Simu za Rais haziwi screened, Liyumba aenda hewani toka gerezani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu za Rais haziwi screened, Liyumba aenda hewani toka gerezani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NDOFU, Sep 2, 2011.

 1. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Akamatwa na simu ndani ya gereza akiwa mfungwa huku sheria za nchi zikiwa zinazuia kitendo hicho!

  Bosi aliyekuwa anawasiliana naye kuhusiana na rufaa yake ndiye aliyemchoma kwa maafisa wa jeshi la Magereza baada ya kuchoshwa na namna alivyokuwa anamsumbua kuhusiana na rufaa yake!

  Atolewa mahabusu na kwenda kuhojiwa kituo cha police...

  SOURCE: WAPO FM
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, heading yako na thread mbona vipo tofauti ebu ipitie tena uone jinsi gani ulikebishe
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,273
  Likes Received: 22,030
  Trophy Points: 280
  Pole play boy
   
 4. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Wamuongezee hata miaka 30,wa2 ka hao ha2wataki huku uraian kabisa.
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mle ndaniweni wana simu na maafande nd wanapewa kuzichaji............
   
 6. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimekuelewa mkuu' nilichokuwa nakimaanisha ni kuwa kosa kama alilokutwa nalo bwana Liumba adhabu yake ni kuongezewa miezi sita! Samahani kwa usumbufu!
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Sasa anamsumbuaa nini wakati muda wake ulishaisha???atulie sasa baada ya kupata miezi 6 mingine!
   
 8. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, nashukuru kwa kunielewasha tupo pamoja
   
 9. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amehojiwa kituo cha Sitaki shari' Bosi aliyemchoma ni mkubwa wizara ya mambo ya ndani' inadaiwa wakuu wa gereza walikuwa wanajua kuwa Liumba ana simu,Yule bosi alifanya kama kuwatishia "mbona mnaruhusu mfungwa kuwa na simu" kuona hivyo ikabidi wamgeuke Liumba.

  Lengo la yule bosi ilikuwa ni kuondoa usumbufu na maudhi aliyokuwa anayapata kwa kupigiwa simu na Liumba kuhusiana na mpango wa kumsafisha kupitia rufaa! Adhabu yake ni kifungo cha miezi sita zaidi kutoka kifungo cha mwanzo.
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Hajaota majipu kweli huyo mtuhumiwa? Kama bado wamuongeze tena kama nyundo 10 hivi ili akirudi uraiani vicheche vyake vimzomee.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Halafu oohh Kikwete hafanyi kazi, mngemuona Liyumba jela kama si Kikwete?
   
 12. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kalaghabaho!. Mzee wa visasi. Liyumba alikuwa mashine tata..alilamba vidosho vya jemedari..jk mwenyewe..ndo maana akamkomesha..ukitaka unyee debe fasta nyemelea vibinti vya "baba"..zengwe mapema,keko!
   
 13. b

  ben genious Senior Member

  #13
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh! msukule wa nape huo umeibuka, IDDY MUBARACK FF,tunajua unasumbuliwa na swaumu ya sita unasubili daku
   
 14. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Liyumba matatani tena, akutwa na simu gerezani

  Friday, 02 September 2011 21:04
  MWANANCHI

  James Magai

  [​IMG]

  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela, ameingia matatani tena akidaiwa kukutwa na simu gerezani aliyoitumia kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete.

  Liyumba kwa sasa anatumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili katika Gereza la Ukonga, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma wakati wa akifanya kazi BoT.

  Wakati bado akiwa anaendelea na adhabu hiyo, taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile zilisema Liyumba alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga na kuhojiwa kwa kosa la kukutwa na simu gerezani.

  Habari hizo zilifafanua kwamba Liyumba alifikishwa kituoni hapo saa 3:00 asubuhi kwa gari la Magereza lenye vioo vyeusi na kuhojiwa kwa muda wa takribani dakika 30 kuhusu tuhuma hizo.

