Simu yangu moja tu ikasababisha nyumba nzima tuwekwe kizuizini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,274
Mnamo tarehe Machi,15, msafiri mmoja aliiingia Tanzania majira ya saa kumi jioni.
Msafiri huyo ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, ambaye aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda.

Baadaye ikathibitishwa kuwa msafiri huyo alikuwa ni mgonjwa wa kwanza wa corona Covid-19

Basi baada ya siku kadhaa serikali ikatangaza ukiona una dalili za Covid-19 basi piga simu namba 112.

Siku kadhaa mbele akaja baba yetu mkubwa kutoka Aberdeen Scotland. Naye tangu amefika analalamika kichwa, mafua, kukosa pumzi, viungo kuuma nk

Basi tangazo likawa linapita mara kwa mara kwenye TV kuwa tukiona dalili hizo tuwajulishe serikali.

Basi baba mkubwa akaniomba niwajulishe serikali. Nikapiga 112, nikaanza kuulizwa maswali mengi, nikayajibu kadiri ya uwezo wangu.

Wakaniuliza location ya tulipo. Rangi ya nyumba, mjengo wa aina gani, rangi ya pal, inatazamana na nini, imepakana na nini? Yaani walitaka Crystal clear picture ya nyumba yetu.

Basi baada ya dakika kama ishirini tu nyumba yetu ilikuwa imezingirwa na mapolisi, madaktari, na watu wengine wengi wakiwa kwenye nguo kama za kwendea kwenye anga za mbali.

Walikuja wakiwa na Land Cruiser 3 nyeupe zenye msalaba wa kijani na moja lenye msalaba mwekundu, Land Cruiser 2 za Polisi na 110 Land Rover moja. Hakika ujio wao ulikuwa na utisho wa hali ya juu.


Wakatupima nyumba nzima, wakamchukua baba mkubwa na kutuacha sisi wengine tukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Polisi walitufungia na makufuli yao kwa siku tatu wao wakabaki nje wakitulinda.

Hawakujali mates ya watu tuliopo ndani, majirani, ndugu, jamaa na marafiki hawajuruhusiwa kabisa kuikaribia nyumba yetu.

Polisi walileta unga na maharage kilo chache tu.

Baada ya siku kadhaa walipojiridhisha kuwa hamna mwenye dalili mwingine kuaakatuachia huru na kuondoa ulinzi wao.

Kwa kweli Covid-19 ya kwanza ilikuja na taharuki kubwa. Pongezi kwa john pombe magufuli kwa kuweza kui control ile taharuki. Tungekufa kwa shida na tabu za maisha.
 
Kilichowatokea hapo kwenu kimetokea familia nyingi kwenye nchi za watu huko. Covid 19 kwa kweli ilileta taharuki kubwa mno.

Mpaka leo sijutii kitendo cha JPM kuidhibiti hofu iliyotaka kujipa nafasi hapa Tz.

Pia sijutii hatua za SSH za kuzuia maambukizi mapya kwa kuhakikisha wenye mazingira hatarishi wanachanjwa.
 
Hapa sina amani kbs..
Kile kipindi sisi watu wa utalii tulipitia kipindi kigumu sana.sitashau.
Sasa naona hali ile inataka kujirudia.

Eeehh mola wetu tupishe na hiki kikombe
 
Mungu atulinde
Hapa sina amani kbs..
Kile kipindi sisi watu wa utalii tulipitia kipindi kigumu sana.sitashau.
Sasa naona hali ile inataka kujirudia.

Eeehh mola wetu tupishe na hiki kikombe
 
Hatari nipo natengeneza maswali ya focus group discussion sijui itakuwaje na awamu hii ya kovidii!!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom