Elections 2010 Simu za mikononi kudhibiti wizi wa kura na rushwa?

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Sina hakika ni kwa kiasi gani zitasaidia, lakini naamini kwa wakati huu hata silaha ndogo inahitajika katika mapambano.

Siku hizi simu za mikononi zenye camera na uwezo wa kurekodi sauti na hata muvi zimeenea sana miongoni mwa wananchi.

Naamini kuwa wakati wa kampeni na upigaji kura kutakuwa kuna faulu za hapa na pale. Nawashauri wananchi, wagombea, mawakala na wasimamizi wa uchaguzi, watumie mbinu zote ikiwezekana hata simu za mikononi kurekodi maongezi, picha, muvi n.k kwenye matukio ambayo wanaamini yanaashiria vitendo vya rafu...

Pia matumizi ya simu kurekodi sauti za wakuu wa vituo wakitangaza matokeo ya vituo husika, na kupiga picha karatasi za matokeo kwenye kila kituo ili kuwa sehemu ya kumbukumbu. Camera za kawaida zitasaidia zaidi kama zitapatikana...

Pia wenye vifaa kama iPod ni rahisi kutumia bila hata kuonekana kirahisi kurekodia sauti na picha...
 
Hii ni njia nzuri kupata ushahidi wa vitendo vya rafu katika uchaguzi ikiwemo vitendo vya rushwa. lakini swali ni je ni watanzania wangapi wanamiliki simu zenye uwezo wa kupiga picha au kurekodi sauti? na kama wanazo ni wangapi wanaweza kuzitumia?
 
Hii mbinu ni muhimu sana wakati huu inabidi vyama vya upinzani waingie gharama na kuhakikisha kila kituo kuna simu ya camera kuzuia wizi wa kura.MDC ya Zimbabwe walipiga picha matokeo ya kila kituo na siku ya pili walikuwa na jumla ya kura zote wakitumia simu za mkononi na kufanya wizi wa kura kuwa mgumu sana kwa Mugabe kama alivozoea chaguzi zilizopita.Hii inawezekana kila raia apige picha ya matokeo ya kituo chake hata kwa camera ya kawaida iwe kumbukumbu.Iran pia katika kituo kimoja Tehran wapiga kura wote walirudi siku ya pili na kuomba warudishiwe kura yao kwakuwa wote 18,000 walimpigia Mussavi na kituo kikatangaza Ahmedinejad anaongoza kituoni hapo.WIZI WA KURA HAUKUBALIKI KARNE HII!!
 
Kwani kuiba kura maana yake nini? Kwa sababu kama MDC walifanya hivyo kama unavyosema lakini badi Tsvangirai hakushinda kuna umuhimu gani sasa wa kufanya hivyo?
 
Kwani kuiba kura maana yake nini? Kwa sababu kama MDC walifanya hivyo kama unavyosema lakini badi Tsvangirai hakushinda kuna umuhimu gani sasa wa kufanya hivyo?

Tvangirai alishinda na matokeo yakacheleweshwa zaidi ya mwezi tume ikaamua urudiwe na Tsvangirai akajitoa lakini bado MdC wana wabunge wengi kushinda Zanu-pf.
 
Kwani kuiba kura maana yake nini? Kwa sababu kama MDC walifanya hivyo kama unavyosema lakini badi Tsvangirai hakushinda kuna umuhimu gani sasa wa kufanya hivyo?

Pia itasaidia kama zikiibwa, kila mtu anajua kwamba zimeibwa. Unakumbuka kenya TV zilivyowaumbua?

Nadhani ilisaidia leo Raila ni Waziri Mkuu, the same to Tsvangirai...
 
Back
Top Bottom