Simu na Mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu na Mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Aunty Lao, Jan 21, 2009.

 1. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Za leo wa ndugu, naomba kuuliza je ni fanye nini na tabia ya mume wangu kuhusu simu(mobile phone) Kwa kweli ni jambo lililokuwa likinisumbua kwa mda mrefu sana. My hubby anatabia ya kutopokea simu sometimes, yn cmu yake inaweza kuuita kwa mda mrefu bila yeye kupokea. Then, hasemi ni nani anakaa kimya tuu! Ila kwa investigations zangu mara nyingi huwa ni rafiki zake wa kiume. Je nivema kuwa namuuliza kuwa ni nani au je ni vipi watu huu behave wanapoishi wawili katika maswala ya simu. Maana sipendi kukwazika na sipendi kumkwaza pia.
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kwakuwa wewe mwenyewe umeona maranyingi ni rafiki zake wanapiga na hapokei, hapo kunaweza kuwa na mambo kadhaa kama:

  1) Kawaahidi rafiki zake wataonana baadae, unajua tena washkaji hivyo akiwa
  nyumbani anaghairi kutoka na kutopokea simu.
  2) Inawezekana anadaiwa, maana watu wanaodai wanajua kweli kukumbushia
  madeni yao.
  3) Labda ni mwanamke anapiga ila amehifadhi(save) namba ya simu kwa
  kutumia jina la rafiki yake/zake unaowajua.

  Mweleze wazi kuwa iyo hali inakukera halafu uone atafanyaje pia mshauri kama hataki kupokea simu akiwa nyumbani atoe sauti.
  Ni vizuri kila mtu akawa hana tabia ya kugusa simu ya mwenza wake, maana mara nyingi utahangaika kupekua na kupata presha za bure. Pia simu ya mkononi ni ya mtu binafsi siyo watu.
  Hamna kitu kizuri kama wanandoa/wapenzi kutokupekua vilivyoandikwa ndani ya simu ya mwenza wako JAPO ni gumu sana kutekeleza hili.
   
 3. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Asante sana ndugu, yani ushauri wako huo wakutoa sauti nilikuwa sina kabisa. Na kuhusu no. ya demu kusave kama ni jamaa yake, hapo uhakika ni nnao maana hata mimi kabla ya kuolewa (enzi za usichana wangu) nakumbuka niliwahi kumfanyia jamaa mmoja hivyo maana hakuwa na muelekeo wa mapenzi na mimi na akawa na wivu. So that trick is in my finger tips. Stay blessed.
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kila la kheri. Kuongea ni vizuri unapokuwa na dukuduku ila kama kuna hali ya kutoelewa au ugomvi kujitokeza wakati unamgusia hilo, nyamaza kimya ili kuepusha shari zaidi.

  Mimi mwenyewe huo mtindo wa ku-save jina tofauti na jinsia ulinitokea, mwanamke kaandikwa 'uncle fulani' ambaye namjua nikawa sina wasiwasi ila kuna siku kushika simu na kuona hizo message za huyo aitwaye uncle na mpenzi wangu nilichanganyikiwa sana. Iliniuma nikasema simu ya watu basi.

  Lakini ndizo changamoto tulizonazo kwenye dimbwi la mapenzi.

  Cheerz!
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...(try)IGNORE hizo simu zake, kama ushauri mwambie awe ana mute simu yake. Hizi mobile fone sumu sana kwenye maisha ya ndoa, UKIZIENDEKEZA!
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Duh! Am speechless!
   
 7. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Aunty Lao; Hawa wababa ukiwafuatilia sana unaharibu afya yako. Ikibidi na wewe anza kuwa busy na simu yako hasa jioni na usiku, mwambie hata shoga yako awe anakupigia usiku wa manane halafu pokea simu na ukimbilie bafuni kuongelea. Ikiwezekana anza kutoka siku za week end peke yako au na shoga yako (toka mchana) umwonyeshe kwamba huna time naye. Au pale anarudi nyumbani kama ni jioni basi akukute umeulamba na unamwambia unadharula kidogo unatoka, Uone naye kama roho haitamdunda. Hiyo inaweza kumfanya aanze kuwa karibu saana nawewe (jaribu tu). Hakuna dawa mbadala au solution katika haya tunajaribu tu. Nakutakia kila la heri
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Matamizi ya simu ni tricky . Ni kama messenger tu anavyoweza kupeleka barua yako binafsi nyumbani kwako , na mwenzi wako akaisoma.
  Kila mtu kwa mfano ,ana namba ya simu ambayo imekaa kichwani sana.Pengine shauri unaipiga mara nyingi sana au unatuma msg mara nyingi sana kiasi vidole vimezoea .

  Wakati fulani unaweza kutuma msg kwa namaba hiyo bila kujijua halafu unakumbauka kuwa umekosea wakati imeshaenda . Au unaipiga kumbe ulitaka kumpigia mtu mwingine. Hii inawezekana hasa kama uko bussy namna fulani.

