Simu 2000 Ltd

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Kampuni nyingine iliyoundwa na fisadi Mkapa ili kutimiza ufisadi wake.

Serikali yapokea bil. 18/- za kampuni ya simu
JIBU LA SWALI LA MBUNGE JIMBO LA LUPA

na Irene Mark na Rahel Chizoza, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

JUMLA ya sh 18,327,520,531.90 zilipelekwa serikalini baada ya mauzo ya mali za iliyokuwa Kampuni ya Simu 2000 Ltd.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Maua Daftari, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM).

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua pamoja na mambo mengine aina ya mali za Kampuni ya Simu 2000 na kiasi kilichopatikana baada ya kuuzwa kwa mali hizo.

Dk. Daftari alisema tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka 2000 hadi lilipomaliza muda wake Desemba 31, mwaka jana, mali za kampuni hiyo ni majengo 103 na viwanja 30.

Kiasi kilichopatikana na sh 18,327,520,531.90 zilizogawanywa mara mbili. Sh 12,827,520,531.90 kwa ajili ya malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliohama Kampuni ya Simu Tanzania zilizolipwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Fedha nyingine kiasi cha sh 5,500,000,000 zilizolipwa na wizara kama gawiwo serikalini. Mali zilizobaki zimehamishiwa Consolidated Holding Corporation chini ya sheria namba 10 ya mwaka 2007.

Awali, Dk. Daftari alisema kuanzishwa kwa Kampuni ya Simu 2000 Ltd kulifanywa chini ya sheria ya makampuni kifungu namba 212. Majukumu ya kampuni hiyo yalikuwa ni kuchukua dhamana ya deni la wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kampuni hiyo pia ilitakiwa kuchukua mali za TTCL zisizokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na biashara ya simu kulingana na tangazo la Serikali namba 87 la 2001 na baadaye tangazo namba 331 kwa ajili ya mali zilizoruhusiwa kubaki TTCL kwa miaka miwili.

Kampuni hiyo ilitakiwa kuchukua kesi za madai zilizokuwa mahakamani kwa kuepelekwa na TTCL au dhidi ya TTCL kulingana na kifungu namba tano cha tangazo la Serikali namba 87.
 
Mbunge, alitakiwa pia kuuliza... au aulize siku nyingine nadhani nafasi na muda bado upo... how much was the operation cost for the said period of existence of that company?
 
Mbunge, alitakiwa pia kuuliza... au aulize siku nyingine nadhani nafasi na muda bado upo... how much was the operation cost for the said period of existence of that company?

Angeuliza pia, hivi nani alimteua Peter Maro, mtoto wa Anna Mkapa na Mzee wa Rombo? Na je, nyumba ngapi alimuuzia mama yake?
 
na angeuliza tena! hatima na wafanyakazi waliokuwa ttcl, na shirika la posta na simu ya afrika mashariki waliokuwa wapangaji wa hizo nyumba alizouza peter maro na mama yake iko wapi?
 
Bilioni 18 ni za marejesho. Ingekuwa vizuri ikajulikana pia thamani ya mali iliyouzwa je, iliuzwa kwa hasara?
 
Yaani hiyo ndio imeshatoka hiyo tena......watu wameshauziwa...mikataba wanayo........
 
Bilioni 18 ni za marejesho. Ingekuwa vizuri ikajulikana pia thamani ya mali iliyouzwa je, iliuzwa kwa hasara?

pia kama taratibu za sheria ya manunuzi zilifuatwa, majengo kama Ilala flats (Lamada hotels), plot opp na udsm etc. au hata mali nyingine mama ndio alishinda zabuni!!
 
Back
Top Bottom