Simu za mikononi katika Mahusiano | Mwenendo wa Walezi/Wazazi kwenye familia

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
Simu ni moja ya kifaa cha msingi katika maisha yetu ya kila siku, ndiyo inatuunganisha kirahisi pale tunapokuwa hatupo katika uwepo wa wale tunaotakiwa kuwasiliana nao. Zaidi ya kuweza kuendesha maisha yetu kijamii na kikazi, simu ina uwezo wa kuboresha mahusiano kama ambavyo ina uwezo mkubwa wa kudhoofisha mahusiano hayohayo kutegemeana na matumizi yake.

Leo nitajikita kwa wazazi/walezi majumbani dhidi ya matumizi ya simu na mwenendo wao kwa familia haswa watoto hadi kupelekea tabia na taratibu zao nyingi kuendeshwa na simu za mkononi wanazomiliki aidha kwa kutambua ama kutotambua. Napenda nitumie fursa hii kutathmini yale nitakayowasilisha, tutoe maoni yanayolenga kuboresha.

Uimara na ukaribu wa wanafamilia unategemea kwa kiasi kikubwa namna ambavyo familia hiyo inahusiana. Kuhusiana vizuri huambatana na matendo ya upendo, heshima na mawasiliano. Hata hivyo, kwa dunia ya leo imekuwa ni Changamoto kuweza kuhusiana vema majumbani, simu ikiwa moja ya sababu kubwa ya upungufu huo. Swali la msingi la kujiuliza, wewe kama Mzazi/Mlezi matumizi yako ya simu yanajenga au kudhoofisha/kubomoa?

Swali.png
Kuweza kufahamu kwa urahisi nafasi zetu katika matumizi ya simu, ni muhimu kuangalia, makosa ambayo wazazi/walezi huyafanya na simu.

Baadhi ya Makosa ambayo wazazi/walezi huyafanya na simu.

1. Kuona Teknolojia ya Kidigitali haifai kwa mtoto

Si kweli mtazamo huu. Endapo kama Mlezi anauwezo wa kumnunulia mwanao kifaa cha Kidigitali, inashauriwa kumwezesha mtoto toka akiwa na umri wa miezi 12 (kwa kumsimamia maudhui), na toka umri wa 0 - Miezi 12 akiwa yupo na mzazi pamoja bila kumuachia.

Angalizo: Ni mhimu kuzingatia aina ya maudhui unayompatia mwanao ili kuhakikisha inaendana na umri wake kuhakikisha unaepusha athari za aina yoyote ile kwa Mtoto.

2. Kumuwezesha/milikisha Mtoto kifaa cha Kidigitali bila misingi ya matumizi

Kuna msomo "Too much is harmful" ndivyo ilivyo hata katika matumizi ya vifaa vya Kidigitali, si kwa watoto tu, bali hata kwa watu wazima. Vifaa vya Kidigitali kawaida huwa na ‘Settings’. Ni vyema mzazi kufahamu ni namna ipi unaweza kuweka settings ambazo zinawezesha kumlinda katika matumizi. Mfano, unaweza ukaset mtoto wako atumie kifaa hicho masaa mawili asubuni na mawili jioni.

Angalizo: Hii hufanya kazi vema zaidi, pale Mlezi anapokuwa kajenga utaratibu wa shughuli na ratiba ya za mtoto, ikihusisha vitu kama michezo, masomo n.k

3. Kuwezesha mtoto kifaa bila ya kufahamu namna ya kumlinda

Hili huathiri haswa wale wazazi ambao huwapatia watoto wao Smart phones wakiwa ni wadogo ama ndiyo wanachipuka (miaka 9-16). Ni vema kufahamu kifaa kinatumika vipi, anawasiliana na nani na kwa nini ama vitu vipi.

Angalizo: Teknolojia imekua sana. Kama ni mtoto mjanja au anashirikiana na watt wa ganga, anaweza kuwasiliana na watu kwa kificho hata kama unakagua kifaa hicho bila kufahamu. So ni mhimu mzazi kuwa makini zaidi na mjanja pia (hata kwa kuuliza wataalam au wale wenye ufahamu.

4. Kumwezesha mtoto kupata Intaneti bila mipaka

Internet haichagui mtu na wala haikagui endapo anayeitumia ni mtoto au mtu mzima hadi kwenye baadhi ya sites ambazo hutaka umri ili kuweza kujisajili (ambalo mtoto mjanja ataongopa tu). Watoto haswa mashuleni husimuliana masuala mengi na ndiyo chanzo ya watoto wengi kutembelea sites ambazo si salama kwao na hata kwa kukutana na kesi za watu wazima kuwarubuni na takati mwingine hadi wakabahatika kuwadhuru.

Ushauri: Kama ukiweza kupata wataalam wakakusaidia (haswa wale wenye WiFi majumbani) unaweza kuomba ISP to block sites kama hizo.

5. Kuwapatia watoto simu kwa ajili ya kuchezea

Katika hoja hii tunajikita kwenye yeye kutumia simu ‘yako’ kama kifaa cha kuchezea (siku nyingine nitagusia umri sahihi unaoshauriwa mtoto kuwa na simu). Kuna tofauti ya mtoto kumiliki simu akiwa kanunuliwa na mzazi, na mzazi kumpatia mtoto simu awe anachezea. Kumpa mtoto simu achezee ni njia mojawapo rahisi ya kumridhisha mtoto kiasi kwamba atatulia hapo bila usumbufu wowote ule. Mzazi gani hataki apumzike mtoto asimkere au kumsumbua ? Ni wengi. Bahati mbaya, ni wazazi wachache ambao wanafahamu namna ya kuweka/kubadilisha matumizi ya vifaa hivyo ili viwe kwenye mfumo wa matumizi ya mtoto (kid mode). Na mbaya zaidi, wazazi wengi huitumia kama kumtuliza mtoto wakifuata njia rahisi na badala ya ile ndefu ya kuweza kumkatalia mwanae kwa kumwelewesha kuwa si wakati wote ni wa kuchezea simu na hivyo kujenga mtoto ambaye anaona anastahili kila kitu kilichopo machoni pake bila kujali simu hiyo ni ya mgeni ama lah.

Madhara: Yameorodheshwa mwishoni kabisa mwa hoja hii

6. Kuweka taswira ya mtoto kila kitu kuwa wazi kwa jamii toka kazaliwa kwa ulimwengu

Hii huwa shida si kubwa pale mtoto anapozaliwa, ila anapoendelea kukua kuna stigma inampata mtoto huku mtaani, mashuleni na hata katika jamii. Anakuwa kanyimwa kabisa faragha binafsi na kumfanya kuwa very self conscious akikua. Kutumia simu mfurulizo kwenye mkusanyiko wa jambo mhimu wa Kifamilia. Dunia ya Kidigitali inatisha na siku zanavyosonga, suala la Data binafsi kwa ajili ya usalama inakuwa. Mlezi bila kufahamu, unamfanya mwanao awe 'vulnerable' na kumhatarisha

Angalizo: Ni mhimu wazaziii tukumbushane kuwa maisha ni safari, hatujui ya kesho. Mfano mtoto anaweza kuanikwa maisha yake hivyo wakati akiishi maisha ya fahari na ya wazi kwa dunia. Unakuwa umenyima haki ya mtoto kujitambua bila uoga wa ulimwengu utakavyo ona maamuzi yake hata ya kawaida ya kimaisha.

7. Kuipa simu umiliki wa akili na msingi wa maamuzi awapo nyumbani

Hili limekuwa suala la kawaida sana kwa wazazi/walezi wengi mara wafikapo nyumbani. Wanashinda kwenye shughuli siku nzima mbali na nyumbani, lakini bado wakifika nyumbani wanakuwa ‘busy’ na simu haswa kwenye ku-chati, kutembelea mitandao ya kijamii na kufuatilia masuala mbalimbali ya kiulimwengu kupitia kiganja na hivyo kupuuzia kabisa mwenza/mpenzi pamoja na watoto. Kiasi kwamba kuna wakati anaona kero hata pale mtoto anapokuwa anahitaji umakini (attention) yake kwake. Mbaya zaidi ni kwa zile familia ambazo wazazi/walezi wote wawili wametekwa na simu, hivyo watoto huleana wenyewe zaidi au na dada wa kazi (ikitokea naye hajatekwa na simu).

8. Kutoweka misingi au mazoea ya kuzungumzia Matumizi ya Teknolojia hususani Mitandao ya Kijamii

Endapo familia yako mnakubali na kutumia Teknojojia ya Kidigitali vilivyo, ni vema kuwema mazoea ya mara moja moja kuzunguzmia kile ambacho kila mmoja anakutana nacho kama changamoto, ikiwa ni njia ya kufungua mazungumzo ya fursa na changamoto ya Mitandao ya Kijamii, hapo hapo kutoa nafasi ya kuelimishana namna watoto wanaweza kujilinda haswa katika Mitandao ya Kijamii na Mawasiliano.

