Simkubali Haji Manara na ana Matatizo yake, ila kwa hili la Clatous Chama namuamini 100% na wana Simba SC tusidanganywe na Uongozi wetu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nakumbuka KEROZENE nilipochangia Uzi wakati Chama alipouzwa nilisema hapa hapa kuwa ile ilikuwa ni Gia tu, ila muda mchache atarudi Tanzania na Kutua Yanga SC.

Kuna sababu Kuu Nne ambazo niliziona wakati nachangia huo Uzi kuwa Chama atatua Yanga SC moja ikiwa ni ukaribu wake na Ridhiwani Kikwete, Haji Manara Mwenyewe, Familia ya Rais Mstaafu Kikwete na Kutoelewana Kwake na Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Mo Dewji.

Sijui ni kwanini wana Simba SC wenzangu leo tunakubali Kudanganywa na Uongozi wetu kuwa Chama ana Vipengele vinavyomzuia Kutua Yanga SC wakati kwa Ushahidi uliopo CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez aliweka wazi juu ya hilo kwa Mchezaji Luis Jose Miquissone tu na siyo kwa Clatous Chota Chama.

Achilia mbali yote haya ila kama ukiwa Mfuasi ( Follower ) wa Mchezaji Clatous Chota Chama ( hasa Instagram ) kwa jinsi ambavyo huwa 'anakomenti' hasa kwa 'Kejeli' na 'Dharau' pindi Simba SC ilipofungwa na Yanga SC Ngao ya Hisani, ilipofungwa na Jwaneng Galaxy katika Kombe la Klabu Bingwa Afrika na ilivyotoka Sare katika Mechi zake za mwanzo katika NBC Premier League huwezi si tu Kuamini bali hata Kukubali kuwa anarejea / atarejea Simba SC yetu.

KEROZENE nauheshimu sana Uongozi wangu wa Simba SC na naipenda mno Klabu yangu ya Simba SC ila kwa hili la Chama kurejea Simba SC au ana Vipengele vya Kumzuia kutua Yanga SC nalikataa na nasema ni Uwongo wa Mchana kweupe na sijui kwanini Wametudanganya na kwamba ikitokea kweli akatua Yanga SC watatueleza nini.

Counter pekee ambayo Simba SC wanaweza Kuifanya kwa haraka ili Kujiweka salama ni wao pia kufanya 'Umafia' wa Kumsajili Kiungo Khalid Aucho ( ambaye ndiyo Roho ya Yanga SC ) kwa sasa au Kusajili Wachezaji Mahiri zaidi ya Aucho na Bangala na siyo hizi 'porojo' zao wanazotupa na bahati mbaya Mashabiki wengi wa Simba SC wanaamini / wanawaamini.

Kwa Chama kuja tena Simba SC tusahau.
 
Sijui ni kwanini wana Simba SC wenzangu leo tunakubali Kudanganywa na Uongozi wetu kuwa Chama ana Vipengele vinavyomzuia Kutua Yanga SC wakati kwa Ushahidi uliopo CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez aliweka wazi juu ya hilo kwa Mchezaji Luis Jose Miquissone tu na siyo kwa Clatous Chota Chama.
Na hata kama hivyo vipengele vipo bado kuna mazingira ya kufanya vipengele visifuatwe...

Lazima pawe na kifungu kinachompa haki Chama kutengua hicho kifungu au mkataba mzima!!

Kwa mfano, Yanga wanamtaka Chama na wapo tayari kumlipa mshahara wa $100K, wakati Simba wapo tayari kumlipa ONLY $50K (assuming other things remain constant), hapo huwezi KUMLAZIMISHA Chama akacheze kwenye maslahi duni wakati yeye mpira ni kazi yake!

Kutokana na hilo, anaweza kuvunja mkataba na Berkane na kulipa gharama za kuvunja mkataba, na akishafanya hivyo hicho kipengele kinachombana will not exist anymore!

Suala litabaki kwa Kolo na Berkane... je, kuna kipengele kinachosema something like "ikiwa Chama anavunja mkataba na Berkane ili arudi Tanzania kucheza soka, basi Berkane watakiwa kulipa % ya pesa iliyolipwa kwenye uvunjaji wa mkataba" kama compensation dhidi ya kifungu kilichomtaka Chama asicheze Tanzania except kwa timu yake ya zamani!!

Lakini pamoja na suala la maslahi bora/duni, Chama anaweza kurudi Simba only if he's willing to do so lakini kama HATAKI, huwezi kumlazimisha kwenda kwenye klabu asiyo tayari kuichezeaunless kama upo tayari kumlipa mshahara wakati he doesn't deliver!!

