Simu za kisasa/Smart Phones zitasababisha baadhi ya vitu kutoweka huko tuendapo

deejaywillzz

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
637
224
Simu za kisasa zinakuja na functionality nyingi kiasi cha kwamba kuna baadhi ya vitu vitatoweka kabisa huko tuendapo. Kwa mfano

Redio, Tochi, Calculator, Kamera, cd player, marafiki wa ukweli (Sio wa facebook), matangazo ya redioni na televisheni, Saa za mononi, barua, na vingine vingi unaweza ukaongezea kwenye list

Ooh bila kusahau smart phone imetowesha peace of mind... PEOPLE ARE GETTING MENTAL, PHONES ARE GETTING SMART
 
Hata games siku hizi ziko kwenye simu..... watoto wetu hawatacheza tena kombolela au mchezo wa kibaba baba na kimama mama...kujipikilisha
 
Ooh bila kusahau smart phone imetowesha peace of mind... PEOPLE ARE GETTING MENTAL, PHONES ARE GETTING SMART


Maneno yako yana ukweli sana - hasa hapa, na hasa ukizingatia vijana wengi kwa sasa wanatumia smartphones na wamewekeza maisha yao huko zaidi (mitandaoni).
 
pia upande wale wasomaji wa vitabu sasa husumbuki kupekua kurasa nyingi za vitabu vikubwa badala yake unabofya tu.mfan0 kuna mwandishi maarufu wa vitabu vya dini moja maarufu aitwaye ellen g white aliandika vitabu vingi sana. ili upate copy zake zote ilikuwa inakugharimu pesa nyingi sana lakini sasa vitabu vyake vyoooote utavipata playstore tena bureee.smartphone raha sana
 
Bila kusahau mapishi tunajifunzia humuhumu kwenye smart phone zetu, unagugo tuu upendacho, hata kuoga unagugo tuu, I love u smart phone
 
Bila kusahau kununua magazeti (hardcopy ) nilikuwa muumini sana wa kununua magazeti sasa baada ya kupata smartphone biashara hiyo ilikoma
 
Nahisi zinaelekea kusababisha na magonjwa mengi ya akiri na kansa ukiachilia mbali kuwaharibu wanaume kukosa nguvu za kiume kwa kuwa obssessed sana na porn videos
 
Back
Top Bottom