  Ikatokea ukamtumia msg mpenzi wako asubuhi like Darling , how are you this morning ? then ukakosea ikaenda kwa mkeo au mumeo ambaye ndio kwanza mmeachana asubuhi hiyo hiyo dakika tatu zilizopita.

  Hiyo inakuwa messenger kaleta balaa. So watch out enyi cheaters.
   
 9. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hizi simu ni kama shetani hivi,, you will be tempted to scan thro your partners phone just to be sure or kama vijitabia vyake vinakupelekea kumshuku... ukikutana na vijmessage vya kimapenzi hivi baaaaaaasi.. heri tu ujitahidi jikeep busy....achana na simu za watu for your sanity's sake... utajitia vikuli vya roho bure.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...tena ni kaugonjwa kabaya sana hako,...ACHA!

  ...usipoacha itakupelekea kuanza kunusa chupi zake kabla hujazifua!

  ...ama, kukesha usiku kumsubiria aote na kumtaja 'mgombea mwenza!'

  ...kaugonjwa hako katakupelekea kukereka vipindi vya Televisheni anavyoangalia, au jinsi anavyozidi unadhifu, au anavyotembea kwa madaha, hata anavyoangalia warembo wengine...ACHA!

  ...hako ka-ugonjwa (kitaalamu) kanabeba symptoms zote za Obsessive-Compulsive Disorder!

  endelea kujielimisha; Obsessive-compulsive disorder - Wikipedia, the free encyclopedia
  soma pia; Attention-deficit hyperactivity disorder - Wikipedia, the free encyclopedia
   
 11. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Masuala ya kujibu simu yanaleta maswali yake. Kwa mfano kama mko na mwenzi wako unakuta simu inaita halafu anakuacha anaenda mbali kidogo kuongea ila ukiwa mdaku ndio matatizo yanapoanzia. Ni vyema ukajifanya huna habari kama alikuwa anaongea na mtu usipate pressure bure. Akipenda atakueleza mwenyewe. Jaribu kutojihusisha sana na simu ya mwenzi wako.
   
 12. C

  Camfu Member

  #12
  Jan 22, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu yangu, hali hiyo kwangu tayariinafahamiak kwani nami pia some times huwa sipokei simu...lakini kwangu mara nyingi inatokea kama na fahamu issue ni nini na sina hoja za kuwwwweza kumlidhisha mtu, so kwa upande wako nadhani kasumba hiyo ni ya kawa kwa wanaume, wanaphichology wanasemaga kuwa you ladies are more smart na ni wastaarabu zaidi kuliko sisi wanaume, ndio maana inakukela. Namshukuru Mungu kuwa tayari ni mume wako lakini ingekuwa washikaji tu moja anaweza kudhani kuwa jamaa anamshikaji mwingine, so ningekusihi uongee naye tu na kumwambia kuwa ustaarabu wa kupokea simu ni kitu kizuri kwa marafiki au wapenzi. Atakuelewa tu dear, ikiongea naye pole pole
   
 13. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante shosti, yawezekana na mimi nilijibwetesha sana kwa kuwa ndoa bado changa mwaka na nusu tuu na kuwa mtiifu ki hivyo mpaka kumpelekea na yeye kujisahau. Huku nilipo norway kwa kweli bado nimgeni sijapata mashoga bado.
   
 14. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa vile ameonyesha tabia yake ya simu kuwa hiyo kwa maana hiyo na mimi nifanye hivyo pia! au hapa inakuwaje sasa. Maana kwa upande wangu sijawahi kumuonyesha nyendo hizo hata siku moja.
   
 15. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa mtindo huu kweli kuna uaminifu hapa! maana matendo yako ndio yatanipelekea mimi kujenga uaminifu kwako kumbuka hili pia. au sio my dear unasemaje.
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hao mashoga ndio waogope sana tu! Rafiki wa kweli ni yule atayekwambia 'usinyimwe usingizi kwa "kelele za mlango" ' kwani mumeo unaye hapo ndani- nyumbani!
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Bora uwe mbogo(mkali) na mashoga zako kuhusu mumeo.

  mashoga zako ni rafiki zako tu,wasizoee 'shemeji' wala nini...marafiki wabaya sana!

  ukiwapata mashoga huko uwe mwangalifu!
   
 18. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbuu ndugu yangu, asante kwa ushauri. Ila methali yako au niseme msemo wako sijui, wala sijauelewa kakangu. Hebu nifafanulie mweee!
   
 19. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Shosti, sasa nikiwa mbogo ntawapata na hao mashoga! Cha msingi mimi naona ni heri niendelee kuwa kivyangu vyangu au nitafute mashoga walioko kwenye ndoa zao pia. Au sio! Maana thio thiri mimi toka nyumbani sipendi mashoga na nikiwa naye si shey naye mambo yangu ya ndani. Au vipi shosti belinda!
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Maana yake ni kwamba usihangaike sana wala usisumbuliwe na hizo simu maadamu una mumeo ndani hayo mengine just ignore
   
Loading...