyika ilikuwa ni kununua majengo marefu (Towers) mengi jijini Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Mwanza. Hiyo ndiyo ikawa biashara yao kubwa. Fedha zilizobakia wakahifadhi kwenye akaunti. Maisha yao sasa yakawa ya furaha, magazeti yakaanza kuandika habari zao kwa fujo!

“Lakini kuna jambo moja bado!” Mariam akamwambia Tom.

“Jambo gani?”

“Lazima usimame tena!”

“Unamaanisha nini?”

“Pesa itaongea, lazima tutafute tiba mpenzi wangu!”

“Hapana, sitaki!”

“Kwanini?”

“Nilishasema kabla, nitasimama siku Mungu mwenyewe akiamua!”

“Lakini Mungu alisema jisaidie nami nitakusaidia!”

“Mimi sitaki hivyo, nataka anisaidie yeye mwenyewe akitaka!”

“Haya na tusubiri!”

Wiki moja baadaye, Tom akamwagiza Mariam akamwite Mchungaji wa Kanisa wanaloabudu, alitaka kufanyiwa maombi maalumu nyumbani kwake. Zoezi hilo lilifanyika haraka sana, kila Jumapili yule Mchungaji alikuwa akifika nyumbani kwa akina Tom na kusali pamoja naye.

Wiki nne tu baadaye, wakiwa katikati ya maombi, Tom alishangaa akipata nguvu za ajabu sana, akasimama. Halikuwa jambo jepesi kuamini, hata Mchungaji mwenyewe hakuwa anaelewa jambo hilo kwasababu alikuwa amefumba macho.

“Yesu ahsante, nasema ahsante sana Mungu wangu...siamini kama kweli leo nimesimama tena!” Tom akapiga kelele huku akiimba.

Mchungaji akafumbua macho, hakuamini macho yake, akaendelea kumuomba Mungu bila kukoma. Mariam aliyekuwa nje, aliingia ndani baada ya kusikia kelele za Tom ndani. Naye akashangazwa sana na jambo hilo, akaungana na mumewe kumshukuru Mungu.

“Mungu wa ajabu jamani, leo ameamua kumuamsha mume wangu kitandani!”

“Amen!”

Ilikuwa ni furaha kubwa kuliko kawaida, Jumapili iliyofuata Tom alikwenda Kanisani, akapanda Madhabahuni kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu. Hapakuwa na machozi tena baada ya pale, wakaishi kwa amani na furaha katika maisha yao. Mapenzi ya kweli ndiyo yaliyotawala maisha yao.

“Nakushukuru kwa yote mke wangu, umenivumilia katika kila hali Mariam. Sitaki kukumbuka tena maisha yetu ya nyuma, lakini Mungu ni shahidi wa hilo kwamba wewe ni mwanamke sahihi wa maisha yangu, mkombozi wangu. Naamini uliandaliwa kwa ajili yangu, nakushukuru sana mke wangu, wewe ndiye wangu wa milele, nakuahidi sitakusaliti tena, tuyaache yaliyopita yaende zake, tuanze maisha mapya yaliyojaa mapenzi! Uliyonionyesha ni Zaidi ya Mapenzi, ahsante sana Mariam,” Tom alisema akiwa kifuani mwa Mariam, huku machozi yakimiminika kama maji machoni mwake.

“Nilipanga kukupa mapenzi ya kweli kama zawadi yangu kwako, wewe ndiye mwanaume wangu wa kweli, nakupenda sana!” Mariam akasema, naye akishindwa kuzuia hisia zake, akajikuta akimwaga machozi.

Haya yalifanyika nyumbani kwao Mbezi, muda mfupi baada ya kutoka Kanisani. Wakaendelea kukumbatiana zaidi, hawakuwa na kitu kingine vichwani mwao zaidi ya penzi la kweli.



Mwisho.
 
KURA*KURA KURA** 🔥 🔥 🔥

SIMULIZI TATU ZA MWISHO, MSIMU HUU WA PILI, BAADA YA KUTUMA SIMULIZI SABA JAMII FORUM NA BURE SERIES

CHAGUA SIMULIZI IPI TUANZE NAYO.

1. SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua

2. DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha

3. MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi

4. OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi



Simulizi yenye kura 10. itatumwa, kura hazijafika 10 msimu wa pili utaishia hapa
 
CHAGUA SIMULIZI IPI TUANZE NAYO.

