Simulizi: Akwelina

SEHEMU YA 46 YA 50.



WARDA ?? Kesho inatakiwa tuanze safari ya kwenda katika kampuni yenye jina lako ili tukamalize ushetani uliopo ndani ya kampuni ile daah natamani nimuone mwanangu ????



AKWELINA ?? Pole sana usijali utamuona mtoto wako kesho tunaenda kumsaidia mtoto wako mimi nahitaji kumsaidia baba yangu kipenzi kakinga nimemkumbuka sana baba yangu .



Walilala baada ya kuzungumza mambo mengi kuhusu safari yao. Yalipofika majira ya saa tisa usiku warda alikuwa bado hajalala alisimama akachukua sindano ya madawa ya kulevya akamchoma akwelina , Akwelina alistuka ghafla akalala tena warda alisimama akautafuta ufunguo kwa muda mrefu kwa bahati nzuri aliupata ufunguo ule akachukua begi lake akaondoka moyoni mwake alisema :-

“” Nisamehe sana akwelina kwa hiki nilichokutendea inabidi nimpelekee ufunguo Julius ili nimpate mtoto wangu ”’



Warda aliondoka alipofika barabarani alipanda gari moja kwa moja hadi gest ( nyumba ya wageni ). Asubuhi palipopambazuka warda alichukua gari akaanza safari kuelekea katika kampuni, Safari ilikuwa ndefu sana warda akiwa ndani ya gari alisikia gari linasimama ghafla dereva wa gari hilo alishuka na kukimbia warda alishindwa kuelewa akatoka kwenye gari alipotazama mbele ya gari alimuona akwelina akiwa ameshika bunduki Warda ali……





Warda alipatwa na mshangao mkali sana kwa kile alichokiona mbele yake alianza kurudi nyuma huku akiwa anatetemeka , Akwelina alimfuata akiwa na hasira zilizojaa moyoni mwake, Warda alipiga magoti akasema :-



WARDA__ Nisamehe akwelina najua nimekosa sana lakini nilifanya kitendo kile kwa ajili ya maisha yako , sikia akwelina kwa hali yeyote pamoja na uwezo ulionao hauwezi kupambana na askari waliopo ndani ya kampuni ile kifupi kuna askari wengi wenye nguvu na uwezo wa juu sana na ndio maana niliamua kuchukua ufunguo huu ili nikamsaidie mtoto wangu nafahamu Julius anahitaji ufunguo huu pekee na ningekueleza haya usinge kubali akwelina binti yangu Mimi ningefanyaje Mimi akwelina ?



AKWELINA ___ Siku zote baba yangu aliniambia kwamba “” Binti yangu akwelina katika maisha yako usimuamini binadamu yeyote hata Mimi japo nimekulea lakini usije ukaniamini kwa sababu nafsi zetu huwa zinabadirika muda wowote ishi maisha yako yote lakini kumbuka binadamu sio wa kumuamini”” Kupitia maneno ya baba niliishi na wewe kwa akili sana na sindano ile niliibadirisha ili bila wewe kujua na ndio maana leo hii unaniona hapa. Sitaki kuzungumza mengi kwanza naomba ufunguo pili utaendesha gari hili hadi katika kampuni hiyo najua kwa uwezo wa mungu nitashinda tu.



Akwelina alichukua ufunguo toka kwa warda kisha akampandisha kwenye gari kwa nguvu , Warda akaendesha gari kuelekea katika kampuni hiyo. Monna alishindwa kuvumilia utumwa katika mikono ya Patrick kutokana na kukosa uhuru, Monna aliishi maisha ya mateso katika mikono ya patrick, siku zote monna aliishi akiwa anajuta kwa vitendo alivyomfanyia kakinga monna alikumbuka siku moja walipokuwa wanaishi kijiji kabla monna hajampokea akwelina, kakinga alimwambia monna :-



“” Mke wangu naomba nikueleze maneno haya kwa sababu nakupenda sana mbali na kukupenda sisi ni yatima wewe na mimi sote hatuna wazazi katika dunia hii, Wewe ndio mama yangu hali kadhalika na Mimi ndio baba yako kwahiyo nakuomba mke wangu nipende kama nilivyo katika maisha yako yote kwani ninaamini katika dunia hii hakuna mwanaume anaekupenda kama Mimi chunga sana tamaa, Dunia hii kuna wanaume wengi lakini wengi wao ni waongo na wenye mapenzi ya dhati kama Mimi tupo wachache sana mke wangu __????



Monna alilia sana kwa kumbukumbu hizo alijuta sana kwa kuruhusu kumpoteza mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwake , Wakati huo upande wa kakinga alikuwa na mawazo sana kwa kwa kumwamini sana monna , kakinga akiwa katika mawazo hayo alimtazama mtoto wake bilali akamuona bilali analia sana Kakinga alipojaribu kumgusa bilali alimuona bilali anapiga magoti mbele yake bilali akasema :-



BILALI__ Nisamehe sana baba yangu sikutambua kama Julius alikuwa ananidanganya nimekutesa baba yangu daaah najilaumu sana nisamehe sana baba yangu nisamehe baba .



