Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,541
50,303
Korona haina tiba wala haina kinga. Njia zote zinazoshauriwa ili kujikinga na korona ni za dhahania na nadharia tu. Ndiyo maana hakuna mahala popote walipofanikiwa kuiondoa na kuimaliza korona. Hizo chanjo zimekaa kisiasa na kibiashara tu. Mafua yana karne nzima mpaka leo hakuna kinga, ukimwi una nusu karne mpaka leo hakuna chanjo, halafu leo miezi 9 tunaambiwa Kuna chanjo ya korona! Rubbish!!

Njia na mbinu zinazopendekezwa kuchukuliwa kuepuka korona hazitekelezeki na zinaongeza tatizo. Tumeona maandamano na mabishano hata katika mataifa makubwa kama Marekani, Brazil, Ujerumani na kwingineko wananchi wanapinga makatazo na masharti mbalimbali ya kujikinga na korona yanayowekwa na viongozi wao.

Sasa watanzania wenzangu mnaoshinikiza na kumtaka JPM atoe tamko kuhusu korona naombeni mnijibu. Mnatakaje? Alishasema tumuachie Mungu. Sasa kelele za nini?

Hivi mnataka JPM atangaze kitu gani kifanyike hapa nchini ili kuizuia korona zaidi ya kumwachia Mungu?

Awafungie watanzania ndani? Hawa hawa watanzania wanaokula kwa kufanya umachinga na uchuuzi? Hawa hawa wanaolima na kuvuna ndipo wapate mlo? Hawa hawa wanaochunga mifugo yao kwa kuzunguka nayo maporini? Ulaya kuna zero grazing. Hapa Tanzania na nchi zote za Afrika tutauwa watu na mifugo kwa njaa.

Na ndiyo maana South Africa hali ilikuwa tete, na pale Kenya ulifanyika usanii tu wa kuzuia watu kutoka usiku, halafu mchana kutwa wako majiani. Usanii mtupu. Uganda wamejikanyaga wakashindwa. Usiitolee mfano Rwanda. Kale kanchi ni kadogo sawa na kisiwa cha Unguja ndiyo maana wanagawana gunia kumi za unga kwa siku na zinawatosha.

Halafu hii kunawa nawa, nayo pia ni ujinga tu. Unanawa halafu unaingia kwenye daladala kubanana? Mnashea kikombe cha maji ya kunywa nyumba nzima? Mnashea kete za bao, kopo la mbege, komoni na wanzuki? Acheni zenu bhana! BTW, kirusi kinauawa kwa kunawa? Sanitizer inauwa kirusi? Unazijua tabia za kirusi?

Virus is immortal. Why? This is because Virus is the RNA/DNA particle. Na ndiyo maana mpaka leo ukitaka DNA/RNA ya dinosaurs walioishi miaka milioni150 iliyopita utapata.

Mnataka atangaze watanzania wavae barakoa? Hawa hawa wanaokosa hata leso ya kufutia kamasi? Hawa hawa wanao omba mia tano ya kununua kipande cha muhogo?? Hapa tutasababisha mlipuko wa magonjwa mengine. Maana watu wanaweza kuvaa kitambaa mwezi mzima bila kukifua.

Tumuunge mkono JPM (simtaji kama mheshimiwa Rais kwa kuwa ushindi wake katika uchaguzi wa 2020 mpaka siku nakufa sitaukubali), lakini kwenye suala la korona namuunga mkono 100%.

Tuweke pembeni chuki na tofauti zetu zote za kila aina tuangalie uhalisia. Msimamo wa JPM katika suala la korona unaendana na uhalisia na ndiyo njia bora ya kuifuata. Hayo mataifa yanayojitia kuwafungia na kupiga sanitizer watu wake wamefanikiwa kiasi gani kujikinga na korona?

Halafu hivyo vifo Cha mmoja mmoja vinavyotokea mbona ni kidogo sana kuliko vile vya magonjwa kama malaria, TB, ajali, ukimwi, n.k?? Kwann hivi havihesabiwi??

Wewe mwenye unafuu wa maisha kaa ndani tuache walala hoi tuendelee kuzurura na kupengeana makamasi ili miili yetu ijenge kinga asili dhidi ya korona. (Kajisomee types of immunity, kuna natural na artificial).

Nimemaliza.
 
Naona umeweka hisia zako zaidi.

Kinachopingwa zaidi ni kauli za "hakuna corona, tumemuomba Mungu akaiondoa"....kuhusu tahadhari basi kila mmoja ataona nini cha kufanya.

Hata huko kwingine wanapingana na hatua zinazowekwa kukabiliana na corona lakini hawakatai kwamba tatizo lipo.
 
Duh
 

Attachments

  • FB_IMG_1611682021201.jpg
    FB_IMG_1611682021201.jpg
    53 KB · Views: 7
Ndo maana unakujaga na thread mara mwanamke mara mwanaume...

Kwahiyo watu wanakufa na madaktari hata kushindwa kutoa tahadhari Kwa uwazi ndo msimamo sahihi?
Hata watu kuambiana kuna Corona wanaogopa ..ndo msimamo Sahihi?
Chief sasa unataka JPM afanyaje?
Tushambiwa tuvae barakoa, kunawa mikono, tuepuke misongamano isiyo kuwa na lazima.... mambo mengine ni kujiongeza tu

Au mnataka lockdown

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ndo maana unakujaga na thread mara mwanamke mara mwanaume...

Kwahiyo watu wanakufa na madaktari hata kushindwa kutoa tahadhari Kwa uwazi ndo msimamo sahihi?
Hata watu kuambiana kuna Corona wanaogopa ..ndo msimamo Sahihi?
Nafikiri itakuwa ni kupoteza muda kutoa tahadhari kwa jambo lisilo na tahadhari.

Hakuna tahadhari ya korona inayotekelezeka. Sijui unanielewa???
 
Naona umeweka hisia zako zaidi.

Kinachopingwa zaidi kauli za "hakuna corona tumemuomba Mungu akaiondoa"....kuhusu tahadhari basi kila mmoja ataona nini cha kufanya.

Hata huko kwingine wanapingana na hatua zinazowekwa kukabiliana na corona lakini hawakatai kwamba tatizo lipo.
Umeandika nini sasa wewe zaidi ya kuonyesha chuki za kijinga zisizo na Maana

Jibu hoja, Je? Rais aifunge nchi? Na akiifunga, korona ndio itapotea?

Kwa nini haijapotea huko Ulaya walikojaribu kujifungia?
 
Korona haina tiba wala haina kinga. Njia zote zinazoshauriwa ili kujikinga na korona ni za dhahania na nadharia tu. Ndiyo maana hakuna mahala popote walipofanikiwa kuiondoa na kuimaliza korona...
Unaunga mkono kutokufunga biashara au kutokutoa maelekezo ya kunawa, kukaa mita moja na kuvaa barakoa? Kuna mengi sio swala mmoja ya Corona
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nchi hii ina watu wanaodeka kupita maelezo, yaani Rais atangaze korona ipo ndio uchukue hatua? Kila nikisoma comments za watu huwa napata ukakasi sana.

Ugonjwa huu utaendelea kuwepo hata lockdown ya mwaka ikiwepo!! Hakuna maisha bila kukutana kati ya binadamu na binadamu... Hizo za lockdown sijui carfew ni upumbavu mtupu...

Shida ipo kwa waafrika kufikiria walichosema Wazungu
 
Ndo maana unakujaga na thread mara mwanamke mara mwanaume...

Kwahiyo watu wanakufa na madaktari hata kushindwa kutoa tahadhari Kwa uwazi ndo msimamo sahihi?
Hata watu kuambiana kuna Corona wanaogopa ..ndo msimamo Sahihi?
Ni kawaida mtu kuwa na Hasira hasa mtu anapodhani angepata msaada Mahali Fulani ili tu umsaidie, shida inaanzia pale huo msaada unapokuwa umeshindikana ki akili hizi za kawaida!!

Dawa ni kuacha kutegemea kitu kisichoweza kutatua Hilo tatizo!!!

Juice ya uvuguvugu ya limao, ndimu, tangawizi inasaidia ukijaribu kuwa ndio kifungua kinywa chako kila siku asubuhi
 
81 Reactions
Reply
Back
Top Bottom