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua
......(Kura 0/10)

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha.
.....(Kura 0/10)

MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi
......(Kura 3/10)

OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi.
.....(Kura 0/10)

Simulizi yenye kura 10. itatumwa, kura hazijafika 10 msimu wa pili utaishia hapa
 
Bado tunaendelea na Uchaguzi, Simulizi yenye kura 10 itarusha, tupia kura yako.

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua ......(Kura 2/10)

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha......(Kura 0/10)

MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi......(Kura 4/10)


OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi......(Kura 0/10)
 
SEHEMU YA 50 KATI YA 50..............MWISHO

Hiyo ikaendelea kuwa kawaida ya Tom, kila mara alimwita mkewe na anapotaka kusema anaonekana kusahau. Mariam alihuzunika sana, alishindwa kuelewa mumewe alikuwa na jambo gani kubwa kiasi kile, na analisahau kila anapotaka kusema. Mariam akaamua kwenda kwa Dokta wake, ambaye alimwambia kwamba ile ilikuwa hali ya kawaida na kumbukumbu zake zitaendelea kurejea taratibu.

“Kweli Dokta?”

“Ndivyo ilivyo, inaonekana aliumia kidogo, sehemu ya ubongo wake, ndiyo maana anapoteza kumbukumbu, lakini zitaendelea kurudi polepole!”

“Kweli kabisa?”

“Nakuhakikishia!”

“Nashukuru sana Dokta!”

“Ok!”

**********

Ilikuwa ni Jumamosi usiku, tayari Tom na mkewe walikuwa wameshalala. Ulikuwa ni usiku wa saa saba na dakika zake. Mariam akashtuliwa na Tom ambaye alikuwa akimvuta kwa nguvu.

“Kuna nini?”

“Amka, amka haraka sana!”

“Nini saa hizi Tom?”

“Amka nimeshakumbuka, amka haraka kabla sijasahau!”

“Enhee sema!” Mariam akasema akiwa ameshawasha taa.

“Sikiliza kwa makini sana!”

“Nakusikiliza!”

“Nenda nje sasa hivi, pale kwenye ule mlimao, fukua chini kisha utoe kiroba utakachokiona!”

“Kina nini?”

“Kina madini, nilikuwa najitahidi sana kuvuta kumbukumbu, afadhali sasa nimekumbuka!”

“Unasema kweli Tom?”

“Huo ndiyo ukweli, nenda haraka kaangalie kama bado kipo!” Tom alisema haraka haraka huku akihema kwa kasi sana.

Mariam akatoka na jembe usiku huo bila kuogopa, kukuta kile kiroba kungemaanisha kuachana na maisha ya umasikini tena. Maisha yao yangekuwa mapya yasiyo na chembe ya dhiki. Alipofika nje, zoezi la kuchimba eneo la kuzunguka ule mlimao lilianza haraka sana.

Hakufika mbali sana, akaanza kuhisi kitu kigumu, aliendelea kidogo, akaona mfuko wa salufeti, akauvuta kwa nguvu, ukatoka ukiwa na madini ndani yake. Akatoka nao mbio hadi chumbani kwa mumewe. Hakusema kitu, walipoufungua walihisi kuchanganyikiwa! Kile kiroba kilikuwa kimejaa dhahabu tupu!

“Umasikini kwaheri....kwaheri umasikini...” Tom alipiga kelele akiwa haamini kilichotokea.

“Ndiyo maana ulikuwa unasahau kila wakati? Yaani unasahau utajiri?” Marim akamwambia Tom akicheka.

“Yaani acha tu, Mungu mkubwa mke wangu! Sasa andaa safari kabisa, kesho nenda Nairobi ukauze sehemu ya haya madini ili upate nauli ya kwenda Marekani ukaeze dhahabu yote huko!”

“Sawa!”

Usiku huo hawakuweza kulala, walikuwa wakipanga mipango mbalimbali juu ya maisha yao yajayo ambayo yangerejea kwenye utajiri kama kawaida.

“Mayasa alikuwa hafahamu kama pale uliweka hizi dhahabu?”

“Nilimuamini kwa kila kitu, lakini sijui ni kwanini sikumweleza kuhusu pale, ilikuwa ni siri yangu mwenyewe!”

“Hakuna mwingine zaidi ya Mungu mume wangu!”

“Na ni kweli ni Mungu mwenyewe ndiye aliyefanya yote haya!”

Walizungumza mambo mengi sana hatimaye wakalala, masaa manne baadaye walikuwa macho, Mariam akijiandaa kwa safari ya kwenda Nairobi. Saa kumi na mbili kamili, Mariam aliondoka na kwenda Uwanja wa Ndege, kwakuwa alishapanga mipango ya tiketi mapema, haikuwa kazi kubwa sana, alifika na kuondoka na ndege ya saa moja kamili.

Alifanikiwa kufanya mauzo vizuri kisha akarejea Tanzania kabla ya safari nyingine ya kwenda Los Angeles, Marekani. Huko akauza dhahabu yote na kurejea Tanzania akiwa na mabioni yake.

“Pole sana mke wangu!”

“Ahsante baby, sasa ni wakati wa kupanga mipango yetu, hatuna muda wa kupoteza zaidi!”

“Ni kweli!”

Ndicho kilichofanyika, halikuwa jambo gumu sana kwao, kikubwa kilichofanyika ilikuwa ni kununua majengo marefu (Towers) mengi jijini Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Mwanza. Hiyo ndiyo ikawa biashara yao kubwa. Fedha zilizobakia wakahifadhi kwenye akaunti. Maisha yao sasa yakawa ya furaha, magazeti yakaanza kuandika habari zao kwa fujo!

“Lakini kuna jambo moja bado!” Mariam akamwambia Tom.

“Jambo gani?”

“Lazima usimame tena!”

“Unamaanisha nini?”

“Pesa itaongea, lazima tutafute tiba mpenzi wangu!”

“Hapana, sitaki!”

“Kwanini?”

“Nilishasema kabla, nitasimama siku Mungu mwenyewe akiamua!”

“Lakini Mungu alisema jisaidie nami nitakusaidia!”

“Mimi sitaki hivyo, nataka anisaidie yeye mwenyewe akitaka!”

“Haya na tusubiri!”

Wiki moja baadaye, Tom akamwagiza Mariam akamwite Mchungaji wa Kanisa wanaloabudu, alitaka kufanyiwa maombi maalumu nyumbani kwake. Zoezi hilo lilifanyika haraka sana, kila Jumapili yule Mchungaji alikuwa akifika nyumbani kwa akina Tom na kusali pamoja naye.

Wiki nne tu baadaye, wakiwa katikati ya maombi, Tom alishangaa akipata nguvu za ajabu sana, akasimama. Halikuwa jambo jepesi kuamini, hata Mchungaji mwenyewe hakuwa anaelewa jambo hilo kwasababu alikuwa amefumba macho.

“Yesu ahsante, nasema ahsante sana Mungu wangu...siamini kama kweli leo nimesimama tena!” Tom akapiga kelele huku akiimba.

Mchungaji akafumbua macho, hakuamini macho yake, akaendelea kumuomba Mungu bila kukoma. Mariam aliyekuwa nje, aliingia ndani baada ya kusikia kelele za Tom ndani. Naye akashangazwa sana na jambo hilo, akaungana na mumewe kumshukuru Mungu.

“Mungu wa ajabu jamani, leo ameamua kumuamsha mume wangu kitandani!”

“Amen!”

Ilikuwa ni furaha kubwa kuliko kawaida, Jumapili iliyofuata Tom alikwenda Kanisani, akapanda Madhabahuni kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu. Hapakuwa na machozi tena baada ya pale, wakaishi kwa amani na furaha katika maisha yao. Mapenzi ya kweli ndiyo yaliyotawala maisha yao.

“Nakushukuru kwa yote mke wangu, umenivumilia katika kila hali Mariam. Sitaki kukumbuka tena maisha yetu ya nyuma, lakini Mungu ni shahidi wa hilo kwamba wewe ni mwanamke sahihi wa maisha yangu, mkombozi wangu. Naamini uliandaliwa kwa ajili yangu, nakushukuru sana mke wangu, wewe ndiye wangu wa milele, nakuahidi sitakusaliti tena, tuyaache yaliyopita yaende zake, tuanze maisha mapya yaliyojaa mapenzi! Uliyonionyesha ni Zaidi ya Mapenzi, ahsante sana Mariam,” Tom alisema akiwa kifuani mwa Mariam, huku machozi yakimiminika kama maji machoni mwake.

“Nilipanga kukupa mapenzi ya kweli kama zawadi yangu kwako, wewe ndiye mwanaume wangu wa kweli, nakupenda sana!” Mariam akasema, naye akishindwa kuzuia hisia zake, akajikuta akimwaga machozi.

Haya yalifanyika nyumbani kwao Mbezi, muda mfupi baada ya kutoka Kanisani. Wakaendelea kukumbatiana zaidi, hawakuwa na kitu kingine vichwani mwao zaidi ya penzi la kweli.



Mwisho.
Safi sana... Bonge la story...

Chapter Closed...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom