Simu bora unayoiamini ni aina gani?

Maguge Maguge

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
2,734
1,774
Ni karibu miezi miwili iliyopita tangu kampuni inayoaminika sana ya Samsung kutangaza kuondoa toleo moja sokoni la Galax note 7,

Kampuni hiyo Ndiyo kampuni niliyoiamini zaidi, lakini kabla ya kuondolewa kwa simu hiyo ilileta madhara makubwa duniani, kwa kujeruhi watu, licha ya matangazo ya kuiondoa yaliyoathiri watu kisaikolojia na kuleta lapsha, Sina imani nayo kwa sasa!

Je ni smartphone ya kampuni gani unayoitumia wewe, ambayo umetokea kuiamini na kuiona inafaa sana?

c37ad5dbe273f1d3d0b5933952837360.jpg


729f79d347f6fcc146eee48c9e3031fc.jpg
 
Kama hujaona matoleo mengine ya samsung, tecno y3 inakutosha mkuu.
 
Simu bora ninayoiamini ni Motorora Z kuanzia ubora wa camera,Ram kuwa kubwa,na internal memory plus Corning glass 4 ambayo hata uwe na kokoto hauichubui kioo chake!speaker zake balaa
 
Mi sikufichi mzee, ugonjwa wangu ni betri liwe linakaa sana na chaji.
Kwa hiyo simu ninayoiamini sana na nimeitumia sana ni Oukitel K10000.
 
Duuuuuh
Ndo dizaini gani hiyo tena sampuli?
Askwambie mtu!, inakaa na chaji mpaka unasahau kama hii ni android. Sema nzito kishenzi. Uroho wangu wote wa kutumia simu kwa fujo hapa umeisha. Inakaa na chaji kuanzia wiki na kuendelea. Jipimie mwenyewe hapo.
5.5-inches
RAM 2GB
Betri 10,000mAh
Network 4G
Nina mpango wa kutumia android rugged phones, hizo kwa kukaa na chaji Oukitel K10000 cha mdoli, zina zaidi ya 10000mAh, mixer 15000mAh.
 
Back
Top Bottom