Simple message kwa CHADEMA: CCM haina uwezo wala fedha za kujenga au kurepea daraja

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Chadema mnahitaji message simple kwa wana igunga nayo ni CCM haina uwezo wala fedha za kujenga au kurepea daraja kwani
makampuni yao yote yamewashinda na yamefilisika.

Ni nani anayejenga daraja ?? Fedha zinazotumika kujenga madaraja na mabarabara ni fedha zenu za kodi ambazo zinatokana na wananchi wote walio na vyama na wasiyo na vyama.

CCM haina pesa za kufanyia hata kampeni zake yenyewe na ndio maana iliiba pesa kwa kutumia kampuni ya KAGODA. Kwahiyo nyie wananchi ndio mnaojenga daraja na siyo CCM NI UONGO MTUPU KUSEMA WAO NDIO WANA UWEZO WA KUJENGA DARAJA wangekuwa na uwezo wangefufua shirika lao la sukita.
 
Mkuu tatizo Magamba wanataka kuteka akili za wapigakura! Huyu mgombea wao wakati wa mdahalo, alidiriki kudanganya kuwa mkandarasi wa kujenga Daraja keshapatikana, ilhali akijua si kweli, na wagombea wenzie wakamnanga!! Then, akaishia kusema ULIMI ULITELEZA! usijeshangaa kuwa hata Pombe ulimi umemteleza (si ajabu)!!
 
wanaigunga jmn hebu fungukeni mbona hamjitambui hiv ccm imewaloga mmnaumaskin wa kuwafanya mtie huruma lkn hamjielewi kwann?
 
Chadema mnahitaji message simple kwa wana igunga nayo ni CCM haina uwezo wala fedha za kujenga au kurepea daraja kwani
makampuni yao yote yamewashinda na yamefilisika. ni nani anayejenga daraja ?? Fedha zinazotumika kujenga madaraja na mabarabara ni fedha zenu za kodi ambazo zinatokana na wananchi wote walio na vyama na wasiyo na vyama. CCM haina pesa za kufanyia hata kampeni zake yenyewe na ndio maana iliiba pesa kwa kutumia kampuni ya KAGODA. Kwahiyo nyie wananchi ndio mnaojenga daraja na siyo CCM NI UONGO
MTUPU KUSEMA WAO NDIO WANA UWEZO WA KUJENGA DARAJA wangekuwa na uwezo wangefufua shirika lao la sukita.

Kwanza umeisha enda Igunga ? nchi inatekeleza ilani ya chama gani ? je cdm akichaguliwa ataweza kutekeleza ilani hiyo kwa kuwapigia magoti serikali km wafanyavyo sasa ?
 
Na hilo halipo mwaka huu bajeti ishapita.

Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !
 
Wanaigunga waelewe kuwa hata angechaguliwa mbunge wa UPDP mzee wa solar power daraja litajengwa kwani halijengwi kwa pesa za chama.la msingi ni kuchagua mbunge atakaeibana serikali bila kuogopa kutukanwa na wakuu wake,RA na mapesa yote yale kashindwa kujenga hilo daraja,leo hii KAFUMU,KASHINDE,MAHONA(mzee wa hadithi za kufikirika) hawana uwezo huo.

Bahati mbaya majority ya watanzania huchagua wagombea kwa kupewa ahadi hewa zisizotekelezeka, Mangula alimhakikishia yule babu aliyetaka Malambo yote yafufuliwe kabla ya kuisha mwezi wa 10,akaubali hukuakijua kabisa hilo Haliwezekani. Anyway Kwa utitiri wa shule za kata na mwamko wa vijana kujitambua huenda tukafika tuendako Tanzania Yetu Sote
 
Kwanza umeisha enda Igunga ? nchi inatekeleza ilani ya chama gani ? je cdm akichaguliwa ataweza kutekeleza ilani hiyo kwa kuwapigia magoti serikali km wafanyavyo sasa ?

Kazi ya mbunge ni kupeleka na kutetea haki za wananchi wake bungeni na sio kutekeleza miradi ya maendeleo. Kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa inakusanya kodi na kuzigawa kupitia serikali zake mbalimbali ile wananchi wa maeneo mbalimbali waweze kusukuma gurudumu la maendeleo yao. Kwa maana hiyo basi sio mbunge wa chadema wala ccm mwenye uwezo wa kujenga daraja.

Wanachoweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa kilichotengwa kinatumika ipasavyo kwa kuwa "watch dog" mzuri, kazi ambayo kwa sasa mgombea yeyote wa ccm haiwezi.

Kumbuka kuwa CCM sio na haiwezi kuwa serikali!
 
