Simu - Wabunge Chadema wafanyiwa ujasusi, mtoto wa kigogo CCM ahusika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu - Wabunge Chadema wafanyiwa ujasusi, mtoto wa kigogo CCM ahusika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 21, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
  Frederick Werema
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali

  Wabunge CHADEMA wafanyiwa ujasusi


  • MTOTO WA KIGOGO WA CCM ADAIWA KUTUMIKA
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai kugundua mbinu zilizotumiwa na mtoto wa kigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) za kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge wake kutuma ujumbe wa vitisho kwa mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA, Mabere Marando, alisema mtoto huyo wa kigogo ambaye hakumtaja jina, alinunua mitambo hiyo kutoka nchini Israel.

  Alisema nchini Israeli kuna kampuni mbili alizozitaja kwa majina ya Nice System na Verinty System, ambazo zimefanikiwa kutengeneza mitambo yenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya mtu kwa umbali wa kilometa tano na kwamba moja ya mitambo hiyo ndiyo iliyotumiwa kusambaza ujumbe mfupi wa simu kwa Mwigulu, zikionyesha kuwa zimetoka kwa wabunge wa CHADEMA.


  Aliongeza kuwa mfumo uliotumika kuingilia mawasiliano ya wabunge wa CHADEMA unaitwa
  sms proofing, na kwamba inaweza kutumiwa na idara za kiusalama kwa sababu maalum tu.

  “Tuliwauliza wabunge wetu kama wamefanya suala hilo na wakatuhakikishia kuwa hawahusiki, tukashtuka na kama mshauri wa masuala ya kiusalama wa chama tukaamua kuingia kazini kufuatilia hili, tulichogundua ni kwamba mipango hii iko nyuma ya mtoto wa kigogo wa CCM ni mtaalamu wa mitandao na ana fedha nyingi za kufanyia kazi hii,” alisema Marando.

  Alieleza kuwa jambo la kusikitisha ni taarifa walizozipata kuwa
  mwanasheria mkuu wa serikali Jaji George Werema kuwaagiza watumishi wa ofisi yake kuandaa mashtaka kwa ajili ya tukio hilo la kuwahusisha wabunge wa CHADEMA na meseji hizo badala ya kushughulika na watu walioingilia mawasiliano yao.


  Alisema kwa nafasi yake, Werema kama msimamizi mkuu wa sheria nchini anajua wazi kuwa kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine ni kosa la jinai na mhusika anayefanya hivyo anapaswa kushtakiwa.


  “Kitendo cha Jaji Werema kutoa maagizo ya kuandaa mashtaka kwa wabunge ni kuwasaidia wahalifu; tunachoweza kumuambia ni kwamba taarifa tunazo tutakutana mahakamani kuweka masuala haya wazi,” alisisitiza.


  Alisema CHADEMA haitajishughulisha kulifikisha suala hilo mahakamani bali wanasubiri waitwe ili wakaudhihirishie umma namna viongozi wa CCM na watendaji wengine serikalini wanavyotumia vibaya nafasi zao kuwanyamazisha wapinzani wao kisiasa.
  Alibainisha kuwa serikali ya CCM isidhani kuwafunga mdomo wakosoaji wake wa sasa ni suluhisho la ushindi kwao kwamba harakati za kudai uhuru wa kweli hazikuanza sasa na hazitaishia kwa kuwadhuru watu.

  Wiki iliyopita mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu, alisimama bungeni na kuomba mwongozo wa Spika akidai kuwa amepokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA, akitishiwa kuuawa.   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa naamini wapigania mageuzi wako kila kona, kwani hii siri ya mtoto wa kigogo kupata mtambo wa kijasusi kuingilia mawasiliano ya simu ya wabunge wa CCM anayeweza kutoa siri hiyo ni Umoja wa wanawake Tanzania ambao vigogo na watoto wao hulindwa muda wote kama mboni ya jicho kuona wanachokifanya.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kichwa kazi yake sio kuota nywele tu,
   
 4. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  vipi ndiyo unaamka saa hizi?
   
 5. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  hakika MUNGU yu pamoja nasi....Viva chadema,Makamanda tupo nyuma yenu kwa Maombi na Mungu atawalinda daima...:amen:
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi Marais wengine waliopita akina Mwalimu Nyerere, Ali Mwinyi na Benjamin Mkapa hawakuwa na watoto?
  Ni rais huyu tuu ndo mwenye mtoto?
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuishi kimjinimjini ndo familia zilivyotofautiana, nadhani umenipata.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Unalo mwaka huu, mgolo utakushuka!!!
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimekupata vizuri sana mkuu. Wanaishi kiujanja ujanja sana.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni deal iliyosukwa kwa ustaadi mkubwa ikiwahusisha wengi, ndio maana unaona Mwanasheria Mkuu wa Serikali analivalia njuga kudai kutaka kuwashtaki wabunge wa Chadema juu ya hilo bila kufanyia uchunguzi. Kuna kitu kinachoendelea nyuma ya pazia.

