kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema idadi ya simu feki imepungua kutoka asilimia 30 hadi 18 nchini.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, wakati akiwaeleza wabunge jinsi mitambo ya miamala ya simu inavyofanyakazi na kueleza kuwa ifikapo Juni, mwaka huu, simu zote feki zitazimwa.
Alisema hakutakuwa na msamahakatika suala hilo, kwa kuwa lengo ni kuongeza usalama, kudhibiti wizi wa simu na kuiwezesha nchi kupata kodi halisi katika sekta hiyo.
Alisema wakati wanafanya uhakiki wa simu feki' Disemba mwaka jana, walibaini asilimia 30 ya simu zilizopo nchini ni feki, lakini kwa mwezi huu zimepungua hadi kufikia asilimia 18 na wanatumaini hadi ifikapo Juni, mwaka huu zitaondoka zote sokoni.
Akijibu ombi la baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, waliotaka kuongezwa kwa muda zaidi kwa kuwa wafanyabiashara watapata hasara na serikali pia na kujikita katika kuwatafuta walioruhusu kuingizwa kwa simu hizo, Mungy alisema msimamo utabaki kuwa huo kwa kuwa lengo ni jema kuhakikisha simu zote zinazotumiwa nchini ni halisi.
“Kama mmefuatilia kwa karibu simu 'feki' zinaweza kutumiwa na magaidi kwa kuwa wanajua haziwezi kutafutwa taarifa zake na kupatikana, hivyo tunahitaji kuwa na simu halisi ili tujihakikishie usalama wetu kwa kiasi fulani,” alisema.
Alisema simu feki pia zina madhara ya kiafya kwa wananchi ikiwamo kusababisha milipuko.
Baadhi ya wabunge, Amina Mollel (Viti Maalum CCM) na Ester Matiku wa Tarime Mjini (Chadema), walitaka TCRA kuongeza mbinu za kupambana na uhalifu mtandaoni kwani watu wanaibiwa fedha na mitandao ya simu inahusika.
Matiku alisema mara kadhaa wavamizi mtandaoni (hackers) wamezima simu yake huku ikiendelea kutumika wakachukua fedha zote na kuomba watu mbalimbali kwa kueleza (Ester) amepata matatizo anahitaji fedha kwa haraka.
“Nimeshapoteza zaidi ya Sh. milioni 3 kwenye simu, mara ya kwanza ni wakati wa uchaguzi mkuu walifunga simu yangu ya Vodacom kwa wiki moja na hivi navyoongea tangu juzi wamefunga simu yangu tena inaonesha haina mtandao lakini ukipiga inapatikana nimewafuata Vodacom wameshindwa kunisaidia. Kwa muundo huu ni wananchi wangapi wanaibiwa fedha zao, tunawaomba mtusaidie,” alisema.
Akijibu, Mungy alisema wanashirikiana na polisi kwa karibu ikiwamo kuwapa vifaa vya kisasa na mafunzo na kwa mujibu wa sheria kosa kama hilo anayetendewa anapaswa kuripoti polisi ambao wanaweza kupeleka maombi ya kupewa ushahidi wa kuwakamata watuhumiwa.
Chanzo: NIPASHE