Kuna siku nilielezea jinsi jamaa alivyo pigwa marufuku na mke wake kushika simu yake na alimwambia akishika ataipasua hiyo simu,sasa jana jamaa kaja tena na malalamiko mengingine, anasema ilikuwa muda wa saa tatu usiku mkewe alikuwa sebuleni yeye chumbani,mke wake akawa ameacha simu yake kitandani,akiwa pale akaona sms imeingia,maana anasema siku hizi mke wake huwa simu anaiweka silent,akaamua kuisoma kama kawaida yake alikutana na ujumbe unasema hivi"darling nashukuru sana maana mama g......amenielezea na sasa hivi mb.....inataka kutoboa ch.....,"baada ya kuisoma hapo hapo alimwita mkewe na kumwambia kuna sms yako,mama alipo isoma tu na kuifuta,jamaa akamuuliza ninani katuma hiyo sms amwambia sijui amwambia lete tumpigie akasema nimeshaifuta,kwanini bahati mbaya,sasa jaama anaomba ushauri kweli hapa kuna ndoa endelevu tena?maana aonavyo yeye mama anachakachua ndoa yao,wanajf mnasemaji kwa hili?