ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
RAIS Jakaya Kikwete anasema simu yake ya mkononi iko wazi kwa yeyote anayetaka kuwasiliana naye. Namba ambayo wengi tunaifahamu ni 0754 777775.
Akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema amekuwa akiwasiliana na wananchi moja kwa moja kwa simu ya mkononi.
Aliwaambia, "…simu yangu ile ipo wazi muda wote. Watu wananitumia sms (ujumbe mfupi wa simu), wananipigia, wengine wananieleza matatizo yao mbalimbali. Nazungumza nao. Nanyi nawaomba msisite kufanya hivyo."
Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa viongozi hao uliolenga kufahamisha kilichomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi aliyosaini hivi karibuni.
Rais aweza kuwa anajibu simu; na kama alivyosema wakati mwingine hujibu ujumbe aliotumiwa kwa njia ya kupiga badala ya kuandika.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna mwenye uhakika iwapo Kikwete anaitumia simu hiyo kupata taarifa kwa ajili ya umma au ni taarifa binafsi. Hii ni kwa kuwa simu ya rais inashikwa na rais mwenyewe.
Ndiyo maana taarifa zinasema, kila anayetuma ujumbe kwa rais hujibiwa na rais mwenyewe.
Baadhi ya wale ambao wamewasiliana naye na ambao nimehojiana nao, wanasema muda mzuri wa kutuma ujumbe kwa Kikwete; na ili ujibiwe, ni kuanzia saa saba usiku."
CHANZO: Gazeti la MwanaHalisi
Wakati Nyerere alikuwa akitumia muda mwingi kusoma na kuandika vitabu na makala za kisomi baada ya kutumia kichwa kufikiri sana, huko tunakoelekea ni kubaya zaidi kwa kuwa tumennza kupata viongozi wasiotumia hata chembe ya muda kufikiri kisomi juu ya dhamana walizonazo kitaifa, ni kizazi cha kushinda kwenye "online games" na "chatings" za sms.
Ni kizazi kinachotegemea zaidi mawazo ya wengine kuendesha fkrra zao kwa kusikia kupitia vyombo vya habari na udaku.