KAKINGA ___ Usijali kijana wangu yote haya sio makosa yako ni mipango yake mungu pekee sisi wanadamu siku zote ni wakosaji mwanangu usijali nimekusamehe .



Bilali alimkumbatia baba yake akiwa anatokwa na machozi kwa wingi sana Kakinga alimtuliza bilali. Baada ya siku mbili Akwelina na warda walikuwa bado wapo njiani akwelina alimuuliza warda baada ya kukaa ndani ya gari kwa muda mrefu :-



AKWELINA __ Bado muda gani tufike ?



WARDA ___ Bado kama siku tatu tufike binti yangu .



AKWELINA __ Ongeza mwendo .



Usiku wa siku hiyo mama mzazi wa akwelina alikuwa ndani ya chumba chenye kutisha , Chumba ambacho kilikuwa na wadudu wengi na chenye kutoa harufu mbaya sana mama wa akwelina aliteswa mno na wadudu waliokuwa ndani ya chumba hicho. Mama wa akwelina akiwa ndani ya mateso hayo kwa mbali alisikia sauti yenye huzuni ya mwanaume ikiomba maji ya kunywa, Mtu huyu aliomba maji kwa muda mrefu ilibidi mama wa akwelina aifute ile sauti alipofika karibu alimuona mtu amechakaa kama chizi amekaa chini akiendelea kuomba maji mama akwelina alipomtazama vizuri alistuka kumuona mtu yule ni STEVEN mume wake kipenzi ….
 
SEHEMU YA 47 YA 50.





Mama akwelina alipomtazama vizuri alistuka kumuona mtu yule ni STEVEN mume wake kipenzi, ilikuwa vigumu sana moyo kuamini kile macho ilichokuwa inakitazama, Miguu ilikuwa mizito na kusababisha mama wa akwelina kushinda kupiga hatua zaidi akaondoka chini. Steven alistuka baada ya kusikia kishindo karibu yake.



“” Nani wewe nisaidie maji nahitaji maji ya kunywa ninakiu cha maji pia nina njaa siku ya pili leo sijala chochote njaa inaniuma mwambie Julius mdogo nahisi njaa tafadhali” Maneno hayo ya Steven yalimuumiza sana mama akwelina na kushindwa kuvumilia akaruhusu mvua ya machozi katika macho yake. Kilio kikali kilichotoka kwa mama akwelina kilizidi kumshangaza Steven na kumfanya ajiulize maswali mengi sana :-



“” Kwanini unalia wewe ni nani ? Steven alimuuliza mama akwelina, Kwa sauti yenye huzuni ndani yake mama akwelina alimjibu Steven:



“” Ni Mimi mume wangu ??

“” Wewe nani mbona hujibu unalia tu?

“” Mimi daaah ?? ni Mimi JAMILA ..

“” Jamila !! jamila yupi acha kulia niambie ili nikufahamu binti .



Jamila ( mama wa akwelina ) alizidi kupata maumivu baada ya kutambua mume wake amemsahau hadi sauti yake , Jamila alijikaza akamjibu :



“”_ Ni mimi mke wako jamila mume wangu .

“”_ Niniiii !! mke wangu jamila ni wewe kweli hapana niliambiwa umekufa mke wangu kumbe upo hai siamini.

“”_ Nipo hai mume wangu umesahau hadi sura yangu jamani niangalie vizuri mume wangu .

“” _Daah sioni Mimi mume wangu Julius shemeji yako alinipulizia dawa na kusababisha leo hii nimepoteza nuru katika macho yangu sioni mimi mke wangu .



Jamila alizidi kulia akasimama japo alikuwa hana nguvu akamsogelea Steven ( mume wake ) akamkumbatia , walikumbatiana kwa muda mrefu sana Steven alimwaga machozi kwa wingi katika mgongo wa jamila japo machozi ya steven yalikuwa ya furaha ndani yake.



Yalipofika majira ya asubuhi na mapema askari waliingia katika chumba alichokuwepo bilali na baba yake wakawachukua wote wakaondoka nao moja kwa moja hadi katika uwanja mkubwa uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo, Bilali na baba yake walipofika katika uwanja huo waliona watu wengi wapo katika mateso makali upande wa pili katika uwanja huo kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanakatwa vichwa, hali hiyo ilimpatia wasiwasi bilali ghafla Julius alitokea akamshika bega bilali akamwambia :



“” _ Kijana unajua kwanini upo hapa ? Hahaha acha kuogopa nimekuleta hapa ili utambue kama Mimi sio mtu wa mchezo na huwa sipendi dharau kipigo ulichonipatia sijakisahau kabisa leo nahitaji nikupatie adhabu kali ili nijue kama wewe kweli ni jasili huu ndio unaitwa UWANJA WA KIFO.



Baada ya maongezi hayo askari walimchukua bilali wakamfunga kamba katika mikono yake alafu wakamtupa ndani ya kisima chenye maji mengi, Kakinga alihitaji kumsaidia bilali askari walimchukua wakaenda nae katikati ya uwanja alafu wakaanza kumpiga, Kakinga aliwashambulia askari wote waliokuwa wanampiga Julius akachukua bunduki akampiga Kakinga risasi ya kifua, kakinga alidondoka chini papo hapo.



Majira hayo hayo monna akiwa na Patrick alipatwa na wasiwasi mkubwa katika moyo wake akasema kwa nguvu “” KAKINGA “” moyo wake ulizidi kwenda mbio hofu iliutawala mwili wake wote monna anamtazama sana Patrick akasema:-



“” Kakinga yupo wapi ?

“” hahaha wewe hujui kakinga yupo uwanja wa kifo leo hawezi kupona .

“” Hapana hapana haiwezekani



Alimaliza kwa maneno hayo monna akasimama akatoka nje akiwa anakimbia kuelekea uwanja wa kifo. Bilali alisumbuka sana ndani ya maji hayo baada ya kukaa kwa muda mrefu kidogo pumzi ilimuisha bilali akajitahidi kamba zikafunguka akaongelea kwenda juu kwa bahati nzuri alifika juu akatoka nje ya kisima akatazama mbele yake akamuona mwanajeshi mmoja anauvuta mwili wa kakinga kwa sababu kisima kilikuwa karibu na sehemu ambayo kakinga alipopingwa risasi, Bilali hakuamini akamtazama Julius akamuona Julius anacheka sana akiwa ameshika bunduki bilali alishikwa na hasira aka……





Bilali alishikwa na hasira akasimama japo alikuwa amechoka sana kutokana na kupambana na maji kwa muda mrefu, Kakinga alimnyoshea mkono bilali kuashiria anahitaji msaada toka kwake wakati huo yule mwanajeshi alizidi kumvuta kakinga bila huruma hali iliyozidi kumpatia hasira bilali aliondoka kwa mwendo wa kasi sana akamuua yule mwanajeshi aliyekuwa anamvuta baba yake baadaa kumuua yule mwanajeshi bilali akamtazama Julius kwa muda mrefu sana .



Julius akaweka vizuri bunduki yake akamlenga kichwani bilali alipotaka kufyatua risasi alimuona monna kasimama mbele ya bilali ikabidi Julius ashushe bunduki yake alafu akashuka chini akamsogelea monna akamshika nywele akaanza kumvuta huku na kule katika uwanja huo , Monna aliumia sana akaanza kulia na kuomba msaada hali iliyomfanya kakinga japo alikuwa kapigwa risasi alisimama akamfuata Julius akamshika mkono akapiga magoti mbele yake akiwa anatokwa na damu nyingi katika kifua akasema :-
 
SEHEMU YA 48 YA 50.



“” _Tafadhali muache huyu binti hana makosa mwenye makosa ni Mimi na sio yeye Mimi ndio nahitaji kupata adhabu na kufanyiwa chochote lakini sio hawa tafadhali waache waende .



“” _Hahaha kumbe unajua kuomba eee, Sawa nitawaacha lakini kwa sharti moja unatakiwa uwe mbwa wangu leo na ubweke kama mbwa anavyobweka ukifanya hivyo nitawaacha wakiwa wazima .



Julius aliomba mnyororo akapewa akamfunga shingoni Kakinga kitendo hicho kilimuuma bilali akahitaji kumshambulia Julius, kakinga akamziwia “” Bilali mtoto wangu tuli hatuna uwezo wa kupambana nao angalia baba yako sina nguvu tena nani atakusaidia kijana wangu tulia acha nifanye hivi kwa ajili ya maisha yenu “” yalikuwa maneno ya kakinga akimweleza bilali. Julius alimvuta mnyororo ule Kwa nguvu Kakinga akadondoka chini bilali alishindwa kuvumilia akamvamia Julius wanajeshi walikuja wakamshika bilali, Julius alitoa amri kwa hasira :-



“””” Maliza mbwa wote hao “””

Wanajeshi walichukua bunduki zao walipotaka kuwapiga risasi mama mdogo wa monna ( Madame ) alitokeza akawaziwia wanajeshi wale kwa kusema :-



“”_ Julius mume wangu kwanini upo dhaifu hivyo hawa hawastahili kupigwa risasi wanatakiwa wafe kifo chenye mateso sana au unasemaje ?



“”_ Ni kweli mke wangu umesema neno lenye umuhimu mkubwa hakuna haja ya risasi, Askari wapeleke gerezani hawa panya baada ya siku mbili nitawauwa kwa mikono yangu mwenyewe na kifo chao kila raia aliyopo ndani ya kampuni hii atashuhudia kifo hicho.



Wanajeshi waliwachukua na kuwapeleka gerezani monna hakuamini kama mama yake mdogo amekuwa katili kiasi kile. Walipofika gerezani hali ya kakinga ilizidi kuwa mbaya sana jaraha la kakinga lilizidi kutoa damu kwa wingi , Monna alilia sana akamueka katika katika miguu yake machozi kutoka kwa monna yalikuwa yanadondoka katika sura ya kakinga taratibu mkono wa kakinga ulishika shavu la monna kwa sauti ya chini kakinga alimwambia monna:-



“”_Acha kulia monna unalia nini ?



“”_Nisamehe sana mume wangu bado najuta kwa niliyofanya kwako nafsi inaniuma sana mume wangu japo niliomba taraka lakini bado nakupenda usiniache peke yangu .



“”_Ni ngumu kuivumilia hali hii naumia sana naomba nisikilize monna huyo kijana unaemuona ni mtoto wangu anaitwa bilali ni mtoto wa warda naomba kama nilipoteza maisha leo nitunzie kijana wangu tafadhali.



“”_Haiwezekani ufe baba haiwezekani



Bilali alitazama huku na kule ndani ya gereza hilo kwa bahati nzuri aliona mfupa wa mnyama aliyefia ndani ya gereza hilo , bilali aliutumia mfupa huo kutoa risasi ndani ya kifua cha kakinga, Ilimchukua muda mrefu sana kutoa risasi ile, kakinga alipiga kelele kali kwa maumivu aliyopata kwa bahati njema bilali akafanikiwa kutoa ile risasi kisha akavua shati lake akaziwia damu ili zisiendelee kutoka.



Usiku wa saa tisa Patrick alikwenda gerezani akamkuta monna ametapakaa damu katika mikono yake Patrick alistuka sana akamtuma mwanajeshi mmoja akalete dawa ya vidonda yule mwanajeshi hakuchelewa akaleta dawa hiyo Patrick akampa monna dawa ile alafu akaondoka Monna alimshukuru mungu sana waliitumia dawa ile kumtibu kakinga katika majeraha yake.



Baada ya wiki mbili kupita kakinga alipona kabisa akaanza kupiga mazoezi ndani ya gereza hilo akiwa na kijana wake bilali, Siku hadi siku kakinga na bilali walizidi kuwa imara. Siku hiyo majira ya usiku Julius akiwa kitandani pamoja na Madame alisema



“” Nimemuacha sana kakinga kesho ndio siku yao ya mwisho lazima wafe”



Kama kawaida ya wanajeshi asubuhi ilipofika waliandaa vizuri uwanja wakawapatia taarifa watu wote waliokuwa wanaishi ndani ya kampuni hiyo kuhusu mauaji yatayofanyika siku hiyo baada ya muda kidogo watu walikusanyika kwa wingi sana katika uwanja huo. Kakinga, Monna pamoja na bilali walifungwa kamba katikati ya uwanja huo , Julius alikuwa amekaa juu akicheka sana panga ziliandaliwa kwa ajili ya kukata vichwa vyao. Mwanajeshi mmoja alimfuata monna akaweka panga katika shingo lake akamtazama Julius , Julius akaruhu monna akatwe kichwa yule mwanajeshi kabla hajashusha panga alipigwa risasi akadondoka chini Julius pamoja na watu wote katika uwanja huo walipata mshangao mkali kakinga alipotazama mbele katika mlango mkuu alimuona akwelina …





Kakinga alipotazama mbele katika mlango mkuu alimuona akwelina anakuja baada ya mwanajeshi huyo kupigwa risasi wanajeshi wote waligeuka wakaanza kumshambulia Akwelina , Akwelina alikuwa zaidi ya mnyama aliteketeza wanajeshi kwa wingi kakinga akatumia nafasi hiyo akakata kamba akachukua bunduki akamfuata bilali akamfungua kamba akambeba Monna begani kisha akaondoka hadi katika chumba kilichokuwa wazi katika uwanja huo , kakinga alipofika alimuweka monna chini akamfungua kamba, alafu akampatia bunduki bilali :-



“” Sikia monna hii sehemu sio salama kwako baki hapa hakikisha hauondoki eneo hili umenielewa ?



“” Sawa lakini hakikisha unarudi salama mungu akusaidie .



“” Bilali mwanangu baki eneo hili uwanja wa vita sio salama kwako pia



“” Hapana baba nitakufa na wewe siwezi kubaki hapa siwezi baba.



