Simu za usiku kutoka kwa ndugu wa karibu huwa zinashtua sana

Ni kweli lazima upate mstuko, lakini Kuna simu zingine za usiku haswa toka kwa ndugu ni muhimu kupokea, huwezi jua labda unaweza kuwa msaada na kuokoa maisha ya mtu au vyovyote vile.
Kabla sijalala hua naweka simu silent na hii iliwahi nikuta siku moja nimepigiwa simu saa nane usiku Mama Yangu Mkubwa amefariki ghafla, nakumbuka nilivyo tapa tapa usiku ule bila kua na msaada wowote nikasema si bora hizi taarifa ningepewa asubuhi kuliko mateso haya,

Msiba mwingine wa Magufuli laiti ningekua nishaweka simu silent ile simu ya msiba isingenifanya nikeshe hadi asubuhi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom