Simon Group yakiri kuingiza fedha UDA akaunti ya Idd Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simon Group yakiri kuingiza fedha UDA akaunti ya Idd Simba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Aug 15, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Kampuni ya Simon Group ambayo ina hisa kwenye Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) imekiri kuingiza sh. milioni 400 katika akaunti binafsi ya waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba kama malipo ya mchakato wa kumiliki shirika hilo.
  Akizungumza kwenye mdahalo wa "Sakata la ununuzi wa UDA" uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Robert Kisena alisema pesa hizo ziliingizwa kwenye akaunti hiyo binafsi ya mzee Simba kutokana na sababu mbili ikiwemo kama dhamana ya ununuzi na heshima ya mzee Simba.
  Kisena alisema malipo hayo yalifanyika kabla ya malipo ya ununuzi wa hisa asilimia 51, Februari 22, mwaka huu.
  Akifafanua juu ya pesa zilizowekwa kwenye akaunti ya mzee Simba, alieleza wakati wanajadiliana juu ya ununuzi wa hisa hizo Bodi ya UDA iliitaka Simon Group kutoa pesa kama dhamana ili kuepuka usumbufu.
  Alisema hakuweza kuingiza pesa hizo mpaka walipopatiwa barua ya maelekezo ya kisheria ndipo walipoingiza pesa hizo kwenye akaunti ya Simba.
  Kisena alisisitiza kwamba pesa hizo lazima zitalipwa na jitihada zinafanyika ili zirudishwe haraka na kuingizwa katika akaunti ya UDA.
  Alisema mpaka sasa Simon Group imefanya malipo ya hisa walizonunua kwa awamu mbili ikiwa awamu ya kwanza ililipwa tarehe 22 Februari na Februari 25, mwaka huu.
  Alisema Shirika la UDA lilipoanzishwa lilikuwa linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali. Alisema Jiji lilikuwa na hisa ya asilimia 51 na serikali asilimia 49 kupitia Msajili wa Hazina.
  Alisema katika mchakato wa kununua UDA ilionekana Halmashauri ya Jiji ilikuwa mmliliki mkubwa na baada ya mgawanyo uliofanyika, Halmashauri ya jiji ilibaki kuwa na asilimia 24, Serikali asimilia 23 na Simon Group ikanunu asilimia 52 ambazo zilikuwa hazijakuwa kwenye gawio.
  Alisema thamani ya hisa hizo ni sawa na Sh. Milioni 7.8 na thamani wanazomiliki Serikali na Halmashauri ya jiji ni Sh. Milioni 7.1 pekee.
  Alisema kilichopelekea kwa Shirika hilo kuuza sehemu ya hisa inatokana na Shirika hilo kujiendesha kwa hasara kutokana wanahisa wake wawili kushindwa kuongeza mtaji tangu mwaka 1983.
  Alisema kimsingi kampuni yake kuingia ubia kwenye shirika hilo itawezesha kuweka mtaji mkubwa na kuhakikisha kuanzia mwaka huu magari 200 yatanunuliwa ambapo kati ya hayo mabasi makubwa yanayobeba watu 150 kwa wakati mmoja, yatakuwa 150.
  Hata hivyo alipinga vikali kuwa Simon Group inamilikiwa na baadhi ya vigogo na kueleza huko nyuma mmoja wa wanahisa alikuwa Profesa Juma Kapuya aliyemiliki asilimia tano za hisa lakini kwa sasa amejitoa na Kampuni hiyo inamilikiwa na familia mbili ambazo hazina uhusiano na vigogo.
  CHANZO: THE GUARDIAN
   
 2. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Akizungumza kwenye mdahalo wa "Sakata la ununuzi wa UDA" uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Robert Kisena alisema pesa hizo ziliingizwa kwenye akaunti hiyo binafsi ya mzee Simba kutokana na sababu mbili ikiwemo kama dhamana ya ununuzi na heshima ya mzee Simba.

  HUYU MKURUGENZI MSHENZI NA MJINGA SANA SANA ENZI ZA NYERERE USHENZI KAMA HUU UWEZI KUMWACHA ANAIONA ASBH AKIWA NA MKEWE AMA WAKAMSHUGULIKIE WENZIE AMA ASHINDE JESHINI WAKIMPA MAZOEZIZ BABU MASIKINI LAITI ANGESIKIA UDDAAAAAAAAAAAAAA LOH
   
 3. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbona Idd Simba alisema amelipwa pesa kama mshahuri?

  Kimenuka sasa wanatapatapa, na watasema sana. Wanaiba alafu wanatuletea staili ya kurudisha.

  Huyo Idd Simba ana heshima gani na kwa nani katika taifa hili? wakati aliondoka madarakani kwa kashfa. Hii inaonyesha ni jinsi gani watu wanavyochezea mali za umma,
  Kama hii skendo isingeibuliwa ni nani angefahamu kama kuna pesa za umma kwenye akaunti ya mtu binafsi? ndio taratibu za kiserikali? huu ni wizi na hawa watu wanatakiwa washitakiwe kwa makosa ya wizi wa mali za umma, na uhujumu uchumi.

   
Loading...