Kazi ya mbunge ni kupeleka na kutetea haki za wananchi wake bungeni na sio kutekeleza miradi ya maendeleo. Kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa inakusanya kodi na kuzigawa kupitia serikali zake mbalimbali ile wananchi wa maeneo mbalimbali waweze kusukuma gurudumu la maendeleo yao. Kwa maana hiyo basi sio mbunge wa chadema wala ccm mwenye uwezo wa kujenga daraja. Wanachoweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa kilichotengwa kinatumika ipasavyo kwa kuwa "watch dog" mzuri, kazi ambayo kwa sasa mgombea yeyote wa ccm haiwezi.

Kumbuka kuwa ccm sio na haiwezi kuwa serikali!

Somo zuri sana umempa. Kama ni GT nina imani amekueleawa.
 
wanaigunga jmn hebu fungukeni mbona hamjitambui hiv ccm imewaloga mmnaumaskin wa kuwafanya mtie huruma lkn hamjielewi kwann?

Mwanzoni nilifikiri kuwa Chadema lazima kingeshinda, lakini kadri tunavyokaribia tarehe, nazidi kuwa na wasiwasi kama NEC na Dola wataruhusu CCM ishindwe. Vilevile, ninaona kama wana Igunga mwamko bado kidogo.
 
Chadema mnahitaji message simple kwa wana igunga nayo ni CCM haina uwezo wala fedha za kujenga au kurepea daraja kwani
makampuni yao yote yamewashinda na yamefilisika.

Ni nani anayejenga daraja ?? Fedha zinazotumika kujenga madaraja na mabarabara ni fedha zenu za kodi ambazo zinatokana na wananchi wote walio na vyama na wasiyo na vyama.

CCM haina pesa za kufanyia hata kampeni zake yenyewe na ndio maana iliiba pesa kwa kutumia kampuni ya KAGODA. Kwahiyo nyie wananchi ndio mnaojenga daraja na siyo CCM NI UONGO MTUPU KUSEMA WAO NDIO WANA UWEZO WA KUJENGA DARAJA wangekuwa na uwezo wangefufua shirika lao la sukita.

Well said.
 
Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !

Excess ya nini wewe unayoisemea? Hizo ni kodi zetu Acha kuwadanganya watanzania kama watoto
 
Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !
Wewe ndio GT wa ajabu zaidi kuliko wote niliowahi kukutana nao. unaweza kututhibitishia tangu lini nchi hii ikawa na excess kwenye bajeti yetu...? Unajua 300bn inajenga km ngapi za barabara ya lami?? Kama ndivyo hata njaa inayonyemelea nchi yetu isingekuwepo.
 
Magufuli anatoa Rushwa. Anaahidi kujenga daraja yeye kama nani?
Hiyo ni rushwa.
 
Chadema mnahitaji message simple kwa wana igunga nayo ni CCM haina uwezo wala fedha za kujenga au kurepea daraja kwani
makampuni yao yote yamewashinda na yamefilisika.

Ni nani anayejenga daraja ?? Fedha zinazotumika kujenga madaraja na mabarabara ni fedha zenu za kodi ambazo zinatokana na wananchi wote walio na vyama na wasiyo na vyama.

CCM haina pesa za kufanyia hata kampeni zake yenyewe na ndio maana iliiba pesa kwa kutumia kampuni ya KAGODA. Kwahiyo nyie wananchi ndio mnaojenga daraja na siyo CCM NI UONGO MTUPU KUSEMA WAO NDIO WANA UWEZO WA KUJENGA DARAJA wangekuwa na uwezo wangefufua shirika lao la sukita.

Ukweli ni kwamba wao ndio wanapanga bajeti, lakini wanatumia vibaya maradaka hayo kuwarubuni wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa wananchi ndio wamewapa mamlaka ya kupanga hiyo bajeti kwa hiyo wakiamua wanaweza kuwapokonya hiyo mamlaka.
 
Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !

kwa akili yako unafikiri ccm isipochaguliwa ndo wataacha kujenga hilo daraja? hakuna uhusiano wa kuwajengea daraja na uchaguzi wa igunga , ule ni wajibu wa serikali
 
Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !
Kama wana excess walikuwa wapi muda wote huu kujenga? Kwa nini wanasubiri wakati wa kampeni ndipo watoe ahadi kama hizo?
Na ule mpango wa JK kuibadilisha Kigoma kuwa Dubai umefika wapi?
 
Duh hata bajeti hukufuatilia halafu unajiingiza humu na ww uitwe GT. Magufuli ana excess kwenye wizara yake zaidi ya Tshs 300bn , hawezi kushindwa kujenga daraja pesa ipo yakumwaga !
Kwa hiyo huo ujenzi siku zote kwa nini haukufanyika kwa miaka 50 tangu tupate uhuru? Je ujenzi wa hayo madaraja ulikuwa unamsubiri RA ajiuzulu ndiyo ufanyike? Je RA ndiye aliyekuwa anazuia serikali ya ccm isijenge madaraja jimboni mwake? Magufuli nani asiyemjua kwa kuupepeta mdomo?
 
Back
Top Bottom