Simon Sirro amjibu Makonda tuhuma za kupokea rushwa na kushindwa kudhibiti shisha

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar, Simon Sirro amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuwa huenda amehongwa fedha na wauza shisha ndio imemfanya kushindwa kudhibiti uvutaji wa shisha.

Kamanda Simon Sirro amesema si kweli mapambano hayo yamekufa, kuna watu wafanyabiashara na wauzaji wamekamatwa na majalada yao yamepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



============
Matumizi ya shisha bado yanaendelea mtaani, hadi watu wakadhani kuwa imeruhusiwa, Makonda hakuwa sahihi kumtole shutma mbele ya hadhara lakini Sirro ameonyesha uzembe juu ya hili
Na pengine amepokea rushwa kweli, mwandishi alipaswa amhoji kuhusu matumizi yanayoendelea mtaani ni kuwa hawayaoni?


shisha-smoke-595x350.jpg

wananchi wakivuta shisha mtaani


Uzi wa marejeo

Wale waliopiga marufuku Shisha kwa mbwembwe waje watangaze hadharani kuwa wameiruhusu...
 
Inaonekana mkuu wa Mkoa ana kawaida ya kuchongea wenzake kwa wa kubwa... Ama kwa nia ya kutaka yeye ndio aonekane mtakatifu au ni tabia yake tu ya asili......nasema hivyo nikikumbuka alivyomtuhumu Wilson Kabwe kwa Mheshimiwa Raid juu ya ubadhirufu..........Polisi jitengeni na Siasa..
 
Back
Top Bottom