Kwahiyo kitakachotokea ni kuvunja mkataba ili hatimae kifunmgu husika kuwa void!!

Lakini yote kwa yote, kwa jinsi soka la Tanzania lilivyotawala siasa, usikute hata kwa huyo Konde Boy hicho kipengele hakipo!!

Hivi Mashabiki wa Kolo unawabebea mbereko gani yaani kwa mfano hasa baada ya kuzuka taarifa kwamba "kumbe Konde kwenda Al Ahly ilikuwa ni janja tu ya kutafuta njia ya kwenda Yanga kwavile piga ua Kolo wasingekubali kumuuza kwenda Yanga"!

A smart way ni kuwaambia "kuna kipengele kinachomlazimisha akitaka kurudi TZ, basi lazima iwe Simba"... hapo watu watabaki roho kwaaaatu, tena hata kama unasema "kinachomkataza kusajiriwa na Yanga kama anarudi TZ"!!
 
Hivi tatizo liko wapi Chama kwenda Yanga? kwamba akienda Yanga Simba itakuwa sio timu ya mpira wa miguu tena? kwahiyo unataka kusema malengo ya timu kwa msimu huu kayabeba Chama!? kama hivyo mbona aliuzwa? Chama kabla ya kuja Simba ulikuwa unamjua? Kama ndio,Simba ilikuepo au haikuepo?

Anyway,Chama anategemea kuendesha maisha yake kupitia mpira hivyo anaweza kwenda popote ambapo atapata ridhiki,pia Simba kama timu ya mpira wa miguu imekuwepo kabla ya Chama na bado ipo na itaendelea kuwepo.
 
Mimi pia Ni Simba damu Ila acha chama aende yanga Kama ameridhia mwenyewe mbona hata sisi tulimchukua Morrison ingawa wenzetu Hadi leo hiki kitu kinawauma sana.

Pia ntakuwa mtu wa mwisho kuamini et uongozi wa Simba upo smart ,kitu ambacho si kweli Zaid wamejaa ujanja ujanja tu.
Unawezaje kumuuza chama na Luis kwa wakat mmoja alafu huku ukijua unataka kufika mbali Zaid kisoka? Kibaya Zaid unatamba et pesa ipo ,Kama pesa ipo kipi kiliwafanya muwauze key prayers wawil km sio ujanja ujanja tu na mbaya Zaid mmeuza watu ambao wanatamaniwa Sana na watan zetu .na naomba Sana chama atue yanga ili tujue uhuni wa viongoz wa Simba ulipojificha.

Pia swala la Simba kufanya umafia kwa Aucho hicho kitu hakiwezekan kamwe ,yanga wamejipanga Sana na wako Makin tokea swala la Morrison litokee hawawez fanya uzembe Mara ya pili.

Mtu mwingine anayeharibu mipango Ni Mo mwenyewe kwa kupenda Sana mitandao ,sijui aliwaza nn siku Ile kumwambia namna ile chama ,bahat nzuri chama hakumjibu kitu so Ile kitu nadhan bado ipo moyon mwa chama na hata ungekuwa Ni wewe huwez rudia kufanya kazi na tajir mswahil Kama mo.kibaya Zaid manara yupo close na chama na manara hawaiv na mo ,hapa manara anayofaida ya kuwashawish mabos wake kuwa wotoe dau lolote lengo kiwaumiza Simba pia anayo nafas ya kumshawish chama kwa namna yoyote ile.

Hata mm roho imegoma eti chama atarud Simba ,hicho kitu hakipo kabisa.wajinga waendelee kuamin Ila mm hapana kabisa hii ngoma tushazidiwa huo ndio ukweli.

Iman yangu chama atatua yanga Ila hatakuwa chama yule wa Simba ,niamin mm,maana Simba wanamjua nje ndani ,refer Morrison akikutana na yanga anakuwa Hana maajabu Sana ndivyo hata kwa chama itakuwa Ivo ,Ila atawasaidia pale atakapokutana na timu zingine na had kupelekea kubeba ubingwa maana Ni master wa kutoa assist zenye macho .

Simba itafute namba 10 machachari nje ya chama na huyo aucho huo ndio ukubwa Sasa ,kuweweseka kwa mtu ambaye ushamtumia Ni utoto ,haya mambo waachie yanga na timu zingine pia Simba itafute mshambuliaje machachari kaliba ya Moses phiri yule wa Zambia wakifanya usajili wa nguvu kwa huzo namba mbili tu hakuna wakumgusa Simba na Simba ataendelea kutawala mpira wa bongo maana beki Sina wasisi, viungo wa chini Sina tatizo ,winger wapo wa maana tu swala Ni 10 na 9 hapo ndio pakutibu tu.

