Simu ya aina gani umeshawahi kuitumia na ukaikubali sana?

Nilitamba na Nokia X2-01 mwaka 2012

Hio simu nakumbuka ilinipatia dem mkali sana toka shinyanga kulee nilipoenda kununua mipunga na mchele

Niliipenda sana hio simu lakin baadae nikaigawa kwa First born nae toka 2013 hajawahi kubadilisha hio simu. Kila nikienda likizo namkuta nayo tu mpaka sasa anayo.

Inaonekana kama blackberry flani.
 
Iphone 4s ni simua mbayo naipendaa kama navyompenda mama ako mdogo. Haya matoleo ya steve Job's ndio matoleo bora kwangu..
 
Simu yangu ya kwanza ilikua Motorola bapa, nilipewa zawadi ya simu pamoja na mpira kutoka kwa beberu mmoja hivi kwa kipindi hicho kijiji kizima mwenye simu kali ni mimi hapo nipo darasa la saba...walimu, wanafunzi wao, Afisa Elimu Kata, Wauguzi katika kituo cha Afya wote walipata habari za simu hii. I was a celebrity...
View attachment 1631960

NB: Mabeberu walishatuzoesha na misaada toka tupo underground. Hii ni vita ya kiuchumi ndugu zangu katika kuelekea dona kantri.
Nlitumia pia n moja yaa sm bora sana ezi hzo kwa bongo imewahi kuuzwa had lak3 naa...
 
miaka ya 1998 nilianza na nokia 8210 halafu baadae sonyericson walitisha baba miaka ya kuanzia 2000 halafu pia miaka ya kuanzia 2010 nikaja kuwakubali sana blackberry ila ndo hivyo kazi ya mungu haina makosa wote wako mbele za haki
 
Nokia kwakweli alikuwa bora sana ni vile dunia inaenda kasi mimi bado nazipenda mpaka leo
Walikuwa vizuri saana. Kuna features ambazo zilikuwa kwenye Symbian 60 enzi hizo, zimechukua miaka kuwa kwenye Android. Mfano ku-install application kwenye SD card.

Bluetooth ya Android kwa Android unaweza search for a device mpaka unachoka, na simu ziko karibu kabisa.
 
Nokia express music, mashine hiyo View attachment 1632149
Hiyo ni toleo la Pili, sasa Toleo la kwanza nilinunu 280,000 posta, kama kulikuwa na simu ilitamba sana kwa siye wapenda music ni hiyo express music alikuwa inakuja na Earphones kali sana aseee , mpaka sasa sijaona simu yenye mdundo kuzid hii kitu japo zaidi ya miaka 10 imepita toka niitumie, nilikuja kumuonga mdada toka zenji asee ahh ahh
 

Attachments

  • _front.jpg
    _front.jpg
    131.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom