Simkubali Haji Manara na ana Matatizo yake, ila kwa hili la Clatous Chama namuamini 100% na wana Simba SC tusidanganywe na Uongozi wetu

Na hata kama hivyo vipengele vipo bado kuna mazingira ya kufanya vipengele visifuatwe...

Lazima pawe na kifungu kinachompa haki Chama kutengua hicho kifungu au mkataba mzima!!

Kwa mfano, Yanga wanamtaka Chama na wapo tayari kumlipa mshahara wa $100K, wakati Simba wapo tayari kumlipa ONLY $50K (assuming other things remain constant), hapo huwezi KUMLAZIMISHA Chama akacheze kwenye maslahi duni wakati yeye mpira ni kazi yake!

Kutokana na hilo, anaweza kuvunja mkataba na Berkane na kulipa gharama za kuvunja mkataba, na akishafanya hivyo hicho kipengele kinachombana will not exist anymore!

Suala litabaki kwa Kolo na Berkane... je, kuna kipengele kinachosema something like "ikiwa Chama anavunja mkataba na Berkane ili arudi Tanzania kucheza soka, basi Berkane watakiwa kulipa % ya pesa iliyolipwa kwenye uvunjaji wa mkataba" kama compensation dhidi ya kifungu kilichomtaka Chama asicheze Tanzania except kwa timu yake ya zamani!!

Lakini pamoja na suala la maslahi bora/duni, Chama anaweza kurudi Simba only if he's willing to do so lakini kama HATAKI, huwezi kumlazimisha kwenda kwenye klabu asiyo tayari kuichezeaunless kama upo tayari kumlipa mshahara wakati he doesn't deliver!!

Kwahiyo kitakachotokea ni kuvunja mkataba ili hatimae kifunmgu husika kuwa void!!

Lakini yote kwa yote, kwa jinsi soka la Tanzania lilivyotawala siasa, usikute hata kwa huyo Konde Boy hicho kipengele hakipo!!

Hivi Mashabiki wa Kolo unawabebea mbereko gani yaani kwa mfano hasa baada ya kuzuka taarifa kwamba "kumbe Konde kwenda Al Ahly ilikuwa ni janja tu ya kutafuta njia ya kwenda Yanga kwavile piga ua Kolo wasingekubali kumuuza kwenda Yanga"!

A smart way ni kuwaambia "kuna kipengele kinachomlazimisha akitaka kurudi TZ, basi lazima iwe Simba"... hapo watu watabaki roho kwaaaatu, tena hata kama unasema "kinachomkataza kusajiriwa na Yanga kama anarudi TZ"!!
Hongera sana Chige kwa ufafanuzi uliotukuka,it seems your parents didn't waste their school fees.
 
Bado mnaongelea habari za chama, mbona ilo suala lishamalizwa mda mrefu uliopita sasa hivi watu wanaendelea na mambo mengine, Pale yanga kuna mtu makini anaitwa Senzo mbatha mazingiza, uyu bwana ndo sterling wa kila kitu apewe heshima yake yuko smart sana kwenye masuala ya kiuweledi, uyu mwamba kipindi yuko simba ndie aliefanikisha usajili wa Luis mikson baada ya klabu yake ya Afrika kusini kugomea kumwachia kipindi yuko ud songo kwa mkopo, ivyo suala la chama lilikuwa ni jambo dogo sana kwake kukamilisha mchakato wake ilimradi tu kilichokuwa kinasubiliwa ni ridhaa ya kocha alipomkubali kazi ikakamilishwa kimya kimya, ivyo suala la chama limeshamalizwa kinachosubiliwa ni asilimia 10% tu ya kujiunga na yanga January,
 
Vyovyote itakavyokuwa,.SIMBA inahitaji kutulia na kufanya mipango yake kisayansi.
Iachane na style ya YANGA ( Manara ) ..ni sawa na pressure ya soda.

Sioni YANGA ya kisasa zaidi ya propaganda na soka mitandao. Wanadanganyika na matokeo ya mechi hizi za mwanzo kwamba wako vizuri
.Kumbuka Manara anajaribu kufanya kila analoweza ili kumuumiza MO ..Na ndivyo anavyoshawishi hivyo menejimenti ya YANGA iende kwa mawazo yake,. kinachomuumiza Manara ni MO wala si SIMBA...akiwa pekee yake ana rangi Nyekundu, akija public ni Kijani...Acha amshawishi CHAMA wa 2019/20 2020/21.
Simba ina falsafa yake, fans wake. Ni wakati wa kumpa full support MO...kumuunga mkono. This guy is Simba.

Simba ni kambi kubwa yenye watu wenye BRAINS..Ni wakati wa kuonyesha msuli wenu
 
Mbumbumbu wamezoea kudanganywa.
Kama nyani walivyodanganywa kuhusu Morrison
JamiiForums-1742202904.jpg


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka KEROZENE nilipochangia Uzi wakati Chama alipouzwa nilisema hapa hapa kuwa ile ilikuwa ni Gia tu, ila muda mchache atarudi Tanzania na Kutua Yanga SC.

