Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,738
- 155,426
Nina miezi 8 tu kwenye ndoa lkn nkmemkinai huyu mwanaume hatari. Akiingia chumbani harufu ya mwili wake (body scent) ikinijia tu mm naingiwa na hasira na hapo hapo moyo unajikunja kabisa.
Usiku nakosa usingizi kabisa na kuanza kujuta kwann niliamua kuolewa na huyu kaka.
Namfanyia visa anichokoze nipate sabb ya kumuacha lkn busara, upole na hekima yake vinanipa wakati mgumu sana.
Kuna wakati naamka usiku naingia chooni na simu nampigia video call boyfriend wangu ili tu nimuone au tuzungumze (japo kwa kunong'ona). Basi tutaangaliana kwa muda hata wa dakika kumi halafu narudi kitandani.
Nampenda toka moyoni boyfriend wangu huyu. Sikutaka kuolewa naye kwasabb hela hana, nikaamua niolewe na huyu mwenye hela.
Sasa moyo wangu haumtaki kabisa. Najilazimisha lkn inimeshindwa.
Naombeni ushauri nifanyeje???