9. Kutumia simu wakati wa mikutano/mikusanyiko ya mhimu majumbani

Kama mlezi, ni mhimu kuishi kwa mfano. Kwa dharura si mbaya, ila ikiwa mazoea, hizo ni dalili za dharau kwa wanafamilia, ubinafsi na ukosefu wa nidhamu tabia ambayo haipendezi mwanao aige. Nitolee mfano wa matumizi ya simi patika mlo. Wakati wa mlo ni moja la wakati wa msingi wa familia kujamiiana, kufahamu nini kinaendelea katika maisha ya wanao/wanafamilia na ni wakati mzuri pia wa ku re-connect haswa kwa wazazi ambao siku zote wapo makazini na uwepo wao nyumbani kuwa mfinyu. Pamoja na kuwa mzazi hawekewi masharti ya jinsi ya kulea mtoto wake, na kipi cha kufanya ama kutofanya - kitendo cha mzazi kutumia simu akiwa na familia yake wakati wa mlo ni moja ya njia ya wazi inayoonesha kuwa, wale unaowasiliana nao kwenye simu au kile unachokifanya kuwa muhimu zaidi ya kuwapa ‘full-attention’ familia yako kwa ile nafasi ndogo unayobahatika kuwa nao.

Nasaha: Heshima ni ya pande zote mbili, mkubwa anapaswa kumuheshimu mtoto kama vile ambavyo watoto wanatarajiwa kuwaheshimu wakubwa zao. Njia rahisi ya kumuonesha heshima mtoto hata mwenza/mpenzi ni kumsikiliza na kumpa usikivu, kujali kile kinachomgusa katika maisha yake ya kila siku na pia kuelewa kile anachokutana nacho kila siku bila kujalisha unaweza kutatua au hutoweza.

Athari za kufanya hays ama baadhi ya hoja hizo zilizowasilishwa

1. Kutojenga nidhamu ndani ya familia. Watoto wanakua katika mazingira ya kuonyweshwa kutokuwepo na umuhimu na haja ya muda wa familia na thamani yake. Na pia mtoto kuona ni sawa kudharau ‘ignore’ watu pale ambapo umakini wake unahitajika.

2. Kama mzazi/mlezi unakuwa unapitwa kwa kiasi kikubwa na yale yanayojiri katika maisha ya watoto haswa kama ni wadogo. Watoto wanapenda kusililizwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa. Kuna changamoto ya mapenzi yanayopaswa kuelekezwa kwa mzazi yakatolewa kwa mtu ambaye anaweza kuwa si salama kwa mwanao.

3. Kukosekana kwa nyakati za msingi za kifamilia ambazo hujenga kumbukumbu za msingi kwa mtoto. Kama vile kukaa na kula pamoja, kusali sala ya usiku pamoja, kukaa na kufurahia kitu kwa pamoja.

4. Wazazi/Walezi kutofahamu yale yanayojiri kila siku katika maisha ya watoto wao. Inaweza kuonekana ni sawa, ila watoto nao wana changamoto zao wanazozipitia kila siku ambazo zinahitaji umakini na ukaribu wa wazazi na walezi patika kuwajenga kuwa vijana wazuri katika maisha yao. Wengine hupatwa na unyanyasaji wa kijinsia, na mtoto hutakiwa kujengewa kujiamini na kumuamini mzazi ili kueleza tatizo analokutana nalo, wakati mwingine hata ndani ya familia.

Ushauri kwa Walezi

Tumekuwa wazazi na walezi ambao tupo Katika wakati ambao teknolojia imekuwa kubwa kuliko wakati wowote ule hapa duniani. Ni muhimu sana kuwa karibu sana na watoto wetu, na kuhakikisha hizi simu hazitufanyi mazezeta kiasi kwamba tunasahau majukumu na nafasi zetu pale tunapokuwa majumbani na familia zetu.

Kwa wale ambao kazi zinachukua maisha yako kwa kiasi kikubwa, wanaweza pia kujenga tabia ya kuwa na simu mbili. Simu ya kazi na simu ya nyumbani. Pale unapokuwa umefika nyumbani unazima kabisa simu na kutumia vema muda huo kwa ajili ya nyumbani ili kupunguza usumbufu. Nidhamu hutokana na kujiwekea misingi ya matumizi mazuri ya simu ambayo kwa namna yoyote ile hayataingiliana na nafasi yako kama mzazi/mlezi nyumbani.

Ni muhimu pia kwa familia kujiwekea taratibu za kuhakikisha simu haziruhusiwi kwenye baadhi ya nyakati za ‘family time’ ili kujenga mazingira ya kuwa karibu na kuzingatia wale walio mbele yako na si wanaopatikana kwenye simu.

Baadhi ya Maoni katika mfumo wa Graphic ambazo tunaweza share kwa Familia zeta kukumbushana

#FamiliaYaKidigitali

Swali.png

#FamiliaYaKidigitali
Digial.png

#FamiliaYaKidigitali

FAMILIA.png

#FamiliaYaKidigitali
Settings.png

#FamiliaYaKidigitali

Familia ya Kidigitali.png

#FamiliaYaKidigitali
Simu.png

#FamiliaYaKidigitali
ushauri.png

Nimewasilisha hayo kwa uchache, una maoni, mawazo, ushauri au marekebisho? Tafadhali usisite kuchangia.

Karibuni katika kufahamishana zaidi,
 
Ni mada nzuri.
simu imekuwa ni janga na si baraka tena.
1. Imeingiza familia nyingi kwenye matatizo.
2. wanafunzi kuto zingatia masomo.
3. wafanyakazi kutokuwa makini na kutilia maanani kazi wanazofanya.
4. watu wengi kuzitumia kusambaza habari zisizo za kweli.
5. zimetumika kuangalia picha chafu kwa watu wa rika zote.
6. inaathiri macho na masikio ya vijana wengi, kwani muda mwingi hutumia kutazama au kusikiliza simu.
7. Imetufanya watumwa, kila dakika LAZIMA tuiguse. hatuwezi kuiacha nyumbani asubuhi na kuikuta jioni.
n.k.
Tunahitaji hekima kutoka juu ili kutatua hili.
 
Ni janga hili uzuri matokeo hasi tumeanza kuyaona mapema. Tukiacha simu zitusaidie kwenye makuzi na malezi ya vijana wetu, tutavuna tulichopanda.

Wakati mwengine unaweza pata mgeni nyumbani hata hamjasalimiana vizuri anauliza una charger ya simu "Z" au umeme upo? Nataka nichajishe simu yangu..

Nakaa na kutafakari huo muda wa ziada ambao tunakaa na kuupoteza kwenye hizi simu zetu pendwa "simu janja" tumeutoa wapi?.
 
Ndio mana nasemaga kama kwa mwanaume/mwanamke mwenye FAMILIA kama inatakiwa mkubaliane kwamba ni lazima kuwe na simu ya MEZANI nymbani ambayo ndio itatumika Pindi mama/baba anaporudi nyumbani Ni sheria sio OMBI tukirudi nyumbani wote Tuzime simu zetu au tuweke Flight mode..kwa mwenye Shida na mawasiliano aende kutumia simu ya MEZANI apige.

Kutumia simu zetu za mkononi tunapofika nyumbani ni kweli kbsa kumesababisha kuvunjika kwa maadili,watoto kukua na tabia mbaya kutokana na kukosa muda wa kufundishwa jema na baya na mzazi lakini pia SIMU zimekua chanzo kikubwa cha Chuki kati ya jamiii jambo ambalo kama watu tutapunguza matumizi makubwa ya simu na uhakika JAMII zetu zitarudi ktk mstari.

Mimi mtu akiniuliza leo nini kinaharibu Tabia na maadili ya watu ktk ulimwengu wa LEO ntamjibu ni UWEPO WA SIMU DUNIANI HASA HIZI SMARTPHONE..Tukipunguza matumizi ya simu nina uhakika vitu vingi sana vitakua sawa ktk maisha yetu hapa DUNIANI..
 
Kwangu naona afanye yoote ila siyo kuweka flight mode!!

Siku hizi ukiona mtoto anakufata unampa simu acheze game!

Binafsi naona maisha yangu yameathiriwa mno na simu
Ni muda wa kubadilika sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
simu haijakuathiri wewe tu..ni wengi sana panda dala dala alafu angalia wangapi wapo na simu mikononi? Yani watu wanakaa na simu mda wote wanasubiri kupigiwa,msg ziingie wajibu Hamna anaetaka kukuta mcd call.

Mtu anaweza sikia simu ya mtu imeita akajua kbsa sio yake ila Akaingiza mkono kuangalia yake imeita au haijaita

Mi nadhani watu tubadilike kama mimi simu yangu saivi muda wote iko silent sijaweka hata vibration..Sitaki kbsa kuishika shika naishika muda ninaotaka mimi tuu Nimejiwekea ntashika simu Asubuhi Mchana Jioni MARA 3 TU..Tofauti na hapo labda niwe na emergency.
 