Kuna sababu Kuu Nne ambazo niliziona wakati nachangia huo Uzi kuwa Chama atatua Yanga SC moja ikiwa ni ukaribu wake na Ridhiwani Kikwete, Haji Manara Mwenyewe, Familia ya Rais Mstaafu Kikwete na Kutoelewana Kwake na Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Mo Dewji.

Sijui ni kwanini wana Simba SC wenzangu leo tunakubali Kudanganywa na Uongozi wetu kuwa Chama ana Vipengele vinavyomzuia Kutua Yanga SC wakati kwa Ushahidi uliopo CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez aliweka wazi juu ya hilo kwa Mchezaji Luis Jose Miquissone tu na siyo kwa Clatous Chota Chama.

Achilia mbali yote haya ila kama ukiwa Mfuasi ( Follower ) wa Mchezaji Clatous Chota Chama ( hasa Instagram ) kwa jinsi ambavyo huwa 'anakomenti' hasa kwa 'Kejeli' na 'Dharau' pindi Simba SC ilipofungwa na Yanga SC Ngao ya Hisani, ilipofungwa na Jwaneng Galaxy katika Kombe la Klabu Bingwa Afrika na ilivyotoka Sare katika Mechi zake za mwanzo katika NBC Premier League huwezi si tu Kuamini bali hata Kukubali kuwa anarejea / atarejea Simba SC yetu.

KEROZENE nauheshimu sana Uongozi wangu wa Simba SC na naipenda mno Klabu yangu ya Simba SC ila kwa hili la Chama kurejea Simba SC au ana Vipengele vya Kumzuia kutua Yanga SC nalikataa na nasema ni Uwongo wa Mchana kweupe na sijui kwanini Wametudanganya na kwamba ikitokea kweli akatua Yanga SC watatueleza nini.

Counter pekee ambayo Simba SC wanaweza Kuifanya kwa haraka ili Kujiweka salama ni wao pia kufanya 'Umafia' wa Kumsajili Kiungo Khalid Aucho ( ambaye ndiyo Roho ya Yanga SC ) kwa sasa au Kusajili Wachezaji Mahiri zaidi ya Aucho na Bangala na siyo hizi 'porojo' zao wanazotupa na bahati mbaya Mashabiki wengi wa Simba SC wanaamini / wanawaamini.

Kwa Chama kuja tena Simba SC tusahau.
Kelele nyingiiii ujaonyesha comenti yoyote ya chama pia ujaonyesha icho unachosema hakuna mkataba wa kumtaka kurejea Simba Kama akishindwa. Unaishia kujiumauma tu ooh Mimi simba. Aliyekwambia wewe nyani Nani? Mpaka useme wewe Simba?
 
Hivi watanzania mlirogwa na shetani gani ?Hivi kama simba wangekuwa wanajua bila Chama kuwepo kwenye timu yao hawawi Simba kweli wangemuuza?
Uongo wa kitoto tunaamini kisa kasema try again!
 
Mkuu hapo umeandika $100k ukimaanisha nini?

Ulimaanisha Dollar 100,000?

Kwamba mwamba wa lusaka atakua analipwa na GSM 230,000,000 kwa mwezi?

Watu mna utani sana unajua hata ingekuwa $10,000 bado ni utani, maana ni zaidi ya M 22, yanga inawezaje ku afford hizo gharama kwa kumlipa mchezaji mmoja?
Usipende sana kudakia mambo na kukifanya mjuaji sana mitandaoni. Hapo jamaa katolea mfano na amesema kabisa ni mfano.
 
Kama anataka kujiroga aende yanga basi ajue ndio kituo chake cha kustafia kwanza sasa hivi kwenye timu yake anakaa benchi na kwenye timu ya taifa hajacheza match zote tofauti na mwenzake bwalya aliyeanza kwenye match ya Mauritania.
 
Chama aende yanga, then simba wataenda kumchukua Tuwi la Kisinda eiiiiii patachimbikaaaa hapo
 
Usipende sana kudakia mambo na kukifanya mjuaji sana mitandaoni. Hapo jamaa katolea mfano na amesema kabisa ni mfano.
Hata kama ni mfano, zipo kanuni za kutolea mifano ambazo zinakubalika logically nanmifano yake tunasema ni mifano "hai"

Alichokiandika jamaa hakipo kwenye mizani ya mfano, alichokiandika basically ni utani
 
Mtu mwenyewe ana ngoma miwaya ndio maana waraabu wamemtimua. Wenye kumbukumbu rejea Costantine Kimanda na Methold Mogela.
 
Kwa nguvu ya mpunga na mipango komoa wala sitoshangaa kwetu Yanga kumkosa Aucho na Bangala baada ya kukimbilia SIMBA na pia sitoshangazwa kwa Chama kuja mtaa wa Twiga na Jangwani.......

Muda ni mwalimu mzuri.....

#DaimaMbeleNyumaMwiko
 
Back
Top Bottom