Bilali hakujali chochote kibaya kinachoweza kutokea mbele yake ilibidi Kakinga amkubalie wakarudi kupambana, Milio ya risasi iliwapa tabu sana raia na kuwafanya baadhi ya raia kupoteza fahamu kutokana na milio hiyo, Pamoja na kuwauwa wanajeshi wengi lakini bado walizidi kuongezeka kwa kasi , Akwelina nae hakuchoka alizidi kuwaangamiza wanajeshi bila huruma. Giza lilitanda bado pambano
 
SEHEMU YA 49 YA 50.

lilikuwa linaendelea taratibu taratibu wanajeshi waliaanza kupungua hali iliyompatia wasiwasi Julius wakati huo Patrick alikuwa amejifungia ndani kwa hofu.



Madame alimtuliza Julius baada ya kumuona anawasiwasi mkubwa :-



“” Mtoto wa kiume hupaswi kuwa na wasiwasi lazima ujiamini mume wangu acha kuogopa sawa.



“” Daah sawa mke wangu lakini huyu msichana aliyevamia kampuni yangu sijui ni nani na anataka nini kwangu .



“” Kumbuka wewe ni tajiri lazima utawindwa na wengi cha kufanya ni kuwateketeza hawa wafungwa na raia wote huenda itasaidia kumtuliza huyo msichana .



“” Wazo zuri mke wangu vizuri sana.



Yalipofika majira ya asubuhi bado pambano lilikuwa linaendelea katika uwanja ule ghafla wanajeshi waliacha kupiga risasi wakarudi nyuma akwelina alipopata nafasi hiyo alimfuata baba yake mlezi ( kakinga ) akamkumbatia kwa furaha akasahau yupo eneo hatari :



“”” Nilikukumbuka sana baba yangu nilimuomba sana mungu nikukute salama nimekuja kukusaidia baba yangu nakupenda sana baba nakupenda.



“” Sikia binti yangu hapa sio sehemu salama tupambanie maisha yetu kwanza hayo mengine baadae.



Akwelina alimsikiliza baba yake akaokota silaha yake wakajificha nyuma ya jiwe kubwa lililokuwa ndani ya uwanja huo baada ya kuona wanajeshi wanarudi nyuma. Ulipita muda mchache akwelina na wenzake waliona raia wengi wanaletwa uwanjani na kuuwawa ovyo ovyo wanajeshi walizidi kuua raia kwa wingi. Hali hiyo iliwashangaza sana kakinga na watoto wake, Julius akachukua kipaza sauti akasema:-



“” Kakinga najua unanisikia naomba weka silaha chini pamoja na huyo msichana haijalishi unamfahamu au laa ili kusaidia maisha ya raia hawa vinginevyo nitaendelea kuwauwa kwa sababu yenu .



Julius alitoa ruhusu kwa wanajeshi wake baada ya kuzungumza maneno hayo wakaendelea kuuwa raia kakinga alishindwa kuvumilia akatoka nyuma ya jiwe akatupa silaha chini, Bilali na akwelina nao wakatupa silaha chini Julius alifurahi mno wanajeshi waliwazunguka Kakinga na watoto wake kwa lengo la kuwateka, Wanajeshi walipotaka kuwagusa walipigwa risasi wote Julius alizungusha macho huku na huko kumtafuta aliyewauwa wanajeshi wake ghafla warda akajitokeza akiwa anapiga risasi , Julius akarudi ndani haraka.



Kakinga na watoto wake waliokota silaha zao wakaungana na warda wakawashambulia wanajeshi. Raia walichukia sana wakaokota mawe na kuwapiga wanajeshi, Kutokana na wingi wa raia wanajeshi waliuwawa wote kwa muda mfupi kisha wakatawanyika sehemu zote na kuwafungulia wenzao, Julius alipofika chumbani kwake alimkuta Madame anachukua ufunguo wa gari lake pamoja na pesa zote:-



“” Unataka kwenda wapi na pesa zangu wewe mwanamke ?



“” Kila mtu afe na chake Julius baki na balaa lako Mimi naondoka .



“” Nipatie ufunguo wa gari langu pamoja na pesa zangu .



“” Sikupi pia sahau hilo.



Julius alichukia sana akachomoa bastola akampiga risasi Madame ya kichwa , Madamu akapoteza maisha papo hapo Julius akachukua pesa zake pamoja na ufunguo wa gari akatoka nje akiwa makini sana njiani akakutana na patrick wakaungana, Wakatafuta njia ili watoroke lakini kila sehemu walipokwenda walikutana na raia wakiwa na hasira kali Patrick akamwambia kakinga :-



“” Kaka njia sahihi hapa ni kumchukua kaka yako na mke wake jamila ili tuwatumie kuondoka hapa kwa sababu raia hawa wanawatambua wataogopa na njia tutapa kaka au unasemaje ?



“” Ni kweli kabisa wazo zuri nifuate.



Julius na Patrick waliondoka hadi katika chumba alichokuwepo Steven na mke wake ( Jamila ) Julius aliwachukua kama uchafu bila kujali Steven ni kaka yake, Walitoka nao nje walipofika nje Julius alipiga risasi juu raia walisogea mbali warda akamwambia akwelina :-



“” Wale waliotekwa ndio wazazi wako halali wale ndio waliokuzaa wewe .



Akwelina hakuamini alichokisia kutoka kwa warda, Akwelina akiwa katika mshangao mkali huo Julius alipanda kwenye gari akiwa na wazazi wa akwelina pamoja na patrick wakaondoka, Akwelina alitazama huku na kule akaona pikipiki ya kijeshi akaifuata akapanda kisha akalifuata gari ……





Akwelina alitazama huku na kule akaona pikipiki ya kijeshi akaifuata akapanda kisha akalifuata gari akwelina alikimbiza pikipiki ile kwa mwendo wa kasi sana japokuwa gari lilikuwa na uwezo mkubwa lakini akwelina alijitahidi akalifikia, Patrick akiwa ndani ya gari aliona pikipiki ikiwafuata kwa kasi sana akapata mashaka alipoangalia vizuri alimuona akwelina Patrick alistuka sana akamwambia Julius ambaye alikuwa anaendesha gari hilo :-



“” Nahisi kuna mtu anatufuata nyuma kaka ongeza mwendo .



“” Unasemaje !! nani huyo tena ?



Julius hakupoteza muda aliongeza mwendo taratibu taratibu walianza kumuacha akwelina , Akwelina akiwa juu ya pikipiki alichomoa bunduki yake akarenga taili la gari kisha akapiga risasi, Risasi ilipasua taili lile na kulifanya gari lipate ajali likadondoka nje ya barabarani kwa bahati nzuri patrick na wenzake wote walitoka ndani ya gari wakiwa wazima japokuwa Julius alivunjika mkono. Akwelina alisimama akawafuata Patrick alijaribu kupambana na akwelina lakini ilikuwa ngumu sana kutokana na uwezo wa akwelina katika mapambano, Akwelina aliwafunga kamba Julius pamoja na patrick kisha akawafuata wazazi wake akawakumbatia akiwa analia sana:-
 
SEHEMU YA 50 KATI YA 50..............MWISHO



“” Mama na baba siamini kama ningewaona tena kwa kuwa mbali na ninyi hadi sasa nimekubwa binti mkubwa lakini kwa uwezo wa mungu leo nimewaona siamini.



“” Jamila mke wangu huyo nani anayelia na kuzungumza maneno hayo ?

“” Mume wangu hata Mimi sijamtambua bado , Sikia binti yangu wewe nani mbona sikutambui acha kulia nieleze ili nielewe binti ?



“” Mama na baba ni mimi mtoto wenu HASMA mwenye jina mgongoni kwangu lililoandikwa AKWELINA wazazi wangu ????



“” Hapana sio kweli hapana mume wangu hii sio kweli siamini .



“” Twende kwa msichana uliyenikabidhi kwake nilipokuwa mdogo sana mama nahisi ukimuona utaamini.



Akwelina aliwachukua wazazi wake pamoja na wafungwa wake ambao ni Patrick na Julius akakodisha gari likawapeleka hadi ndani ya kampuni ile. Kakinga , Monna, Bilali , Warda pamoja na raia walimuona akwelina akiingia ndani ya uwanja akiwa na wazazi wake mkononi ameshika kamba iliyomfunga Julius na Patrick, Raia walikuwa na hasira kali sana waliwafuata Patrick na Julius wakawapiga sana kipigo kilipozidi Julius na Patrick walipoteza fahamu raia walichukua kuni na mafuta wakawachoma moto , Warda alilia sana kumuona kaka yake ( Patrick ) anachomwa moto.



Monna alimfuata akwelina akamshika mkono akamsogeza karibu ya jamila alafu akasema :-



“” Dada naomba nikurudishie mtoto wako uliyenikabizi miaka ya nyuma sana Akwelina huyu ndio mama yako mzazi .



Steven hakuamini alichokuwa anasikia ikabidi amwite akwelina ( HASMA ) akapitisha mkono mgongoni kwake akagusa lile jina aliyomwandika akiwa mdogo sana ndipo alipoamini kama kweli ni mtoto wake Steven alimkumbatia Akwelina akiwa anatokwa na machozi mengi sana, Wakati huo kakinga alikuwa mbali kidogo, nae machozi ya furaha yalimtoka :-



“” Mtoto wangu hasma umekuwa binti mkubwa sioni Mimi ningekuona leo mwanangu daah alafu unaufunguo katika mwili wako mwanangu unajua hilo ?



“” Ndio baba na niliutoa kwa sababu watu wengi walikuwa wanautaka ufunguo huo ninao hapa hapa baba.



“” Mungu wangu afadhali naomba ufunguo huo .



Akwelina ( HASMA ) alimpatia baba yake ufunguo , Steven alibonyeza ufunguo ule ardhi yote katika kampuni hiyo ilitetemeka ghafla kilitokea chumba kikubwa chini ya ardhi katika uwanja huo , Steven aligeuka akampatia Akwelina ufunguo kisha akamwambia :-



” Fungua chumba hicho mwanangu ”



Akwelina alifungua chumba kile akashangaa sana kuona chumba chote kimejaa Mali mbalimbali zikiwemo almasi na dhahabu pia kulikuwa na masanduku mengi sana akwelina alipoyafungua aliona pesa zimejazwa ndani ya masanduku yale akwelina alizidi kushangaa na kugeuza macho huku na huko aliona karatasi moja ipo juu ya sanduku akaichukua akaisoma akagundua ile ilikuwa hati miliki ya kampuni hiyo.



Akwelina alitoka nje akiwa na furaha sana cha ajabu alimuona kakinga anaondoka akiwa na bilali Akwelina alimfuata akamziwia akamuuliza :-



“” Unakwenda wapi baba yangu ?



“” Naenda mbali akwelina samahani kwa kukuita jina hilo nimezoea hivyo , Nisikilize Hasma kwa sasa upo salama pia umekuwa binti mkubwa na wazazi wako wale pale wanakuhitaji nenda ukawalinde .



“” Mimi bila wewe hata wao wasingeniona leo, popote utapokwenda nitakuwa nawe pia kampuni hii pamoja na mali zote nakupa wewe bado nitaendelea kuwa chini yako baba yangu tafadhali kubali suala hili .



Kakinga hakuamini kama anaenda kuwa tajiri mkubwa sana duniani alifurahi mno moyoni mwake alisema “” Hakika #WEMA huwa hauozi ahsante mungu “” Kakinga aliingia ndani ya chumba kile akachukua Mali nusu akawapatia raia walikuwa wanateseka ndani ya kampuni hiyo. Baada ya mwaka mmoja kupita kakinga alikuwa tajiri mkubwa sana akaiboresha kampuni ile ikawa kituo cha watoto #YATIMA , Kakinga alitumia Mali nyingi kuyatibu macho ya Steven kwa uwezo wa mungu Steven alipona na akaona tena Akwelina alifurahi sana.



Monna pamoja na warda nao walikuwa matajiri wakubwa japokuwa moyo wa monna ulikosa furaha kwa kumpoteza kakinga katika maisha yake, Kakinga hakuhitaji kuwa na mke kutokana na umri wake kuwa mkubwa, Kakinga aliendelea kuwa tajiri siku hadi siku hadi leo kakinga ni tajiri mkubwa.



#ZINGATIO

Ndugu msomaji kumbuka siku zote katika maisha yako ukiona shida zinakuelemea tambua mafanikio hayapo mbali , Usikate tamaa hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani huwezijua mungu kapanga nini kwako .Tenda WEMA kwa yeyote hata kama humfahamu malipo yake yapo japo yatachelewa.

___ Shukrani kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho





MWISHO
 
KURA*KURA KURA** 🔥 🔥 🔥

SIMULIZI TATU ZA MWISHO, MSIMU HUU WA PILI, BAADA YA KUTUMA SIMULIZI SABA JAMII FORUM NA BURE SERIES

CHAGUA SIMULIZI IPI TUANZE NAYO.

1. SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua

2. DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha

3. MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi

4. OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi



Simulizi yenye kura 10. itatumwa, kura hazijafika 10 msimu wa pili utaishia hapa
 
CHAGUA SIMULIZI IPI TUANZE NAYO.

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua
......(Kura 0/10)

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha.
.....(Kura 0/10)

MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi
......(Kura 3/10)

OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi.
.....(Kura 0/10)

Simulizi yenye kura 10. itatumwa, kura hazijafika 10 msimu wa pili utaishia hapa
 
Bado tunaendelea na Uchaguzi, Simulizi yenye kura 10 itarusha, tupia kura yako.

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua ......(Kura 2/10)

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha......(Kura 0/10)

MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi......(Kura 4/10)


OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi......(Kura 0/10)
 
SEHEMU YA 50 KATI YA 50..............MWISHO



“” Mama na baba siamini kama ningewaona tena kwa kuwa mbali na ninyi hadi sasa nimekubwa binti mkubwa lakini kwa uwezo wa mungu leo nimewaona siamini.



“” Jamila mke wangu huyo nani anayelia na kuzungumza maneno hayo ?

“” Mume wangu hata Mimi sijamtambua bado , Sikia binti yangu wewe nani mbona sikutambui acha kulia nieleze ili nielewe binti ?



“” Mama na baba ni mimi mtoto wenu HASMA mwenye jina mgongoni kwangu lililoandikwa AKWELINA wazazi wangu ????



“” Hapana sio kweli hapana mume wangu hii sio kweli siamini .



“” Twende kwa msichana uliyenikabidhi kwake nilipokuwa mdogo sana mama nahisi ukimuona utaamini.



