SIMIYU: Naibu Waziri Stella Manyanya amemsimamisha Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bunamhala

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,494
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bunamhala, Bw. Ramadhani Said kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, kutokana na utendaji usioridhisha na kumteua Bi. Levina Mrema kushikilia wadhifa huo.

PICHA 1.JPG

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bi. Levina Mrema (kulia) aliyemteua wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja Mkoani Simiyu.
PICHA 2.JPG

Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Bunamhala Ramadhani Saidi (Aliyesimama) akitoa maelezo juu ya chuo hicho kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani) wakati wa ziara yake.
 
Jamaa ana nidhamu. Daah, kasimamishwa na kasimama kweli!
 
Nafikiri serikali ama mawaziri watafute njia mbadala ya Kutumbua majibu. Kwa mtazamo wangu atatokea Mtu ametumbuliwa na yeye hapohapo akamtumbua huyo anayemtumbua hapohapo kwa kichwa ama ngumi ama hata silaha pia.
Chamsingi viongozi wetu waangalie njia nzuri ya kutengua uongozi na si kwenda tu hapo kwa papo na kutoa maagizo kwan naona ipo siku kuna mtu itamtokea puani maamuzi haya yatolewayo kwenye adharani
 
Ni rahisi sana kumfurahisha bwana Mkubwa.....#tumbuatumbua
Hivi mbali na hili la kuwadhalilisha watumishi wa umma, wana lipi jipya?....

wameshugulikia vipi changamoto za Elimu...?...

au ni kutafta sifa tu kwa bwana mkubwa....
 
Mnatoa na kuweka watu wenu kwa kigezo cha kutumbua majipu. Tumewashitua mchezo wenu
Ndo hivo mkuu kazi kudhalilishana tu....mijitu haishughulikii changamoto za elimu, inatafta sifa tu mtukufu...
 
kukomoana kwa kwenda mbereee!! hakuna kuonywa,kupewa muda wa kurekebisha palipobondeka,kusahihishwa unapokuwa wrong,nk. Ni kutimuliwa tuuu mpaka mkome!!!
 
hata hivyo vyuo kwa sasa havina ubora hata fedha za kuendeshea ni tatizo, kwa hiyo hata huyo aliyemteua na yeye atachemka tu, suluhisho ni kuvifufua na kuvirudisha katika ubora wake kama ilivyokuwa mwanzo, kwani vimekuwa vikitegemea misaada kutoka kwa wahisani badala ya serikali
 
Back
Top Bottom