  Ukifuatilia mwenendo bungeni wiki hii Mwanasheria Mkuu wa serikali alivyokuwa na kauli za kupinga na kuwatukana wapinzani na kuwaona vichwa vyao vimeota nywele tu kama akina Lisu bila bongo kufanya kazi, hiyo ndiyo lugha anayoongea bila aibu mtu mkubwa serikalini na ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa serikali. Nini zaidi kuonyesha?
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Huo mdomo wako mnene kama pindo la gunia umeshastukiwa ulikuwa unafikiri ni ujanja kuspoof SMS utakoma mwaka huu ubunge hupati tena
   
 12. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Everyone is a genius, but not by judging ability of a fish to climb a tree!
   
 13. m

  mswald Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hawa wanaweweseka tu, nadhani ni kutafuta agenda.Si wangedandia ya MV SKAGIT na wanakoelekea watakosa imani hata na wake zao, waume zao na familia zao.
  CCM imetuchosha sana sisi wananchi, imeshindwa kuikomboa nchi kiuchumi kwa kutumia rasilimali na stratergic geographical location mungu aliotupa LKN sioni chama makini chakututoa hapa tulipo.
  I once thought CHADEMA was one bt watu hawana imani na taasisi yoyote hapa nchini, polisi, usalama wa taifa, jeshi, TAKUKURU etc etc etc sasa sijui wataunda kila kila kitu upya, tuwape muda gani kufanya hayo.
  Nahofia siku moja watakosa imani na WATANZANIA WOTE, watatufunga wote ili waanze taifa jipya na koo zao!!!!
   
 14. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  JK na Wateule wake waliojaliwa uwezo wa kufikiri kwa kutumia Masabuli!!!! Kweli viongozi wa serikari wengi wao ni viraza. Wrong postions are occupied with wrong people. Werema hauna kitu na mwisho wako ipo siku itafika kwa maana Mungu haachi haki ilaliwe na majuto yatakuwa juu yako kama tunavyomsubilia Chenge, adhabu yunu ni kupiga risasi tu
   
 15. Kenneth Mwazemb

  Kenneth Mwazemb Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndibalema hujui mwana umleavyo ndivyo akuavyo?
   
 16. PRINTABLUE

  PRINTABLUE Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuambie hela ulofungulia akaunti vijana 32 wa kiomboi ulitoa wapi na kwa nini unawatumia kwa maslahi ya kuleta fujo? mbinu zako zote tunazo ndo maana unaogopa kuja mjini unaishia kyengege katani kwako njoo huku mjini kiomboi upige mkutano uone nguvu ya umma ilivyo
   
 17. payroll

  payroll Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo anakunywa nini hiyo? isije akawa anakunywa gongo bungeni maana ndio kinywaji cha kijiji anakotoka huko kwa kina mura
   
 18. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ninachojua bila hofu yoyote ni kwamba Mwiguluu na kakikosi fulani cha wanaojidanganya kwamba wao ni wataalamu wa CCM wamebuni mbinu ya kuidhibiti CHADEMA kwa kutekeleza propaganda kadhaa za kuwafanya wananchi waanze kukosa imani na chama hicho kinachokua kwa kasi sana.

  bahati mbaya sana kwa CCM na mfumo unaobuni na kutengeneza propaganda hizo hawana ujuzi wa propaganda hata kidogo. Wao wanafanya majungu halafu wanafikiri kwamba hayo yanaqualify kuwa propaganda.

  Thank God that their scuffing is always turning against them. However I suffer inside that my country is without propaganda personnel.
   
 19. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Tunaelekea kushikana Mashati Mitaani tuendako itafika mtu anajifungia na mageti sita sita nyumbani kwake kwani wananchi wakiona Ukombozi unazuiwa watashika hatamu wenyewe ndipo pale itafika wakati wa kusaga meno
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Nadhani hii nchi inaongozwa na Polisikwani staili hii ni ya kipolisi zaidi ile ya kubambikiza mtu bangi kisa kakubishia au kakunyima Rushwa sasa tujue tumekwisha... Hivi ile Sheria ya kuruhusu maduka ya Bunduki iliishia wapi ... i need Seven Gun for my Protection Hata nikiona unazuia Maendeleo Bungeni niweze kukushoot sababu ni moja wapo ya Protection ya Maisha Yangu na Yetu Sote
   
Loading...