Elections 2010 Simpendi raisi wangu..

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Raisi wangi muongo, mwingi wa ahadi zisizotekelezeka.
Alipoingia madarakani alianza kwa kulihutubia bunge, hotuba, kali iliyojaa msisimko. Tukajua tumepata raisi anayekuja na kulikomboa taifa letu.

Siku chache baadae,akaja na mpya akasema ana orodha ya wala rushwa wote na atawataja hadharani ili wafikishwe mahakamani na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
hakuwataja.

Siku chache tena baadae, akaja na mpya, ana majina ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, akatuambia atawataja, na watafikishwa mahakamani.
Hakutajwa hata mtu mmoja. Amina wa chifupa akajidai kulivalia njuga swala hili kule dodoma, akajikuta ndio umekuwa mwanzo wa safari yake kuelekea kwenye pumziko la kudumu milele.
kikwete hakuwataja wafanyabiashara hao, na wala hamna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani zaidi ya wale wanaokutwa na kete mbili.

Baadae tena akaja na majina ya wanaofadhili mtandao wa ujambazi nchi, unaovunja mabenki, wizi wa magari na wizi wa kwenye taasisi za fedha. Wimbo wa chiriku wa kikwere ukawa ni ulele.
kimya kikuu.

Uozo unaongezeka kila siku iendayo kwa mungu. Hali ya uchumi imekuwa ngumu kuliko kawaida. Tuliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania, tumepata bora maisha kwa kila mtanzania, na sasa wimbo wao huo wa maisha bora hauimbwi tena, amekaa kimya akitucheka akitucheka tunavyopiga miayo ya njaa.

Haka kajamaa kameshindwa kabisa kutimiza ahadi zake nyingi alizotuahidi. Ametutapeli kura zetu.
Hakika mwaka huu simpi kura yangu hata kwa dawa.
 
ndo ivyo tena ndugu yangu, ni rais wako tayari, upende usipenda keshakalia kiti na atakuongoza tu. cha maana ni kuangalia mawazo ya mlengo wa upande mwingine kwenye uchaguzi ujao....kupenda au kutompenda rais utamia moyo bure..kura yako ndo inaweza kuongea kitu cha maana.
 
Da,
wagombea wetu wenyewe wote chali.
Sijui kwa nini tendwa anaibania ccj?
Huenda ndio wapinzani wa kweli waliotabiriwa na hayati mwalimu.
 
Nakumbuka enzi hizo kila kitu alikuwa anasema serikali yangu itashughulikia sie wanachuo alitahidi hakuna mtoto wa masikini atakayefukuzwa kwa kukosa ada tumemeliza vyou vinatudai 40%zao za 2006
 
Kiranja Mkuu,
Tumia kura yako kumchagua mgombea unayeona anafaa kuongoza. Asiyefaa usimchague.
Kama Rais wako hakufai (umeorodhesha hapo), wakati ujao usimchague yeye, chagua mwingine. Ni haki yako kuchagua unayemtaka.
Pia unaweza kuwaelimisha watu kuwa KURA yao ina maana sana.
Wengi wanaweza kukata tamaa wakidhani kuwa hata wakipiga kura mshindi atatangazwa yuleyule. HII SI KWELI.
 
Nakumbuka enzi hizo kila kitu alikuwa anasema serikali yangu itashughulikia sie wanachuo alitahidi hakuna mtoto wa masikini atakayefukuzwa kwa kukosa ada tumemeliza vyou vinatudai 40%zao za 2006

wow, kumbe aliwaahidi izo ahadi kabambe...aliwapenda kweli. nakumbuka pia mlisukuma gari yake kwa upendo mlokuwa nao kwake...mwaka huu sukumeni tena gari akija kuomba kura.
 
Nasubiri kwa hamu nione mwaka huu atasukumwa na wangapi.
Mbeya kule alipokelewa na watu waliojilaza barabarani ili asipite. Chunya alipigwa mawe.
Watu wamechoshwa sana na utawala wake.
Aangalie ni wapi alipoanguka.
wow, kumbe aliwaahidi izo ahadi kabambe...aliwapenda kweli. Nakumbuka pia mlisukuma gari yake kwa upendo mlokuwa nao kwake...mwaka huu sukumeni tena gari akija kuomba kura.
 
Amina wa chifupa akajidai kulivalia njuga swala hili kule dodoma, akajikuta ndio umekuwa mwanzo wa safari yake kuelekea kwenye pumziko la kudumu milele.
Ufahamu wangu kwa mujibu wa Madaktari na Wauguzi waliomuhudumia ni kuwa aliugua - akafariki, ebu tafadhali nieleweshe ushahidi wa kuvalia njuga suala kuwa chanzo cha kifo chake.
 
Alisema pia kuwa ana majina ya wafanyakazi wa TRA na TPA wanaochukua rushwa bandarini. Mpaka leo hatujayaona.
 
Jana katoa ahadi nyingine kule Moshi baada ya kumaliza kufungua kituo kidogo cha polisi kuwa MIAKA MITANO IJAYO KILA MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATAKUWA NA COMPUTER YAKE! na kasema kwa kuanzia mradi huo utaanza mwishoni mwa mwaka huu na utaanza na shule zaidi ya 3000 katika wilaya 21 lakini hakutaja hizo wilaya
 
Sana sana sitampigia kura huyo mkwere ili hata kama atashinda tena najua si kupitia mgongo wangu. Nitakuwa na amani moyoni mwangu pindi nikifanya hivyo. For sure JK count me out.
 
Raisi wangi muongo, mwingi wa ahadi zisizotekelezeka.
Alipoingia madarakani alianza kwa kulihutubia bunge, hotuba, kali iliyojaa msisimko. Tukajua tumepata raisi anayekuja na kulikomboa taifa letu.

Siku chache baadae,akaja na mpya akasema ana orodha ya wala rushwa wote na atawataja hadharani ili wafikishwe mahakamani na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
hakuwataja.

Siku chache tena baadae, akaja na mpya, ana majina ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, akatuambia atawataja, na watafikishwa mahakamani.
Hakutajwa hata mtu mmoja. Amina wa chifupa akajidai kulivalia njuga swala hili kule dodoma, akajikuta ndio umekuwa mwanzo wa safari yake kuelekea kwenye pumziko la kudumu milele.
kikwete hakuwataja wafanyabiashara hao, na wala hamna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani zaidi ya wale wanaokutwa na kete mbili.

Baadae tena akaja na majina ya wanaofadhili mtandao wa ujambazi nchi, unaovunja mabenki, wizi wa magari na wizi wa kwenye taasisi za fedha. Wimbo wa chiriku wa kikwere ukawa ni ulele.
kimya kikuu.

Uozo unaongezeka kila siku iendayo kwa mungu. Hali ya uchumi imekuwa ngumu kuliko kawaida. Tuliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania, tumepata bora maisha kwa kila mtanzania, na sasa wimbo wao huo wa maisha bora hauimbwi tena, amekaa kimya akitucheka akitucheka tunavyopiga miayo ya njaa.

Haka kajamaa kameshindwa kabisa kutimiza ahadi zake nyingi alizotuahidi. Ametutapeli kura zetu.
Hakika mwaka huu simpi kura yangu hata kwa dawa.
MKUU IMEIPIGA HASWAAA... ni kweli tatizo la rais wetu ni kutoa ahadi na kutokua mkali kuhakikisha zinatekelezwa; as a president unaweza hata kusema jambo na likatekelezwa na mamlaka husika... its just too bad that some of the promises he set were too sensitive and interesting that he ended up disappointing most of us!!

BTW
hivi kuna rais ambaye alitekeleza ahadi zake kama alivyosema??
 
Kiranja Mkuu
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-offline.png
Senior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Join DateThu Feb 2010
Posts247
Thanks : 41
Thanked 80 Times in 57 Posts
Rep Power21Kiranja Mkuu, yupi? si Jk mwenyewe, unataka kusikilizia?
 
Jana katoa ahadi nyingine kule Moshi baada ya kumaliza kufungua kituo kidogo cha polisi kuwa MIAKA MITANO IJAYO KILA MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATAKUWA NA COMPUTER YAKE! na kasema kwa kuanzia mradi huo utaanza mwishoni mwa mwaka huu na utaanza na shule zaidi ya 3000 katika wilaya 21 lakini hakutaja hizo wilaya

Inasikitisha, after 5 years in power, JK still adding his list of promises, without telling us when will he start actioning.
 
Nawasihi kila mtu atumie kura yake vizuri kumchgua mtu anaye fikiri ataifanyia mema Tanzania na sio kuchagua Chama.
 
Back
Top Bottom