Simu kuisha chaji wakati inachajiwa

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
11,008
16,418
Wadau... Hivi inakuaje simu kuisha chaji wakati inachajiwa? Yaani simu mfano ilikuwa 20% baada ya kujaa inapungua... Tatizo hili nimeliona kwa simu ya bi mkubwa.. Anatumia Tecno M6..
 
Iko hivi simu kama inachanjiwa huku inatumika ina maana power inayo be supplied kwa device haitoshi kwa sababu una run task kibao Angalia output ya charge yako kama ni ndogo basi make sure unapochaji unazima simu ili power inayoingia isitumike badala yake ijaze battery
 
Kwahiyo solution hapa ni nini?
 
Aisee, ni kweli Huawei yangu ilianza hiyo tabia then siku moja ikazima kabisa huku ikiwa connected kwenye charge na haikuwaka tena

Inaonekana hili tatizo ni kubwa.. Ngoja tusubiri wataalamu waje tupate msaada..
 
Hata mimi nilikuwa na shida hio kwenye ki Samsung changu. Nikatupa kando nikaenda tecno L6. Hii simu watu hawaijui iko vizuri kiasi chake.
 
Wadau... Hivi inakuaje simu kuisha chaji wakati inachajiwa? Yaani simu mfano ilikuwa 20% baada ya kujaa inapungua... Tatizo hili nimeliona kwa simu ya bi mkubwa.. Anatumia Tecno M6..

chager hiyo badilisha ishakufa
 
Nilijua tuu lazima itakuwa tecno hiyo. Tupa hiyo simu nunua Startimes Mobile Phones

Startimes si king'amuzi, hizo simu kama zipo ni kabila moja na Tecno

Simu ni iPhone, Lg, samsung, htc na sony. Zingine hizo mmh unanunua at ur own risk
 
Uneme wa Tanesco unazingua.

Hapana kiongozi tatizo sio umeme wala nini ni hali tu ya chaja kuwa ndogo then una run task kibao kwa hio phone tanesco minimum ni 180V kwa maeneo ya low voltage sasa chaji yako inatoa 5V yani ata umeme usiwashe bulb na appliances zingine Lazima utachaji simu kwa sababu ina consume power ndogo kweli
 
Hilo tatizo lipo; nina sumsung note 3 imepata shida hiyo: sijajua sorce ni nini nataka nirudi kwa hawa sumsung walioniuzia aisee
 
Back
Top Bottom