Simu iliyopigwa na Prof. Lipumba yawakimbiza Polisi

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
SIMU iliyopigwa na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ‘iliwapoza’ Jeshi la Polisi lililofika kuzuia mkutano huo leo tarehe 12 Machi 2019 na hatimaye kuondoka.

Baada ya kuwepo kwa vuta nikuvute kati ya jeshi hilo na baadhi ya viongozi wa CUF, Prof. Lipumba alitoa simu na kupiga mahali mazungumzo ambayo yalidumu kwa muda mchache.

Baada ya simu hiyo, msimamo wa polisi ulibadilika ambapo magari yaliyokua yamebeba polisi pamoja na moja la maji ya washawasha yaliondoka eneo la tukio huku mkutano ukiendelea.

Hata Prof. Lipumba alipoulizwa alikuwa akiongea na nani, alijibu “nilikuwa naongea na jamaa zangu, mimi ni mtu mzito siwezi kukwambia.”

Awali; Jeshi hilo lilifika katika ukumbi wa mkutano ofisini hapo Buguruni jijini Dar es Salaam na kuamuru kikao hicho kisitishwe kwa kuwa, kuna zuio la mahakama.

Hata hivyo, wajumbe wa mkutano huo walianza kuweka mgoma kutii agizo hilo kwa madai kwamba, hakuna taarifa yoyote ya maandishi iliyofikishwa kwao ikielekeza kuzuia mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano huo kutoka maeneo malimbali nchini walifika kwenye ofisi hiyo kuhudhuria Mkutano Mkuu uliopangwa kuanza leo tarehe 12-15 Machi 2019 pamoja na malengo mengine pia kuchagua viongozi wapya.
Kwenye mkutano huo, Sisty Nyahoza, Naibu Msajili aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba, unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF na kwamba, ndio maana amefika kuwakilisha Ofisi ya Msajili.

Kwenye mkutano huo Nyahoza amewapongeza CUF Lipumba kwa kufanikiwa kusajili Bodi ya Wadhamini pamoja na kuhimili mikiki ya mahakama kwa dhamira ya kulinda chama hicho.

Kufika kwa Jeshi la Polisi kwenye viwanja vya mkutano huo kulibadili taswira ya eneo hilo huku wajumbe wakionekana kukasirishwa na dalili za kutaka kuvuruga mkutano huo.

Prof. Lipumba na wanaomtii walipanga kufanya mkutano huo kwa siku nne mfululizo. Hata hivyo, baada ya wajumbe kuwasili leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mkutano, zoezi la usajili na uhakiki lilianza kutekelezwa.

Wakati zoezi la uhakiki wa wajumbe wa mkutano huo likiendelea, ghafla polisi walifika eneo la mkutano huo na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa CUF.

Hata hivyo, polisi walimtaka Prof. Lipumba kuvunja mkutano huo kwa kuwa, kuna zuio la mahakama. Polisi walianza kuzungumza na viongozi wengine wa chama hicho ikiwa ni pamoja na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya na Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.

Pamoja na taarifa hiyo viongozi hao waliendelea kusema kuwa, watafanya mkutano huo kwa kuwa hawajapokea nakala yoyote inayozuia mkutano huo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, polisi walikuwa na difenda mbili zikiwa na askari polisi na gari moja ya maji ya kuwasha yalikuwa yameegesha nje ya maeneo hayo.

Kelele za chini kwa chini zilianza kusikika “hata kama umekuja na zuio la mahakama sisi hatulipokei kwa sababu wewe huna mamlaka ya kulileta na hapa hatuondoki mkitaka mtuue wote.

Ndipo Prof. Lipumba alitoka na kuanza kufanya mazungumzo na polisi na baadaye kupiga simu ambapo ilisababisha keshi hilo kuondoka na kuacha mkutano ukiendelea.

Simu ya Prof. Lipumba ‘yakimbiza polisi’
 
Huyu lipumba anafanya dhambi mbaya sana kwa WATANZANIA.
Anayafanya hayo huku viongozi wake wa dini wanamuangali tu!
Anaitwa alhaji Ibrahim lipumba.
Ivi huko wanakohidi kunabarisha nini toka kwenye tabia za mtu? Maana tulitegemea mtu alienda kuhiji,anasimama kwenye ukweli sasa lipumba vipi? Mungu mtazame lipumba na viongozi wote wanaofanana naye na kuwahukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza jiuliza kwanini tumeshindwa kufikia malengo kama nchi tumebaki kuhangaika na maneno? jibu tumeamua kuwekeza kwenye ujinga kwa nguvu zetu zote.
Serikali yetu ingeamua kuwekeza kwenye mambo ya maana tungefika mbali, sasa ona ujinga wa kina Lipumba unavyopewa kipaumbele kuliko hata vile viwanda tulivyoahidi kwa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMU iliyopigwa na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ‘iliwapoza’ Jeshi la Polisi lililofika kuzuia mkutano huo leo tarehe 12 Machi 2019 na hatimaye kuondoka.

Baada ya kuwepo kwa vuta nikuvute kati ya jeshi hilo na baadhi ya viongozi wa CUF, Prof. Lipumba alitoa simu na kupiga mahali mazungumzo ambayo yalidumu kwa muda mchache.

Baada ya simu hiyo, msimamo wa polisi ulibadilika ambapo magari yaliyokua yamebeba polisi pamoja na moja la maji ya washawasha yaliondoka eneo la tukio huku mkutano ukiendelea.

Hata Prof. Lipumba alipoulizwa alikuwa akiongea na nani, alijibu “nilikuwa naongea na jamaa zangu, mimi ni mtu mzito siwezi kukwambia.”

Awali; Jeshi hilo lilifika katika ukumbi wa mkutano ofisini hapo Buguruni jijini Dar es Salaam na kuamuru kikao hicho kisitishwe kwa kuwa, kuna zuio la mahakama.

Hata hivyo, wajumbe wa mkutano huo walianza kuweka mgoma kutii agizo hilo kwa madai kwamba, hakuna taarifa yoyote ya maandishi iliyofikishwa kwao ikielekeza kuzuia mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano huo kutoka maeneo malimbali nchini walifika kwenye ofisi hiyo kuhudhuria Mkutano Mkuu uliopangwa kuanza leo tarehe 12-15 Machi 2019 pamoja na malengo mengine pia kuchagua viongozi wapya.
Kwenye mkutano huo, Sisty Nyahoza, Naibu Msajili aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba, unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF na kwamba, ndio maana amefika kuwakilisha Ofisi ya Msajili.

Kwenye mkutano huo Nyahoza amewapongeza CUF Lipumba kwa kufanikiwa kusajili Bodi ya Wadhamini pamoja na kuhimili mikiki ya mahakama kwa dhamira ya kulinda chama hicho.

Kufika kwa Jeshi la Polisi kwenye viwanja vya mkutano huo kulibadili taswira ya eneo hilo huku wajumbe wakionekana kukasirishwa na dalili za kutaka kuvuruga mkutano huo.

Prof. Lipumba na wanaomtii walipanga kufanya mkutano huo kwa siku nne mfululizo. Hata hivyo, baada ya wajumbe kuwasili leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mkutano, zoezi la usajili na uhakiki lilianza kutekelezwa.

Wakati zoezi la uhakiki wa wajumbe wa mkutano huo likiendelea, ghafla polisi walifika eneo la mkutano huo na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa CUF.

Hata hivyo, polisi walimtaka Prof. Lipumba kuvunja mkutano huo kwa kuwa, kuna zuio la mahakama. Polisi walianza kuzungumza na viongozi wengine wa chama hicho ikiwa ni pamoja na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya na Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.

Pamoja na taarifa hiyo viongozi hao waliendelea kusema kuwa, watafanya mkutano huo kwa kuwa hawajapokea nakala yoyote inayozuia mkutano huo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, polisi walikuwa na difenda mbili zikiwa na askari polisi na gari moja ya maji ya kuwasha yalikuwa yameegesha nje ya maeneo hayo.

Kelele za chini kwa chini zilianza kusikika “hata kama umekuja na zuio la mahakama sisi hatulipokei kwa sababu wewe huna mamlaka ya kulileta na hapa hatuondoki mkitaka mtuue wote.

Ndipo Prof. Lipumba alitoka na kuanza kufanya mazungumzo na polisi na baadaye kupiga simu ambapo ilisababisha keshi hilo kuondoka na kuacha mkutano ukiendelea.

Simu ya Prof. Lipumba ‘yakimbiza polisi’
Habari njema ,lakini like hakuna ,kuna namna hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisema hapa na nitaendelea kusema ni wachache sana uwaelewa watu ma geneous kama lipumba, nadhani nami niko kundi hili, aimaanishi anafanya mazuri ila kuna kitu kinaendelea watu hawajajua,

"Haro kwani Mukutano ati wanasema utaleta utangamano gani, wewe enderea arafu namwangalia maarimu nasema hihiiiii"
 
Cuf Lipumba sasa inaanza rasmi kujitambulisha kama chama pandikizi la ccm. Hawana future yoyote huko tuendako.
 
Nilisema hapa na nitaendelea kusema ni wachache sana uwaelewa watu ma geneous kama lipumba, nadhani nami niko kundi hili, aimaanishi anafanya mazuri ila kuna kitu kinaendelea watu hawajajua,

"Haro kwani Mukutano ati wanasema utaleta utangamano gani, wewe enderea arafu namwangalia maarimu nasema hihiiiii"

in someone's voice
 
Back
Top Bottom