Mkuu,

Una mfano halisi wa matatizo ya kifamilia (haswa kwa wazazi dhidi ya watoto) ambao unao na unaweza ‘share’ nasi kwa manufaa ya wengi?

Asante kwa hoja zako, zote naunga mkono.

Ni mada nzuri.
simu imekuwa ni janga na si baraka tena.
1. Imeingiza familia nyingi kwenye matatizo.
2. wanafunzi kuto zingatia masomo.
3. wafanyakazi kutokuwa makini na kutilia maanani kazi wanazofanya.
4. watu wengi kuzitumia kusambaza habari zisizo za kweli.
5. zimetumika kuangalia picha chafu kwa watu wa rika zote.
6. inaathiri macho na masikio ya vijana wengi, kwani muda mwingi hutumia kutazama au kusikiliza simu.
7. Imetufanya watumwa, kila dakika LAZIMA tuiguse. hatuwezi kuiacha nyumbani asubuhi na kuikuta jioni.
n.k.
Tunahitaji hekima kutoka juu ili kutatua hili.
 
Nafurahi Mkuu, kuwa na wewe umeona ni tatizo pia na linastahili kuwekewa uzito wa pekee kabisa.

Huo mfano umetoa, ni mzuri sana kwa kuonyesha ni vipi tumewa watumwa na kuongozwa na simu badala ya sisi kuiongoza. Shukrani

Ni janga hili uzuri matokeo hasi tumeanza kuyaona mapema. Tukiacha simu zitusaidie kwenye makuzi na malezi ya vijana wetu, tutavuna tulichopanda.

Wakati mwengine unaweza pata mgeni nyumbani hata hamjasalimiana vizuri anauliza una charger ya simu "Z" au umeme upo? Nataka nichajishe simu yangu..

Nakaa na kutafakari huo muda wa ziada ambao tunakaa na kuupoteza kwenye hizi simu zetu pendwa "simu janja" tumeutoa wapi?.
 
Mkuu,

Hongera. Inawezekana kweli umefaulu kufanya hivyo (kutowaruhusu kushika simu). Lakini je, umefaulu kuweka simu pembeni na kuwapa wanao muda wako badala ya kuacha muda wote wakiopumbazwa na Cartoon?

Ni kujitune simu isikuharibie mahusiano yako..mm wanangu hawagusi kbs simu yangu...wanapambana na katuni kwa tv...!

Mwe Mungu atusaidie kwakweli
 
Mkuu,

Asante kwa mchango wako. Kwa wale ambao tayari ni mateja na kubadilika ni changamoto, una kitu unaweza kushauri ili kuweka wepesi kuachana na tabia hiyo?

Ndio mana nasemaga kama kwa mwanaume/mwanamke mwenye FAMILIA kama inatakiwa mkubaliane kwamba ni lazima kuwe na simu ya MEZANI nymbani ambayo ndio itatumika Pindi mama/baba anaporudi nyumbani Ni sheria sio OMBI tukirudi nyumbani wote Tuzime simu zetu au tuweke Flight mode..kwa mwenye Shida na mawasiliano aende kutumia simu ya MEZANI apige.

Kutumia simu zetu za mkononi tunapofika nyumbani ni kweli kbsa kumesababisha kuvunjika kwa maadili,watoto kukua na tabia mbaya kutokana na kukosa muda wa kufundishwa jema na baya na mzazi lakini pia SIMU zimekua chanzo kikubwa cha Chuki kati ya jamiii jambo ambalo kama watu tutapunguza matumizi makubwa ya simu na uhakika JAMII zetu zitarudi ktk mstari.

Mimi mtu akiniuliza leo nini kinaharibu Tabia na maadili ya watu ktk ulimwengu wa LEO ntamjibu ni UWEPO WA SIMU DUNIANI HASA HIZI SMARTPHONE..Tukipunguza matumizi ya simu nina uhakika vitu vingi sana vitakua sawa ktk maisha yetu hapa DUNIANI..
 
Mkuu,

Hongera. Inawezekana kweli umefaulu kufanya hivyo (kutowaruhusu kushika simu). Lakini je, umefaulu kuweka simu pembeni na kuwapa wanao muda wako badala ya kuacha muda wote wakiopumbazwa na Cartoon?

Kwakweli najitahid mno mno...km ni percent basi 70% hv....nipo nao karibu sana...!
 
Back
Top Bottom