Simu yangu inapata moto

Linamo

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
9,976
24,488
Habari JF store natumia Huawei y 300 tatizo linakuja inapata sana moto napoiweka kwenye charge au pale napoitumia hasa betri ndo inayopata sana moto..Msaada tafadhali.
 
battery inaelekea kufa kabisa(expire),kwa usalama wa cm yako toa hilo battery mapema kabla haijaleta madhara makubwa.Kanunue battery mpya
 
Jaribu kuiweka kwenye deep freezer tuone kama itaendelea kupata moto.
Ikiendelea ripoti haraka kwa mtaalamu wa simu, anayetibu simu za aina zote kwa kutumia tindikali
 
Ila betri nimeinunua tarehe 15 mwezi uliopita mlimani city...ina mwezi tu....
 
Jaribu kuiweka kwenye deep freezer tuone kama itaendelea kupata moto.
Ikiendelea ripoti haraka kwa mtaalamu wa simu, anayetibu simu za aina zote kwa kutumia tindikali

Kama huna ushauri ni bora ukanyamaza.
 
Jaribu kuiweka kwenye deep freezer tuone kama itaendelea kupata moto.
Ikiendelea ripoti haraka kwa mtaalamu wa simu, anayetibu simu za aina zote kwa kutumia tindikali

Acha ubwege siyo face book hku unakuwa kama mtoto vile kumbe jitu na midevu yake ya kutosha
 
Habari JF store natumia Huawei y 300 tatizo linakuja inapata sana moto napoiweka kwenye charge au pale napoitumia hasa betri ndo inayopata sana moto..Msaada tafadhali.

Na mm pia natumia aina hiyo ya simu na pia ilikuwa inanitokea kikubwa betri kuchemka ni kuwa iko katika matumizi makubwa ya chaji, si kila application si kila sensor au service au antenna iliyo ndani ya simu yako lazima iwe ON, tumia kimoja at a time mfano wakati unachaji waweza zima GPS, wifi, bluetooth au high brightness hata tethering hotspot, ili upunguze matumizi ya chaji pia mobile data waweza iweka kwa 2G au uizime kabisa kama huna matumizi yake makubwa. Pia kuweka kila application iliyo online bila sababu keep it off. Pia nlicho experience kwa simu zangu nyingi ambazo nshawahi tumia simu ikiwa mpya na betri ikiwa haija zoea mitikasi ya matumizi huwa inachemka sana mpaka unafikia hatua ya kuipooza kuogopa kulipuka, lakini jinsi unavyotumia lazima itazoea. Kuchemka unavyochaji nayo inatokana na matumizi makubwa huku ukichaji so reduce matumizi wakati wa kuchaji haita chemka
 
Me nauliza,hivi kusajili laini napaswa kulipia?????
Leo nimeenda kwa wakala mmoja wa airtel nimempa laini yangu nikamwambia nataka niisajili akanitoza pesa,jamani hivi usajili wa line na pesa???
Nimesita kumpa pesa nikaondoka na laini yangu
 
Hakuna cha bure dunian
 
kuna vitu viwili vinavyoweza kusababisha tatizo hilo kwanza simu yenyewe au betri peke yake, kwa upande wa btri maelezo ni hayo kama walivyokupa waliotangulia kwa upande wa sim ni la kiufundi zaidi inabidi ukamuone mtaalam aliebobea ktk matatizo ya namna hiyo kwani si mafundi wote wana utaalam huo.
 
Hiyo simu haina tatizo la kiufundi ni management tu yatakiwa
 
Huawei y300 ninayo itumia ina tatzo la kutoonesha majina mtu akinipigia yaani no nime i save ila akipiga mtu haioneshi jina.msaada tafadhali.
 
Tatizo ni simu za kichina. Ziko simu za kichina ambazo ni original huwa hazina matatizo yoyote na hizo zenye kuchemsha ni kapu jengine.
 
Simu huwa inapata joto hasa wakati processor nafanya kazi sana na hii huendeshwa na shughuli ambazo unafanya na simu.
Kuna app ambazo huwa zinatumia sana nguvu ya simu kama GPS, mwanga wa flash ya simu, display ya simu.

1. Ili simu yako ipunguze joto angalia kama GPS iko on. Ama iko on weka off. Natumia tu wakati unatumia map (Google map)
2. Pia punguza mwanga wa simu yako au weka auto.
3. Uwe unamtindo wa kuzima na kuwasha simu angalau kila siku mara moja.
4. Wakati wa kucharge simu, izime kabisa, hii huondoa joto la processor na battery.
5. Tumia charger original ya simu siku zote.
 
Me nauliza,hivi kusajili laini napaswa kulipia?????
Leo nimeenda kwa wakala mmoja wa airtel nimempa laini yangu nikamwambia nataka niisajili akanitoza pesa,jamani hivi usajili wa line na pesa???
Nimesita kumpa pesa nikaondoka na laini yangu
Piga customer Care ya airtel watakujibu.
 
Back
Top Bottom