samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Hali ya ulinzi na usalama dhidi ya rais kikwete imezidi kuimarishwa siku hadi siku. Pamoja na kuwepo kwa mitambo ya kukagua watu waliokua wakiingia kwenye ukumbi wa chimwaga siku ya uzinduzi na siku ya mahafali ya kwanza. Jana siku ya mahafali ya kwanza ulinzi na usalama viliimarishwa mara dufu ambapo tangazo kutoka usalama wa taifa lilitolewa kuwataka watu WAZIME simu na kamera zao mara tu wakubwa wa high table watakapoingia ukumbini na kwamba wangeruhusiwa kupiga picha na kuwasha simu zao mara wakubwa hao watakapoondoka. Waandishi waliruhusiwa kuendelea na shughuli zao. Taarifa ziliendelea kusema kama usalama wangetumia mitambo yao kumnasa mtu ambaye angekiuka agizo hilo wange m deal. Pamoja na tangazo hilo wengi hawakuzima simu zao lakini picha zilikua zikipigwa kwa kuibia.. NDO ULINZI WENYEWE AU!!