simuelewi kabisa mtu huyu

Zneba

Senior Member
May 12, 2010
192
7
Habari ya mchana huu wanajamvi,,

Ni miezi sita sasa tangu tuachane mimi na yy kwa madai kwamba ndugu zake hawajaridhika awe na mimi maishani ...cha ajabu ni mwezi sasa tangu aanze kunifata na kuniambia bado ananipenda sana na huko anakotaka kuoa moyo wake hauko huko ila ni shinikizo la ndugu.hivi inawezekana kweli?alichoniomba anataka aendeleze mawasiliano na mimi ya simu na hata siku akinikumbuka aonane na mimi kimaongezi kwa madai kwamba siyo yy aloamua hivyo ni ndugu zake ndo wamesababisha tukaachana.swali?hivi huyu anajua nini anataka? au ni kujikosha tu nimuone kwamba yy alikuwa na nia njema na mimi?mpango wangu nikukata mawasiliano kabisa na yy coz sioni sababu ya kuendelea kuwasiliana nae ila kabla sijafanya hivyo nimeona niwaulize wana jf mnishauri.
 
fuata hayo hayo mawazo uliyonayo,mpotezee kabisa atakupotezea muda wako bure
 
wewe mwenyewe umeshaamua kuendelea na maisha yako huna haja kutaka mawasiliano naye..............kama alikuwa anakupenda angeshikilia msimamo wake.........ameamua kufwata ushauri wa nduguzwe basi akubali na matokeo
 
Achana naye huyo hajajitambua, yani ameshachaguliwa mke na ww anakutaka wa nn? akufanye kidumu au?Mwombe mungu atakupa atakae ijua thamani yako!
 
yani huyo mkatie mawasiliano mazima, anatafuta mahali pa kupoozea njaa yake ya ngono!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom