Simu za mikononi katika Mahusiano | Mwenendo wa Walezi/Wazazi kwenye familia

Kwangu naona afanye yoote ila siyo kuweka flight mode!!

Siku hizi ukiona mtoto anakufata unampa simu acheze game!

Binafsi naona maisha yangu yameathiriwa mno na simu
Ni muda wa kubadilika sasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Yeah jitahid kuwakataza...mm hawashiki kbs akishika ujue inaita ananiletea...mie nimewadownloadia app zao kwa laptop..wakichoka.katuni wanaangalia hizo games zao...!..ila malezi ya kipindi hiki ni magumu sana...!
 
Ahsante Asha D!
Kwanza poke busu langu la dhati kabisa!Na kumbato la kindaki ndaki!
Kiukweli niliumiss mwandiko wako. Ahsante sana kwa kurudi hivi!
BARIKIWA.

Katika vitu wazazi walezi tunapotoka ni matumizi ya simu na kutekwa akili nazo hasa tuwapo nyumbani!
SIMU IMEKUWA KIMBILIO
SIMU IMEKUWA MBADALA
SIMU IMEKUWA SULUHISHO
lakini yote haya ni masuluhisho yenye athari zenye kuibua matatizo mengine!

Mimi naomba nijitumie kama mfano
Nilijikuta mhanga wa matumizia ya simu kupita kiasi.
Mi ni aiana ya watu COMMUNICATION is EVERYTHING!
Nilikuwa najaribu kujaza ombwe nililokuwa ninalo moyoni!
We all pass in rough times in our lives, I had to use my phone tu kufil the gap and it helped!
IT HELPED UPANDE MMOJA IKAIBUA LINGINE UPANDE MWINGINE.
nilijikuta nimekuwa mbali na watoto wangu, nilikuwa naweza kushika simu asbh mpk jioni!
natoka JF naingia wasp , natoka wasp naingia Fb, aseeeeh ilikuwa worse!
UNTIL one day nilipoamua kuikataa simu na kuwork on my physical attachment to people hasa watoto wangu!.
Nikaamua kuwekeza muda wangu na akili kwa watoto hasa mdogo nilyekuwa naye, as wengine walishakua na hawakuwa nyumbani tena.
Huyu mdogo najitahisi sana, nisimuathiri na simu!
Tunafanya a lot of learning and entertaining activities pamoja.
tunapika, tunakula, tunaimba, tunachora, tunasoma vitabu,
Although bado naipenda but nimeshatoka kwenye uraibu kwa kiasi kikubwa sana!

Imebaki kuwa a close channel ya kufikia marafiki mana siko mzuri sana kwenye urafiki wa ana kwa ana. , kushiriki ujuzi na uzoefu mbalimbali wa maisha.
Nina mabinti wa kubwa tu but wote sijaruhusu wawe na simu!
Huyu mdogo anajua simu ya yeyote ni out of boundary stuff. So hana tu time na simu!
 
Mkuu,

Asante kwa mchango wako. Kwa wale ambao tayari ni mateja na kubadilika ni changamoto, una kitu unaweza kushauri ili kuweka wepesi kuachana na tabia hiyo?
Kwanza Mkuu mimi nadhani mabadiliko yoyote Huanza na Muhusika binafsi..awe na dhamira kweli ya kuachana na Simu kama sio kupunguza matumizi ya simu wakati wote.

Akishakua na dhamira na kweli kaamua, Jambo MOJA kubwa ili uweze kufanikiwa ni wewe kuyaweka mawazo yako mbali na simu yako na kuwaza vitu vingine Muhimu vya kufanya kwa wakati husika.

Si rahisi kuyaweka mawazo mbali na simu wakati simu ipo mfukoni na umeskia ki notification cha msg ya whatsapp imeingia,au rafiki yako anakupigia simu inaita,nk Nadhani chakufanya ili ufanikishe Hayo si kuzima simu bali ni kuweka SILENT simu yako.

Silent nikimaanisha usiweke hata vibration yani simu ikiita au msg ikiingia hata kama umeishika mkononi usigundue kitu, Kisha baada ya kufanya hatua zote hizo HATUA YA MWISHO ni kujiwekea muda maalumu wa kuishika simu yako.

Kama ukiamua utashika simu Asubuhi kabla hujatoka nyumbani na Jioni ukitoka kazini basi iwe hivyo na si kushika simu tuu lakini kuishika simu kuwe kwa sababu MAALUM sio kwasababu umesema kila asubuhi ntashika simu Na ikafika asubuhi huna cha kufanya kwenye simu basi uishike..HAPANA.

Usiweke simu kuwa ndio njia pekee ya ku kukumbusha vitu vyako...ishi maisha kama huna simu Siku hizi watu hata saa Hawavai kisa tu Simu ina SAA..siku hizi hamna hata zile Alarm za kuamsha watu ASUBUHI kisa tu SIMU ina kila kitu Matumizi ya vitu halisia kulingana na uhitaji wake ktk maisha yetu utatusaidia kujiweka mbali na SIMU.

Siku hizi mtu anavaa ear phone unamkuta anasikiliza radio ya kwenye simu kisa tu Simu ina radio...Kama unajiona unataka kukaa mbali na simu na unapenda Radio basi nunua ka radio kadogo ukitaka kuskiliza sikiliza hiyo..SIMU IWE KWA MAWASILIANO TU.

nadhani kama tukiamua inawezekana....ILA bila maamuzi magumu SIO JAMBO JEPESI ni lazima UDHAMIRIE HASWA.
 
Simu ni moja ya kifaa cha msingi katika maisha yetu ya kila siku, ndiyo inatuunganisha kirahisi pale tunapokuwa hatupo katika uwepo wa wale tunaotakiwa kuwasiliana nao. Zaidi ya kuweza kuendesha maisha yetu kijamii na kikazi, simu ina uwezo wa kuboresha mahusiano kama ambavyo ina uwezo mkubwa wa kudhoofisha mahusiano hayohayo kutegemeana na matumizi yake.

Makala hii ni ya kwanza katika mlolongo wa makala nilizoandaa ikizingatia matumizi ya simu katika kujenga au kubomoa mahusiano ya mtumiaji kwa watu waliomzunguka katika jamii, iwe ni wenza, wapenzi, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi, n.k

Leo nitajikita kwa wazazi/walezi majumbani dhidi ya matumizi ya simu na mwenendo wao kwa familia haswa watoto hadi kupelekea tabia na taratibu zao nyingi kuendeshwa na simu za mkononi wanazomiliki aidha kwa kutambua ama kutotambua. Napenda nitumie fursa hii kutathmini yale nitakayowasilisha, tutoe maoni yanayolenga kuboresha.

Uimara na ukaribu wa wanafamilia unategemea kwa kiasi kikubwa namna ambavyo familia hiyo inahusiana. Kuhusiana vizuri huambatana na matendo ya upendo, heshima na mawasiliano. Hata hivyo, kwa dunia ya leo imekuwa ni Changamoto kuweza kuhusiana vema majumbani, simu ikiwa moja ya sababu kubwa ya upungufu huo. Swali la msingi la kujiuliza, wewe kama Mzazi/Mlezi matumizi yako ya simu yanajenga au kudhoofisha/kubomoa?

Kuweza kufahamu kwa urahisi nafasi zetu katika matumizi ya simu, ni muhimu kuangalia, makosa ambayo wazazi/walezi huyafanya na simu.

Baadhi ya Makosa ambayo wazazi/walezi huyafanya na simu.

1. Kuipa simu umiliki wa akili na msingi wa maamuzi awapo nyumbani
Hili limekuwa suala la kawaida sana kwa wazazi/walezi wengi mara wafikapo nyumbani. Wanashinda kwenye shughuli siku nzima mbali na nyumbani, lakini bado wakifika nyumbani wanakuwa ‘busy’ na simu haswa kwenye ku-chati, kutembelea mitandao ya kijamii na kufuatilia masuala mbalimbali ya kiulimwengu kupitia kiganja na hivyo kupuuzia kabisa mwenza/mpenzi pamoja na watoto. Kiasi kwamba kuna wakati anaona kero hata pale mtoto anapokuwa anahitaji umakini (attention) yake kwake. Mbaya zaidi ni kwa zile familia ambazo wazazi/walezi wote wawili wametekwa na simu, hivyo watoto huleana wenyewe zaidi au na dada wa kazi (ikitokea naye hajatekwa na simu).​

2. Kutumia simu wakati wa mlo (meals)
Wakati wa mlo ni moja la wakati wa msingi wa familia kujamiiana, kufahamu nini kinaendelea katika maisha ya wanao/wanafamilia na ni wakati mzuri pia wa ku re-connect haswa kwa wazazi ambao siku zote wapo makazini na uwepo wao nyumbani kuwa mfinyu. Pamoja na kuwa mzazi hawekewi masharti ya jinsi ya kulea mtoto wake, na kipi cha kufanya ama kutofanya - kitendo cha mzazi kutumia simu akiwa na familia yake wakati wa mlo ni moja ya njia ya wazi inayoonesha kuwa, wale unaowasiliana nao kwenye simu au kile unachokifanya kuwa muhimu zaidi ya kuwapa ‘full-attention’ familia yako kwa ile nafasi ndogo unayobahatika kuwa nao. Heshima ni ya pande zote mbili, mkubwa anapaswa kumuheshimu mtoto kama vile ambavyo watoto wanatarajiwa kuwaheshimu wakubwa zao. Njia rahisi ya kumuonesha heshima mtoto hata mwenza/mpenzi ni kumsikiliza na kumpa usikivu, kujali kile kinachomgusa katika maisha yake ya kila siku na pia kuelewa kile anachokutana nacho kila siku bila kujalisha unaweza kutatua au hutoweza.​

3. Kuwapatia watoto simu kwa ajili ya kuchezea
Katika hoja hii tunajikita kwenye yeye kutumia simu ‘yako’ kama kifaa cha kuchezea (siku nyingine nitagusia umri sahihi unaoshauriwa mtoto kuwa na simu). Kuna tofauti ya mtoto kumiliki simu akiwa kanunuliwa na mzazi, na mzazi kumpatia mtoto simu awe anachezea. Kumpa mtoto simu achezee ni njia mojawapo rahisi ya kumridhisha mtoto kiasi kwamba atatulia hapo bila usumbufu wowote ule. Mzazi gani hataki apumzike mtoto asimkere au kumsumbua ? Ni wengi. Bahati mbaya, ni wazazi wachache ambao wanafahamu namna ya kuweka/kubadilisha matumizi ya vifaa hivyo ili viwe kwenye mfumo wa matumizi ya mtoto (kid mode). Na mbaya zaidi, wazazi wengi huitumia kama kumtuliza mtoto wakifuata njia rahisi na badala ya ile ndefu ya kuweza kumkatalia mwanae kwa kumwelewesha kuwa si wakati wote ni wa kuchezea simu na hivyo kujenga mtoto ambaye anaona anastahili kila kitu kilichopo machoni pake bila kujali simu hiyo ni ya mgeni ama lah.​

Athari

1. Kutojenga nidhamu ndani ya familia. Watoto wanakua katika mazingira ya kuonyweshwa kutokuwepo na umuhimu na haja ya muda wa familia na thamani yake. Na pia mtoto kuona ni sawa kudharau ‘ignore’ watu pale ambapo umakini wake unahitajika.

2. Kama mzazi/mlezi unakuwa unapitwa kwa kiasi kikubwa na yale yanayojiri katika maisha ya watoto haswa kama ni wadogo. Watoto wanapenda kusililizwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa. Kuna changamoto ya mapenzi yanayopaswa kuelekezwa kwa mzazi yakatolewa kwa mtu ambaye anaweza kuwa si salama kwa mwanao.

3. Kukosekana kwa nyakati za msingi za kifamilia ambazo hujenga kumbukumbu za msingi kwa mtoto. Kama vile kukaa na kula pamoja, kusali sala ya usiku pamoja, kukaa na kufurahia kitu kwa pamoja.

4. Wazazi/Walezi kutofahamu yale yanayojiri kila siku katika maisha ya watoto wao. Inaweza kuonekana ni sawa, ila watoto nao wana changamoto zao wanazozipitia kila siku ambazo zinahitaji umakini na ukaribu wa wazazi na walezi patika kuwajenga kuwa vijana wazuri katika maisha yao. Wengine hupatwa na unyanyasaji wa kijinsia, na mtoto hutakiwa kujengewa kujiamini na kumuamini mzazi ili kueleza tatizo analokutana nalo, wakati mwingine hata ndani ya familia.