  Vyanzo hivyo vya habari vilifafanua kwamba, Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ambayo ilibaki kituoni hapo kwa ushahidi.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Julai mwaka huu Liyumba alimpigia simu Rais Kikwete kwa kutumia simu hiyo. Hata hivyo, bado haijafahamika ni nini hasa alichomweleza Rais lakini habari zaidi zinadai kuwa kitendo hicho kilimfanya mkuu huyo wa nchi kuhoji iweje Liyumba amiliki simu wakati ni mfungwa?
  Kutokana na tukio hilo, inadaiwa kuwa maofisa usalama walimwekea mtego na juzi usiku walimdaka akiwa na simu hiyo na asubuhi yake walimpeleka kituoni hapo kwa mahojiano.

  “Sasa hivi kinachofanyika ni uchunguzi katika Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili kujua alichokuwa akikifanya kwenye hiyo simu na uchunguzi huo ukikamilika basi anaweza kupandishwa kizimbani wakati wowote,” kilidokeza chanzo chetu.

  Kifungo cha sasa
  Liyumba alihukumiwa kwenda jela miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 24, 2010 na hadi sasa ameshakaa gerezani kwa muda wa miezi 15 na siku 10 (mwaka mmoja, miezi mitatu).

  Kabla ya hukumu hiyo, alikuwa amekaa mahabusu kwa muda wa miezi 15 na siku 26 tangu siku aliyopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, kisha kupelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

  Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 27, 2009 akiwa na mshirika wake, Deogratias Kweka wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na matumizi mabaya ya ofisi za umma.

  Walikuwa wakidaiwa kutenda makosa hayo kwa kuidhinisha upanuzi wa mradi wa majengo pacha ya BoT, bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi na hivyo kuongeza gharama za mradi tofauti na zilizoidhinishwa na bodi.

  Hata hivyo, baadaye Kweka alifutiwa mashtaka na kubakia Liyumba peke yake ambaye naye alishinda kosa kubwa la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na kubaki na kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambalo lilimtia hatiani.

  Mei 28 mwaka huohuo, kwa kutumia jopo la mawakili walioongozwa na Majura Magafu, Liyumba alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitoa sababu 12 za kupinga hukumu hiyo pamoja na adhabu.
  Katika sababu zake za kupinga hukumu hiyo jopo la mawakili wa Liyumba pamoja na mambo mengine, lilisema Mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria na kiukweli katika kutathmini ushahidi na utetezi.

  Hata hivyo, Desemba 21, 2010, Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa yake na kukubaliana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mahakama za Tanzania hziwezi ku uphold code of Hammurabi. Mara mahakama inahukumu, hukumu inatenguliwa, kutenguliwa nako kunatenguuliwaBasi tabu tupu, hamna hata order wala precedent.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  To me hii inaonyesha ni namna gani JK mwenyewe alivyo mwepesi kiasi kwamba a felon tena akiwa ndani ya gereza anampigia sm! The only reason he could do that ni kwa sababu anafahamu jamaa hana noma. Where is the respect for the presidency???????????? Hivi huyu jamaa hata kama alikuwa karibu say na Mkapa angethubutu kufanya hilo?
   
 17. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  kweli watu wa ulinzi wa nchi hii wamelala, yaani mpaka mfungwa anamiliki vitu kama hivyo na bado walikuwa hawajui?!!!
   
 18. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Kama ameruhusiwa kuendelea kumiliki bastota akiwa gerezani ataweza kuzuiwa kutumia simu, hilo la simu haya magereza yetu imeshakuwa kitu cha kawaida
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kipo hiden hapa! Mawasiliano ya rais na liyumba inawezekana sio ya leo ni tangu mda mrefu, sasa inawezeka kuna kitu wamepishana tu jamaa kaamua kumchomea kwa maafwande!!
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Sep 3, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Je, ingekuwa Nyerere?
   
Loading...