Simu yamchengua Msambaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu yamchengua Msambaa

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by X-PASTER, Nov 24, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Baada ya kutokea msiba huko Lushoto walimtuma ndugu yao mmoja kwenda kuwajulisha ndugu zake waliokuwa nje ya mkoa wa Tanga. Mtani wangu Msambaa aitwae Shemaonge, alikwenda kwenye ofisi za shirika la simu hapo Lushoto. Baada ya kutoa namba aliandikiwa, aliunganishwa na mjomba wake Juma aliyekuwa akiishi Dar es Salaam.

  Baada ya kuunganishwa mambo yalikuwa hivi:

  Juma: Juma hapa, naongea na nani?"
  Shemaonge: Shemaonge, ni Juma?"
  Juma: Ndiyo, shikamoo mjomba."
  Shemaonge: Marahaba, yaani twasikilizana Lushoto na Dashalama?"

  Juma: "Ndiyo mjomba, habari za huko?"

  Shemaonge: "Nakwambia siamini macho yangu, yaani twasikilizana, ama kweli huu ni waya kwa waya."

  Juma: "Mjomba dunia ya teknolojia hii, unashangaa simu tu, mbona kuna mambo mengi ya kushangaza."

  Shemaonge: Haah, si hadithi hii? Sauti yako naisikia vizuri kabisa kama upo sikioni pangu, eeh kweli mzungu mwendawazimu."

  Shemahonge kwa kuishangaa simu alijikuta anamaliza dakika zote alizolipia bila kutoa taarifa ya msiba....
   
Loading...