Simiyu: Mwalimu Mbaroni kwa kufanya udanganyifu mtihani wa la nne

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Shimbale Gaudensia Anyango (45) kwa tuhuma za kufanya udanganyifu wa mitihani ya Darasa la 4 kwa kuwachukua wanafunzi wa darasa 5 na 6 kwa ajili ya kuwafanyia mitihani wanafunzi wenzao 23 ambao ni watoro

"Niwatake Watumishi wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani ya kidato cha 2 na cha 4 kuacha vitendo vyovyote vya udanganifu wa mitihani kwani Kamati ya mitihani ya Wilaya na Mkoa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi halitafumbia macho suala hilo" Shadrack Masiji Kaimu RPC Simiyu
 
Simiyu ndio kila mwaka inongoza..Necta bado hawajawa serious..kuna madudu mengi sana.
Tz iko makini kwenye Jambo gani? Kinachofanyika hapa ndio kama kinachotokea kwenye kila uchaguzi, chama tawala na hao polisi wakiongoza zoezi, kwa makusudi maalum!
 
"Niwatake Watumishi wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani ya kidato cha 2 na cha 4 kuacha vitendo vyovyote vya udanganifu wa mitihani kwani Kamati ya mitihani ya Wilaya na Mkoa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi halitafumbia macho suala hilo" Shadrack Masiji Kaimu RPC Simiyu
DEO na REO kimyaaaaaa kama vile hawapo,
 
Kuna watu wana shida sana
Yaani!
Sasa watu watoro, ye mkuu anasumbuka na nini?!! Kwani hao watoro wa mtihani wangemshushia ufaulu? Mi nilifikiri wastani unatafutwa kwa waliofanya tu, au kwa waliosajiliwa bila kujali amefanya au hakufanya?!! Dunia ina mambo sana hii
 
Ni ujinga kwakweli...
 
Ajali kazini, pole yake sana...

Ajali gani kazini anafanya upumbavu hivyo...?!
Watoto ni watoro halafu anafanya kuwasaidia...!?? Huo ni upunguani!
Angewasaidia kabla namna ya kuepuka huo utoro!
30 zinamhusu...informer wa baraza wamejaa kila mahali hivi sasa!
 
Yaani!
Sasa watu watoro, ye mkuu anasumbuka na nini?!! Kwani hao watoro wa mtihani wangemshushia ufaulu? Mi nilifikiri wastani unatafutwa kwa waliofanya tu, au kwa waliosajiliwa bila kujali amefanya au hakufanya?!! Dunia ina mambo sana hii
watoro wanashusha wastani wa ufaulu katika shule, huyo mwalimu alitaka kuziba ombwe kwa kujaza hao wanafunzi wawafanyie mtihani watoro
 
watoro wanashusha wastani wa ufaulu katika shule, huyo mwalimu alitaka kuziba ombwe kwa kujaza hao wanafunzi wawafanyie mtihani watoro
Alaa, kumbe! Kama hivyo jamaa kumbe alikuwa anajaribu kujiongeza ili kulinda nafasi maana siku hizi ukiwa Wa mwisho kazi unayo....namaanisha cheo hauna
 
Polisi Mkoani Shinyanga wanamshikilia Mwalimu Mkuu wa shule moja mkoani humo kwa kujaribu kufanya udanganyifu kwenye mtihani kwa kuwapanga Wanafunzi wa darasa la 5 na darasa la sita kufanya mitihani wa darasa la nne.

"Ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Simbale iliyopo Bariadi anaitwa Gaudensia Anyango (45), alichokifanya aliwachukua Wanafunzi wa darasa la tano na baadhi ya darasa la sita jumla yake 23 akawaingiza kwenye chumba cha mtihani ili wafanye mtihani kwa niaba ya Wanafunzi wenzao"

"TAMISEMI wamekuwa na taratibu kwamba Shule zinazofanya vizuri wanawatambua kwa kuwapa zawadi, pengine hii inaweza kuwa kichocheo kwamba Shule yake ingefanya vizuri zaidi angepewa zawadi, jingine ni kwamba Watoto hawa waliofanyiwa mitihani walikua ni Watoro basi pengine angeweza kuuza hizo nafasi siku za mbeleni"
 
Inashangaza. Walimu wengi wa shule za msingi hawajifunzi kutokana na makosa kama hayo yaliyofanyika hapo awali. Inashangaza pia wengi wao bado wanaendelea kukopa fedha kwenye taasisi zinazotoza riba ya kutisha kwa matarajio ya kulipa mikopo hiyo pindi watakapostaafu. Walimu chukueni hatua madhubuti msije mkalia hapo baadae.
 
Back
Top Bottom