Akwelina aliwachukua wazazi wake pamoja na wafungwa wake ambao ni Patrick na Julius akakodisha gari likawapeleka hadi ndani ya kampuni ile. Kakinga , Monna, Bilali , Warda pamoja na raia walimuona akwelina akiingia ndani ya uwanja akiwa na wazazi wake mkononi ameshika kamba iliyomfunga Julius na Patrick, Raia walikuwa na hasira kali sana waliwafuata Patrick na Julius wakawapiga sana kipigo kilipozidi Julius na Patrick walipoteza fahamu raia walichukua kuni na mafuta wakawachoma moto , Warda alilia sana kumuona kaka yake ( Patrick ) anachomwa moto.



Monna alimfuata akwelina akamshika mkono akamsogeza karibu ya jamila alafu akasema :-



“” Dada naomba nikurudishie mtoto wako uliyenikabizi miaka ya nyuma sana Akwelina huyu ndio mama yako mzazi .



Steven hakuamini alichokuwa anasikia ikabidi amwite akwelina ( HASMA ) akapitisha mkono mgongoni kwake akagusa lile jina aliyomwandika akiwa mdogo sana ndipo alipoamini kama kweli ni mtoto wake Steven alimkumbatia Akwelina akiwa anatokwa na machozi mengi sana, Wakati huo kakinga alikuwa mbali kidogo, nae machozi ya furaha yalimtoka :-



“” Mtoto wangu hasma umekuwa binti mkubwa sioni Mimi ningekuona leo mwanangu daah alafu unaufunguo katika mwili wako mwanangu unajua hilo ?



“” Ndio baba na niliutoa kwa sababu watu wengi walikuwa wanautaka ufunguo huo ninao hapa hapa baba.



“” Mungu wangu afadhali naomba ufunguo huo .



Akwelina ( HASMA ) alimpatia baba yake ufunguo , Steven alibonyeza ufunguo ule ardhi yote katika kampuni hiyo ilitetemeka ghafla kilitokea chumba kikubwa chini ya ardhi katika uwanja huo , Steven aligeuka akampatia Akwelina ufunguo kisha akamwambia :-



” Fungua chumba hicho mwanangu ”



Akwelina alifungua chumba kile akashangaa sana kuona chumba chote kimejaa Mali mbalimbali zikiwemo almasi na dhahabu pia kulikuwa na masanduku mengi sana akwelina alipoyafungua aliona pesa zimejazwa ndani ya masanduku yale akwelina alizidi kushangaa na kugeuza macho huku na huko aliona karatasi moja ipo juu ya sanduku akaichukua akaisoma akagundua ile ilikuwa hati miliki ya kampuni hiyo.



Akwelina alitoka nje akiwa na furaha sana cha ajabu alimuona kakinga anaondoka akiwa na bilali Akwelina alimfuata akamziwia akamuuliza :-



“” Unakwenda wapi baba yangu ?



“” Naenda mbali akwelina samahani kwa kukuita jina hilo nimezoea hivyo , Nisikilize Hasma kwa sasa upo salama pia umekuwa binti mkubwa na wazazi wako wale pale wanakuhitaji nenda ukawalinde .



“” Mimi bila wewe hata wao wasingeniona leo, popote utapokwenda nitakuwa nawe pia kampuni hii pamoja na mali zote nakupa wewe bado nitaendelea kuwa chini yako baba yangu tafadhali kubali suala hili .



Kakinga hakuamini kama anaenda kuwa tajiri mkubwa sana duniani alifurahi mno moyoni mwake alisema “” Hakika #WEMA huwa hauozi ahsante mungu “” Kakinga aliingia ndani ya chumba kile akachukua Mali nusu akawapatia raia walikuwa wanateseka ndani ya kampuni hiyo. Baada ya mwaka mmoja kupita kakinga alikuwa tajiri mkubwa sana akaiboresha kampuni ile ikawa kituo cha watoto #YATIMA , Kakinga alitumia Mali nyingi kuyatibu macho ya Steven kwa uwezo wa mungu Steven alipona na akaona tena Akwelina alifurahi sana.



Monna pamoja na warda nao walikuwa matajiri wakubwa japokuwa moyo wa monna ulikosa furaha kwa kumpoteza kakinga katika maisha yake, Kakinga hakuhitaji kuwa na mke kutokana na umri wake kuwa mkubwa, Kakinga aliendelea kuwa tajiri siku hadi siku hadi leo kakinga ni tajiri mkubwa.



#ZINGATIO

Ndugu msomaji kumbuka siku zote katika maisha yako ukiona shida zinakuelemea tambua mafanikio hayapo mbali , Usikate tamaa hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani huwezijua mungu kapanga nini kwako .Tenda WEMA kwa yeyote hata kama humfahamu malipo yake yapo japo yatachelewa.

___ Shukrani kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho





MWISHO
Asante kwa simulizi nzuri
 
Back
Top Bottom