Ushauri

Tumekuwa wazazi na walezi ambao tupo Katika wakati ambao teknolojia imekuwa kubwa kuliko wakati wowote ule hapa duniani. Ni muhimu sana kuwa karibu sana na watoto wetu, na kuhakikisha hizi simu hazitufanyi mazezeta kiasi kwamba tunasahau majukumu na nafasi zetu pale tunapokuwa majumbani na familia zetu.

Kwa wale ambao kazi zinachukua maisha yako kwa kiasi kikubwa, wanaweza pia kujenga tabia ya kuwa na simu mbili. Simu ya kazi na simu ya nyumbani. Pale unapokuwa umefika nyumbani unazima kabisa simu na kutumia vema muda huo kwa ajili ya nyumbani ili kupunguza usumbufu. Nidhamu hutokana na kujiwekea misingi ya matumizi mazuri ya simu ambayo kwa namna yoyote ile hayataingiliana na nafasi yako kama mzazi/mlezi nyumbani.

Ni muhimu pia kwa familia kujiwekea taratibu za kuhakikisha simu haziruhusiwi kwenye baadhi ya nyakati za ‘family time’ ili kujenga mazingira ya kuwa karibu na kuzingatia wale walio mbele yako na si wanaopatikana kwenye simu.

Nimewasilisha hayo kwa uchache, una maoni, mawazo, ushauri au marekebisho? Tafadhali usisite kuchangia.

Karibuni katika kufahamishana zaidi,
Great article mjomba.
 
Mkuu,

Una mfano halisi wa matatizo ya kifamilia (haswa kwa wazazi dhidi ya watoto) ambao unao na unaweza ‘share’ nasi kwa manufaa ya wengi?

Asante kwa hoja zako, zote naunga mkono.

Ahaaa haaa haaa
Mimi nimepishana na mke wangu mara kadhaa. Hasa nilipokuwa admin wa group la o-level.
Lkn sasa najitahidi SANA kupunguza matumizi nikiwa nyumbani.
 
N
Kwanza Mkuu mimi nadhani mabadiliko yoyote Huanza na Muhusika binafsi..awe na dhamira kweli ya kuachana na Simu kama sio kupunguza matumizi ya simu wakati wote.

Akishakua na dhamira na kweli kaamua, Jambo MOJA kubwa ili uweze kufanikiwa ni wewe kuyaweka mawazo yako mbali na simu yako na kuwaza vitu vingine Muhimu vya kufanya kwa wakati husika.

Si rahisi kuyaweka mawazo mbali na simu wakati simu ipo mfukoni na umeskia ki notification cha msg ya whatsapp imeingia,au rafiki yako anakupigia simu inaita,nk Nadhani chakufanya ili ufanikishe Hayo si kuzima simu bali ni kuweka SILENT simu yako.

Silent nikimaanisha usiweke hata vibration yani simu ikiita au msg ikiingia hata kama umeishika mkononi usigundue kitu, Kisha baada ya kufanya hatua zote hizo HATUA YA MWISHO ni kujiwekea muda maalumu wa kuishika simu yako.

Kama ukiamua utashika simu Asubuhi kabla hujatoka nyumbani na Jioni ukitoka kazini basi iwe hivyo na si kushika simu tuu lakini kuishika simu kuwe kwa sababu MAALUM sio kwasababu umesema kila asubuhi ntashika simu Na ikafika asubuhi huna cha kufanya kwenye simu basi uishike..HAPANA.

Usiweke simu kuwa ndio njia pekee ya ku kukumbusha vitu vyako...ishi maisha kama huna simu Siku hizi watu hata saa Hawavai kisa tu Simu ina SAA..siku hizi hamna hata zile Alarm za kuamsha watu ASUBUHI kisa tu SIMU ina kila kitu Matumizi ya vitu halisia kulingana na uhitaji wake ktk maisha yetu utatusaidia kujiweka mbali na SIMU.

Siku hizi mtu anavaa ear phone unamkuta anasikiliza radio ya kwenye simu kisa tu Simu ina radio...Kama unajiona unataka kukaa mbali na simu na unapenda Radio basi nunua ka radio kadogo ukitaka kuskiliza sikiliza hiyo..SIMU IWE KWA MAWASILIANO TU.

nadhani kama tukiamua inawezekana....ILA bila maamuzi magumu SIO JAMBO JEPESI ni lazima UDHAMIRIE HASWA.
Nimepractise Hizi.

Na nikafanikiwa
 
Asante kwa kuileta mada hii.
Binafsi naona simu inakufanyia kile unachokitamani ikufanyie.
Ndo maana kuna msemo wa kiingereza usemao " too much of everything is harmful".
Hivyo tuzingatie kanuni hii ya kufanya kila kitu bila kuzidisha kipimo.
Simu ukitaka ikuongezee kipato,inawezafanya hivyo. Ukitaka ikufilisi inaouwezo wa kufanya hivyo.
Ukitaka iwe miguu na midomo yako kwa uzuri au kwa ubaya inauwezo wa kufanya hivyo.
Ushauri wangu ni tujifunze kwa waliotutengenezea simu toka Enzi hizo wanatumia
mbona hazijawadhuru badala yake wanazidi kuendelea.

Kwa habari ya malezi ya watoto,fanya utafiti utagundua
familia zenye kipato cha kati au chini watoto wao
wanaongoza kwa maadili hata kufanya vizuri shuleni
ukilinganisha na hawa wanaolilia simu za wazazi wao
na wakati mwingine kununuliwa za kwao kabisa.Ni vizuri
tukajifunza kuwaelimisha watoto kushika sana masomo
na wale wadogo tuwazoeshe kucheza michezo
kama ile ya kuendesha/kuchezea na kuunda magari
au baiskeli na mingine kama hiyo isiyo na madhara
kwenye mboni za macho n.k,
Tumewageuza watoto wetu kama glass za vioo
wakilia kidogo tunajilaumu na kuwapa wanacholilia bila
kuangalia athari zitakazojitokeza mbele.

Kwa muda niliotumia simu nje na mawasiliano
nimegundua ukianza mambo ya games,kila siku
unataka ucheze game mpya.Matokeo yake
unajijengea tabia ya kutafuta mambo mapya
kila kukicha. Kama hukujiwekea limit
unajikuta umefika mbali na kurudi ulikotoka ni ngumu
jiulize akili ya watoto ilivyo na udadisi na kutaka kujua kila kitu
kwa kasi kasi, itakuwaje?
 
jiulize akili ya watoto ilivyo na kasi inakuwaje?
 
Asante sana kwa mleta mada kwani kwa upande wangu ni jambo ambalo ninapambana nalo kila siku.

Nilinunuliwa simu yangu ya kwanza na wazazi nikiwa form 3 na mpaka sasa nakiri nikiwa O-level nilikuwa na nidhamu tele ya matumizi ya simu na natamani sana nirudie ile hali.

Kwa sasa baada ya kutafakari sana kuhusu athari za matumizi ya simu niliyoyapata niliamua kuchukua hatua kadhaa japo bado nahisi sijalimaliza tatizo. Hatua hizo kwa ufupi ni:-

1. Kwa makusudi nimebakiwa na application moja tu ya watsup ambayo kwangu ninaona ni rahisi kuwasiliana na wapendwa wangu.

2. App ya Facebook nimeidelete kwenye simu na nikitaka kuitumia mpaka kwenye lap top. Hii imenisaidia kutokuwa na mambo mengi ya kuyafungua nikiwa na simu.

3. IMO nimefuta moja kwa moja.

4. Tweeter na Instagram niliamua kwa makusudi kutozitumia.

5. Mwaka mzima simu nimeiweka silence mode.

6. Nikiwa kwenye mazungumzo na mtu au outing siigusi kabisa simu na kama nipo nyumbani naiacha chumbani.

7.Nikiawa nakula simu na naiacha chumbani kabisa. Na usiku nikilala naizima. N.k.

Kusema ukweli tutashuhudia sana kizazi chenye msongo wa mawazo na hofu tukiendelea kupuuza matumizi mema ya mtandao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom