Simle anaylsis: Matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini za USGN ndio yataamua timu mbili za kufuzu kundi "D"

Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania.

Kwahiyo, timu zitazoifunga hii timu ya USGN nyumbani na ugenini, ndio zina nafasi kubwa ya kusonga mbele na hapa naona Simba teyari wamejiweka katika mazingira magumu baada ya kupata sare leo hii dhidi ya hii timu.

Simba, RS Berkane na Mimosas, wote wana nafasi za kushinda mechi zao zote za nyumbani ila sio ugenini. Mechi ya ugenini ambayo kila timu kati ya hizi timu tatu wanazoweza kushinda, ni ile tu ambayo timu hizi watakutana na USGN (kibonde) huko Niger.

Kwa maana hiyo, matokeo ya nyumbani na ugenini baina ya hizi timu tatu dhidi ya USGN (matokeo ya kushinda), ndio yataamua timu zipi zifuzu.

USGN ikiendelea kuwa kibonde(isipobadilika), Simba watakuwa na nafasi finyu sana ya kusonga mbele baada ya kukubali sare na hawa vibonde kosa ambalo RS Berkane na Mimisosa sidhani kama watalifanya.

Simba kurudisha matumaini, ni lazima ishinde walau mechi moja ya ugenini au itoe sar na na si kushinda za nyumbani kwani kuna kila dalili timu zote zinaweza kushinda mechi za nyumbani isipokuwa hao vibonde (unless nao waacha kugawa point) na ndio maana naseme mechi na huyu kibonde ndio zitaamua wa kufuzu( Simba teyari wamefanya kosa leo).

Mwisho, mshindi wa kwanza na wa pili katika hili kundi anaweza kupatikana kwa kigezo cha idadi ya magoli ya kushinda kwa timu za RS Berkane na Mimosas.

Japo ni mapema sana, lakini huu ndio muelekeo.
Mkuu ingekuwa busara sana ukarudi kwenye uzi wako na “kuchambua” tena baada ya matokeo ya USGN vs Asec
 
Back
Top Bottom