Simpendi E.Lowasa, ila kwa hili la Arusha ana hekima mara elfu kuliko Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simpendi E.Lowasa, ila kwa hili la Arusha ana hekima mara elfu kuliko Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King Suleiman, Jan 8, 2011.

 1. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ndg zangu wana jamvi salaamu kwenu,
  sio siri, kwa matukio aliyoyafanya huyu mzee hapo nyuma huwa simpendi yeye na wenzake wote waliohusika kutuletea mazingaobwe ya hasara kwa nchi yetu, weather direct or indirect.

  nikirudi kwenye isu ya Arusha, nakumbuka msemo wa wa wahenga "myonge mnyongeni haki yake mpeni" Lowasa pamoja na mapungufu yake aliona mbali akatoa tahadhari kwa wakubwa wenzake kwamaba jamani tuzungumze Arusha ni kama meli iliyotoboka tuizibe mapema mana dhoruba yake ni kali.

  akibuka mzee mmoja aliyezoea kukurupuka na kusema hovyo (sijui huwa anaota) akamkaripia vikali kigogog mwenzake huyo wa chama amabae angalau aligundua uozo uliofanyika kwamaba inabidi kusafishwa sio kupulizia pafume kwenye uchafu kama alivyofanya Makamba.

  chakushangaza badala hata ya kuoana haya akaibuka teana baada ya tukio la Arusha kuwalaani Chadema tena kwa kutumia maandiko matakatifu ( kama shetani atumiavyo maandiko kurubuni watu wema), na hakuishia hapo akalilia mali za chama chake badala ya watu walio poteza maisha.

  ndg zangu, sina nia ya kumsafisha Lowasa, ila nimemchukua kama sample kupima uelewa wa Makamba ambaye haishi vituko, je ametumia busara kwa nafasi yake kama katibu wa chama chake? TUMJADILI,
  NAWAKILISHA MADA.
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lowasa Pamoja na ushiriki wake katika Ufisadi lakini anajua kuangalia alama za nyakati na anajua hali halisi ya Arusha. Ukizingatia kua Arusha ni kwao na endapo yatatokea mabaya anajua kwa namna fulani yeye binafsi au ndugu zake wa karibu au rafiki zake wataathirika directly au indirectly.
  Hali hii inamfanya afikiri mara mbili katika swala la Arusha.

  Hii ni kwa mtazamo wangu
   
 3. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I agree. Kabla hujazua au kutatua mgogoro ni vizuri ukawaelewa watu wa eneo lile. Inawezekana kwa staili ya Makamba angeweza kufanikiwa huko Bumbuli lakini Arusha huwezi kutumia ubabe watu wakasahau kirahisi. Lowassa anaelewa sana watu wa Arusha na migogoro inavyokuwa complicated kutatua pale wanapokua- provoked. Nafikiri Makamba huwa anasema ndio baadaye anakuja kufikiri wakati wengine wanafanya opposite. CCM waisahau kabisa Arusha kwa miaka mingi ijayo na Polisi wakae chonjo na familia zao maana I know this is not over! Nimezaliwa Arusha, nimekulia Arusha nawaelewa watu wa Arusha vizuri sana. Mark my words : This is not over!
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Huwa nasema siku zote ni heri Lowassa mwizi anajulikana kuliko Pinda aliyevaa ngozi ya kondoo.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  View attachment 19930 [​IMG]

  Endeleeni kumsafisha!!
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Hapa mkuu tunaangalia choo kipi kisafi lakini vyote ni vyoo tu.
   
 7. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Sam taim EL, anajaribu kutafuta kuungwa mkono na Majority.

  Baada ya kusoma alama za nyakati kwani, pia aliwahi kutoa kauli hii:

  "...naishangaa sana Serikali kwa kuja na kauli mbiu yake ya Kilimo Kwanza...badala ya Elimu Kwanza."
   
 8. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  upo sawa ndg yangu, kwa hapa alitumia busara kdg though mtu huyu ananitisha sana na mambo yetu yaleee. bt he think big than Makamba
   
 9. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  hapana ndg yangu K, simsafishi huyu mtu, najua ni hatri kwa taifa letu, but kama ulinisoma vizuri kwenye post yangu, simsafishi ila nimemtumia kama sample tu ya kumpima Makamba na fisadi huyu, kwamba pamoja na ufisadi kamzidi busara
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Katika vitu nitakufa nikiamini ni kuwa Lowassa ni mtu mwenye akili sana na busara pia,tatizo ni namna alivyoamua kuitumia kwenye nchi hii na kufanya mambo ambayo yametugharimu sana kama taifa.Na hili ni tatizo kubwa si tu kwa Lowassa bali watu wengi,uwezo waliopewa wametumia kudhulumu,kudanganya,kufilisi na kuharibu.Hakuna wizi nchi hii umefanywa na watu wajinga na wasioujua wanalofanya hata kanisani ndo hivyo hivyo.Huwezi daima kumlinganisha na Makamba,ukiacha kuwa wako wote CCm but ni watu wawili wasiofanana kabisa labda kwenye hilo la ufisadi.
   
 11. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hana lolote yuko kimaslahi zaidi kwani biashara zake nyingi ziko arusha anaogopa zitadorora. huyu jamaa ana hoteli nyingi za kitalii A town na anategemea sana utalii, yangetokea mwanza ungeona asingesema hata kidogo.

  Mtu yeyote aliye CCM ni wa kumwogopa kama ukoma. Hata sasa walioapa kuwashughulikia mafisadi sasa wako wapi na tunaona Dowans inalipwa hivi hivi.

  Hawana jipya wasubiri karne ijayo labda watawaimpres watz.

  Peoples Power.
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pia nashauri makamba apingane na Nahodha pia! Lowasa asingekuwa na uelewa mkubwa wa mambo angekuwa ndani toka enzi za Baba wa Taifa, lakini anajua sana kunusa kabla ya "kupiga bomu".
   
 13. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hapo alitoa wazo zuri hakukurupuka kama makamba!
   
 14. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hili nalo ni NENO, mh hebu tuanze kutafakari.
  Nimeipenda hii.
   
 15. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  pia unaweza kusema ni heri shetani unayemjuwa, kuliko Malaika usiyemfahamu.
   
 16. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma vilivyo japo ni 'short n clear'.
  Kumbe huwa unatulia on political issues eeh,,,
   
 17. kuberwa

  kuberwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 568
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  anafahamu fika Arusha na wamaasai si wakulima ndo maana anaopt elimu badala ya kilimo! Ndo maana hata Arusha anajaribu kukemea kwa sababu ni kwao, ingekuwa kwingine angekaa kimya tu au kutoa utumbo kama wa makamba. Ningemwona wa maana angekemea uchaguzi wa meya ulogubikwa na ulaghai. Huyu kwa ufupi ni mbinafsi na hana lolote
   
 18. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Ni wapi nisipotulia Mpevu,ha ha ha haaaaaaaaaa! kwenye utani ni utani but on serious issues am serious kama wewe!:playball:
   
 19. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mtayumbishwa na hawa mafisadi hadi mkome ubishi, badala ya kuwakomalia wauaji mnamgeukia mwizi mwingine wa Dowans.
   
 20. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  huwa ukiwa kuleeeeeeeee kwenye forum za 'kijamiii'...........mmmmmh, huwa nakufurahia, yaani nimeshangaa kwa ulichokitoa leo
   
Loading...