Simba waache siasa Kama kweli wapo serious tofaut na hapo hawatakuwa na utofaut na yanga wazee wa matukio .propaganda wachane nazo kabisa ,km swala haliwezekan wawambie mashabik ukwel km linawezekana pia wasema Ila sio uongo uongo maana mbele ya safar wataua uamini kabisa kwa wanachama na wapenz wa simba na uongo Ni LAANA mbaya Sana.

Pia waache kushindana na manara maana yule Ni mlemavu pia Ana igo so anajifichia kwenye uzeru zeru wake kuwapanikisha na mnavyohangaika nae kwake ndio kete ya ushindi .
Kuzima Kiki ya manara ilipaswa viongoz wa Simba Waite press kuwa hatuna shida na mchezaj tulie wahi mtumia tuliona hatufai ndio maana tulimuuza hivyo Kama Kuna club inamhitaj ikamsajir maana tayal mazingira yamemshinda huko.
 
Hivi tatizo liko wapi Chama kwenda Yanga? kwamba akienda Yanga Simba itakuwa sio timu ya mpira wa miguu tena? kwahiyo unataka kusema malengo ya timu kwa msimu huu kayabeba Chama!? kama hivyo mbona aliuzwa? Chama kabla ya kuja Simba ulikuwa unamjua? Kama ndio,Simba ilikuepo au haikuepo...
Wakikujibu inavyotakiwa nakutumia vocha ya buku. Yaani dunia nzima Hakuna kama Chama? Na Chama akirudi Simba itakuwa kama Madrid?

Wakati mwingine ni vema tukaujua mpira na kukoment kama tunaojua tunashabikia nini.
 
Hivi tatizo liko wapi Chama kwenda Yanga? kwamba akienda Yanga Simba itakuwa sio timu ya mpira wa miguu tena? kwahiyo unataka kusema malengo ya timu kwa msimu huu kayabeba Chama!? kama hivyo mbona aliuzwa? Chama kabla ya kuja Simba ulikuwa unamjua? Kama ndio,Simba ilikuepo au haikuepo?

Anyway,Chama anategemea kuendesha maisha yake kupitia mpira hivyo anaweza kwenda popote ambapo atapata ridhiki,pia Simba kama timu ya mpira wa miguu imekuwepo kabla ya Chama na bado ipo na itaendelea kuwepo.
Umemaliza yote nashangaa wanakuza Jambo dogo kuonekana kubwaa...Kuna ubaya gani chama kwenda yanga
 
Na hata kama hivyo vipengele vipo bado kuna mazingira ya kufanya vipengele visifuatwe...

Lazima pawe na kifungu kinachompa haki Chama kutengua hicho kifungu au mkataba mzima!...
Mkuu hapo umeandika $100k ukimaanisha nini?

Ulimaanisha Dollar 100,000?

Kwamba mwamba wa lusaka atakua analipwa na GSM 230,000,000 kwa mwezi?

Watu mna utani sana unajua hata ingekuwa $10,000 bado ni utani, maana ni zaidi ya M 22, yanga inawezaje ku afford hizo gharama kwa kumlipa mchezaji mmoja?
 
Kaa kwa kutulia ndugu kwanza kabisa bangala sio size yetu kabisa simba labda aucho na kuhusu chama hata chama mwenyewe alishaweka wazi bado yupo morocco sana,, cool down guy
 
Nitakuwa wa mwisho kuiamini 'Propaganda' hii ambayo nahisi imetolewa sasa ili tu kushusha Presha Klabuni Simba.
Ishu kama hii mi siioni kama ni jambo jipya sana kiasi linishangaze na kunifanya niamini taarifa hii kua ina ukweli wowote

Stastistics zinainesha kuwa yanga mara nyingi wamekua na kawaida hiyo ya kutangaza taarifa za tetesi za kuwasajili wachezaji ambao wanavinasaba na simba

Kwani kile kipindi ambapo chama na miquon wanauzwa, chama alipotangazwa kuwa amesajiliwa berkane halafu kwa miquson kukawa na ukimya, hukusikia tetesi kwamba miqson anaenda yanga?

Tena zile tetesi za mwanzo kuhusu miqson zili catch attention za watu sana kuliko hata hii ya chama, lakini haikuwa hivyo matokeo yake tukaja kumuona miqson al ahly
 
Mimi pia Ni Simba damu Ila acha chama aende yanga Kama ameridhia mwenyewe mbona hata sisi tulimchukua Morrison ingawa wenzetu Hadi leo hiki kitu kinawauma san...

Umeeleza vyema kabisa
 
Back
Top Bottom